Kabla ya kupunguza gharama za kuingiza umeme kuwa 27000, wangefanya huduma hiyo kuwa ya haraka kwa bei ya zamani

Zoezi la 27000 halina logic ya kiutendaji uwezekano wa kubuma ni mkubwa sana!

Inakuwa kama MTU aliyelala uchi na mwanamke usiku kucha kashindwa kula mzigo, sasa kumekucha mbele ya macho ya watu kibao ndo anajitutumua kumpetipeti ili watu waone anaweza! Kumbe hanithi mkubwa!

Ni wapi huko huwa mnakula mzigo mbele ya watu? Mifano mingine ni ya kipumbavu kutajwa humu!
 
Kwa maisha ya kiafrika
Jitahidi kwenye simu yako kwenye sile namba muhimu muhimu zisikosenane za TRA, Tanesco, uhamiaji, NEMC, halmashauri ya wilaya, mkuu wa shule etc etc kutegemeana feeding yako

Mkuu wa shule ipi?
 
Tshs 2,700 - 10,000 kwa mita moja ya LUKU!
Sidhani kama uko sahihi mkuu.
Mita ya LUKU (Single Phase) si chini ya Tshs 80,000/-
Nadhani Shirika hili limeanza kutoa huduma sasa.
Kama tunaweza kulipia Service Line kwa Tshs 27,000/- tu wakati mita inanunuliwa kwa Tshs 80,000, hii ni hatua kubwa sana ya huduma.
Hapo tunaongelea mita tu bila kuhusisha vifaa vingine kama: waya, nguzo, vikombe, bracket, labour, transport & contingencies!
 
Unadanganya bila aibu! Yaani mita kiwandani ichukuliwe elf 80? Ebu kama hujui jaribu kuuliza hata wale waagizaji wakubwa kina Manji waliuziwa mita tsh ngapi huko China!

Bei za luku order huko kiwandani ni chini ya elf 10 hadi elf 2700! tu,
 
Tangazo la kushusha gharama za kuunganisha umeme lilitoka lini mkuu?.
 
Huyu waziri ni wale wale autopilot hana jipya ni wa kupumzisha hana lolote!! Atawafokea Tanesco wakati yeye mwenyewe ameongea vitu bila planning!! Shame!!
 
Umeongea point ila mm kelo yangu ipo upande wa pili ya watu wa dawasco nakushauli fungua uzi khsu watu wa dawasco hawa ni maboya waliopiliza sio kwa mita wala bill za maji aise huku tanesco kwa ss washatengenezewa vishoka ulaji hakuna jinsi ilo lipo wazi lipa elfu27 watengeneze waze za mboga maisha yasonge
 
Juzi nilipita ofisi moja ya tanesco kufuatilia inshu zangu ,foleni ya waliokuja kuchukua form ya kuunganishiwa umeme ni hapa na mbinguni.
 
Hiyo 27000 mliyokuaga mnaililia imetengeneza mwanya mwingine wa rushwa

Haya mambo nchi kuondoka ngumu sana
Labda kizazi kilichopo sasa chote kihangamieee

Ova
 
Natamani inchi yangu ijifunze kuangalia kipaumbele cha kero!

Ni kweli kabisa gharama za kuingiza umeme hazitakiwi kuwa kubwa namna ile kutokana na mazingira kwamba Luku na miundo mbinu si Mali ya mteja Bali ni Mali ya mtoa huduma!

Lakini kutokana na mipangilio mibovu, pamoja na kuwepo ile gharama kubwa ya awali lakini wateja walioomba umeme walikaa miezi na miezi kusubiri kuunganishiwa umeme huo!
Hivyo ukitazama hapo kero haikuwa bei kubwa mjini, Bali kero kubwa ilikuwa kwenye ucheleweshwaji wa huduma!

Hivyo kitaalam katika utatuzi wa kero; kama kweli serikali inania njema na wananchi ingehakikisha inaboresha huduma kwanza kiasi cha kufunga luku ndani ya siku 1,2 au 3 mwisho, kwa bei ile ile kubwa ya awali! Halafu ndipo baadae waje na mpango mkakati wa kupunguza bei mijini!

Nasema hivyo kwasababu;

1. Kama bei kubwa walishindwa kuitumia kwa faida ya kutoa huduma bora na haraka, sasa hivi watawezaje kwa bei ya 27000? (Simple logic)..

Yaani ni kama vile magari ya mwendokasi yatangaze kupakia bure wakati pamoja na kulipia nauli msongamano ni mkubwa itakuwaje ikiwa bure watu si watakalia hadi kiti cha dereva?

