Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kwa kuanza naomba niwaulize JE TANZANIA INAFUATA DINI GANI?
Kuhuliza huko kunatokana na hii hoja ya MAHAKAMA YA KADHI!!.Hoja hii kwa mara ya kwanza ilianzishwa na ndugu yetu Mrema akiawa mbunge wa temeke kwa chama cha NCCR,ikaishia hewani hewani. Mara ya pili ikazushwa tena na mbunge mwingine anaetokea mkoa huo huo wa ndugu Mrema akiwa mbunge kwa chama cha TLP ambacho mwenyekiti wake ni ndugu A.L.Mrema!!.

Ni jambo la kushangaza kwani hawa wote ni wakristu na hoja hiyohiyo ilikuwa inatolewa na mtu mmoja tu! huyu Ndesamburo ametumwa tu lakini mmiliki wa hoja hiyo ni Mrema.Kwa hili nadhani alikuwa anatafuta umaharufu wa kisiasa kwa Waislam bila kujua impact yake (kipindi kile shule ilikuwa ndogo kwake).Kwa ufahamu wangu mimi mahakama zote za hajabu hajabu zilifutwa mwaka 1963 na Mheshiwa waziri Chifu Abdalha Fundikira (TENA HUYU NI MUHISLAM SWAAAFI).Sasa ndugu yetu Mrema baada ya kuona umaharufu umeshuka akataka kuunyanyua kwa kuwapitia waislam.Jamani nchi yetu haiongozwi na sharia.Nashukuru kwa sasa baada ya kujua hana mvuto tena kwa wabongo ameamua kukaa kimya!.

Nayo serikali ya JK baada ya kuona imepoteza mvuto wake (labda uzuri wa sura ndiyo umezidi!!)inafufua tena hoja hiyo ili kuwawini waislam! sasa leo tunakuwa na mahakama ya waislam,kesho wakristu nao wanadai mahakama yao, keshokutwa wahindu nao watadai na madhehebu mengineo tuliyonayo hapa nchini pia yatadai. Je tunaelekea wapi?

Serikali ya JK na wabunge wake wanaolipwa pesa nyingi kwa kodi zetu (mpaka mungu hapendi!) badala ya kukaa na kujadili jinsi ya kuwaondolea au kuwapunguzia Watanzania ukali wa maisha wanaanza kuzungumzia shari. Nasema SHARI kwa sababu kwenye hali ya AMANI hakuna mtu anyefikiria kwenda mahakamani! Kwa jinsi wanavyolivalia njuga namuunga mkono Mh. Bush na Mchungaji Mtikila.

Tunataka kuongeza mimahakama tuu badala ya kujadili maendeleo.Ndugu zangu labda niwaulizwe maswali haya:
1.Je muislam akigombana na mhumini wa dini nyingine kesi hiyo itapelekwa mahakama gani?
2.Hukumu za sharia ni za kikatili, je wezi watakatwa mikono? au wagoni watapondwa na mawe?

Hayo mojawapo ya maswali ya kujiuliza je hii mahakama itakuwaje? tumekaa kwa amani lakini hawa warafi wa siasa wanataka kutupeleka pabaya.

Hayo ni mawazo yangu juu ya hoja hiyo! kama limekuuma utajiju!!!
 
mzee kuingia na vitimbi haisaidii.. jenga hoja iache isimame.. mambo ya "utajiju".. ni mambo yaliyopitwa na wakati.
 
Tanzania inafuata dini, dini haitakiwi kuhusisha serikali ni wananchi na makanisa au misikiti yao. Tanzania ikianza kufanya hizi mahakama basi katiba haina maana tufuate dini kwenye kila kitu na sio mahakama tu.
 
Kwa kuanza naomba niwaulize JE TANZANIA INAFUATA DINI GANI?
Kuhuliza huko kunatokana na hii hoja ya MAHAKAMA YA KADHI!!.Hoja hii kwa mara ya kwanza ilianzishwa na ndugu yetu Mrema akiawa mbunge wa temeke kwa chama cha NCCR,ikaishia hewani hewani. Mara ya pili ikazushwa tena na mbunge mwingine anaetokea mkoa huo huo wa ndugu Mrema akiwa mbunge kwa chama cha TLP ambacho mwenyekiti wake ni ndugu A.L.Mrema!!.

Ni jambo la kushangaza kwani hawa wote ni wakristu na hoja hiyohiyo ilikuwa inatolewa na mtu mmoja tu! huyu Ndesamburo ametumwa tu lakini mmiliki wa hoja hiyo ni Mrema.Kwa hili nadhani alikuwa anatafuta umaharufu wa kisiasa kwa Waislam bila kujua impact yake (kipindi kile shule ilikuwa ndogo kwake).Kwa ufahamu wangu mimi mahakama zote za hajabu hajabu zilifutwa mwaka 1963 na Mheshiwa waziri Chifu Abdalha Fundikira (TENA HUYU NI MUHISLAM SWAAAFI).Sasa ndugu yetu Mrema baada ya kuona umaharufu umeshuka akataka kuunyanyua kwa kuwapitia waislam.Jamani nchi yetu haiongozwi na sharia.Nashukuru kwa sasa baada ya kujua hana mvuto tena kwa wabongo ameamua kukaa kimya!.

Nayo serikali ya JK baada ya kuona imepoteza mvuto wake (labda uzuri wa sura ndiyo umezidi!!)inafufua tena hoja hiyo ili kuwawini waislam! sasa leo tunakuwa na mahakama ya waislam,kesho wakristu nao wanadai mahakama yao, keshokutwa wahindu nao watadai na madhehebu mengineo tuliyonayo hapa nchini pia yatadai. Je tunaelekea wapi?

Serikali ya JK na wabunge wake wanaolipwa pesa nyingi kwa kodi zetu (mpaka mungu hapendi!) badala ya kukaa na kujadili jinsi ya kuwaondolea au kuwapunguzia Watanzania ukali wa maisha wanaanza kuzungumzia shari. Nasema SHARI kwa sababu kwenye hali ya AMANI hakuna mtu anyefikiria kwenda mahakamani! Kwa jinsi wanavyolivalia njuga namuunga mkono Mh. Bush na Mchungaji Mtikila.

