KERO Utaratibu mbovu malipo Kodi ya Majengo kwa wenye zaidi ya Mita 1 za Umeme unatutesa Wananchi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kutoka Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Kata ya Kiseke, Mtaa wa Nyabusaru kuna hii kero ya Kodi ya Jengo, mwanzo Serikali ili tangaza kuwa kama unamiliki Mita Mbili za umeme au zaidi ya hapo ndani ya jengo moja, basi utapaswa kufika TRA na kujaza fomu ili kuchagua Mita 1 kati ya hizo 2 au 3 zilizopo kwenye jengo lako ili iwe ina tumika kulipa Kodi ya Jengo.

Mwanzo huduma hii tulikuwa tunaipata TRA lakini kwa siku za hivi hapa karibuni tumejaribu kufatilia huduma hii, Ofisi za TRA Mwanza tunaambiwa huduma hii haipo TRA imehamishiwa Halmashauri.

Hivyo anayehitaji anapaswa kwenda Halmashauri ya Ilemela, ukienda hapo napo unaambiwa kuwa “Huduma hiyo kwetu haipo, nenda TANESCO ya eneo lako”.

Ukifika TANESCO napo unaambiwa wao hawahusiki na huduma hiyo na kukutaka urudi TRA, sasa imekuwa ni kuzungushana haijulikani ni ofisi ipi inahusika na jambo hili, tunaomba msaada kwenye idara zai wawasiliane na kutoa muongozo.
 
Back
Top Bottom