Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi


That is radiculous, you can not join organizations without consulting the People.

Tanzania comprises of Christians, Islams, and others. The Citizens of TZ must be involved in such issues. I think it is unethical and unmerital doing what they are doing without consulting pioneers.

Who do they think they are?
 
Mkandara

Mimi nijuavyo serikali inataratibu zake za ndoa wala haifuati utaratibu wa kikristu ama kipagani ama kiislamu,ila serikali inazitambua ndoa hizo.

Serikali yetu kwa kua haina mambo ya dini yenyewe inatambua NDOA kwa mtu yeyote aliyeishi na mke ama mme zaidi ya miezi sita.Kama nimekosea nirekebishe.

Na ndio ikitokea kumtimua mke/mme na mmeishi pamoja zaidi ya miezi sita na mkaenda mahakamani mahakama inahukumu mali mlizochuma pamoja kwa mda huo.
Tatizo liliopo na kua mara nyingi watu wamekua hawaendi mahakamani na kuamuliwa na wazee wa mabaraza ama ndugu mjomba nk.

sasa unapotaka serikali ifuate sheria za dini fulani hapo ndipo tunaanza kuhoji,Na lazima waiislamu watambue wanapoingiza swala hili ndani ya KATIBA inakua ni haki ya msingi ya kila mtanzania kujadili suala hilo maana katiba ni yetu wote na si kuwaingilia ama kuwazibia kama wanavyojaribu kuweka ngao.
Ila kama suala hili lingekua BAKWATA na dini zingine kuliingilia kujadili kweli ingelikua tunawaingilia.
 
au ndio maana mkakati wa KADHI umepamba moto ikiwa moja ya mkakati wakuelekea huko?

Ni ngumu kua mwanachama wa AFRICAN UNION wakati nchi ni ya Amerika kusini.
 

Kinachofanyika hapa ni;
Kwanza; kujiunga na OIC
Pili; kuimarisha Mahakama ya Kadhi
Tatu, . . . . ? !!?
 
Can we join as an Observer Nation before commiting to full membership?
 
http://en.wikipedia.org/wiki/Organization_of_the_Islamic_Conference
Angalia nchi wanachama za OIC na mwaka zilizoingia uanachama



Mkuu.

Pongezi kwako kwa hili.
Unajua mawazo ya kibaguzi huwa hayaletwe na mtu ila ni sisi wenyewe.Nyinyi wachangiaji wenzangu hapo juu,mngeweza hata kufanya uchambuzi tu kidogo wa hayo malalamiko yenu alafu ndio mlete hapa.

sasa ona hata Nigeria imo kwenye hii organisation,kama wafatiliaji wa mambo mnakumbuka Nigeria ndio BIAFRA ilipo,hiyo ndio hata ilimfanya Nyerer agombane na Amin lakini agalia hata wao leo wamo kwenye OIC.
tufikiri kwanza kabla ya kuleta UBAGUZI wetu kwa wenzetu
 
Mie nafikirir ni vizuri wananchi wote wakashirikishwa. Ifanyike referendum na si JK kum-push Membe kuleta hii hoja.
 
Mimi binafsi naona sehemu kulipo na mapungufu ktk sheria ni
pale mtoto anapopatikana kwa tendo la kujamiaana la siku moja, ama noa ya makubaliano ya masaa ama dakika na mtoto anapatikana.Lakini maeneo mengine serikali kama serikali ipo sahihi sana tena sana.

Tatizo hapa ni pale kundi fulani linapotaka mwelekeo wake na kanuni zake zitambulike na hukumu ya serikali iende ktk kanuni za kundi hilo kama serikali isipozitambua basi lazima kianzishwe chombo msambamba ktk katiba ya nchi .

Hii sawa kabisa na wakristu wakatoliki kuiibuka na kusema NDOA ni SAKRAMENTI na hivyo muumini ili atimeze IMANI yake lazima awe na SAKRAMENTI ya ndoa ama UTAWA, zikijumuika na SAKRAMENTI zingine mfano mpako wa wagonjwa ,kitubio n.k.