Tunataka kuongeza mimahakama tuu badala ya kujadili maendeleo.Ndugu zangu labda niwaulizwe maswali haya:
1.Je muislam akigombana na mhumini wa dini nyingine kesi hiyo itapelekwa mahakama gani?
2.Hukumu za sharia ni za kikatili, je wezi watakatwa mikono? au wagoni watapondwa na mawe?

Hayo mojawapo ya maswali ya kujiuliza je hii mahakama itakuwaje? tumekaa kwa amani lakini hawa warafi wa siasa wanataka kutupeleka pabaya.

Hayo ni mawazo yangu juu ya hoja hiyo! kama limekuuma utajiju!!!

Kwanini kuna tatizo gani iwapo Mwizi kama JK, EL watakatwa mikono? Watu kama hao wanaoibia Taifa pesa hawafai kuwapeleka jela kwa sababu wanaliongezea taifa hasara.

Pili katika nchi nyingi kuna mahakama za kutafuta usuruhishi (Court of Arbitration). Mahakama hizi zinatafuta ufumbuzi pale pande zinazotofautiana kukubali maamuzi ya mahakama hizo na vile vile kuwa tayari kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hizo. Na kama hawakubaliani basi wanakwenda kwenye mahakama ya kiserikali. Mahakama hizi hazijishughulishi na makosa ya JINAI.

Kwa nchi kama Tanzania ambayo bado kuna watu wanaoa na kurithi kwa kutumi mila zao au imani za kidini sioni sababu ya kutokuwepo kwa Court of Arbitration. Tena zinatakiwa ziwe nyingi tu. Wasukuma wanaotaka msukuma mwenzao atoe maamuzi kuhusiana mila zao waende kwenye mahakama yao iwapo pande zinazohusika zitakubali uhamuzi wa mahakama yao.

Tena zisiishie kwenye mila au dini ziende mpaka kwenye michezo. Simba na Yanga watatue matatizo yao kwenye mahakama hizi na sio kupotezea muda mahakama za kiserikali.

Wakatoliki wanaoamini kuwa ndoa haiwezikutenganisha, wanaweza kuwa na mahakama yao pia. Nchi lazima iwe na flavor.
 
Kwa mujibu wa shirika la utangazaji Tanzania (TBC) kwenye taarifa ya habari RTD saa mbili usiku huu, JK amelizungumzia suala hilo kwenye sherehe ya kumsimika askofu mkuu wa KKKT DR Mwalasusa

Nimeweza ku'comprehend' yafuatayo

-kwamba suala hilo limesababisha kuwepo kwa dalili za kuvunjika kwa upendo na mshikamano baina ya wakristo na waislamu
-kwamba mwanzilishi wa hilo suala sio yeye bali aliyekuwa mbunge wa Temeke, Mh. Agustine Mrema kupitia bunge
-kwamba suala hilo sio lake yeye binafsi kwa vile halijaanza kipindi chake
-kwamba tume iliyoundwa itamaliza kazi yake februari mwakani kwa hiyo wananchi wawe na subira
-kwamba serikali haitaamua kinyemela kuhusu suala hilo na kwamba maslahi ya pande zote zinazohusika yatazingatiwa.

Then nadhani kuanzia hapa tunaweza kuwa na mahali pa kuanzia....nadhani pia magazeti yatakuwa na a detailed report on this....
 
Nakulilia Tanzania,
Shukrani sana mkuu, tena umejnga hoja safi... safi sana kwa maelezo mafupi na wazi.

haya sasa mbona ukweli unaonyesha wazi kuwa hizi ni mbinu chafu za kutaka kugombanisha watu!... Taarifa ndogo hapo juu imedhihirisha tofauti kabisa na jinsi Mtikila alivyoijengea hoja...Hoja ambayo imezua kipengele cha kwanza hapo juu..kwamba suala hilo limesababisha kuwepo kwa dalili za kuvunjika kwa upendo na mshikamano baina ya wakristo na waislamu.

Je, kuna haja ya kumwita aliyewakilisha muswada huu ndugu Mheshimiwa Mrema - Gaidi?
 
mwenye habari,hivi mrema alisema nini kuhusu suala la kadhi.mie napatwa na hasira kama kuna watu wa type ya mrema wanaotaka kuharibu katiba ya nchi yetu..mie najua kesho MREMA atajibu tuhuma hizi..
mie siungi mkono mahakama ya kadhi
 
Mkuu ukombozi, to the best of my knowledge nadhani pia mrema wakati akitaka umaarufu na hasa kutoka Temeke kipindi hicho ndo aliibuka kweli na hoja hiyo...na to be honest hiyo hpja ilifufuliwa na mrema miaka hiyo ya tisini, kilichotokea kama 'kosa' ni CCM kuiingiza kwenye ilani yake mwaka 2005 na hapo ndipo waislamu wana ushahidi ama niseme baseline ya madai yao kwa sasa...
 
Nakulilia Tanzania,
Shukrani sana mkuu, tena umejnga hoja safi... safi sana kwa maelezo mafupi na wazi.

haya sasa mbona ukweli unaonyesha wazi kuwa hizi ni mbinu chafu za kutaka kugombanisha watu!... Taarifa ndogo hapo juu imedhihirisha tofauti kabisa na jinsi Mtikila alivyoijengea hoja...Hoja ambayo imezua kipengele cha kwanza hapo juu..kwamba suala hilo limesababisha kuwepo kwa dalili za kuvunjika kwa upendo na mshikamano baina ya wakristo na waislamu.

Je, kuna haja ya kumwita aliyewakilisha muswada huu ndugu Mheshimiwa Mrema - Gaidi?

Mkuu Mkandara, heshima mbele, mi kwa maoni yangu hili neno 'ugaidi' ni just another catchy 'phrase' mkuu, watu wanachagua maneno kudraw attention, vile kipindi cha mrema hilo neno halikuwa maarufu kiasi lilivo sasa hadi kwua na ssheria inayojitegemea. Kwa hiyo mrema kuwa au kutokuwa gaidi itategemea kama tutaangalia mambo in a retrospective way, lakini nadhani Mrema binafsi ana hoja ya kujibu kwenye hili in the light of the current constitution ambayo inasema wazi serikali haina dini....
 
