Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

JK hana hoja, hili swala limemshinda. Anasema sio lake wakati yeye ni Mwenyekiti wa CCM na wakati huo huo lipo kwenye ilani ya uchaguzi ya 2005. Anaposema atatimiza ilani ya uchaguzi hajui kwamba moja wapo ni la kadhi? Maelezo yake ni upupu, hakuna la maana. Nilifikiri atasimama na kusema swala la kadhi HALINA MJADALA AU LIJADILIWE ? HAWEZI KUKWEPA HATA KIDOGO. Kesho atatuambia kuwa CCM sio ya kwake kwa kuwa iliundwa wakati wa Nyerere na sio yeye.
 
Kwamba ilani ilitungwa na kina Mkapa na Ngombale Mwilu,
Kwa maana hiyo hapaswi kulaumiwa katika hilo?

Kaanza kuikana ilani, yeye kama yeye anatekeleza aliyotumwa na nani kama hazingatii yaliyo kwenye ilani ya chama chake?
Alikuwa akijinadi kutumia nini?
Hivyo basi, aeleze aliyoyatunga yeye kwenye ilani ayatekeleze na mengine atutangazie kuwa hayo hayamhusu na asipotekeleza asilaumiwe!!!!!

Rais wetu amezidi kulalamika badala ya kutatua matatizo!
 
Mengi muhimu yamechambuliwa na wanaJF kwa upeo mkubwa.It is very unfortunate.Haya majibu ya huyu bwana yamenisikitisha sana binafsi.Inafanya nizidi kuondoa hata kale kaimani kadogo kalikosalia kuhusu utafutaji wa suluhu kwa mambo mazito yanayokabili taifa kwa sasa.Those answers are too cheap when someone analyses just by using a common sense.
 
Nadhani Rais ambaye kwa dini ni mwislamu alilazimika kuonyesha mbele ya jamii ya wakristo kwamba chimbuko la wazo lenyewe lilitoka wapi? Na sasa nini kinafanyika, kwa mkristo wa kawaida anadhani hili linakuja kwa kuwa rais ni mwislamu.

Ilikuwa ni muhimu kuonyesha kwamba yeye sio mwasisi wa hiyo mahakama ya kadhi... Lakini hata hivyo hebu tuangalie CCM iliahidi nini?

Sura ya Nane "MAENEO MENGINE MUHIMU", IBARA 108 (b) ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2005. inasema na ninanukuu!!!


Ukisoma vizuri hii sio ahadi kwamba Mahakama ya Kadhi itaanzishwa; hii ni ahadi kwamba suala hili litajadiliwa, litachambuliwa na kwa pamoja kuwa na msimamo mmoja na kuweza aidha kuanzisha au kutoanzisha, huu ndio uelewa wangu, naomba musome hayo maneno ya Ilani ya Uchaguzi hapo juu!!!

Na kwa kweli nadhani mchakato ulishaanza ikiwa ni pamoja na tume ya kurekebisha sheria kuwa hiyo ni agenda yao... what else was needed guys!!!

Sasa tume haijasema kitu... ndio hivyo tena ramli zimeanza... au hili suala mlitaka JF ndio wapewe walifanyie kazi?



Kulipatia ufumbuzi maana yake ni kutatua tatizo sio kulizungumza,

Huyu JK anaonyesha alivyo na uwezo mdogo, pia serikali ya awamu ya nne wanaonyesha jinsi walivyo na ubongo mdogo, kwani wakati wa tatizo la umemem LOWASSA alisema kuwa hilo sio tatizo la serikali yao ila lilitokana na awamu ya tatu.

Leo JK naye anasema kuwa hilo sio la kwake, hapa kuna tatizo la kimsingi kama JK haijui ilani iliyomweka madarakani ,basi hawezi kamwe kuitekeleza na hivyo hafai kuendelea kutekeleza kitu ambacho hakijui ama hajashiriki kukiandaa,

Namlaumu rais wetu kwa kusema kitu ambacho ni zaidi ya uwongo kwani alishawahi kusema kuwa atatekeleza ahadi zote zilizoko kwenye ilani ya CCM na zile alizoziita ahadi za papo kwa hapo.