2. Ukitembelea China na south afrika watengenezaji/ Viwandani wanauza luku kwa bei ya chini kabisa kati ya 2700 ~10000 kulingana na kiwanda, Je, selikali ilishindwaje kubajeti pesa za wateja wa awali walizolipia gharama kubwa mijini ili iagize Luku nyingi za kutosha ili ziwe zinasubiri wateja, badala ya wateja kusubiri Kuwekewa luku kwa mda mrefu? Haioni kwamba kipaumbele kilikuwa ni huduma na si bei?

3. Ni matarajio yangu kama serikali wangekuwa serious na bei ile ile kubwa ya mwanzo! Wangeweza hata kulink na halimashauri ili mtu anapoanza ujenzi wa msingi tu Dawasco na Tanesco wamtembelee mteja na kumsogezea huduma ya mda, halafu akikamilisha ujenzi wanamfungia permanent. Ujenzi unahitaji umeme kwa ajili ya kukata nondo,drill na kupump maji! Hivyo hata mauzo ya Unit yangeongezeka!

4. Kwa bei ile ile ya zamani mijini, wangeweza kuwachukulia masaveyor mikopo ya vigari vidogo vyenye 4wheel (Suzuki Jimmy) ambavyo vingekuwa rasmi kwa ajili ya kufanya savey tu, kwanza vinatumia mafuta kidogo, pia wangevifunga GPS, hivyo zoezi la savey lingekuwa rahisi mno kuwafikia wateja!

Yapo mengi sana kuwashauri...lakini kusema ukweli KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHA UMEME PASIPO KUYAFANYIA KAZI HAYO mmejidanganya!

Serikali itaaibika kwa msongamano mkubwa utakajitokeza!
Halafu mahitaji yatakuwa Mara NNE zaidi ya mwanzo! Maana yake automatically na mda wa kusubili LUKU utakuwa Mara dufu hadi mwaka au miaka miwili!

MTAWAPA KAZI BURE TAKUKURU KUFUATILIA RUSHWA zitakazojitokeza kwa mipango mibovu ya kisiasa!

Mijini kero kubwa haikuwa bei kwa sasa, Bali huduma kwanza!
Ukikaa na wafanyakazi wa Tanesco utaelewa kwanini mambo hayaendi, wao kwa wao hawaheshimiani, hawapendani, hawaelewani, inasadikika wanapigana sana juju, hata akili zao waliowengi si nzuri, wanatukanana matusi ya nguoni hadharani, labda ningeshauri, wasilipwe mishahara kimazoea, walipwe kwa idadi ya connection za umeme walizofanya
 
Tangazo la kushusha gharama za kuunganisha umeme lilitoka lini mkuu?.
Mwezi uliopita
Ukikaa na wafanyakazi wa Tanesco utaelewa kwanini mambo hayaendi, wao kwa wao hawaheshimiani, hawapendani, hawaelewani, inasadikika wanapigana sana juju, hata akili zao waliowengi si nzuri, wanatukanana matusi ya nguoni hadharani, labda ningeshauri, wasilipwe mishahara kimazoea, walipwe kwa idadi ya connection za umeme walizofanya
Hilo nalo neno
 
Upo sahahi lakini mdiyo hivyo...
Ilitakiwa tanesco wajiendeshe kwa fedha za mauzo yao wenyewe! Kuliko kusubiri huruma ya hazina kuwagawia mgao wa mahitaji yao!.

Ambapo pesa za wateja wao wanazolipia huduma badala ya kuleta vifaa huwa zinapelekwa kutekeleza majukumu mengine kama barabara, madawa n.k
Badala ya kutumika kuletea vifaa kwa wakati ( kiufupi serikali iache kujikopesha pesa ndipo watafanikiwa kutoa huduma haraka)
 
Zoezi la 27000 halina logic ya kiutendaji uwezekano wa kubuma ni mkubwa sana!

Inakuwa kama MTU aliyelala uchi na mwanamke usiku kucha kashindwa kula mzigo, sasa kumekucha mbele ya macho ya watu kibao ndo anajitutumua kumpetipeti ili watu waone anaweza! Kumbe hanithi mkubwa!
Ukitoa hoja bila kuweka mifano ya kizinzi hutaeleweka?
 
Ilitakiwa tanesco wajiendeshe kwa fedha za mauzo yao wenyewe! Kuliko kusubiri huruma ya hazina kuwagawia mgao wa mahitaji yao!.

Ambapo pesa za wateja wao wanazolipia huduma badala ya kuleta vifaa huwa zinapelekwa kutekeleza majukumu mengine kama barabara, madawa n.k
Badala ya kutumika kuletea vifaa kwa wakati ( kiufupi serikali iache kujikopesha pesa ndipo watafanikiwa kutoa huduma haraka)
Lakini wanapata jeuri kwakuwa wana uhakika wa mshahara mwisho wa mwezi, wangeambiwa wanalipwa kwa kwa idadi ya wateja wanaowafungia umeme wangetia adabu
 
Back
Top Bottom