Mahakama ya Kadhi, tatizo ni elimu kwa wananchi wetu! mpaka sasa hivi pande zote zina hoja! ingawa niliyoiona inawakera wakristo ni ugharimiaji wa mahakama hiyo kutoka bajeti ya serikali kuu na sio waislamu wenyewe. hoja ya waislamu ni kwamba hiyo itakuwa sehemu ya judiciary services ambazo gharama zote hadi leo zinagharimiwa na system iliyoko leo ya judiciary.
Kumbukeni kwamba sehemu kubwa ya mahakama hii ni kwa mambo ya ndoa zaidi. na hayana athari yoyote kwa madhehebu nyingine na hata waislamu wengine wanaweza kuamua kutoitumia hiyo mahakama kama ilivyo sasa munafunga ndoa bomani.
 
Hii hoja haina msingi, Mrema siyo mtawala, na hana Ilani ya uchaguzi ya kufanya jambo hilo. Ni aibu kwa Rais kudai lawama zimuendee Mrema wakati chama chake ndio kilichoidaka hoja hiyo tangu wakati wa Mkapa na ni wao walioiweka kwenye Ilani yao siyo Mrema aliyewawekea. Hoja ya Mahakama ya Kadhi imekuwepo kwa muda mrefu, Mrema ni kiongozi wa kwanza aliyeiweka hadharani (badala ya watu kunung'unika chini kwa chini).

Kama CCM wanaona hoja hii ni ya "mrema" basi waiondoe kwenye Ilani yao na kuwaomba radhi watanzania kuwa waliingiza hoja ya Mpinzani kwenye Ilani yao na ya kwamba hoja hiyo haitekelezeki, na hiyo angalau itakuwa ni ahadi ya kwanza ya CCM ambayo hawataweza kuitekeleza rasmi. Na kutoka hapo basi tutasonga mbele. Serikali yetu haina tabia ya kukubali makosa hata kama yanawakodolea usoni!
 
NakuliliaTanzania,
Heshima mbele mkuu mbona unanipiga chenga kwa mbali?... swala hili tunalizungumza leo hii na mhusika ni Mrema inakuwaje leo yeye asiwe gaidi isipokuwa JK ama huyo gaidi ni lazima awe Muislaam.

Unajua wazi kuwa neno hili ni mhuri unaotumika kwa waislaam wenyesiasa kali tena wenye malengo ya kuua kwa sababu ya dini, haliwezi kuwa phrase tu kama vile ni neno dogo la mtaani. Kisha basi toka Mtikila amesema alosema umeona mwenyewe hasira za wakristu humu kiasi kwamba wameshindwa kufikiria ama kujiuliza umuhimu wa hiyo korti na kui discredit badala yake wamejenga hoja zzinazotokana na imani ya Mtikila. besides it's not true ni uzushi kuwa JK amekubali ama kupitisha korti hizi zifunguliwe.

Mbona kuna korti za wazee wetu za kiasili, na hata wajumbe wa nyumba kumi ambao maamuzi yao hutambulika kisheria..who granted the the right of doing so!.

Binafsi, kama hatutaki korti za kadhi basi ni lazima tuweke sheria kikatiba itakayoweza kuwalinda watoto na wanawake wa kiislaam sio kuacha slam dunk suhindi kwa wanaume wa kiislaam ambao hawafuati taratibu za dini wala serikali.

Hivi nikuulize wewe mtoto alozaliwa nje ya ndoa anaponyimwa haki yake ya mirathi tunatumia sheria gani hivi sasa!..

Sheria inasema nini kuhusu wake zaidi ya mmoja. Maanake ktk ukristu naweza sema mke atachukua half lakini kumbuka ktk Uislaam bado kuna wake wengine wako ndani ya ndoa.. how do U solve this issue?.. Tuachane na maswala ya korti ya kadhi, badala yake tujaribu kujenga hoja itakayoweza kuzuia kuanzishwa kwa korti hii.

Ni kama swala la Uraia wa nchi mbili nimeona watu wakipinga tuuu bila kueleza mazuri ama mabaya ya Mzawa kuwa na uraia wa nchi mbili kiasi kwamba mjadala wa swala hilo umechukua miaka mingi sana.. nakumbuka toka Mkapa akiwa madarakani tumekuwa tukisikia habari hizi bila ufumbuzi. Hakuna swala Tanzania linaloweza kuchukua muda mfupi kutolewa ufumbuzi bali miaka na kila kikao ni fedha zetu zinatumika bila solution. Leo hii wanalaumiwa viongozi wanaojaribu kulizungumzia...

Mrema nadhani alikuwa na haki ya kuwakilisha kile alichotumwa na wananchi wake..Kama Chadema wanavyowakilisha Majimbo kama muswada. Hii sio sheria tujenge hoja zinazopingana na sio kutazama nani kaleta huo muswada huo. Nina hakika kama CCM ndio wangesema kuhusu Majimbo leo hii Wadanganyika wote wangeipokea kwa mikono miwili....Mjomba tuna matatizo makubwa sana.
 
Mbona hajasema kwanini CCM walihiweka kwenye sera zao za uchaguzi?kweli muungwana mbabahishaji,ananza kutafuta mchawi?
 
Mkuu Mkandara, apo juu msingi wa hoja yangu ni kuwa sula la mrema kuwa au kutokuwa gaidi inategemea unaliangalia toka upande gani, na nadhani hakuna sehemu inayosema kuwa JK au yeyote ni gaidi mkuu kutokana na hilo suala....hoja ni kuwa mrema alipoikumbushia hii mada kama alivosema Mzee Mwanakijiji hapo juu hakuna aliyemwita gaidi au niseme halikuchukua mkondo huu ilivo sasa hadi kwenda mahakamani...

Na kwa upande mwingine, JK naona kuwa JK amelazimika kulijibu hili (again kwenye jukwaa la kidini kama alivofanya arusha) kwa vile waislamu wanajua lipo kwenye ilani.
Na nadhani Mkuu kimsingi hakuna anayekataa kuanzishwa kwa korti hii, kinachobishaniwa hapa ni namna yake ya uanzishwaji ukilinganisha na korti zinazofanana na hizo

Na umezungumzia korti za asili, yes, zipo, lakini nadhani utakumbuka pia kuwa hizo haziendeshwi kwa kodi za wanachi! mabaraza ya ukoo yapo mengi tu na yanafannya kazi nzuri ya kusuluhisha migogoro ikiwemo ya ndoa za kimila nk lakini sijasikia wakiitaka serikali iwaanzishie hayo mabaraza!
 
