Live on Star TV: Je, Daudi Bashite atajibu maswali haya?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,685
119,325
IMG_20170517_061936.jpg

lemutuz_nation-1495140857028-jpg.512654

Youtube sechi makonda

Wapo Star TV
Wanabodi,

Hili ni bandiko la uhamasishaji, ili kuhakikisha leo, you make sure you don't miss this session!. Macho na masikio yetu yote tumeyaelekeza Star TV, asubuhi hii itakuwa ndio kwa mara ya kwanza kwa Daudi Albert Bashite kujitokeza rasmi hadharani kuzungumzia tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Swali la msingi ni jee atajibu maswali yote ya msingi, yakiwemo maswali yangu haya?. Na, jee ungekuwa ni wewe ungependa kumuuliza swali gani Mhe. Daudi Albert Bashite?.

Kanuni ya kwanza ya haki kote duniani ni "No one is condemned un heard", yaani hakuna mtu anaweza kuhukumiwa bila kusikilizwa!, mtu yoyote mwenye tuhuma zozote, kabla hajahukumiwa, lazima kwanza apewe fursa ya kujieleza na kujitetea.

Wakati Tume ya Mwakyembe ilipomhukumu Edward Lowassa bila kumpa nafasi ya kusikilizwa, sisi wengine humu tuliilaani na kuishutumu kamati ile.

Ni kwa muda mrefu sana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Albert Bashite, ametuhumiwa kwa tuhuma lukuki zikiwemo kughushi vyeti vya elimu, kutumia majina yasiyo ya kwake, kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake kama mtumishi wa umma, kuvamia kituo cha Clouds TV akiwa na askari wenye silaha za moto na mavazi ya makirikiri etc. etc.

Hakuna hata wakati mmoja, mtuhumiwa huyu alipewa fursa ya kujieleza na kusikilizwa, bali alifikia hadi kuhukumiwa na Jukwaa la Wahariri TEF, bila kusikilizwa.

Lakini hatimaye kituo cha Televisheni cha Star TV, kwa busara kubwa, leo, siku ya Jumatatu, kimeamua kumpatia fursa na haki ya kusikilizwa tena akiwa live, mubashara moja kwa moja kutokea studio, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi hiI.

Ni matumaini yangu, wapenzi wote wa haki za binaadamu, wapenzi wa the right to information, wapenzi wa freedom of expression, na wapenzi wa nothing but the truth, wataiunga mkono hatua hii nzuri ya Star TV, na wale wenye nafasi, watahakikisha, they never miss this very interesting session, kwa kuangalia na kusikiliza.

Mimi kwa upande wangu, leo asubuhi nimesitisha shughuli zangu zote na kuelekeza macho na masikio yangu kwa Star TV, ili nisikie mwenyewe kwa masikio yangu huku nikishuhudia kwa macho yangu, tone ya kujibu maswali, pulse ya adrenaline, na eye contacts,ili tukidanganywa, tuwaeleze members humu kipi amesema kweli na kipi amedangaya bila hata ya kutumia lie detectors.

Tuhuma ni nyingi na maswali ni mengi kumhusu Daudi Albert Bashite, lakini nimependekeza machache haya, swali ni jee maswali haya yatajibiwa?.

Muongozo kwa waulizaji maswali, wasiulize maswali kwa mtindo wa simple questions, bali wamuulize kwa mtindo wa interrogations, ili wauliza maswali kuonyesha, they did their homework well.

Maswali 10 ya mwanzo ni intro tuu kwa kumwambia ajitambulishe kwa simple questions na maswali 14 ya pili ni specific with concrete evidence yaliyofanyiwa research hivyo kuhitaji majibu yaliyo nyooka, hakuna room ya kupinda pinda au kukwepa kwepa, ni solid questions zilizofungwa bila mlango wa kutokea, lazima mtu aseme ukweli.

1. Alizaliwa lini, wapi, na aliitwa kwa majina gani?.
2. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
3.Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale Kolomije, alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani?, shule gani na matokeo ni nini, alipasi au alifeli .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5. Alitumia majina gani matatu sekondari, Pamba, alihitimu mwaka gani na alipata matokeo gani?
6. Alijiunga chuo cha Nyegezi kusomea nini, mwaka gani, kwa cheti gani na majina gani?.
7. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa cheti gani chenye majina gani? .
9. Alijiunga chuo cha Ushirika kusomea nini, mwaka gani kwa vyeti vipi, alihitimu lini?
Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
10. Alipoteuliwa alitumia majina gani.

