Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kwa kuanza naomba niwaulize JE TANZANIA INAFUATA DINI GANI?
Kuhuliza huko kunatokana na hii hoja ya MAHAKAMA YA KADHI!!.Hoja hii kwa mara ya kwanza ilianzishwa na ndugu yetu Mrema akiawa mbunge wa temeke kwa chama cha NCCR,ikaishia hewani hewani. Mara ya pili ikazushwa tena na mbunge mwingine anaetokea mkoa huo huo wa ndugu Mrema akiwa mbunge kwa chama cha TLP ambacho mwenyekiti wake ni ndugu A.L.Mrema!!.

Ni jambo la kushangaza kwani hawa wote ni wakristu na hoja hiyohiyo ilikuwa inatolewa na mtu mmoja tu! huyu Ndesamburo ametumwa tu lakini mmiliki wa hoja hiyo ni Mrema.Kwa hili nadhani alikuwa anatafuta umaharufu wa kisiasa kwa Waislam bila kujua impact yake (kipindi kile shule ilikuwa ndogo kwake).Kwa ufahamu wangu mimi mahakama zote za hajabu hajabu zilifutwa mwaka 1963 na Mheshiwa waziri Chifu Abdalha Fundikira (TENA HUYU NI MUHISLAM SWAAAFI).Sasa ndugu yetu Mrema baada ya kuona umaharufu umeshuka akataka kuunyanyua kwa kuwapitia waislam.Jamani nchi yetu haiongozwi na sharia.Nashukuru kwa sasa baada ya kujua hana mvuto tena kwa wabongo ameamua kukaa kimya!.

Nayo serikali ya JK baada ya kuona imepoteza mvuto wake (labda uzuri wa sura ndiyo umezidi!!)inafufua tena hoja hiyo ili kuwawini waislam! sasa leo tunakuwa na mahakama ya waislam,kesho wakristu nao wanadai mahakama yao, keshokutwa wahindu nao watadai na madhehebu mengineo tuliyonayo hapa nchini pia yatadai. Je tunaelekea wapi?

Serikali ya JK na wabunge wake wanaolipwa pesa nyingi kwa kodi zetu (mpaka mungu hapendi!) badala ya kukaa na kujadili jinsi ya kuwaondolea au kuwapunguzia Watanzania ukali wa maisha wanaanza kuzungumzia shari. Nasema SHARI kwa sababu kwenye hali ya AMANI hakuna mtu anyefikiria kwenda mahakamani! Kwa jinsi wanavyolivalia njuga namuunga mkono Mh. Bush na Mchungaji Mtikila.

Tunataka kuongeza mimahakama tuu badala ya kujadili maendeleo.Ndugu zangu labda niwaulizwe maswali haya:
1.Je muislam akigombana na mhumini wa dini nyingine kesi hiyo itapelekwa mahakama gani?
2.Hukumu za sharia ni za kikatili, je wezi watakatwa mikono? au wagoni watapondwa na mawe?

Hayo mojawapo ya maswali ya kujiuliza je hii mahakama itakuwaje? tumekaa kwa amani lakini hawa warafi wa siasa wanataka kutupeleka pabaya.

Hayo ni mawazo yangu juu ya hoja hiyo! kama limekuuma utajiju!!!

Tatizo ni nini? mimi sijakuelewa hapo.
 
Tanzania inafuata dini, dini haitakiwi kuhusisha serikali ni wananchi na makanisa au misikiti yao. Tanzania ikianza kufanya hizi mahakama basi katiba haina maana tufuate dini kwenye kila kitu na sio mahakama tu.

Mbona hapa hapa Tanzania, huko visiwani kuna mahakama ya kadhi na hakuna tatizo la katiba kuhusu hilo? au unamaana Tanganyika "ikianza kufanya kazi hizi"...?
 
