Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Kithuku,
Labda wanasheria mnisaidie hapa. Kama tatizo ni kutambulika kisheria kwa hukumu za kidini, hivi hakuna kipengele chochote cha sheria zilizopo kinachowapa waislamu uhuru wa kutatua migogoro mbalimbali kidini, na kwamba hukumu zake zinakubalika kisheria mradi zisiwe kiyume na katiba ya nchi? Kama hakipo basi kiwekwe kipengele hicho ambacho kitawawezesha kuanzisha mahakama hiyo kama mojawapo ya taasisi zake, ielezwe inashughulikia kesi zipi,na utaratibu wa rufaa uwekwe, na itajwe kwamba waislamu wenyewe watagharamia mahakama hiyo kama wanavyogharamia taasisi zao nyingine. Mimi nilidhani utaratibu wa kutatua migogoro kwa taratibu za kidini upo nchini, na asiyeridhika na utaratibu wa kidini anafungua kesi rasmi mahakamani

Mzee wangu haya ndio maneno ya kiutu uzima unakata issue na sio kujenga chuki hali swala hili dogo sana. Korti za kadhi hazifai lakini kuna solution gani?... hakuna mtu alokuja hapa akaweka vitu sawa kama wewe hata kama kuna mtu hakubaliani nawe budi atupe sababu zake ama solution nyingine badala ya kupinga tuu hali mzigo bado upo mabegani mwetu.
Shukran...
 
leo nimeamini huyu kikwete ni zero tena ni sifuri kubwa na ni mbabaishaji number moja,hii kitu kikatiba hairuhusiwi fullstop na hivyo visingizio vya wakristo hawataki hiyo court kwa sababu ya gharama ni uwongo mkubwa sana huo,ukweli hawataki kwa sababu moja tuu UDINI au kwa lugha nyingine uislam(in this case) kuingizwa katika moja ya vyombo muhimu sana katika mfumo wetu wa kiutawala(Judicial)...na msijidanganye hapo watu hawatakubali hata kwa dawa na wata fight this tooth & nail kuona hii kitu haiendi popote,na huyu kikwete mwache alege lege na hapa ndio atagundua watu hawana michezo na issue kama hizi...eti Mrema? can you believe that? kama mafisadi walichukiwa sasa hapa cha mtema kuni watakiona kutuletea huu upuuzi!
 
Ukibishana na watu wenye IQ ndogo utapata taabu. Court of Arbitration haitoi maamuzi ya kumpa mtu adhabu. Hiyo ni kazi za mahakama ya kiserikali. Kwanza pande zinazohusika ni lazima zikubaliane kutumia hiyo mahakama na kukubali uhamuzi huo. Kwa mfano kwenye masuala ya ndoa au mirathi.

Ukiwa marekani kuna judge Judy, Judge Mathis, Joe Brown na Divorce court wanaendesha mahakama zao kwenye TV na watu wakipata burudani. Unafikiri wanachofanya pale ni mchezo wa kuigiza. Wanachofanya ni kutoa maamuzi ambayo pande zinazohusika watayakubali.

Au unaposikia pande mbili zimekubaliana kupata usuluhishi nje ya mahakama unafiriki wanafanya vipi?
 
Kisiasa naweza kusema CCM imeonyesha wazi kwama sera nyingi ama hata mawazo mengi ya wapinzani hutumika moja kwa moja ama kwa namna ambayo wao wakiifanya sera haiwezi kutekelezeka .Tumekuwa tukisema kwamba CCM haina sera ial za kuokota na kuzifanya sera while they know nothing about implemention .Leo mmeona wenyewe .Haiwezi kuingia akilini mwenzako aseme neno wewe ulichukue na hata kuliingiza kwenye maandishi. Kisa unataka ushindi wa kishindo no .

JK anajibu hoja hii kanisani badala ya kujibia kule alikokuwa anaombea kura na kuwaahidi ?Jamani Mzee JK get serious at least once
 
Nadhani kitu ambacho JK amekosea hapa ni kuanza kutupiana mpira, nadhani angelichukulia hili jambo kama rais. Wakati mwingine najiuliza uwezo wake kama rais. Mh. Rais kama hujui, mambo yote yaliyofanywa na serikali zilizopita you are responsible nayo. Nyerere aliongea kitu cha maana sana, unapoingia madarakani unachukua yale mazuri na kuacha mabaya na tunazidi kwenda mbele. Sasa wewe unaanza mara Kingunge hana dini, mara Mrema.. who cares.
Kwa upande mwingine naona watu mnachanganya kati sera na Ilani. Hii kitu iko kwenye Ilani ya uchaguzi 2005-2010 na siyo sera za CCM. Ilani imeeleza simple and clear kwamba CCM itaisisitizia Serikali kulipatia ufumbuzi suala ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania bara. Haijasema itaanzisha au itailazimisha serikali. You tell me what's wrong na kutafutia ufumbuzi?
 