Baada ya hapa, ndipo waje na interrogation questions

11. Uchunguzi wetu umeonyesha ulianza shule mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije ukitumia majina ya Daudi Albert Bashite, na mwaka 1991 ulirudia darasa la nne, kulitokea nini hadi akarudia darasa?.

12. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition), na uliishi kwa Mama Kamese, jee ulifanya kosa gani hadi kufukuzwa kwa Mama Kamese na nguo zako kwenda kutupwa Stendi ya Kolomije, wasamaria wema wakaziokota na kuzipeleka kwa wazazi wako?.

13. Uchunguzi wetu umeonyesha Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 shule ya Nyanza, lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali, uliwezaje kujiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba mwaka 1997 kwa kidato cha kwanza wakati ulifeli Nyanza?.

14. Inasemekana Mwaka 2000 ulihitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero) lakini mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002. Jee uliwezaje kupata cheti cha Paul Christian?, ulikiiba au alikupa mwenyewe?

15. Inasekana Mwaka huohuo 2002 ukitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005, kwa nini uliendelea kutumia majina ya Paul Christian badala ya kubadili majina baada tuu ya kujiunga Nyegezi?.

16. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yako ya uvuvi, kwa nini aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada kilimo bila kubadili majina ya watu?.

17. Baada ya kukosa nafasi kusoma Sokuone, uliwezaje kwenda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta wakati hamna undungu wa aina yoyote?.

18. Mwaka 2006, alipopata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa nini uliendelea kutumia vyeti vyako halali vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani) lakini kwa kutumia majina ya Paul Christian?.

19. Ulipojinga Chuo cha Ushirika, ulidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting na mwaka 2007 ulimaliza first year, kwa nini ulishindwa kuendelea na 2nd year?.

20. Mwaka huohuo 2007 kwa nini uliomba Admission upya? lakini mwaka uliofuata wa 2008 kulitokea nini hadi ukaamua kuacha chuo? na badala yake akaenda kuomba tena udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine wakati mwanzo uliishajaribu lakini akakosa?.

21. Kwa nini mwaka 2009 ulirudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya kwa kaachana na CMA ulisomea hapo mwanzo, na badala yake ukachukua Community & Economic Development (CED)?.

22. Mwaka 2012 alipohitimu shahada yako ya kwanza ya Community & Economic Development, kwa nini uliendelea kutumia jina la Paul C hristian badala ya majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?.

23. Ulipo kula kiapo mahakamani cha kubadili majina, kwa nini uliendelea kuapa kiapo cha uongo kwa kutumia majina ya wizi ya Paul Christian Muyenge na kuwa Paul Christian Makonda ya badala ya kutumia majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?. Jee unajua kula kiapo cha uongo mahakamani ni kosa la jinai?.

24. Kwa nini ulitumia jina la uongo kuolea mke, jee unajua kiapo cha uongo kwenye ndoa, kinaweza kuibatilisha ndoa?. Pia umetumia majina ya bandia kuombea hati ya kusafiria ya Tanzania, jee unajua ni kosa la jinai?.

Naomba niishie kwenye maswali kuhusu jina tuu, hayo mengine yote ya kumiliki mali ni wivu tuu wa maendeleo yake, na kule kuvamia Clouds ni uzushi tuu, the real game ni kwenye forgery, cheating, impersonation, na self pretense, ambayo yote ni makosa ya jinai.

Mambo yalianzia humu humu jf, tarehe 12 Machi, 2016, kwa baadhi yetu kumkubali sana na kumpigia chapuo
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi ...

October 17, 2016
Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito | Page 17 ...

Baadaye tukamshinikiza
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu ...
Makonda, only the truth will set you free! | Page 2 | JamiiForums ...
Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa ...
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya ...
Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo ...
Madawa ya Kulevya: Kumbe Makonda Alizuiwa Kutaja Majina!. Anaamini ...
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi ...
Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko ...
Heko Rais Magufuli kwa msimamo thabiti. Shikilia hapo hapo. Kelele ...
Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent ...
Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...

If you have time, never miss this thing now.

Nakutakia Jumapili Njema.

Paskali,
Update.

Session imeanza, DAB ndani ya nyumba, 15min za mwanzo zimekatika wakizungumzia mambo ya Dar es Salaam. Wakianzia na mambo ya barabara. Watu tunashauku zaidi kusikia hoja za ubashite kwanza mengine yote yatafuatia.