Mahakama Kuu leo imefutilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mtikila na Kanisa lake kupinga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi. Majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo ya kikatiba wamesema kuwa uamuzi wao huo unatokana na kubaini kuwa katika kesi hiyo, Mtikila hakujiandaa ipasavyo.
Lakini Mtikila amesema kuwa huko ni kuvunjika kwa kioleo tu na uhunzi utaendelea kwani anapanga kukutana na wanasheria wake ili kuikarabati kesi hiyo na kuirudisha tena mahakamani
 
Mtikila unawacha kuwashitaki mafisadi mahakamani wakati ushahidi wote upo unahangaika na la kadhi, hilo litakushinda kaka.
 
Kwa kinywa chake mwenyewe Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete alituahidi wakati wa kusimikwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania(KKKT)Mhasham Alex Malasusa kwamba Ifikapo mwezi februari 2008 serikali itatoa tamko au uamuzi kuhusu swala la Kadhi wa Tanzania.

sasa huu ni mwezi April unaelekea kwisha na hakuna dalili ya serikali kusema chochote.jee mheshimiwa Kikwete amesahau ahadi yake au ndiyo kama alivyosema kuwa hakuhusika na uandikaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo ndiyo chanzo cha sakata lenyewe?

Ama pia kama alivyosema mwenyewe kwamba jambo lenyewe la kadhi halikuanzishwa na CCM badala yake lilianzishwa na mheshimiwa Mrema na baadaye kushabikiwa na Thomas Ngawaiya akiwa Mbunge kupitia chama cha TLP kabla ya kurejea CCM kwenye sera "zinazoeleweka?
 
Kwa kinywa chake mwenyewe Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete alituahidi wakati wa kusimikwa Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania(KKKT)Mhasham Alex Malasusa kwamba Ifikapo mwezi februari 2008 serikali itatoa tamko au uamuzi kuhusu swala la Kadhi wa Tanzania.

sasa huu ni mwezi April unaelekea kwisha na hakuna dalili ya serikali kusema chochote.jee mheshimiwa Kikwete amesahau ahadi yake au ndiyo kama alivyosema kuwa hakuhusika na uandikaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo ndiyo chanzo cha sakata lenyewe?

Ama pia kama alivyosema mwenyewe kwamba jambo lenyewe la kadhi halikuanzishwa na CCM badala yake lilianzishwa na mheshimiwa Mrema na baadaye kushabikiwa na Thomas Ngawaiya akiwa Mbunge kupitia chama cha TLP kabla ya kurejea CCM kwenye sera "zinazoeleweka?

Kikwete alianza kuonyesha udhaifu na flip flopin pale alipoanza kumsukumia Mrema hii issue as if Mrema ndiye serikali. Hii kitu imemkalia vibaya Kikwete na kama kawaida yake hawezi kufanya maamuzi kwenye mambo magumu kama haya. Yuko very slow hadi inatisha!
 
Game Theory,

..mbona alishalisemea!!??

..alisema suala la kadhi lilichomekwa kwenye ilani wakati Benjamini Nkapa akiwa Mwenyekiti.

..Kwa msingi huo suala la kadhi aulizwe Benjamini.
 
Game Theory,

..mbona alishalisemea!!??

..alisema suala la kadhi lilichomekwa kwenye ilani wakati Benjamini Nkapa akiwa Mwenyekiti.

..Kwa msingi huo suala la kadhi aulizwe Benjamini.

kwa maana nyingine unataka kutuambia kwamba CCM siyo chama chenye muunganiko wa mambo na kwamba kila mwenyekiti ana jinsi ya kuendesha mambo ndani ya chama hicho.

Basi kwa mantiki hiyo yale mabango yaliyokuwa yanaeleza kwamba Kikwete ataendeleza yale yaliyoanzishwa na mkapa yalikuwa yamejaa Ghiliba za Kisiasa!
 
hivi kwanini hiyo ofisi ya kadhi ni big deal kisiasa? naomba kueleweshwa..lakini hii kitu sio yale mambo ya kuleta sharia law au vitu vinavyofanana kidogo?
 
kila kikicha tunambiwa SERIKALI YA TANZANIA HAINA DINI LAKINI WATANZANIA WANZO IMANI ZA KIDINI

at the same time serikali hiyo hiyo inawachagulia waislam watawala wao..kwa sasa ni BAKWATA

 
Game Theory,

..mbona alishalisemea!!??