sam that is a great point na ndiyo niliiweka kwenye sehemu ya kwanza ya makala yangu ile kuwa sijui ni nani alisoma ilani hiyo. Hakuna mahali ambapo CCM imesema itarudisha mahakama ya Kadhi na nikaonesha hata mawaziri wawili wa sheria chini ya JK wote walirudia kauli hiyo hiyo.
 
Nadhani Rais ambaye kwa dini ni mwislamu alilazimika kuonyesha mbele ya jamii ya wakristo kwamba chimbuko la wazo lenyewe lilitoka wapi? Na sasa nini kinafanyika, kwa mkristo wa kawaida anadhani hili linakuja kwa kuwa rais ni mwislamu.

Ilikuwa ni muhimu kuonyesha kwamba yeye sio mwasisi wa hiyo mahakama ya kadhi... Lakini hata hivyo hebu tuangalie CCM iliahidi nini?

Sura ya Nane "MAENEO MENGINE MUHIMU", IBARA 108 (b) ya Ilani ya Uchaguzi wa CCM 2005. inasema na ninanukuu!!!
b. Kulipatia Ufumbuzi suala la kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi Tanzania Bara.

Ukisoma vizuri hii sio ahadi kwamba Mahakama ya Kadhi itaanzishwa; hii ni ahadi kwamba suala hili litajadiliwa, litachambuliwa na kwa pamoja kuwa na msimamo mmoja na kuweza aidha kuanzisha au kutoanzisha, huu ndio uelewa wangu, naomba musome hayo maneno ya Ilani ya Uchaguzi hapo juu!!!

Na kwa kweli nadhani mchakato ulishaanza ikiwa ni pamoja na tume ya kurekebisha sheria kuwa hiyo ni agenda yao... what else was needed guys!!!

Sasa tume haijasema kitu... ndio hivyo tena ramli zimeanza... au hili suala mlitaka JF ndio wapewe walifanyie kazi?
 
CCM wao wakona wazo limeanzishwa na upinzani na kama linaonekana kuwa na lengo la kuvuta wapiga kura Bai CCM huirukia tu na kusahua kuwa CCM ni chama tawala na kuingiza kwenye ilani yake ni karibu sana na kuingiza kwenye katiba ya nchi!

UHUNI HUU ULISABABISHWA NA MKAPA AMBAYE KAMA MWENYEKITI WA CHAMA TAWALA ALISHINDWA KUONA MADHARA YA KUINGIZA MAHAKAMA YA KADHI KATIKA ILANI YAKE!

NI UHUNI ULE ULE ALIOUFANYA WA KUCHUKUA MAJENGO YA SERIKALI MOROGORO NA KUKABIDHI KUNDI FULANI LA DINI FULANI SIMPLY TU KWA KUWAFURAHISHA ILI CHAMA CHAKE KIPATE KURA!!

HUYU MKAPA IKITOKEA VURUGU KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTU ITABIDI AWAJIBIKE MHUNI MKUBWA HUYU!

SASA WAO WANAANZA KUSEMA LILIKUWA SUALA LA MREMA!

HUYU MREMA ALIKUWA NI MHUNI LAKINI HAKUWA ANATAWALA NCHI KWA MSINGI WA KIAPO CHA KATIBA AMBAYAO NCHI YETU NI SECULAR.

CCM ACHENI KUVAMIA VAMIA AGENDA NA KUZIFANYA ZA CHAMA,

MARA UTASIKIA AKINA MAKAMBA OHHH ETI CHADEMA NI CHA KIFAMILIA JE CCM ILIYO NA MME MKE MTOTO NA WAJUKUU WOTE HUMO NA GENGE LA WATOTO WA WAKUBWA WA CCM NI CHAMA CHA UKOO!!!!!!!!!!

VIONGOZI WA CCM WAWE WANAFIJKIRIKA KABLA YA KUTAMKA, HASA MAKAMAB YOU HAVE AT LEAST TO TAKE A MINUTE TO THINK BEFORE YOU SAY A WORD.