Paskali
My Take.
Mahojiano yamemalizika, Wauliza maswali hawakujiandaa hivyo wakashindwa kumuuliza maswali magumu ya kumbananisha as a result, wameuliza maswali magumu ,Bashir akakwepa likiwepo swali la msingi sana kuhusu kufoji vyeti, Bashite amechomoa, waandishi makini walipaswa kumbananisha with facts and datas, walipaswa kuwa persistent lakini badala yake, wamempa an easy ride kwa Bashite kuwa outshine na hivyo kuibuka mshindi.

Interview kama hiyo ingekutana na mtu kama mimi, hicho kiti alichokalia kingewaka moto na amini usiamini Bashite angelia machozi.

Next time kukitokea a controversial figure, Star TV wamtumie mkongwe Dotto Bulendu angeweza kumbananisha kwenye kona na sio kumpa mteremko wa kuhutubia.

All and all, generally it was a good interview, very interesting, sijilaumu kuvunja shughuli zangu na kuangalia.

Kipindi cha PPR kitaomba appointment ya mahojiano na Bashite, akikubali, just a 15 minutes zinatosha kumaliza kazi.

Hongera zao Star TV kufungua njia.
Nakiri Daudi Albert Bashite ni mzuri kwa kujieleza.

Paskali
 
Mimi ningekuwa ni mkuu wa vipindi na manegement ya Star TV ningefanya hiki kipindi kikawa kama episode kwa sababu ni fursa ambayo haiwezi kuja mara kwa mara.

Ningedonoa donoa ili kufanya episode nyingi zaidi na kila episode inaacha maswali ambayo yatajibiwa na episode nyingine ili kuongeza na ku-maximise matangazo ya biashara.

Hakuna ubishi kuwa hiki ni kipindi kitakachoangaliwa na watanzania wengi na ninadhani kitavunja rekodi kitaifa.

Ninafahamu kuna baadhi ya watu wanasema kwa unafiki kuwa hawawezi kuangalia lakini hao hao watakuwa wa kwanza kufungua luninga zao.

Makonda ni fursa adhimu kwa mfanyabiashara makini!

Wafanyabiashara makini hutumia dhana inayosema, ''If you can't beat them, join them''.
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la uhamasishaji, kesho make sure you don't miss this session!. Macho na masikio yetu yote ni Star TV, wakati kesho itakuwa ndio mara ya kwanza kwa Daudi Albert Bashite kujitokeza rasmi. Swali la msingi ni jee atajibu maswali haya, jee ungekuwa ni wewe ungependa kumuuliza swali gani?.

Kanuni ya kwanza ya haki kote duniani ni "No one is condemned un heard", yaani hakuna mtu anaweza kuhukumiwa bila kusikilizwa!, mtu yoyote mwenye tuhuma zozote, kabla hajahukumiwa, lazima kwanza apewe fursa ya kujieleza na kujitetea.

Wakati Tume ya Mwakyembe ilipomhukumu Edward Lowassa bila kumpa nafasi ya kusikilizwa, sisi wengine humu tuliilaani na kuishutumu kamati ile.

Ni kwa muda mrefu sana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Daudi Albert Bashite, ametuhumiwa kwa tuhuma lukuki zikiwemo kughushi vyeti vya elimu, kutumia majina yasiyo ya kwake, kumiliki mali nyingi kuliko kipato chake kama mtumishi wa umma, kuvamia kituo cha Clouds TV akiwa na askari wenye silaha za moto na mavazi ya makirikiri etc. etc.

Hakuna hata wakati mmoja, mtuhumiwa huyu alipewa fursa ya kujieleza na kusikilizwa, bali alifikia hadi kuhukumiwa na Jukwaa la Wahariri TEF, bila kusikilizwa.

Lakini hatimaye kituo cha Televisheni cha Star TV, kwa busara kubwa, kesho siku ya Jumatatu, kimeamua kumpatia fursa na haki ya kusikilizwa tena akiwa live, mubashara moja kwa moja kutokea studio, kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 3:00 asubuhi.

Ni matumaini yangu, wapenzi wote wa haki za binaadamu, na wapenzi wa the right to information, wapenzi wa freedom of expression, wapenzi wa nothing but the truth, wataiunga mkono hatua hii nzuri ya Star TV, na wale wenye nafasi, watahakikisha, they never miss session, watasikiliza.

