Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Plan B ifanyiwe kazi kwanza.
Ruksa kwa waislamu kuunda Mahakama chini ya Imani yao lakini isiwe idara ya serikali ya JMT.
Hapa sielewi; Tatizo ni mshahara na malupulupu toka serikalini au ni nini??
 
Eeeeeeee!!!!!

Mod, pls, pls pls X .......


Naomba uiondoe hii mada hapa kwani inakoelekea kutakuwa hakutoshi. Kila mtu ana IMANI yake na linapokuja suala la IMANI ni rahisi sana kubaguana.

MIMI kwa asilimia ZOTE nawasapoti wale wa SIDE A. na nina HOJA zangu nyingi tu, sifikirii kusema hoja za upande fulani kuwa hazina mantiki ndio kuhalalisha kuwa za kwako ziko sawa na zina logic.

Ondoa hiii mada pls. Ama ihamishie sehemu za DINI kule. Tukajadiliane kwa kina na kila mtu atoe hoja zake.
 
Hapo nipo SIDE B na mimi.
Point hii siielewi kabisa
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

Kuwa na ubalozi ni sawa na kuwa na mahakama?
 
Nipo side B
Kimsingi sipingi kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi ila ninachopinga ni kwamba tayari suala lenyewe linapingana na katiba ya JMT.
Katiba imeshasema nchi haina dini, ukiingiza tena suala la imani ya dini,kila mtu atataka atambulike.
Mizozo ya imani ikiibuka huwa ni kama petrol ishikavyo moto na haiishi mapema(Rejeeni mwaka jana yalivyoanza yale malumbano Novemba 2007 hadi dola ikaingilia kuzuia kwa kusema serikali inalishughulikia na majibu kutolewa february 2008,lakini hayakutoka).

Masuala ya imani ikiwa ndiyo ni ndiyo na ikiwa siyo ni siyo sasa yakiingizwa tena katika katiba itakuwa balaa kweli.
 
Last edited:
Mimi sioni ubaya kukiwa na taasis au mfumo wa kuendeleza ibada..swala ninaloliona linaleta utata ni bajeti.. Mahakama y akadhi ikihuishwa kwenye mfumo wa serikali maana yake itabidi serikali iwajibike kwa kila namna. Je walipa kodi wasio wa dini husika kwanini wachangie? Mahakama hizo zinapaswa kujitegemea bila kutumia pesa za serikali.
 
Yani Kuna watu wanafiki...Dunia ya sasa Unaweza ukadhani una akili kumbe pumba tupu!!
Hakuna mota wowote ulio waka!! kama hata Zitto Kabwe nae Leo alionekana ana Busara!! basi sio tatizo sana!!!

Wabunge mana tu let down!!
 
Hapo nipo SIDE B na mimi.
Point hii siielewi kabisa
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.

Kuwa na ubalozi ni sawa na kuwa na mahakama?

Mtu mwingine atakuja pia aseme tuvumiliane maana kuna balozi yetu IRAN na mahusiano ya karibu ya kidepromasia na PALESTINA.
 
Eeeeeeee!!!!!

Mod, pls, pls pls X .......


Naomba uiondoe hii mada hapa kwani inakoelekea kutakuwa hakutoshi. Kila mtu ana IMANI yake na linapokuja suala la IMANI ni rahisi sana kubaguana.

MIMI kwa asilimia ZOTE nawasapoti wale wa SIDE A. na nina HOJA zangu nyingi tu, sifikirii kusema hoja za upande fulani kuwa hazina mantiki ndio kuhalalisha kuwa za kwako ziko sawa na zina logic.

Ondoa hiii mada pls. Ama ihamishie sehemu za DINI kule. Tukajadiliane kwa kina na kila mtu atoe hoja zake.

Mkuu
ningependa kukuliza swala moja nategemea utanijibu sawa sawa si kimutazamo wa dini.
Swali zinakuja.
Imekua je ukatambua kitu kidogo kama hiki yani thread hii iko ktk sehemu ya DINI ,ukaacha kuona kabisa swala la KADHI ambalo ni DINI asilia lijadiliwe bungeni na wana SIASA.?

Je KADHI ni suala la Kisiasa?

Je Kadhi ni suala la KIDINI?

Je kundi fulani likitaka kujenga Msikiti ni lazima lipelekewe mswaada kwa wanasiasa BUNGENI?
Je kundi likitaka kujenga kanisa ama hekalu ni lazima lifowardiwe kama mswaada bungeni?

Je Kadhi na Miskiti ni lipi kati yao lilo mhimu zaidi ktk imani ya uislamu?
 
kadhi????...........hukumu Zitakuwa Antagonistic Na Current Legal System....

Issue Ya Kenya Ni Tofauti ...uchache Wa Waislamu Pale Pia Unafanya ...hii Mahakama Isiwe Na Umuhimu Mkubwa ..tofauti Na Hapa Ambapo Waislami Ni Zaidi Ya Asilimia 35%.....na Kuna Wengine Wengi Tu Wanaabudu Dini Za Asili.....