Mahakama ya kadhi ni ahadi ya ccm kama zilivyo ahadi nyingine , na kama tukisema kuwa hii sio ahadi basi hakuna haja ya kudai ahadi nyingine zitekelezwe kwani pia zimo ndani ya ilani.

Kusema ni hoja ya Mrema ni kufilisika kimawazo, na je?Mrema alishiriki kuandaa ilani ya CCM? ama yeye ni consultannce wa CCM?

Mwenyekiti wa ccm hana budi kufafanua kuwa ilikuwaje hoja ya mrema ikaingizwa kwenye ilani ,wakati yeye kwa wakati huo alikuwa ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM aseme kuwa hajui na hakushiriki kuandaa ilani wakati wao ndio walipitisha ilani hiyo?

Inamaana kuwa vikao vya ccm alikuwa anaenda kusinzia ama alikuwa anafuata nini hadi asikijue kitu alichokuwa anakipitisha kwenye vikao?

Naendelea kuuona uwezo wa ubongo wa rais wetu na majukumu tuliyompa naona hawezi kama huku ndio kufikiri kwake na kuona hii ni kauli ya kutoa mbele ya maaskofu na waumini wa kkt basi kuna haja ya uchunguzi wa kina juuu ya uwezo wake.
 
Ukweli ni kwamba JK yuko ktk wakati mgumu sana ndipo kujua na kukumbuka maneno ya Mwalimu 'ikulu si pahala pa kukimbilia' Wakristu wana baraza lao la usuruhishi kuhusu suala la ndoa, mirathi, na makosa mengine na linaongowa na Mchungaji wa kanisa hilo au Padri au Paroko. Hivi hamkuwahi kusikia yule mwimbaji alinyimwa unyumba ni mkewe alienda wapi kama si kwa Baba Paroko? Hivyo kuna mambo mengi tu yanatatuliwa kabla ya kufika mahakamani na bila kudai yawe ktk katiba

Kule kijijini kesi yoyote kufika mahakani na marachache sana nyingi zinaishia ktk mabaraza ya wazee tu na hakuna gharama zozote kutoka kwa serikali

Hivi sungusungu ilianzishwa kikatiba?

Ilikuwa inapata pesa/ruzuku serikalini?

Lakini ilikuwa inatoa hukumu tena kali mno kwa wale walio aware na kazi za sungusungu hasa wale wa kanda ya magharibi ilifanya kazi moja nzuri sana ya kukomesha wizi hasa ng'ombe waliokuwa wanaibiwa hata mchana kweupe maeneo yale miaka ya 80's.

Hivyo suala la kadhi linaweza kuanzishwa tu ndani ya uislam bila hata kuihusisha serikali kama wanavyofanya wakina baba paroko ktk Ukristu. likahudumia waumini wake watakao kuwa wanahitaji kesi yao isikilizwe ktk kadhi court. Na asiyehitaji aende mahakama ya serikali kama hata wakristo leo hii wanavyofanya. Mfano mingi ipo ktk ukristo kuwa mume akimshtaki mkewe kwa paroko watakutanishwa wote wawili kwa usuluhishi kama hatakubali mmoja wao wanaadhabu zao ikiwa ni pamoja na kutengwa ndani ya kanisa. Atakuwa hapati huduma za kiroho kifungo ambacho kinauma sana hasa kama alikuwa ni muumini wa kweli.

Hivyo mimi nashauri hii mahakama ianzishwe kama taasisi ndani ya uislamu na ili iweze kuhudumia waumini wake ktk matatizo ambayo yanawaumiza hata bila kuihusisha serikali na wananchi wengine wasio waislamu. Nani alikuwa anajua kama ktk ukristo kuna mahakama na jaji ni mchungaji au paroko? kama si yule muimbaji alipoimba wimbo wa baba paroko?
 
Tatizo ni kwamba umenukuu ya mbele yaliyotangulia ukayaacha.

Alichotangulia kusema ni kuwa suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi si lake binafsi bali la chama na ilani hakuiandika yeye.

Hivyo kama atatekeleza hilo atakuwa akitekeleza ilani ya chama chake. Hakuna mahala alipotamka,au kumaanisha, kuikana Ilani ya chama chake.