Shukran za dhati ziende kwa Mwanakijiji kwa kumwelewesha
kadogoo.Kusemakweli kadogoo ni vigumu sana kuificha nia yako hapa
kwenye mijadala ya wazi,maelezo yako kwa asilimia flani yana kamantiki
flani lakini nia yako haiwezi kujificha!Mwanakijiji ameshakueleza
kuhusu Vatican,Iran,Saudi nk,so sio nia yangu kurudia tena,ila mimi
sikuwa upande wowote ule!ila sikufurahishwa na madai ya kuvunja
uhusiano na vatican kwa sababu huo ndio mwanzo wa migawanyiko na ndio
maana nikasema wakristo nao wanaweza kudai ufutwaji wa uhusiano na
nchi hizo amabazo ofcourse zinatumia quran kama katiba yao!Mambo ya
Bush,Mtikila,na porojo nyinginezo ulizozitaja ndio zimeonyesha wazi
kabisa kwamba umetoka nje ya mstari kwa kuhusisha kauli zangu na
misimamo ya kina Bush amabayo hata mimi mwenyewe
sikubaliani!umeshindwa kujificha hapo!umeshindwa kuonyesha
ukomomavu!Kama unataka kujua msimamo wangu basi ungesoma baadhi ya
maoni yangu ambayo nimeshawahi kuposti humu ndani ya forum.Nilishawahi
kusema kwamba Waarabu na Wazungu walituletea dini zao ambazo
zilitugawanya na bado zinaendelea kututenganisha na
kutupiganisha!Lakini kwasababu tayari tumeshaingia kwenye huo mhezo
mchafu,hatuna budi kujadili mambo kama hayo hata kama hatupendi.Mimi
sijali kama kutakuwepo na mahakama ya kadhi,ila je ni kweli kwamba
itatekelezwa?na je wananchi walishaulizwa maoni yao kabla ya
utekelezaji huo?je mambo kama haya ya kupigania ni utamaduni gani kati
ya huo wa mzungu na huo wa muarabu ni wa maana zaidi utatusaidia vipi
kutuletea umoja na maendeleo ya kweli?Ni lini tutapata muda wa
kujadili ni kwa namna gani tutaweza kuja pamoja na kuiletea nchi yetu
maendeleo ya kijamii na kiuchumi?Je tutafika?
- Show quoted text -
On Nov 9, 2007 4:02 PM, JamboForums.com <webmaster@jamboforums.com> wrote:
> Dear jmushi1,
>
> You are subscribed to the thread "Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!" by Kadogoo, there have been 8 post(s) to this thread, the last poster was Si Kitiyi.
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=7011
>
> These following posts were made to the thread:
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97061#post97061
> Posted by: Kadogoo
> On: 9th November 2007 02:43 AM
>
> JMUSHI1, MC na wengine:
>
> Kwanza wanabodi nawasalimia nyote munaonifahamu na musionifahamu kwani ni muda mrefu sana sikuwa nikiandika bali niliamuwa kuwa mtazamaji tu baada ya kuona ushabiki umezidi nani atachaguliwa na nani...
>
> Sasa nikirudi ktk ujumbe wangu wa kuunga mkono tamko la viongozi wa Kiislamu dhidi ya Serikali nadhani baadhi yenu munaufahamu mdogo sana juu ya uhusiano baina ya Serikali na Vatikano kwa upande mmoja na mahusiano na Serikali zenye kuongozwa Kiislamu! kwa kweli kama mutakuwa munajibu hoja kiushabiki shabiki bila ya uchunguzi basi hii inathibitisha mapungufu fulani!
>
> Waislamu wanazungumzia kusitishwa uhusiano ulio rasmi na Vatikano yaani Serikali kuwa na uhusiano wa kiBalozi! sasa munaposema Kama Serikali itasitisha uhusiano na Kanisa Katoliki basi haina budi kusitisha uhusiano na Serikali za Saudia, Iran au Sudan!!!! POINTLESS!!!!!
>
> Kama munakumbuka Miaka 7 iliyopita Maaskofu wa Baraza la Kanisa la Pentekoste la Tanzania(PCT), walitoa kitabu kinachoitaka serikali iitishe kura ya maoni kwanza, kabla ya kuamua kujiunga na Jumuiya ya Mkutano wa Kiislamu, (OIC), ili kupata ridhaa za Watanzania.
>
> Kitabu hicho, kilichopewa jina la "Amani katika Tanzania italindwa kwa:kutenganisha Dini na Mamlaka ya nchi", kinaeleza kuwa kitendo cha serikali ya Tanzania kutaka kujiunga na OIC si jambo dogo. Nijambo linalowahusu Watanzania wote, Waislamu na wasiokuwa Waislam, na hata wale wasiokuwa na dini yo yote.
>
> Kwa mujibu wa kitabu hicho inaelezwa jambo hilo, halifai kujadiliwa kijuujuu tu, kwa kupitia katika vyombo vya habari, na wala haifai kuachiliwa Bunge peke yake kuamua juu ya jambo zito kama hilo.
>
> Halmashauri Kuu ya Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, kwa kupitia katika kitabu hicho, imesisitiza serikali iitishe kura ya maoni ili ipate kuelewa msimamo wa Watanzania wote, wa dini mbalimbali, juu ya jambo hilo.
>
> Katika kutaka kufafanua zaidi juu ya jambo hilo, Halmashauri hiyo imesema, "Lakini si kazi ya Bunge kutunga sheria za kidini, kwa kuwa OIC ni taasisi ya kidini, ni muhimu taasisi nyingine za kidini zilizopo hapa nchini nazo zishirikishwe kikamilifu katika uamuzi mzito kama huu."
>
> Kwa ufupi, Maaskofu wa Kanisa la Pentekoste, katika kitabu hicho, wametilia mashaka uhusiano huo kama utaanzishwa. Wamedai kuwa lengo la misaada inayotolewa na taasisi hiyo ni kwa ajili ya kutaka kueneza imani ya dini hiyo katika nchi wanachama. Maaskofu hao wamesema kuwa kama Tanzaniai tajiunga na taasisi hiyo basi itakuwa ni sawa na kuwasilimisha Watanzania bila ya nidhaa yao!
>
> Inaonekana kuwa kitabu hicho kimetolewa na Kanisa la Pentekoste, kama ni onyo kwa serikali isijiunge na OIC, baada ya kumsikia mgombea wa kiti cha urais wa Zanzibar mwaka 2000, kwa tiketi ya CCM, Rais Amani Karume katika madahalo ulioandaliwa na shirika la utangazaji la BBC, akisema kuwa serikali imekwishafanya utafiti na imeona kuwa Tanzania ijiunge na taasisi hiyo, kwa kupitia serikali ya Muungano, na siyo kupitia serikali ya Zanzibar.
>
> Kwa vyovyote vile, mtazamo huo wa Maaskofu, umekosa uadilifu kama ulivyo msimamo wenu hapa wanabodi. Ni mtazamo ulioelekezwa katika kuuangalia upande mmoja tu wa shilingi na kuupuuzia upande wa pili. Ni mtazamo chongo! Ni sawa na mtu mwenye macho mawili lakini akaamua, kwa makusudi, kufumba jicho moja na kuangalia kwa jicho moja.