..kuna Nchi Kama Turkey Zina Waislamu Asilimia 99% Yet Zipo Circular...what Are They Loosing?...afteral Sheria Zetu Hazimuonei Mtu...

Hii Italeta Migogoro Ya Bure ..tumeshuhudia Waislamu Hapa Wakigombana ...na Kupindua Masheikh Wa Mikoa ...kupindua Misikiti..kushindwa ..bakwata Ina Kuwa Mismanaged..yet Wanashindwa Kuunda Chombo Tofauti..ambacho Watakitii Kama Bakwata Hawaitaki.je Tunataka Waanze Vita Za Kugombea Ukadhi....?...au Kukataa Hukumu Zao?....kama Hata Redio Yao Wameshindwa Kuiendesha Kutokana Na Tofauti....je Nani Atawalipa Makadhi Mshahara.....

Iwapo Waislamu Wapo Tayari Kusimamia ,kuiendesha Na Kugharamia Ofisi Ya Kadhi Na Wakidhibitisha Hilo..kama Haitagharamiwa Na Kodi Zetu Basi ..na Haitaingiliana Na Sheria Zilizopo Au Kuwaadhibu Wasio Waislamu.....tuwaunge Mkono....
 
..ISSUE YA VATICAN WATU WASIICHUKULIE KWA CHUKI ZA KIDIDI....KWANI VATICAN NI NCHI ....NA NI MWANACHAMA WA UMOJA WA MATAIFA....INA SIFA ZOTE ZA TAIFA....INA HAKI YA KUWA NA MABALOZI SEHEMU YEYOTE DUNIANI ...HATA KAMA ASILIMI 99.999% YA WANANCHI/WAKAZI WA VATICAN NI WAKIRISTO WAKIKATOLIKI.....PIA KUNA NCHI KAMA PALESTINA .IRAN ,IRAQ....ets AMABAZO ASLIMIA 99% NI WAISLAMU...NA WANAO WAWAKILISHI HAPA...............VATICAN NI TAIFA KAMA TAIFA LINGINE LOLOTE......NDIO MAANA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA AKIITISHA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI.....VATICAN HUHUDHURIA CHINI YA PAPA.....
 
Big up Side B.
Hoja zenu zimekaa sawa.

WaTangayika lazima tuwe makini kwenye issue kama hizi.Ukweli ni kwamba waislamu wanaotaka hiyo mahakama kuna kitu wanataka ndani ya nchi ya Tanzania.

Mkubukeni yule president alietaka kuifanya Tanzania iwe The United Islamic Rep.Of Tz,wajanja tukamshtukiaa.
 
Last edited:
Sasa tatizo lipo wapi,naona kama Waislamu kuna mambo ambayo ni lazima yafuatwe na ili kuwakata makali wale wakaidi wanaokimbilia katika mahakama za serikali ili kukimbia mikono ya sheria za dini na haswa katika mambo ya kurithiana na kuowana ,talaka na engage inafaa kabisa kuwepo na mrengo ambao waislamu kwa baadhi ya mambo wangeweza kuruhusiwa kuyapeleka ndani ya mkondo wa sheria za dini yao,aidha kama itakuwa ngumu,labda kwa sababu binafsi za upande unaopinga,basi kungelianzishwa kitengo ambacho kingeruhusu kesi au madai yanayohusiana na waislamu yasikilizwe kwenye njia za Kiislamu ,na hii itapelekea zile kesi zinazozama zaidi katika mambo ya kiislamu ,mbona mabenki mengi siku hizi yanafuata muundo wa islamic bank tena huko huko maulaya kwenye wakirstu watupu walio wengi na hata wakiristo wamekuwa na afueni katika kukopa benki kwa kupitia njia hizo.Ni maamuzi tu na ubinadamu wa kuona wenzetu hawa jambo hili kwao ni muhimu.Na ndio watu wanavyoishi kindugu na mapenzi yanavyozidi baina yetu ,lakini sio kuekeana vigingi,maana kama walivyosema kuna uitalia kuna ukatoliki yote haya ni mariziano ya wananchi wenyewe kwani ukiangalia mambo hayo hayatakiwi kuwepo.Sasa ukianza kuona upande mmoja unalotaka kulifanya silo basi na wao watakuja juu na kukwambia basi na hili liondolewe.
 
Wadugu mnamkumbuka yule president alietaka kuifanya Tanzania iwe The United Islamic Rep.Of Tz,wajanja wakamshtukiaa???
 
Mwiba
Hapa mimi binafsi ninavyoona si kwamba watu wanapinga kadhi ila wanahoji iweje ipitishwe kwenye katiba ya nchi?

sawa ikikubalika kupita na je wapagani nao wakiomba mahakama yao ipitishwe na serikali itakubalika??

Je ? wakija wa kristu naao wakaomba mahakama yao itakubalika?? kwanini ilazimishwe kwenye katiba ya nchi?