Mimi kwa upande wangu, kesho asubuhi nitasitisha shughuli zangu zote na kuelekeza macho na masikio yangu kule Star TV, ili nisikie mwenyewe kwa masikio yangu huku nikishuhudia kwa macho yangu, tone ya kujibu maswali, pulse ya adrenaline, na eye contacts,ili tukidanganywa, tuwaeleze members humu kipi amesema kweli na kipi amedangaya bila hata ya kutumia lie detectors.

Maswali ni mengi kumhusu Daudi Albert Bashite, swali ni jee maswali haya yatajibiwa?.
Muongozo kwa waulizaji maswali, wasiulize maswali kwa mtindo wa simple questions, bali wamuulize kwa mtindo wa interrogations, ili wauliza maswali kuonyesha, they did their homework well.

Mswali 10 ya mwanzo ni intro tuu kwa kumwambia ajitambulishe kwa simple questions na maswali kumi ya pili ni concrete questions zilizofungwa bila mlango wa kutokea, lazima mtu aseme ukweli.

1. Alizaliwa lini, wapi, na aliitwa kwa majina gani?.
2. Majina matatu ya Mzee Makonda ( baba) ni nani? .
3.Majina matatu ya Makonda (mtoto) aliyoandikishwa Primary pale Kolomije, alianza Shule ya msingi mwaka gani na kumaliza darasa la 7 mwaka gani?, shule gani na matokeo ni nini, alipasi au alifeli .
4. Baada ya kumaliza la 7 alijiunga na sekondari gani mwaka gani?.
5. Alitumia majina gani matatu sekondari, Pamba, alihitimu mwaka gani na alipata matokeo gani?
6. Alijiunga chuo cha Nyegezi kusomea nini, mwaka gani, kwa cheti gani na majina gani?.
7. Alijiunga Mbegani mwaka gani kwa cheti gani chenye majina gani? .
9. Alijiunga chuo cha Ushirika kusomea nini, mwaka gani kwa vyeti vipi, alihitimu lini?
Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.
10. Alipoteuliwa alitumia majina gani.

Baada ya hapa, ndipo waje na interrogation questions

11. Uchunguzi wetu umeonyesha ulianza shule mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije ukitumia majina ya Daudi Albert Bashite, na mwaka 1991 ulirudia darasa la nne, kulitokea nini hadi akarudia darasa?.

12. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition), na uliishi kwa Mama Kamese, jee ulifanya kosa gani hadi kufukuzwa kwa Mama Kamese na nguo zako kwenda kutupwa Stendi ya Kolomije, wasamaria wema wakaziokota na kuzipeleka kwa wazazi wako?.

13. Uchunguzi wetu umeonyesha Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 shule ya Nyanza, lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali, uliwezaje kujiunga na Shule ya Sekondari ya Pamba mwaka 1997 kwa kidato cha kwanza wakati ulifeli Nyanza?.

14. Inasemekana Mwaka 2000 ulihitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero) lakini mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002. Jee uliwezaje kupata cheti cha Paul Christian?, ulikiiba au alikupa mwenyewe?

15. Inasekana Mwaka huohuo 2002 ukitumia cheti cha Ndg. Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005, kwa nini uliendelea kutumia majina ya Paul Christian badala ya kubadili majina baada tuu ya kujiunga Nyegezi?.

16. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yako ya uvuvi, kwa nini aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada kilimo bila kubadili majina ya watu?.

17. Baada ya kukosa nafasi kusoma Sokuone, uliwezaje kwenda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta wakati hamna undungu wa aina yoyote?.

18. Mwaka 2006, alipopata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa nini uliendelea kutumia vyeti vyako halali vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani) lakini kwa kutumia majina ya Paul Christian?.

19. Ulipojinga Chuo cha Ushirika, ulidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management & Accounting na mwaka 2007 ulimaliza first year, kwa nini ulishindwa kuendelea na 2nd year?.

20. Mwaka huohuo 2007 kwa nini uliomba Admission upya? lakini mwaka uliofuata wa 2008 kulitokea nini hadi ukaamua kuacha chuo? na badala yake akaenda kuomba tena udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine wakati mwanzo uliishajaribu lakini akakosa?.

21. Kwa nini mwaka 2009 ulirudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya kwa kaachana na CMA ulisomea hapo mwanzo, na badala yake ukachukua Community & Economic Development (CED)?.

22. Mwaka 2012 alipohitimu shahada yako ya kwanza ya Community & Economic Development, kwa nini uliendelea kutumia jina la Paul C hristian badala ya majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?.