Na sakramenti ya NDOA ni MKE/MME mmoja Hivyo Wakaitaka SERIKALi kutambua yakwamba mkatoliki haruhusiwi KUOA mke mwingine na lazima iwe hivyo maana kufanya hivyo atakua hatimizi IMANI yake.Ama serikali inamapungufu ktk hukumu ya utimizo wa sakaramenti ya ndoa ktk Ukatoriki hivyo KAtoliki nayo itake kupeleka hoja hiyo ktk katiba yetu ili kuwepo na chombo ktk ukatoliki kitakachoshughurikia SAKRAMENTI Ya ndoa sambamba na mirathi maana SERIKALI haiwapi nafasi WAKATOLIKI kutimiza IMANI yao.
 
mimi nafikili MODS wafikirie kubadirisha Heading ya hii thread au mwenye nayo ajaribu ku-edit
 
Mkuu.

Pongezi kwako kwa hili.
Unajua mawazo ya kibaguzi huwa hayaletwe na mtu ila ni sisi wenyewe.Nyinyi wachangiaji wenzangu hapo juu,mngeweza hata kufanya uchambuzi tu kidogo wa hayo malalamiko yenu alafu ndio mlete hapa.

sasa ona hata Nigeria imo kwenye hii organisation,kama wafatiliaji wa mambo mnakumbuka Nigeria ndio BIAFRA ilipo,hiyo ndio hata ilimfanya Nyerer agombane na Amin lakini agalia hata wao leo wamo kwenye OIC.
tufikiri kwanza kabla ya kuleta UBAGUZI wetu kwa wenzetu

wewe unaijua ama ni historia tuu mkuu wangu??

waiislamu nigeria wana nguvu sana ,hukumbuki hata mwaka jana ama juzi walihukumu mwanamama kupigwa mawe hadi kufa baada ya kuzini bila ndoa??

Mpaka haki za binadamu walipoingia kati?? kuiweka kiti moto serikali ya nigeria acha bwana.

Nchi karibia zote hapo ktk list ni waislamuu tu kwenda mbele
 
Unachozidi kukosea ni pale unapotunga sababu kwa kufikiria tu kwamba labda hivi ndivyo ilivyokuwa...Lakini mimi bila kutazama rangi za watu nazungumzia reality na ndivyo ilivyokuwa..
Kwanza umesema ati East African Muslim Welfare Society (EAMWS) kilikuwa hakipendwi na waislaam kwa sababu kilikuwa chama cha wahindi badala ya Waswahili... mkuu hili umetoa wapi?... lini maswala ya dini yakaingiliana na rangi za watu.. hivi kweli unataka kunambia kuna kanisa hata moja ama shirika la dini ambalo limewahi kukataliwa kwa sababu ni la wazungu?.. hao hao wazungu, Waarabu na wahindi ndio waliotuletea dini ama ustaarabu wa imani hizi leo iweje mswahili asiyekuwa na dini wala elimu ya dini hiyo akatae mwongozo unaotaka kuieneza dini hiyo...

Nimeyatoa wapi? Nimeyatoa hapa:

The few Moslems who turned against the socialist politics were mostly of Asian origin. Some of the Moslem resistance was in the beginning channeled through the East African Muslim Welfare Society (EAMWS). It was founded in Mombasa in 1945 by the then Aga Khan with the aim of promoting Islam and raising the standard of living for the East African Moslems. Asian Shiites, especially Ismaili, dominated and financed the organisation, but Aga Khan recommended that all Moslems regard EAMWS as an organization with pan-Islamic ambitions.

Tafsiri yake:

The East African Muslim Welfare Society kilianzishwa Kenya kuendeleza maslahi ya waislam. Mmoja wa waanzilishi na financiers wake wakuu alikuwa Aga Khan, kiongozi wa wa Ismailia ( ambao wengi wenu hata hamuwakubali kuwa ni waislamu). Hiki chama kilionekana na baadhi yenu kuwa kinalinda maslahi ya wahindi na waarabu badala ya waswahili. Ukizingatia wakati ule wa mapambano ya kugombea uhuru wa Afrika , hii ilikuwa sababu tosha ya kukipiga marufuku.

Matatizo ni kuwa hautaki kuangalia upande wa pili wa argument. Udhaniavyo wewe unataka iwe hivyo. Ili ujenge hoja unaniwekea maneno kinywani mwangu. Nilichosema ni kuwa chama cha EAMS kilianzishwa Mombasa na mmoja wa waanzilishi wake na financier mkubwa alikuwa ni Aga Khan, kiongozi wa waismailia. Hapa nimekosea wapi? Ukisoma nilichokitoa kwenye mtandao, kinasema " waislamu wachache waliopinga siasa za ujamaa walikuwa wale wakutoka Asia ( waarabu na wahindi maana sidhani kulikuwa na wachina waislamu wakati huo). Sehemu ya upinzani huu (wa siasa ya ujamaa) ulipitishwa kwenye EAM............Chama hiki kilianzishwa Mombasa 1945..........Waislamu wa ki-asia wa dhehebu la Shia hasa waismailia ndiyo waliokuwa na nguvu na ndiyo waliokidhamini........Aga Khan alishauri kuwa waislamu wote wakione kuwa ni chama chao wote bila kujali madhehebu" mwisho wa kunukuu. Ukiendelea kusoma zaidi, mwandishi anasema:

Because of the pan-Islamic tendencies and the capitalist oriented leadership of EAMWS, pro-TANU Moslems opposed it. The organization, it was claimed, constituted a threat to the ruling party. The antagonism culminated in 1968, when the organization was declared illegal in Tanzania.

"Kutokana na mtazamo huu ( wa kujaribu kuunganisha waislamu wote) na kupinga siasa ya ujamaa, waislamu waliokuwa upande wa TANU walikipinga chama hiki na hii ilihatimaishwa na kufutwa kwake."

When its headquarters were moved from Mombasa to Daressalaam in 1961, the Nyamwezi chief and TANU opponent Abdallah Fundikira, regarded as Nyerere's principal political rival in the 60's, became the president of the organization. EAMWS concentrated on building schools and mosques, providing scholarships and spreading literature. There were also plans for founding an Islamic university in Zanzibar or Mombasa, but they were never realized. However, the Muslim Academy founded in Zanzibar in early 50s continued to exist as a training college for teachers of Arabic and Islamic education until it was closed down by the autonomous Revolutionary Government of Zanzibar in 1966.

Tafsiri: "Makao makuu ya chama hiki yalipohamishiwa Dar es Salaam kutoka Mombasa, Chifu wa wanyamwezi na mpinzani mkubwa wa Nyerere katika miaka ya sitini akawa rais wake. EAMWS kiliendelea kutilia mkazo kujenga shule na misikiti, kutoa skolaship na kusambaza vitabu..............ingawa mipango ya kujenga Chuo kikuu cha kiislamu Zanzibar haikufanikiwa, taasisi ya kiislamu iliyoanzishwa miaka ya 50 iliendelea kama chuo cha walimu wa kiarabu na elimu ya uislamu hadi hapo kilipofungwa mwaka 1966 na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar."

ukifuata mtiririko wa haya yote, kwangu mimi yafuatayo ni dhahiri:

1) EAMWS ilianzishwa na kufadhiliwa zaidi na waasia. Hawa wengi wao walikuwa ni wafanyabiashara kwa hiyo kwa wao siasa ya ujamaa haikuwavutia.

2)Kwa vile wafadhili wa EAMWS walikuwa waasia na kiongozi wake wa kwanza hapa kwetu alikuwa mpinzani wa Nyerere, chama hiki kilionekana kina agenda ya siasa na sio dini. Imani hii ilijengwa zaidi hasa walipoona kuwa inataka kuwaunganisha waislamu wote.

3)Mwandishi amesema wapinzani wake wakuu walikuwa waislamu waliokuwa TANU. Sidhani kama wa-asia wengi walikuwa wanachama wa TANU ndiyo maana nikasema "Hiki chama kilionekana na baadhi yenu kuwa kinalinda maslahi ya wahindi na waarabu badala ya waswahili". Wewe unasema:


Kwanza umesema ati East African Muslim Welfare Society (EAMWS) kilikuwa hakipendwi na waislaam kwa sababu kilikuwa chama cha wahindi badala ya Waswahili... mkuu hili umetoa wapi?... lini maswala ya dini yakaingiliana na rangi za watu.. hivi kweli unataka kunambia kuna kanisa hata moja ama shirika la dini ambalo limewahi kukataliwa kwa sababu ni la wazungu?.. hao hao wazungu, Waarabu na wahindi ndio waliotuletea dini ama ustaarabu wa imani hizi leo iweje mswahili asiyekuwa na dini wala elimu ya dini hiyo akatae mwongozo unaotaka kuieneza dini hiyo..