..alisema suala la kadhi lilichomekwa kwenye ilani wakati Benjamini Nkapa akiwa Mwenyekiti.

..Kwa msingi huo suala la kadhi aulizwe Benjamini.

Mwacheni mzee wetu apumzike. I hope this is the answer which is likely to be given!

Lakini kwa sasa hivi hii sio issue ya kusumbua watu, labda inaweza kutumiwa na watu kuepuka zigo kubwa la EPA na mengine!
 
Mheshimiwa Spika, kuna makundi ya Watanzania ambao wanautofauti wa kidini na kusema uhuru wa kuabudu upo nchini. Waislamu kuna mambo yao ambayo ni lazima yatendeke kwa misingi ya kiislamu ..... Mh. Mbunge Hemed Mohammed, Hemed - Chonga (30 July 2007)

Waislamu nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwepo na Mahakama ya Kadhi katika Tanzania itakayoangalia na kushughulikia mambo maalum ambayo yanajumuishwa zaidi na Sharia za Kiislamu kuliko Sheria za Mahakama za kawaida.
Ukweli kwamba tayari ipo Mahakama ya Biashara (Uchumi), Mahakama ya Ardhi ni uthibitisho tosha kwamba mambo maalum (ya aina moja) yanahitaji kushughulikiwa na Mahakama maalum ambayo vitabu vya Sheria vya kawaida huyafafanua kwa akali (uchache).
Kwa mantiki hii, ni wakati muafaka kwa Waislam kusoma kusoma kitabu chao na kuonyesha mapendekezo kadhaa yanayoweza kuisaidia Mahakama ya Kadhi iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na kupatikana madaraka kamili ya kisheria ya Mahakama ya Kadhi.
Mswada unalenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi katika kila Wilaya ya Tanzania, ili kuangalia mambo yote yahusianayo na Sharia ya Kiislamu katika masuala ya Ndoa, talaka, haki ya kulea watoto, mgawanyo wa mali, Urithi n.k. pale ambapo wahusika wa utata huo ni Waislamu, waliooana kwa mujibu wa sharia na desturi ya ndoa za Kiislamu.
Ukweli ni kwamba makusudio ya mswada huu ni mazuri, na ili Mahakama iweze kupata hadhi yake ni vyema basi yawepo maandalizi yenye michango ya madhehebu yatakayo wawezesha Makadhi katika wilaya mbali mbali wakifikia kwenye uamuzi wa kesi zinazofanana kimsingi, wasitowe hukumu zinazopingana kwa kiasi kikubwa.
Hivyo, upo umuhimu wa kukiandaa kitabu makhususi cha Sheria za Kiislamu kitakachotumika kama Mwongozo wa Makadhi ili kuiepuka migongano.
Hapo zamani mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo lilipitisha “Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo)” iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu.
Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kama ulivyokubaliwa na wanachuoni wa Sharia za Kiislamu kutoka Madh-hebu matatu Kiislamu Shafi’i, Hanafi na Shia).
Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.
Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya ‘Ndoa’ kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.
Hata hivyo, kanuni ya Sheria ya Ki-Islamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge. Na kwa sababu sasa serikali inakusudia kuanzisha Mahakama za Makadhi katika kila Wilaya, ni wakati muafaka wa kufufua tena mswada wa sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 ili ufanyiwe kazi na kazi hii ianzie pale ilipoachiwa.
Jambo muhimu hapa ni kuepusha uwezekano wa Makadhi kutoa hukumu zitakazoleta utata. Vinginevyo, mzigo wa kazi za Mahakama Kuu utaongezeka kwa kuwa rufani kutoka Mahakama za Makadhi zitajazana kwenye Mahakama ya Rufaa.
Madhehebu za Makadhi wa Wilaya:
Kwa vile Waislamu wengi wa Tanzania ni wafuasi wa Madhehebu ya Shafii ni vizuri makadhi wa Wilaya watokane na Madhehebu ya Shafii.
Lakini iwapo wahusika au mhusika wa mgogoro ni wa Madhehebu isiyo ya Shafii, inapendekezwa kuwa Kadhi wa Wilaya asaidiwe na wanachuoni wa madh-hab inayohusika.
Hii itafuta uwezekano wa kutolewa hukumu isiyo sawa na itawapa imani ya kutendewa haki wahusika au mhusika. Wasaidizi wa Kadhi wa Wilaya waliotajwa hapo juu itabidi watayarishwe katika kila Wilaya na wanaweza kuangaliwa upya (kuteuliwa) muda baada ya muda. Hii inalenga kwa kiasi kikubwa kuwatendea haki na usawa Waislamu wote nchini.
Hivyo majadiliano yetu yawe namna ya kuboresha, ima kuzuia katu haiwi kwani hili ni suala la wakati tu. Linalo mfaa Kaizar mpeni.
 