>
> Kama serikali ya Tanzania haifai kujiunga na OIC, bila ya kuitisha kura ya maoni, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! kama vile Saudia na Iran!!
>
> Uhusiano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikano, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo! tena na nyinyi wana Forum munaendeleza wimbo uleule wa kudai Vatikano ni nchi Kamili! tangu lini Taasisi ya kidini ikawa nchi ndani ya nchi!
>
> Mwaka 1992 Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ilitaka kuwa mwanachama wa O.I.C.ili ijikwamue kiuchumi kutokana na misaada na mikopo isiyo na riba inayotolewa na jumuiya hiyo ya Waislamu.
>
> Hatua hiyo ya Serikali ya Mapinduzi ilizua mtafaruku ndani ya Bunge, CCM, Serikali na katika vyombo vya habari, kwamba ililenga kuiingiza Zanzibar katika Sharia za Kiislamu na hatimaye kuisilimisha Jamhuri ya Muungano.Lakini Bunge, Serikali na hasa Mwalimu Nyerere, waliipinga kweli kweli, Mwalimu Nyerere kwa mikutano ya hadhara na ya waandishi wa habari alipinga hatua ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano kujiunga na Shirika la O.I.C.",
>
> Mtu yoyote mwenye akili timamu anatambua O.I.C. haina malengo ya kusilimisha bali kusaidia nchi wanachama wake kuboresha hali za kijamii kama Msumbiji ni nchi yenye Wakiristo wengi lakini ni mwanachama wa OIC wala hakuna anaesilimishwa huko!
>
> Mlokole Bush alipotaka kuitawala Iraq alidai Sadam anasilaha za maangamizi kama anavyodai Mlokole Mtikila kuwa mahakama za Kadhi ni ugaidi na zikianzishwa basi Wakiristo watakatwa vichwa!! upuuzi ule ule kama madai ya BUSH!!
>
> Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?
>
> Mbona Zanzibar na Kenya mahakama za kadhi zinafanya kazi kwa ufanisi mzuri sana wala hatujasikia watu kukatwa vichwa!!
>
> Tuache udini na tujibu hoja!
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97064#post97064
> Posted by: Mzee Mwanakijiji
> On: 9th November 2007 03:01 AM
>
>
*
> Waislamu wanazungumzia kusitishwa uhusiano ulio rasmi na Vatikano yaani Serikali kuwa na uhusiano wa kiBalozi! sasa munaposema Kama Serikali itasitisha uhusiano na Kanisa Katoliki basi haina budi kusitisha uhusiano na Serikali za Saudia, Iran au Sudan!!!! POINTLESS!!!!!*
>
> I have seen spin in my life, sir this one is up there!!
>
>
> ---Quote---
> Kama serikali ya Tanzania haifai kujiunga na OIC, bila ya kuitisha kura ya maoni, eti kwa sababu OIC ni taasisi ya kidini; basi lazima tukubali kuwa kwa hoja hiyohiyo, serikali hiyo ya Tanzania itakuwa imefanya kosa kuanzisha uhusiano, tena wa kibalozi, na Vatikano, ambayo ni taasisi ya kidini, na siyo nchi yenye raia! kama vile Saudia na Iran!!
> ---End Quote---
> Ukichunguza utaona kuwa VAtican ni nchi kamili ambayo ilipata uhuru wake kamili 1929 kwa mkataba wa Laterani kati ya Papa na Mfalme wa Italia. Ni nchi kamili inayochagua kiongozi wake, yenye serikali yake kamili, nembo yake, bendera yake, sarafu yake, posta yake na hata jeshi lake! Siyo TAASISI ya kidini. Kanisa Katoliki ni taasisi, lakini Vatikani ni nchi.
>
>
> ---Quote---
> Uhusiano huo wa serikali ya Tanzania na Vatikano, ingawa ni uhusiano baina ya nchi hii na Kanisa Katoliki duniani, lakini jambo la kustaajabisha hakuna yeyote anayehoji juu ya uhusiano huo, si serikali wala makanisa ya Kikristo! tena na nyinyi wana Forum munaendeleza wimbo uleule wa kudai Vatikano ni nchi Kamili! *tangu lini Taasisi ya kidini ikawa nchi ndani ya nchi*!
> ---End Quote---
> unaendelea kujizungusha wewe mwenyewe. Saudi Arabi ni nchi na ndani yake kuna miji mitakatifu ya Maka na Medina. Sisi tuna uhusiano wa Kibalozi na Saudi Arabia, je Serikali yetu ina uhusiano na dini ya Kiislamu? Vatikani ni nchi kamili na haiko ndani ya nchi nyingine!!!! ina mipaka yake inayotambulika kimataifa. Na ndiyo nchi ndogo zaidi duniani.
>
>
> ---Quote---
> Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?
> ---End Quote---
> Sasa kama haiwahusu kwanini wanaitaka CCM itimize Ilani wakati ndani ya CCM kuna Wakristu au utakuwa ni mjadala wa Wana CCM waislamu peke yao? Na kule Bungeni ambako wanataka sheria ipitishwe watakuwa na kikao cha Bunge la Waislamu watupu na Wakristu hawatatakiwa kuchangia? Kama kuna ndoa yenye kuhusisha wakristu au wakristu hawana haki zozote kwenye hiyo Mahakama ya Kadhi na kama hawana kwanini wakubali wake zao wafuate maamuzi ya mahakama hiyo? Kama hawataki wakristu watolee maoni wajianzishie na waendeshe wenyewe nadhani hakuna mtu atakayelalamika.
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97066#post97066
> Posted by: YournameisMINE
> On: 9th November 2007 03:20 AM
>
> Hovyoooooooooo na tena bure kabisa........hao waislam na wakristo wanaopiga makelele yasiyo na msingi wote ni "extremists" hawana tofauti na bin Laden, Pat Robertson au Marhum Jerry Falwell. Ndugu zangu WaTz mnatakiwa kuya-reject mawazo kama hayo huko juu kwa hii thread kwani ni pungumfu mno na primitive kushinda hata amoeba, watu wanatakiwa ku-concentrate kwenye vitu vya maana, issues za maendeleo kwa taifa zima regardless na imani zao za kidini!!!!. Uislam na Ukristo kwanza zote ni dini za KIFISADI, kikoloni na kufikirika..............tupeni kwenye trash udini!!!! Atheist wa Kibongo, yes sir, I said so. Nasubiri kuvurumishiwa kashfa na kubezwa, msipoteza muda kwani yatakuwa makelele ya chura.
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97081#post97081
> Posted by: Mzee Mwanakijiji
> On: 9th November 2007 06:23 AM
>
>