Kwa kifupi alikuwa anawajibu wale wanaotaka kumuhusisha yeye binafsi kama Rais Muislam na suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi.
Nungunungu! Ka-kana ushiriki Inakuwaje hivyo? basi hata hayo matamshi aliyotowa atakuja kukana aseme secretary wake kaandika na hakushirikishwa!! ebo!

Yote tisa lakini kutokujua hiyo ilani itasema nini..
...“Ndugu zangu napenda mtambue kuwa, mgombea urais ahusiki na uandaaji wa Ilani, wala ahusishwi… nawasihi tu tuwe watulivu na tuiache kamati ifanye kazi yake, ni watu wenye busara, naamini hawatafanya maamuzi mabaya,” alisema.
Yaani I can't figaa aut!
 
mie na uhakika kwa kauli hii,Lazima kamati kuu ya chama tawala imhoji Rais?inakuwaje akubali kutelekelza ilani ya chama na leo aseme kuwa hausiki,Kisa kuondoa hoja ya kudhania kwamba yeye kama Muislamu atahakikisha mahakama ya kadhi inakuwapo..
Hoja ni kwamba je suala la kadhi litaingilia Katiba yetu?tatizo Muungwana amekuwa mtu wa blah blah,Hajibu hoja kwa hoja,anajibu hoja kwa vioja..angalia sual la Mafisadi,ALijibu nini?
 
Yaelekea Tume itatoa maoni yake hapo februari 2008.Lakini ingelikuwa ni jambo la maana pia kupata mawazo kutoka kwa watanznia wenyewe hapa nchini.
 
Safi Sana Mahakama Ya Kadhi Kuundwa Sio Lazima Kushirikisha Serikali ..hatuwezi Kuipatia Union Seal Na Bajeti Au Kuitambua Kikatiba Wakati Katiba Inasema Nchi Yetu Haina Dini....mahakama Iwepo Tu Ndani Ya Misikiti Lakini Adhabu Zake Haziwezi Kutekelezwa Na Serikali....na Wala Hawawezi Kutoa Adhabu Zinazovuka Mipaka Au Kuvunja Haki Za Binadamu..

Hata Makanisani Kuna Mabaraza Ya Usuluhishi..mbona Hayaombi Kutambulika Kiserikali...hata Mabohora Na Hindu Nao Wana Utaratibu Wao Wa Kushitakiana Usio Husisha Serikali..hata Vijijini Tunayo Mabaraza Ya Jadi Na Mila..so Why Care About Kadhi...let Them Waazishe ,ili Mradi Haituhusu Wengine
 
Jk aache mzaha,hili suala si la kisiasa kama anavyotaka kulifanya.
Ni nani aliyemtuma kuidaka hii hoja na kuifanya mtaji wa kisiasa.Sasa hapo inabidi acheze kama Pele otherwise hili suala litafikia hatua limwelemee au aache mzigo kwa serikali zijazo.
Kama leo hii kuna doa tayari ktk uhusianao wa wakristo na waislam.It will be nonesense kwa Prezzo kuanza kutoa lawama kwa Mrema ili hali yeye kama aliona si sahihi alikua na option ya kuachana nalo.Kwa mfano nimuulize leo hii anijibu kwa macho makavu kabisa,JE wewe mheshimiwa Rais suala la mahakama ya kadhi lina umuhimu wowote au la? Hapo sasa ndipo nitakapoaanza kumjengea hoja
 
Hili suala sio gumu kama watu wengi hapa wanavyotaka kulifanya na jibu lake ni simple . Kwa nini tunaogopa kuiangalia katiba yetu inasema nini kuhusu hiyo ishu , majibu yapo kwenye katiba tuache bla bla !

With all due respect naipinga hoja ya JK , simply kwa sababu hakutunga hiyo ilani aimaniishi ya kuwa tutakuwa free pass, mbona wakati wa kampeni hukusema hayo maneno . Wakati ule wimbo ulikuwa ilani yetu ni bora kuliko wapinzani, sasa kuna flaws kwenye hiyo ilani anajaribu kukwepa swali . Tatu nashindwa kabisa kuelewa correlation kati ya Mrema na ilani ya CCM...................
 