Wapi niliposema waislamu wa TANU ndiyo waislamu wote? Au kwa vile nilitumia neno "baadhi yenu"?. Utakuwa naive kusema kuwa maswala ya dini hayaingiliani na rangi! Wengi wa hao tunawatambua sasa kama wapigania ukombozi wetu hawakutofautisha kati ya wakoloni (wazungu) na ukrisu na bila shaka waarabu na uislamu. Walikataa kwa sababu walioleta hizi dini walitaka wakubali kuwa wao ni inferior na kwa hiyo ni haki yao kufanywa watumwa, watwana na wasio na ustaarabu. Walikuwa na imani zao na utamaduni wao ambao walikuwa tayari kuufia au kufungwa. Wakina Jomo Kenyatta na Mau Mau waliwapinga wakoloni kwa misingi hiyo hiyo. Ustaarabu gani ambao ulimfanya mtu mweusi kuwa mtumwa hadi miaka ya sabini na kwengine hadi leo? Ni ustaarabu gani ambao ulikataa mtu mweusi kuwa kiongozi wa dini (wa Mormon)hadi hivi karibuni? Ni mawazo kama haya ndiyo yaliyowafanya hao waislamu wa TANU kuwastukia wenzao! Kumbuka, tunazungumzia miaka ya sitini na bado watu walikuwa hawajasahau kuwa walifanywa watanwa na watumwa kutokana na rangi zao na hao hao waliowaletea hizi dini.

Ni wapi niliposema EAMWS kilipigwa marufuku kutokana na Abdallah Fundikira? Nilichokisema ni kuwa Aga Khan alikuwa mmoja wa waanzilishi na Abdallah Fundikira, mmoja wa wapinzani wakuu wa Nyerere kisiasa ndiye alikuwa Rais wake wa kwanza. Naam, nimewataja wote Fundikira na Mwinyi kwa vile ni waislamu na sidhani kama wangeshindwa kukirejesha chama hiki kama walngeona kuna umuhimu wa kufanya hivi.

Aga Khan hajawahi kufukuzwa Tanzania. Mali zake, kama za wengine, zilitaifishwa, pamoja na jengo la IPS. Usichanganye Kenya na Tanzania. Ni kwa sababu ya uwingi wa waislamu Tanzania ndiyo maana walikihofia chama cha EAMWS. Kenya hawawezi kukihofia maana wanajua wako wachache na hamna wanaloweza kufanya.

Unakana kuwa Aga Khan alikuwa mmoja wa waanzilishi lakini unakubali kuwa alikuwa sponsa? Are you serious?


Tatu, Upinzani wa kutaifishwa mali haukutokana na chama cha kiislaam hata kidogo unless unataka kusema hata kina Kambona pia walikuwa waislaam halafu basi tazam report inavyojigonganisha yenyewe.. Ikiwa waislaam ndio walikuwa na upinzani mkubwa wa utaifishaji badala ya wahindi na waarabu iweje tena hao hao waislaam wafurahie kutaifishwa kwa shule za wakristu?.. Mkuu mara nyingi habari kama hizi soma between the lines...

Unataka kusema kuwa waislamu WOTE walifurahia siasa ya ujamaa? Bibi Titi alikuwa mkristu? Utawatenganishaje waarabu na wahindi na waislamu? Au unataka kuniambia hakuna waislamu wahindi na waarabu? Aga Khan ni kabila gani na ni dini gani? Mabohora nao ni dini gani? Hawa nao walifurahia utaifishwaji wa mali?

yet hao hao wazungu na wakristu ama dini nyinginezo walipokuwa wakipigania Uhuru wao iwe Marekani, France, Uingereza wote hawa walitumia maneno hayo hayo..Kwanza walikamata makanisa wakachukua imani za watu na kuwatumia kupigana vita yao.. hakuna Mfalme hata mmoja hakuwa na uhusiano wa juu na kanisa ktk kila maamuzi na neno la Mungu lilikuwa ndio hamasisho la ushindi wote wa vita wa chi zote za Ulaya...Leo mwarabu ati kwa sababu tu anasema Kiarabu kwa maandishi ya kiarabu kuwa Mungu ni mkubwa - Allah Akbar basi bila shaka wanatumia Uislaam kueneza chuki..sijui mwarabu mkristu atasemaje tofauti na mwarabu muislaam anapofikia mahala pa kusema Mungu ni mkubwa..

Hapa unataka kusema nini? Wafalme gani unaowazungumzia? Wafalme wakiingereza dhidi ya warumi? Wamarekani dhidi ya waingereza? Wafaransa dhidi ya wajerumani? Ya mwarabu imeingia vipi humu?

Hizi ndizo propaganda nazozipiga vita. propaganda ambazo zinatugawa sisi kwa rangi zetu badala ya kutazama kitu kilichopo mbele yetu. na kama umeisoma vizuri hiyo makala uliyoiweka hapo nyuma utaona yapo madhara makubwa ya korti ya kadhi kama nilivyoisema huko nyuma kuwa cha muhimu ni kuzingatia WATU na MAZINGIRA waliyopo..period
Kuna kipande hiki hapa nimekipenda sana na ndivyo nilivyosema toka awali kwa sababu mkuu mimi huwa sisahau yaliyopita.