EAC set to reap big from OIC business forum
Written by STEPHEN NUWAGIRA
Tuesday, 24 June 2008
THE BUSINESS WEEK

KAMPALA, UGANDA - The just concluded 1st Organisation of Islamic Conference (OIC) business forum held in Uganda last week could be one of the ingredients that the East African region has been looking to bolster its economic potential and marshal its development efforts.
By the end the two- day conference, a lot of private individuals and companies worth over US$3 billion put together had pledged to set up shop in the region with Uganda as their base. The most prominent of these are the Islamic Corporation for the Development of the Private Sector (ICD), a subsidiary of the Islamic Development Bank (IDB) which had already started talks on possible partnerships with Ugandan banks which would act as its agents in the country.

Another financing institution the International Investment House (IIH) which is going to set up the first Islamic bank in East Africa, the National Islamic Bank of Uganda (NIBU) by the end of this year. It will mainly focus on lending to SMEs and other small private businesses.

Foras East Africa has also pledged to set up shop in Uganda from where it will finance projects in selected areas the region. These are mainly areas that are expected to accelerate economic growth of the region and create more jobs for the region's thousands of unemployed youth. These sectors are agriculture, road construction, cotton and textiles pharmaceuticals and energy. In Uganda focus will first be put on cotton and textiles and coffee processing.

ICD deals in development finance and equity banking among others and according to the banks chief executive officer Mr. Khaled Al - Aboodi, the bank finances projects that could help create jobs, and reduce on the country's dependence on imports. "We finance projects of a minimum of US$2 million to US$5 million, but we can extend line of financing through local banks which then give finding to smaller projects run by mostly SMEs," he said.

He said the bank gives up to 40% funding for any projects and they do not require security for one to get a loan.

However, they also only provide the required assets, equipment or machines that one might be in to do their business and 'charge rental for using the assets instead of interest on the loan. He said that he would extend funding to projects dealing in agriculture, food processing, medicines, technology and ICT because they are vital in the development of the region.

In Sub Saharan Africa ICD operates in Senegal, The Gambia and Mauritania, but this will change when its operations in the region start. The bank started 1999 and has over $500million core capital with about US$1 billion share capital. It operates in 23 countries in Africa, the Middle East and Central Asia.

The President of the Islamic Chamber of Commerce and Industry, Sheikh Saleh bin Abdullah Kamel also told the participants that the chamber was preparing an investment plan which is to be implemented soon in the region. He said that he was impressed with Uganda's tourism potential. He, however, revealed that ICC&I plans to start a state of the art coffee plant in Uganda.

According to the vice chairperson of the East African Business Council Mr. Keli Killu, the region is an emerging economy with a lot of potential which has not yet been tapped. With funding such from the rich OIC members, the region, the second largest market in Africa would be ready for take off.
"With over 120 million people in the EAC and a further 400 million people in the COMESA region you can't go wrong," he said.

He said that OIC private investors can take advantage of the good policies in the region to start projects in the oil industry, organic cotton production and commercial food production to take advantage of the gap that has been created by the industrialisation of China and India the two major rice producers in the world.