Mimi nadhani kadhi ikianzishwa kama ilivyo BAKWATA ni vyema zaidi maana itakua taasisi ndani ya uislamu,yani ya kwamba kama waislamu wakishitakiana ktk mahakama za kawaida wote kwa pamoja wakaomba kesi yao ihamishiwe kwenye taasisi ya KADHI na iwe hivyo na si katiba.

DINI ni imani na hiari na si SHERIA yani KADHI ikipitishwa na BUNGE ktk katiba mimi naona kama inageuka kua kama sheria si hiari tena yani inakua lazima kitu kilicho na defination ktk hiyo Kadhi lazima kitimilike.

Mfano tuseme ustadhi fulani kaachana na mkewe na KADHI inahukumu tuseme mali zigawiwe nusu watoto ,robo baba na robo mama ,lakini huyu ustadhi akakataa kufuata hukumu hiyo je ? atafanyiwa nini zaidi.Je Kadhi itamhukumu jela? Je kadhi itamhukumu kupigwa mawe .je kadhi itaingia kumchukua vitu hivyo kwa nguvu?

Na mfano mwingine kama ustadhi mwingine akifanya kosa akakataa kwenda ktk mahakam ya kadhi na akaenda ya public kadhi itamfanyia nini?je itatuma polisi kwenda kumtia korokoroni? na Kama haitafanya hivyo kwanini ipitishwe kimsingi ya sheria badala ya hiari?

Mimi nafkiri Kadhi wanataka kuipitisha kikatiba ili kuiapa msumeno .Yani mfano ieleweke ni mfano kua kama ktk mahakama ya kadhi kunakipengele kinasema ni mwiko mtoto wa kiislamu kuolewa na mkristu ikitokea akaolewa ,hukumu ya msichana huyu ni kupigwa mawe hadi kufa.Sasa kama kadhi ikiwa inatamburika kisheria inamaana huyu binti itampasa atakeleze adhabu.
 
nadhani tusizunguke nje ya ulingo yapo masuala ya kitaratibu za imani mbali mbali

nasema waislamu wana miongozo yao kwa nini mahakama yao ya kadhi isiwe ndani ya dini yao je lazima iwe ni sheria ya katiba kama siyo ina uonevu fulani na je mahakama zatu zinatambua sheria mbali mbali za kiisilamu kama zinatumika watupe taarifa ya kuwa je zimeenda wapi kinyume na matakwa yao

na je mahakama ya kadhi kadhi huyo huteuliwa na nani na gharama za kuendesha mahakama hii zitalipwa kwa kodi za watanzania wote ama ni kwa utaratibu wa waislamu kuiendesha je kama hivyo ndivyo kuna haja gani ya bunge kupitisha mswada wa kuendesha mahakama ya kadhi ??? kwanini nini waisilamu wasitengeneze umuhimu wa kuweka utaratibu katika uendeshaji wa shughuli zao za imani ama je kwani siasa ina husika vipi na imani yao
 
mbona Kanisa Katoliki lina Mahakama zake na hakuna anayegomba tena wao hadi kukata rufaa ni Vatikani kwenyewe?
 
Yani Kuna watu wanafiki...Dunia ya sasa Unaweza ukadhani una akili kumbe pumba tupu!!
Hakuna mota wowote ulio waka!! kama hata Zitto Kabwe nae Leo alionekana ana Busara!! basi sio tatizo sana!!!

Wabunge mana tu let down!!

Zitto leo bwana alikuwa anatafuta umaarufu tu wa kwamba na yeye alichangia. Point yake pekee ilikuwa ni kidokezo cha utafiti wa REDET kuwa katika kila watanzania 10 ni wawili tu wanaoaminiana. Basi. After that akaanza kutoa hotuba badala ya hoja kama vile kuhimiza umoja, kwamba watu waache kugwanyika kwa misingi ya dini, etc) ili kujaza time slot.
 
mbona Kanisa Katoliki lina Mahakama zake na hakuna anayegomba tena wao hadi kukata rufaa ni Vatikani kwenyewe?
Wewe sasa mchokozi!
Hizi mahakama zinatambuliwa na sheria za nchini mwetu? Ziko katika katiba ya nchi? Au ni kwa ajili ya wakatoliki na asiyetaka kuzitumia (hata kama ni mkatoliki) halazimishwi?
 
Wewe sasa mchokozi!
Hizi mahakama zinatambuliwa na sheria za nchini mwetu? Ziko katika katiba ya nchi? Au ni kwa ajili ya wakatoliki na asiyetaka kuzitumia (hata kama ni mkatoliki) halazimishwi?

siyo uchokozi nina maana mbili:

a. Kwanza mahakama za kidini zinawezekana tanzania kwani tayari zipo (kwa wakatoliki na hata waanglikana wanazo)

b. Pili hazihitaji baraka ya serikali kwani haziko katika mfumo wa utoaji haki wa serikali. NI sehemu ya dini.

sasa hapa uchokozi ni upi?
 
Back
Top Bottom