> ---Quote (Originally by YournameisMINE)---
> Hovyoooooooooo na tena bure kabisa........hao waislam na wakristo wanaopiga makelele yasiyo na msingi wote ni "extremists" hawana tofauti na bin Laden, Pat Robertson au Marhum Jerry Falwell. Ndugu zangu WaTz mnatakiwa kuya-reject mawazo kama hayo huko juu kwa hii thread kwani ni pungumfu mno na primitive kushinda hata amoeba, watu wanatakiwa ku-concentrate kwenye vitu vya maana, issues za maendeleo kwa taifa zima regardless na imani zao za kidini!!!!. Uislam na Ukristo kwanza zote ni dini za KIFISADI, kikoloni na kufikirika..............tupeni kwenye trash udini!!!! Atheist wa Kibongo, yes sir, I said so. Nasubiri kuvurumishiwa kashfa na kubezwa, msipoteza muda kwani yatakuwa makelele ya chura.
> ---End Quote---
> kwa mtu ambaye ni atheist kuingia kwenye thread ya mambo ya dini nadhani ndiyo kelele za chura. Ila kuwa atheist nayo ni imani na una haki nayo, sawa sawa kabisa na mtu ambaye anaamini kuwa mwezi umeundwa kwa jibini!
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97088#post97088
> Posted by: YournameisMINE
> On: 9th November 2007 07:22 AM
>
>
> ---Quote (Originally by Mzee Mwanakijiji)---
> kwa mtu ambaye ni atheist kuingia kwenye thread ya mambo ya dini nadhani ndiyo kelele za chura. Ila kuwa atheist nayo ni imani na una haki nayo, sawa sawa kabisa na mtu ambaye anaamini kuwa mwezi umeundwa kwa jibini!
> ---End Quote---
> Muungwana sana MKJJ,
> Kama nilivyotegemea....yakuwa kwamba utakuwa najibu, unanifanya nakuwa disappointed kwani upo predictable kupita kiasi. Kuna siku ulisema kwa kudhani kwamba nipo naive, nadhani tume-trade hiyo kitu......kumbuka haya ni mapambano ya kifkra. (hint, achana na huo mchezo wa umesema/ulisema.....ungekuwa mtu aliyesoma MUCHS ungeelewa, hiyo inaitwa SUMU. Kwa bahati mbaya inaonekawa tayari ni victim). Issues za kidini ziacheni!!!!.
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97092#post97092
> Posted by: YournameisMINE
> On: 9th November 2007 07:45 AM
>
> Politics za nani Mslam au Mkristu ndizo ambazo Nyerere alizikandamiza kwa nguvu zake zote. Ktk mambo machache ninayokubaliana naye hilo mojawapo......leo nimepata lunch hooters, muhudumu mmoja wapo ni demu mzuri wa Kimorocco(tokana na jina lake). Nikamuuliza kama yeye ni mslam, akasema ndio!! nikauliza kama ana-practice, akasema ndio tena hamsa salawat......basi moyoni nikasema alaaaa, kumbe tupo kwenye globalization, watu wanapeta tu. Sasa ninyi jibunguzieni possibilities tu na udini ulopitwa na wakati.
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97098#post97098
> Posted by: kweku
> On: 9th November 2007 08:19 AM
>
> Eeeh hii kali. Inabidi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa ki mataifa aanzishe darasa.
> ************
> Re: Serikali isitishe uhusiano na Vatican mara moja!!
> http://www.jamboforums.com/showthread.php?p=97122#post97122
> Posted by: Si Kitiyi
> On: 9th November 2007 10:59 AM
>
>
> ---Quote (Originally by Kadogoo)---
> JMUSHI1, MC na wengine:
>
>
> Wakiristo wa TZ inawahusu nini kuanzishwa mahakama za Kadhi? pilipili ziko shamba zawawasha nini? kama Biblia haina sheria za kuhukumia waumini wake kwanini Waislamu wasiruhusiwe kutumia baadhi ya sheria za Kurani kama vile mirathi na ndoa?
>
> Tuache udini na tujibu hoja!
> ---End Quote---
>
> Inatuhusu kwa sababu mnataka kutumia pesa zetu za kodi kuendeshea mambo yenu ya kidini na vilevile tunaiheshimu katiba yetu ambayo hairuhusu ubaguzi wa kidini, rangi wala kabila.
>
> Jambo linalotia shaka, kwa nini mnadai Mahakama ya Kadhi itashughulika n a baadhi ya sheria za Quran kama ndoa na Mirathi; Kwa nini isiwe zote? Kutakuwa na manufaa na tofauti gani kutekeleza baadhi ya sheria zenu kwenye mahakama ya Kadhi na zingine kuziacha kwenye mfumo wa Mahakama zingine za Serikali? Kwa nini mnataka hivyo? Mimi sipati picha.
>
>
>Shukran za dhati ziende kwa Mwanakijiji kwa kumwelewesha
kadogoo.Kusemakweli kadogoo ni vigumu sana kuificha nia yako hapa
kwenye mijadala ya wazi,maelezo yako kwa asilimia flani yana kamantiki
flani lakini nia yako haiwezi kujificha!Mwanakijiji ameshakueleza
kuhusu Vatican,Iran,Saudi nk,so sio nia yangu kurudia tena,ila mimi
sikuwa upande wowote ule!ila sikufurahishwa na madai ya kuvunja
uhusiano na vatican kwa sababu huo ndio mwanzo wa migawanyiko na ndio
maana nikasema wakristo nao wanaweza kudai ufutwaji wa uhusiano na
nchi hizo amabazo ofcourse zinatumia quran kama katiba yao!Mambo ya
Bush,Mtikila,na porojo nyinginezo ulizozitaja ndio zimeonyesha wazi
kabisa kwamba umetoka nje ya mstari kwa kuhusisha kauli zangu na
misimamo ya kina Bush amabayo hata mimi mwenyewe
sikubaliani!umeshindwa kujificha hapo!umeshindwa kuonyesha
ukomomavu!Kama unataka kujua msimamo wangu basi ungesoma baadhi ya
maoni yangu ambayo nimeshawahi kuposti humu ndani ya forum.Nilishawahi
kusema kwamba Waarabu na Wazungu walituletea dini zao ambazo
zilitugawanya na bado zinaendelea kututenganisha na
kutupiganisha!Lakini kwasababu tayari tumeshaingia kwenye huo mhezo
mchafu,hatuna budi kujadili mambo kama hayo hata kama hatupendi.Mimi
sijali kama kutakuwepo na mahakama ya kadhi,ila je ni kweli kwamba
itatekelezwa?na je wananchi walishaulizwa maoni yao kabla ya
utekelezaji huo?je mambo kama haya ya kupigania ni utamaduni gani kati
ya huo wa mzungu na huo wa muarabu ni wa maana zaidi utatusaidia vipi
kutuletea umoja na maendeleo ya kweli?Ni lini tutapata muda wa
kujadili ni kwa namna gani tutaweza kuja pamoja na kuiletea nchi yetu
maendeleo ya kijamii na kiuchumi?Je tutafika?
>