CCM NI CHAMA TAWALA KWA HIYO VIONGOZI WAKE KUWENI MAKINI SANA
 
Kithuku,

Labda wanasheria mnisaidie hapa. Kama tatizo ni kutambulika kisheria kwa hukumu za kidini, hivi hakuna kipengele chochote cha sheria zilizopo kinachowapa waislamu uhuru wa kutatua migogoro mbalimbali kidini, na kwamba hukumu zake zinakubalika kisheria mradi zisiwe kiyume na katiba ya nchi? Kama hakipo basi kiwekwe kipengele hicho ambacho kitawawezesha kuanzisha mahakama hiyo kama mojawapo ya taasisi zake, ielezwe inashughulikia kesi zipi,na utaratibu wa rufaa uwekwe, na itajwe kwamba waislamu wenyewe watagharamia mahakama hiyo kama wanavyogharamia taasisi zao nyingine. Mimi nilidhani utaratibu wa kutatua migogoro kwa taratibu za kidini upo nchini, na asiyeridhika na utaratibu wa kidini anafungua kesi rasmi mahakamani.


Mzee wangu haya ndio maneno ya kiutu uzima unakata issue na sio kujenga chuki hali swala hili dogo sana. Korti za kadhi hazifai lakini kuna solution gani?... hakuna mtu alokuja hapa akaweka vitu sawa kama wewe hata kama kuna mtu hakubaliani nawe budi atupe sababu zake ama solution nyingine badala ya kupinga tuu hali mzigo bado upo mabegani mwetu.
Shukran...

Mkandara, Niko na wewe mkuu!!!


Waislamu ni watu huru, waanzishe mahakama hiyo kama sehemu ya kuwawezesha kufuata imani yao (ndivyo ninavyoelewa), kama suala ni kutambulika kisheria, basi itungwe sheria ya kutambua hukumu za mahakama hiyo kwa muktadha wa nchi isiyo na dini, yaani bila kuathiri wale wasio na dini hiyo, na utaratibu wa kukata rufaa.

Kithuku na Hili ndilo waislamu wanalolitaka nothing less nothing more!!! Mahakama ya kadhi haitashughulika na mambo ya Jinai, madawa ya kulevya, biashara etc...

Kwa maana nyingine ukiwa na mahakama ya kadhi inayotambulika,,, Mahakama kuu na ya Rufaa italazimika kuwa na watu wanayoielewa sheria za ndoa na mirathi za kiislamu,,, hivyo kuwezakuhudumia rufaa zitakazokatwa panapokuwa na umuhimu huo!!!

Swali:
ile haki ya katiba ya kukata rufaa unapoona hujatendewa haki na vyombo vingine, je ipo sasa? maana mahakama kuu na ya rufaa wakipatashauri la ndoa na mirathi za kiislamu inabidi warudishe kwa mashekhe,,, sasa haki wapi hapa?

Nchi haibadilishwi kuwa ya kidini, na wala sidhani kuna haja ya kuchokonoa katiba,,, ni sheria tu ya mahakama inaongezewa katawi, kama mlivyoongeza vitawi vya ardhi, etc etc... it is all about "recognition" sasa waumini watatumia kweli mahakama hiyo au la! hilo ni jambo lingine, lakini kumbukeni siku hizi watu wengi wanaenda bomani zaidi... na trend inaonyesha ongezeko,,, kwa hiyo Watanzania ni watu wazuri hakuna hidden agenda hapa.

Nadhani hatuelewani mambo madogo sana...as I said ni elimu kwa wote ndio muhimu.

Wakati mwingine solution ni kuendelea kuongea kwa miaka mitano kumi zaidi, provided waislamu wawaelimishe wenzao kwa nini ni muhimu na kwa kiasi gani haiwa-affect wengine wa imani nyingine
 
CCM wao wakona wazo limeanzishwa na upinzani na kama linaonekana kuwa na lengo la kuvuta wapiga kura Bai CCM huirukia tu na kusahua kuwa CCM ni chama tawala na kuingiza kwenye ilani yake ni karibu sana na kuingiza kwenye katiba ya nchi!

UHUNI HUU ULISABABISHWA NA MKAPA AMBAYE KAMA MWENYEKITI WA CHAMA TAWALA ALISHINDWA KUONA MADHARA YA KUINGIZA MAHAKAMA YA KADHI KATIKA ILANI YAKE!

NI UHUNI ULE ULE ALIOUFANYA WA KUCHUKUA MAJENGO YA SERIKALI MOROGORO NA KUKABIDHI KUNDI FULANI LA DINI FULANI SIMPLY TU KWA KUWAFURAHISHA ILI CHAMA CHAKE KIPATE KURA!!

HUYU MKAPA IKITOKEA VURUGU KATI YA WAISLAMU NA WAKRISTU ITABIDI AWAJIBIKE MHUNI MKUBWA HUYU!