The managing director of Roofings Uganda Limited Mr. Sikander Lelani said that these projects provide a good opportunity for Ugandan business community that has long been suffering with exorbitant interest rates on loans that has hindered the growth of the local industries.

"Funding from OIC rich nations will be a timely intervention, the kind that women entrepreneurs who most of the times are denied loans by local banks would benefit from. This will give us better opportunities to expand our small businesses to increase our production and even create more jobs for Ugandans," the chairperson Uganda Women Entrepreneurs Association, Dr. Eve Kasirye - Alemu said. Kasirye, however, said that women entrepreneurs are should be given priority when the financing banks open for business because they have been marginalized for long.

During the conference the Uganda Investment Authority executive director Dr. Maggie Kigozi took participants through the investment opportunities in the country.

She said that some of the priority areas investors from the OIC countries can invest in include manufacturing, agriculture, tourism, ICT, mining, petroleum, services - education, health, financial-, industry, forestry, construction, infrastructure and energy.
 


Another financing institution the International Investment House (IIH) which is going to set up the first Islamic bank in East Africa, the National Islamic Bank of Uganda (NIBU) by the end of this year. It will mainly focus on lending to SMEs and other small private businesses.

Point of correction.
It is not going to be the first Islamic Bank in East Africa.
There are already at least two that I know of based in Kenya "First Community Bank and Gulf African Bank"

see http://www.bdafrica.com/index.php?option=com_content&task=view&id=4076

Yeza kuwa hata TZ tayari yako!
 
Japokuwa muswada haujawasilishwa bado, tamko la waziri wa sheria kuhusu kupokea rasimu ya muswada wa mahakama ya kadhi ili ushughulikiwe na serikali kabla ya kuwasilishwa bungeni imechochea mjadala mkubwa sana leo hii kuhusu Mahakama ya kadhi.

Nimesummerize hoja zilisotolewa ili kupata picha ya hali ilivyo miongoni mwa wabunge kuhusu hoja hii.

Side A: Hoja toka kwa wabunge wanaounga mkono:

1. Kwa nini kadhi aliondolewa 1963?
2. Ilani ya CCM iliahidi kumaliza suala la Mahakama ya Kadhi. (Plus ni ilani iliyotengenzwa chini ya Mkapa kwa hiyo msimsakame Kikwete kuwa anataka kupendelea Waislam)
3. Mahakama ya Kadhi iko nchini Kenya ambako asilimia kubwa ya wananchi ni Wakristo. Tujifunze kutoka kwao.
4. Inafaa tuvumiliane. Waislam wamevumilia wakristo (eg. kuwa na Ubalozi wa Vatican na ubalozi wa Italy), kwa hiyo Wakristo nao wawe wavumilivu uwepo wa Mahakama ya Kadhi.
5. Mahakama ya Kadhi sio serikali ya Kiislamu, bali ni mwendelezo wa ibada kwa waislamu (Baaadhi ya maswala ya msingi ambayo Mahakama itashughulikia kama vile mirathi, na ndoa ni sehemu ya Ibada kwa waislamu kwa hiyo kwa kutokuwa na mahakama ya kadhi wanashindwa kutimiza ibada)

Side B: Hoja toka kwa wabunge wasiounga mkono:

1. Ilani ya CCM sio katiba wala sheria. Ni ahadi tu, ambazo utekelezaji wake utategemea na hali halisi ya wakati tuliopo.
2. Mahakama ya kadhi italeta mgogoro wa kikatiba. Katiba inatoa uhuru wa kuabudu lakini inakataza vyombo vya kidini kuwa sehemu ya serikali. Hivyo kabla ya muswada wa mahakama ya kadhi kujadiliwa inatakiwa muswada wa kurekebisha katiba la sivyo mjadala wa muswada wa kadhi utakuwa kinyume cha katiba.
3. Kuwa na parallel legal system ni kosa kikatiba. Sheria zitakazosimamiwa na mahakama ya kadhi zinafaa kujumusihwa katika mfumo wa sheria Tanzania na sio kuundiwa a parallel legal system.
4. Mahakama ya Kadhi iundwe kama taasisi ya dini ya kiislam, na sio taasisi ya kiserikali. Mfano wakatoliki wana internal judiciary system ambayo inaanzia parokia mpaka Vatican na inasimamiwa na viongozi wa dini hiyo. Wanahukumu kwa kufuata canonical law. Kwa hiyo waislam nao waunde system kama hiyo ya ndani. Wahukumiane huko kwa kufuata misingi ya imani yao.
5. Mahakama ya Kadhi itatengeneza precedent isiyofaa maana watu wa imani zingine nao wanaweza kujenga hoja kuwa wawe na mahakama zao kama ya kadhi.
6. Endapo mahakama itaundwa Jaji Mkuu wake atateuliwa na Raisi, je endapo Raisi atakuwa sio Mwislam, waislamu watakuwa tayari Jaji ateuliwe na Kaffir?
 
Mimi niko SIDE B on this one! Sioni mantiki ya kuwa na mahakama ya kadhi kwa nchi isiyo na dini! Hoja zinazotolewa na walioko SIDE A hazina mvuto na zinaonekana kujengwa na wabunge wasio mahiri.Waziri mkuu alilitolea suala hili majibu mazuri sana na aliizungumzia issue ya kenya kuwa na kadhi kwa upana na kwakweli nilimuelewa na nilifikiri na wabunge wengi walimuelewa pia lakini naona wanatafuta cheap popularity kwa mgongo wa mahakama ya kadhi kama ambavyo sisiemu walivyoitumia kwenye ilani yao kwaajili ya kupata kura 'kula' katika uchaguzi wa mwaka 2005.
 
katiba yetu hairuhusu. nashangaa hata hao wabunge kama huwa wanasoma katiba kwa makini. rais ameshindwa kuitetea na kuilinda katiba kabisa
 
Mimi niko SIDE B on this one! Sioni mantiki ya kuwa na mahakama ya kadhi kwa nchi isiyo na dini! Hoja zinazotolewa na walioko SIDE A hazina mvuto na zinaonekana kujengwa na wabunge wasio mahiri.Waziri mkuu alilitolea suala hili majibu mazuri sana na aliizungumzia issue ya kenya kuwa na kadhi kwa upana na kwakweli nilimuelewa na nilifikiri na wabunge wengi walimuelewa pia lakini naona wanatafuta cheap popularity kwa mgongo wa mahakama ya kadhi kama ambavyo sisiemu walivyoitumia kwenye ilani yao kwaajili ya kupata kura 'kula' katika uchaguzi wa mwaka 2005.

Na mimi naunga mkono upande uliochagua. Kwa mtu yeyote mwenye kuelewa ni wapi tulikotoka na wapi tunaelekea atakubaliana nami kuwa KUNDI B lina sababu za msinji kabisa.

Kifupi ni kwamba Mwinyi alianza kuua umoja wa kitaifa kwa kuruhusu kutambulika watu kiimani na hiyo ililte migogoro mingi ya kidini na hasa katika mwaka wa 1994 ambapo kulikuwa na hali mbaya ya chuki za kidini na katika mwaka huo mkutano wa kitaifa wa UKWATA uliahirishwa baada ya njama za kuwachoma wanafunzi wakristo kwenye mkutano huo kugundulika. Hali ni mbaya sana kwani kuruhusu mavazi yanayotambulika kidini katika shule za msingi na sekondari nacho kilikuwa kitu kibaya kwani kilitugawa watanzania kidini. Kuna mambo mengi mabaya yamejitokeza kutokana na maamuzi mabaya yasiyojali hali halisi.

Na sasa watu wanataka kwenda mbali zaidi ya hapo kwa kuangalia watoke vipi na wao wasikike. Hili la KADHI ni bora waachiwe walionalo na sisi tuendelee na misingi tuliyoijenga tangu mwanzo.
 
Back
Top Bottom