>
 
HI WE KADOGOO NGOJA NIKUULIZE SWALI MOJA,NA UKIWEZA KULIJIBU THEN UTAKUWA UMEELEWA NINA MAANA GANI"JE SERIKALI ZA SAUDI ARABIA NA IRANI SI ZA KIDINI?"WAKRISTO NAO WAISHTAKI SREIKALI?MHH HAYA WE TUNAKOELEKEA!
KADOGOO ULISHASEMA WAZI KUWA HUWEZI KUAMINI KWAMBA SERIKALI YETU INAUHUSIANO NA "VATICANO"SIKUTAKA KUKURUPUKA NA KUJAJI HUO MSIMAMO WAKO MBOVU WA KUTOAMINI!SIKUTAKA KUSEMA KUWA UNAONYESHA MWELEKEO FLANI KUTOKANA NA KAULI YAKO HIYO AMBAYO NI WAZI INAMWELEKEO WA KIUSLAMU VS UKRISTO,ULIPEWA NAFASI KWASABABU WANA JAMBO WANA BUSARA!LAKINI WEWE MWENYEWE UMEJILETA WAZI KWA KUANZA KUSHUTUMU WENZIO NA KUTAKA KUWALAZIMISHA WACHAGUE UPANDE!KWANGU UMEKOSEA,SICHAGUI UPANDE WOWTE ULE,SITAKI SERIKALI YETU ISITISHE UHUSIANO NA VATICAN NA VILEVILE SITAKI ISITISHE UHUISIANO NA IRAN NA SAUDI.SINA SHIDA NA MAHAKAMA YA KADHI ILIMRADI IMEJADILWA NA KUPATA BARAKA ZA WANANCHI!JE WE KADOGOO,NINA SWALI MOJA KWAKO;UKIAMBIWA UJITAMBULISHE,JE UTATANGULIZA UTAMBULISHO WA UTANZANIA KWANZA AMA WA DINI KWANZA?UTAMBULISHO GANI UTAUTANGULIZA?"ARE YOU A TANZANIAN FIRST THEN MOSLEM/CHRISTIAN OR ARE YOU MOSLEM/CHRISTIAN FIRST AND THEN TANZANIAN?
 
katika siku ambazo jk ameongea UTUMBO ni leo.....sikumuelewa kabisa nadhani ana tatizo ..

1.it was untimely kuongelea ile ishu pale ..wana philosophy kwa kuchambua maneno yake pale watabaki na maswali mengi kuliko majibu...

2.JE UJUMBE WA RAIS KWA MAASKOFU NI UPI..KWAMBA HOJA YA KADHI HAKUIAZISHA YEYE MUISLAMU BALI NI MKRISTO AGUSTINO L MREMA??

3.ALIPOSEMA HOJA IMETUMIWA NA WANASIASA KWA MTAJI WA KISIASA ..ANA MAANA CCM WALIINGIZA KWENYE ILANI YAO ILI KUPATA KURA ZA WAISLAMU TU...KWA HIYO INA MAANA ILANI YA UCHAGUZI WA CCM NI YA UWONGO?? KWA MAANA YA KULENGA MAKUNDI MBALI MBALI KIMAHITAJI KWENYE ILANI ILI KUTOA AHADI ZA UWONGO KUPATIA KURA??

4.KAMA HOJA NI YA MREMA ...KWANI MREMA NDIO ALIYEANDAA ILANI YA CCM??