Yote hayo unayoyapinga nimeyatoa humo. Soma, uelewe.

Umezungumza mengi lakini haukunijibu. Tukubali kutofautiana .
 
wewe unaijua ama ni historia tuu mkuu wangu??

waiislamu nigeria wana nguvu sana ,hukumbuki hata mwaka jana ama juzi walihukumu mwanamama kupigwa mawe hadi kufa baada ya kuzini bila ndoa??

Mpaka haki za binadamu walipoingia kati?? kuiweka kiti moto serikali ya nigeria acha bwana.

Nchi karibia zote hapo ktk list ni waislamuu tu kwenda mbele


Heshima mbele mkuu,

Sawa nakubari,kumbuka kwamba Nigeria hiyo hiyo on the late 70's kulikua na CHRISTIANITY STATE maarufa kama BIAFRA mpaka leo lipo kama jimbo.

Ambayo Tanzania iliitambua uwepo wake ilipotaka kujitenga kutoka serikali kuu sijuu upo hapo
 
Darwin kama jina langu

Pale Zanzibar ilipotaka kujiunga kwenye hii jumuia mbona Tanganyika walitaka hata kuvunja muungano na kuinyooshea kidole.
Haya sasa kumetokea nini mpaka sasa Tanganyika yenye wakiristo na sie kina Darwin kujiunga na hio jumuia?

Hii ndio inayoonyesha dhahiri kwamba wazanzibari hawawezi kuamua mambo yao wenyewe wanayoona yataifaa jamii ya waunguja na wapemba
 
...........nimeangalia hiyo link kumbe zanzibar ..si tu kuwa ilijaribu bali ilijiunga kabisa..na someni maelezo waliyopeleka huko yanakatisha tamaa..

hizo uganda ilijiunga na OIC wakati wa IDDI amin DADA ambaye inajulikana dhahiri alitaka kuifanya uganda ISLAMIC REP.....NA moja ya strategy ya kwanza aliyoanza nayo ilikuwa OIC...mnajua kila kitu huanza kwa kuingiza kichwa....then unazama..."hata ngamia ukimruhusu aingize kichwa utamuona analazimisha kuingiza mwili mzima ..japo asilani hautaingia....."
 
...msumbiji waliingia kipindi kile baada ya kutoka kwenye vita ..kwa hali ya uchumi waliyokuwa nayo walikubali ofa yeyote ambayo ingekuwa na masilahi kwao....lakini ni uganda na msumbiji tu ..ambazo sababu zilikuwa za udini wa amin na masilahi..kwa msumbiji.......kumbukeni juhudi za msumbiji kusaka maslahi baada ya vita ndefu zilifanya waombe pia uanachama wa COMMONWEALTH
 
Hata watu wa Uganda na Msumbiji!!?

watanzania hatuendelei kutokana na mawazo tegemezi.

watu tunapenda sana kufanya mambo kwa kufuata mkumbo eti fulani mbona kipo ama kafanya hivi.

Angalia na jenga hoja kulingana na mazingira yako sio kuangalia nani kivipi?

Mfano hatuwezi kufuata mfano URA wa uganda sisi tanzania kujitafutia demokrasia.

Kila kitu kinategemea mazingira ,
ndio maana wahenga wakasema ukiiga kwa tembo kunya kinyesi kikubwa utapasuka matako.
 
watanzania hatuendelei kutokana na mawazo tegemezi.

watu tunapenda sana kufanya mambo kwa kufuata mkumbo eti fulani mbona kipo ama kafanya hivi.

Angalia na jenga hoja kulingana na mazingira yako sio kuangalia nani kivipi?

Mfano hatuwezi kufuata mfano URA wa uganda sisi tanzania kujitafutia demokrasia.

Kila kitu kinategemea mazingira ,
ndio maana wahenga wakasema ukiiga kwa tembo kunya kinyesi kikubwa utapasuka matako.

Hasa kilichokushangaza kwenye hilo swali ninini?

Mimi nimeshangaa halafu waniletea sijui kavaa chupi sijui kavua.

Kwanza hebu angalia jina langu ndio utajua msimamo wangu kwamba siko kwenye mambo yenu ya uislamuu na ukiristuuu
 
Back
Top Bottom