Hizi ni huduma ambazo Serikali ingetakiwa izitoe bure kabisa

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,721
Hizi hapa ni huduma ambazo serikali ilitakiwa izitoe bureee kabisaa,

Kuingiza umeme kwenye makazi na biashara, ukimuuliza kila mtu gharama alizotumia kuingiziwa umeme kila mtu atakupa ya kwake,

Ikiwa gharama rasmi ya serikali inajulikana mfano 27000 lakini mtu anatumia 150000 inaenda kwa mtu mmoja na huyo mtu huchukua kila sehemu kwa kiasi chake,

Basi serikali ili ipate mapato hiyo huduma waifanye bure kabisa tena isiwe na mzunguko na itangeze kwa uma kuwa kuingiziwa umeme ni bure hata kwa sehemu zisizozidi nguzo zaidi ya tatu,

Je, Serikali itapataje mapato?

Mtu atakapoingiziwa umeme atakuwa anakatwa pesa kila mwezi kulingana na gharama aidha kwenye nguzo na hiyo gharama atakatwa ndani ya mwaka mmoja.

Naamini hata kama ni luku ya 30 kwa mwezi mtu atapambana mpaka tu anunue,

Huu mfumo utafanya serikali ipate mapato bila ya mwananchi kuumizwa na hasa wafanyakazi wa tanesco,

Vipimo kwenye mahospitali, yaani mgonjwa anapimwa tu bure halafu atafute tu hela ya matibabu.

Usafiri kwa wanafunzi hasa wa mijini, kwanza kabisa serikali ina magari mengi sana ambayo ni mazima lakini hayatumiki

Nikikaa nikafikiri jinsi mwanafunzi wa dar anayeanza darasa la kwanza mpaka sec mambo anayokutana nayo kila siku hasa kwenye usafiri wa uma kidogo inaumiza,

Serikali iuze magari ambayo hayatumiki inunue magari ya wanafunzi yawe makubwa kama yale yanabeba wafanyakazi hasa wa viwanda kila shule ipate kulingana na wanafunzi, hapa nazungumzia shule za mjini,

Haya magari kazi iwe ni moja tu kubeba wanafunzi na wanafunzi watachangia miambil kila siku halafu dereva na konda walipwe na serikali hii miambili ya nauli atakayotolewa na mwanafunzi itakuwa ni kama gharama tu ya kuongeza nguvu za uendeshaji wa hiyo huduma ya usafiri,

Kama serikali inatumia pesa nyingi kuwekeza kwenye elimu ya juu naamini kwa hili haitashindwa

Kuingiza maji hii iwe tu kama utakavyokuwa umeme,

Maoni yangu ni hayo tu. ongeza na ya kwako ewe mdau wa JF
 
Back
Top Bottom