23. Ulipo kula kiapo mahakamani cha kubadili majina, kwa nini uliendelea kuapa kiapo cha uongo kwa kutumia majina ya wizi ya Paul Christian Muyenge na kuwa Paul Christian Makonda ya badala ya kutumia majina yako halisi ya Daudi Albert Bashite?. Jee unajua kula kiapo cha uongo mahakamani ni kosa la jinai?.

24. Kwa nini ulitumia jina la uongo kuolea mke, jee unajua kiapo cha uongo kwenye ndoa, kinaweza kuibatilisha ndoa?. Pia umetumia majina ya bandia kuombea hati ya kusafiria ya Tanzania, jee unajua ni kosa la jinai?.

Naomba niishie kwenye maswali kuhusu jina tuu, hayo mengine yote ya kumiliki mali ni wivu tuu wa maendeleo yake, na kule kuvamia Clouds ni uzushi tuu, the real game ni kwenye forgery, cheating, impersonation, na self pretense, ambayo yote ni makosa ya jinai.

Mambo yalianzia humu humu jf, tarehe 12 Machi, 2016, kwa baadhi yetu kumkubali sana na kumpigia chapuo
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es ...
Mafanikio ya Makonda ni Uthibitisho Wa Jiwe Walilolikataa Waashi ...

October 17, 2016
Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito | Page 17 ...

Baadaye tukamshinikiza
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu ...
Makonda, only the truth will set you free! | Page 2 | JamiiForums ...

Ndugu, Jamaa na Marafiki, Njooni Tumtetee Makonda Dhidi ya Mapapa ...
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya ...
Mchungaji Gwajima ni Mtumishi wa Mungu wa kweli au? Asema Uongo ...
Madawa ya Kulevya: Kumbe Makonda Alizuiwa Kutaja Majina!. Anaamini ...
Je, wajua Rais aweza kuteua yeyote hata darasa la saba?. Teuzi ...
Watanzania ni watu wa ajabu sana!, Wanamwaminije Gwajima kuliko ...
Heko Rais Magufuli kwa msimamo thabiti. Shikilia hapo hapo. Kelele ...
Media Kususia Habari za Fulani: Jee Tanzania Tuna Independent ...
Insane Anahitaji Huruma, Kusaidiwa. Sio Kulaumiwa, Kulaaniwa na ...
Kuwa Kichaa Sio Mpaka Kuokota Makopo!. Jee Tanzania Tuna Vichaa ...

If you have time, never miss this thing tomorrow!.

Nakutakia Jumapili Njema.

Paskali,
[/QUOTE]
Mjinga hutumwa kufanya ujinga Wa kijinga hakuna mwenye akili atakaye kaa na kupoteza mda kwa ajili ya bashite

Imenikera nimeshindwa kukukera zaidi

Kwanza star tv haina utofauti na TBC ujinga mtupu Leo mnamtangaza mjinga mwenzenu
 
Mbona tunasikiwa wanahabari mlikubaliana kumsusia huyu jamaa. Au mmempa tena fursa au wanahabari mna vikundi vikundi ambavyo vingine haviathiliwi na maamuzi ya Chama chenu.

Kila mtanzania Dukuduku litatoka atakapojibu hayo maswali ya msingi uliouliza changamoto atayajibia wapi?.Kwa hiyo mkuu pasco Uko upande wa wananchi kutaka kujua majibu ya maswali ya msingi na sumbufu yaliyodumu muda mrefu sasa au uko upande wa chama cha wanahabari kwamba wanachokifanya Star TV ni kukiuka makubaliano yao?
 
Sahara Media Group Inajitia Majaribuni Yenyewe Na Kila Mtu Anaona Mchana Kweupe
Huwezi Kujiweka Kwenye Hatari Unawezaje
Kumpa Airtime DAB Wakati Maamuzi Ya kuomba Radhi Aliyopewa Na Jukwaa La Wahariri Ameshindwa Kutekeleza

*Najiuliza Tu Hao Watakaomuuliza Maswali DAB Wakiwa Live Hawataona Aibu ?

*Jamii Ya Habari Itawachukuliaje ?

*Watanzania Watawaonaje Hao Watangazaji ?
 
Toka lini StarTV wakauliza maswali ya kiwaki kama hayo kwa mpendwa wa Rais, tushang'amua kuwa unapiga promo kiaina kesho watu wamuangalie mtu ambae anatumia nguvu kubwa kuwaaminisha watu kuwa ni msafi
 
Back
Top Bottom