Ila naona ni lesson nzuri sana kwake,kwamba ikulu si lelemama na mahali pa kukimbilia.Ule usemi wa ndege mjanja hunasa tundu bovu unajidhihirisha taratibu.Tuona atakavyojinasua
 
Huyu Rais wetu bwana, yaani mpaka tutachoka kumchambua. Yaani alienda kwenye uchaguzi kuuza ilani ambayo yeye mwenyewe haiamini ay ndio anataka kutuambia nini? Hoja ilikuwa ya Mrema, so? More questions than answers.Anatia huruma sana kwa kweli.
 
huyu jamaa uwezo wake mdogo sana kichwani kuwa Raisi wetu!
 
Ila naona ni lesson nzuri sana kwake,kwamba ikulu si lelemama na mahali pa kukimbilia.Ule usemi wa ndege mjanja hunasa tundu bovu unajidhihirisha taratibu.Tuona atakavyojinasua


Huyu mshikaji kweli amenasa, na sioni atatokea wapi? Labda mkuu FMES anajua!
 
huyu jamaa uwezo wake mdogo sana kichwani kuwa Raisi wetu!


Yeap! Kuna watu tulisema sana hili wakati wa mchakato wa kugombea ndani ya CCM kule bcs, lakini tulizomewa sana! Natamani zile posts kama zingerudishwa hapa. Nakumbuka niliandika article moja iliyosema "Sababu 15 kwa nini CCM wamteua SAL", Mashambulizi yaliyotoka ndani ya bcs yalokuwa mazito. Two years down the line, sysmpathisers wa huyu mshikaji ndani ya hizi forum sasa nafikiri hawafiki 1/8! Yes, today, here we are, our worries about this gentleman's capacity to lead our country are being confirmed day after day!
 
Naona sisiemu wameondoa faili la ilani hii katika tovuti yao, kwani kiungo chake ni hiki, http://ccmtz.org/documents/ilani.pdf. Siku chache zilizopita niliona kipengele cha mahakama ya kadhi katika ilani hii, lakini kwa kuwa lengo langu halikuwa kuangalia mahakama ya kadhi, sikutilia maanani umuhimu wa kusoma kipande hicho. Ningependa kama kuna yeyote mwenye hio ilani katika soft copy anitumie nami nisome kwa undani kilichomo. Natanguliza shukrani kwa wana JF.
 
mie na uhakika kwa kauli hii,Lazima kamati kuu ya chama tawala imhoji Rais?inakuwaje akubali kutelekelza ilani ya chama na leo aseme kuwa hausiki,Kisa kuondoa hoja ya kudhania kwamba yeye kama Muislamu atahakikisha mahakama ya kadhi inakuwapo..
Hoja ni kwamba je suala la kadhi litaingilia Katiba yetu?tatizo Muungwana amekuwa mtu wa blah blah,Hajibu hoja kwa hoja,anajibu hoja kwa vioja..angalia sual la Mafisadi,ALijibu nini?


There you are.
Nadhani washauri wa muungwana wana mushkeli kidogo. Sishangai muungwana kujibu suala la kadhi kuisanii sanii na vioja, kwani ni kawaida yake. Akiwa Norway, alisema kuwa Watanzania tunasaini mikataba ya ajabu ajabu kwa sababu hatuna wataalamu wa sheria wa kuangalia mikataba hiyo. Hapa juzi aliulizwa kuwa 'Kwa nini Tanzania masikini hadi leo, miaka zaidi ya 40 baada ya uhuru'? Akajibu kuwa hajui sababu. Sasa mtu wa namna hii anaposema kuwa suala la mahakama ya kadhi lilianzishwa na Mrema sishangai sana, maana jamaa ni mkwepa hoja aliyekubuhu. Sasa kama hajui chanzo cha umasikini wa waswahili, yuko pale ikulu kufanya nini?
Tunaomba afafanue hoja hii ya mahakama ya kadhi kwa undani kama waa JF mahiri walivyochambua hapo juu, kwani suala hili liko katika ilani iliyomweka madarakani.
 
Hata wakiiondoa kwenye soft copy bado ipo kwenye hardcopy na tunazo.

ama kweli Ukitaka kujua Tanzania na watanzania angalia viongozi wake , hivi Shein naye hakushirikishwa kuandaa ilani?kwani huyu alikuwa mtaalamu wa kukariri ilani wakati wa mchakato, hebu naye ajitokeze kumwokoa JK kwani hawezi kujinasua pekeyake tena.
 
Back
Top Bottom