Ninachoweza kuona ni kuwa rais anatoa majibu mepesi kwenye hoja nzito na sasa AMEDHAMIRIA KU DIVERT ATTENTION YA WANANCHI KUTOKA KWENYE KUMDAI AHADI YA KADHI KUPELEKA MGONGANO KATI YA WAISLAMU NA MTIKILA NA MREMA ...WAKATI INGETAKIWA WAISLAMU WAMBANE YEYE ..WAKATI MUDA UNASOGEA ITAFIKA MWAKA 2010 ..AMBAPO CCM WATAAMUA KUIONDOA AHADI HII KWENYE ILANI..KWANI KIUKWELI HAITAWEZEKANA...NDIO MAANA AKASIMAMA MBELE YA MAASKOFU KUTUBU.KUWA HATAFANYA KINYEMELA[KUSILIMISHA NCHI]

kimsingi rais analeta siasa ...na kwa bahati mbaya waislamu watabaki wanawalaumu wakristo kama kikwazo cha kadhi badala ya kuilaumu CCM kwa kuwaghilibu kura zao kwa ahadi isisyotekelezeka..
 
kimsingi rais ametumia elimu yake ya propaganda ..kumrushia zigo la ahadi ya kadhi kwa mrema..na kama mnavyojua naye mrema ni professor ..na alikuwa mwalimu wa usalama na propaganda kule mbweni ..elimu aliyosomea yugoslavia na urusi...so kuanzia kesho itazuka majibu ya kipropaganda kwenye magazeti ..huku mambo yanaenda..so anataka badala ya mtikila kugombana na jk na lowassa aanze kubishana kwanza na mrema[mkristo mwenzie] aliyeleta hoja ya kadhi..na waislamu wabaki wanamuona mtikila na wamisheni wengine kama kikwazo kwao..so kimsingi hapo atakayechochea UVUNJIFU WA AMANI NI RAIS ..kama moja ya njia ya kujinasua kwenye makombora ya moja kwa moja kutoka kwa waislamu ambao wanaamini kikwete atawapa kadhi ...huku yeye akijua hawezi na wala hadhubutu!!!!
 
Nakulilia Tanzania,
Shukrani sana mkuu, tena umejnga hoja safi... safi sana kwa maelezo mafupi na wazi.

haya sasa mbona ukweli unaonyesha wazi kuwa hizi ni mbinu chafu za kutaka kugombanisha watu!... Taarifa ndogo hapo juu imedhihirisha tofauti kabisa na jinsi Mtikila alivyoijengea hoja...Hoja ambayo imezua kipengele cha kwanza hapo juu..kwamba suala hilo limesababisha kuwepo kwa dalili za kuvunjika kwa upendo na mshikamano baina ya wakristo na waislamu.

Je, kuna haja ya kumwita aliyewakilisha muswada huu ndugu Mheshimiwa Mrema - Gaidi?

Mukandara,

Jibu ni rahisi ingawa naona watu wanazunguka tu kwa kuingiza hisia zao badala ya kuzama kwenye msingi wa swali lako. Kwamujibu wa kauli za Mtikila kuhusu lengo la mahakama hiyo, Mrema naye (kwa tafsiri na mazingira ya sasa) NI GAIDI. Tatizo liko wapi? Lakini hoja ya Waislamu iko pale pale...na CCM kwa kuwa ndiyo iliahidi na kushinda ikashika dola, IWAPE mahakama yao! La sivyo, ifanye kama Mwanakijiji anavyoshauri...ikiri kwamba iliiga sera ya watu kwa kujipendekeza kisiasa, na kwamba sasa mambo yameshindikana, na iwaruhusu waislamu kuanzisha mahakama yao wanavyojua kama wakristo walio na mahakama zao nje ya bunge. Basi! JK aache kutapatapa na kutafuta wachawi.
 
anakuliliaTanzania,
Ikiw umekubali kuwepo kwa korti za asili narudisha swali kwako. je, umeuona huo muswada ukiomba fedha za serikali kuendesha korti hizi? je, sii kweli muswada unaomba sheria ya kuundwa kwa korti hii ili Itambulike Kitaifa kulinda maslahi ya baadhi yeu wanaoonewa..

Naomba mtu aliyekuja na hoja ya serikali kugharamia hili atupe kipengele kinachosema hivyo. Kisha ndio tuanzishe ubishi ama hoja zinazoendana na kipengele hicho laa sivyo naona hapa tuazunsha vitu tu kwa kutazma rangi zetu za dini.

Kisheria kutakaa kuweka kipengele ktk katiba ya nchi ni dalili ya kukataa haki ya waumini wa dini hiyo. Huwezi kutambua uhuru wa ku pratice dini fulani kisha ukaacha kuwapa sheria ambayo inawalinda.

Unajua nimesoma baadhi ktk mada tofauti, nakuhakikishia kuwa sisi wenyewe ndio wadini kuliko hao waliowakilisha muswada. Soma mada ya Uhusiano wetu na Vatican utaona kuwa wale wote wanaopinga swala hili kule nwanalipongeza na kuzua sababu za maana kwa gharama hiz hizo. na wote wamegawanyika rahisi kumjua nani Muislaam na nani Mkristu. Ukiuliza sababu za kupinga eti gharama mbona upande ule wa pili wahakuziona gharama hizo?..

Kisha, swala la Musada haliwezi kuondoka ktk Ilani ya chama kama limewahi kupokelewa bungeni kwa sababu ati ni jukumu la CCM wao ndio watalawa. Ni kama vile kesi mahkamani hata ichukue muda gani haijapata muda wa kuzungumziwa hubakia hadi pale mshiktaki atakapo ondoa mashtaka hayo.

Ni mrema alioleta hoja na kaikumbushia kwa hiyo JK kila anapokwenda huulizwa swala hilo na hawezi kupuuza kujibu ati kwa sababu wakistu hawaitaki. maswala ya muungano Zanzibar, ipo miswada kibao bungeni ambayo haijakamilika na hatuwezi kuwalaumu CCM kwa nini bado wameiweka hali wananchi wa bara hawataki kuisikia.

Swala litashughulikiwa na haliwezi kutoa ushindi ikiwa sisi tunashindwa kujenga hoja za msingi isipokuwa msukomo wa dini na viongozi wetu. Nina hakika hata hiyo mada ya JK kuvunja Uhusiano na Vatican imeanzishwa kutokana na mchungaji fulani wa kiiislaam kuhoji safari ile, kisha manazi wakadakia na kuifanya deal!

Jamani kwa heshima ya JF inabidi tujenge hoja huu mpango wa vioja kama alivyosema Mzee Nyani ni kujipa magonjwa ya moyo out of nothing.

Tukumbuke tu kamba kila ua la rose has it's Thorn!..Ukijali sana mwiba hutaweza kuona uzuri wa ua hilo. haya ni mambo ya kawaida kabisa yana muda wake kama fashion yatakuja washinda.
 
Back
Top Bottom