SASA WAO WANAANZA KUSEMA LILIKUWA SUALA LA MREMA!

HUYU MREMA ALIKUWA NI MHUNI LAKINI HAKUWA ANATAWALA NCHI KWA MSINGI WA KIAPO CHA KATIBA AMBAYAO NCHI YETU NI SECULAR.

CCM ACHENI KUVAMIA VAMIA AGENDA NA KUZIFANYA ZA CHAMA,

MARA UTASIKIA AKINA MAKAMBA OHHH ETI CHADEMA NI CHA KIFAMILIA JE CCM ILIYO NA MME MKE MTOTO NA WAJUKUU WOTE HUMO NA GENGE LA WATOTO WA WAKUBWA WA CCM NI CHAMA CHA UKOO!!!!!!!!!!

VIONGOZI WA CCM WAWE WANAFIJKIRIKA KABLA YA KUTAMKA, HASA MAKAMAB YOU HAVE AT LEAST TO TAKE A MINUTE TO THINK BEFORE YOU SAY A WORD.

CCM NI CHAMA TAWALA KWA HIYO VIONGOZI WAKE KUWENI MAKINI SANA


Mkuu nadhani unaweza kufikisha ujumbe huo huo kwa kutumia maneno mengine kuliko hayo unayotumia. Haimaanishi usipo tumia maneno kama UHUNI etc ujumbe hautafika najua unapoit unatoa lakini inaweza kuwa na uzito huo huo au hata zaidi kama utatumia manuno ya kawaidi maana watu wakisoma wanaona imeandikwa ni mtu serious na si vinginevyo. Ni hayo tuu mkuu tuendelee kukata issue.
 
Mimi katika mtazamo wangu kipindi kile Mrema alipata umaarufu mkubwa kwa Jamii ya Waislamu kwa hoja ya kwamba atahakikisha Mahakama ya Kadhi inaanzishwa Tanzania tena akabeza kwamba haoni sababu kwanini Mahakama hii ilifutwa, kwa kufanya hivi aliweza kuwa na washabiki wengi sana na kwa kweli Mrema akawa vinywani mwa wengi. Baada ya kuona hilo CCM wakaona ni bora nao waingie katika staili ya namna hii kupigia debe Mahakama ya Kadhi ili kunyang'anya mashabiki waliokuwa kwa Mrema. Baada ya Mrema kutoka Bungeni suala la Mahakama ya Kadhi likaenda kwa serikali moja kwa moja. Nikisema Serikali nina maana ya CCM wa bila kuangaslia athari zake eti wakaliweka katika ILANI YAO. Na kwabahati kweli wakawini kuingia madarakani kwa ahadi nyingi ikiwamo KADHI KADHI. Hata hivyo suala hili ni wazi kabisa kwamba ikiwa litatekelezwa na CCM itakuwa ni kutekelezwa kwa ILANI yenyewe lakini pia ni kukiukwa kwa katiba kwasababu kwa kiasi fulani uendeshaji wa mahakama hizi litakuwa ni jukumu la serikali kitu kinachojikanganya kwa sababu serikali yetu haina dini (secular govnt. Kwa hiyo mgawanyiko huu kati ya wakristo na waislamu unasababishwa na serikali yenyewe kwa maana hii kuna kila sababu kwa serikali kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo.
 
Sihusiki na suala la Kadhi - JK

2007-11-12 08:38:01
Na Simon Mhina

Rais Jakaya Kikwete, `amenawa mikono` kuhusu sakata la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi Mkuu na kukumbusha kuwa suala hilo halikuanzishwa na serikali yake au yeye binafsi bali liliibuliwa na Mwenyekiti wa TLP, Mbunge wa Temeke Bw. Augustine Mrema.

Rais Kikwete ameyasema hayo jana wakati wa ibada maalum ya kusimika Mkuu mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Azania Front jijini Dar es Salaam.

Aidha alisema licha ya suala hilo (la Kadhi) kuonekana katika Ilani ya uchaguzi ya CCM iliyomwingiza madarakani kwa kishindo mwaka 2005, bado yeye hahusiki.

Alisema kwa mujibu wa taratibu za CCM mgombea hahusiki wala hashirikishwi katika kuandaa Ilani.

Alisema ilani ya uchaguzi huandaliwa mwaka mmoja kabla ya uchaguzi.

`Hii ina maana kwamba mgombea hashirikishwi kwenye kutunga ilani, ili asije akatunga mambo rahisi na kuyatekeleza, kisha akajipatia umaarufu wa bure.

Ilani ninayoitumikia sasa sio mimi niliyoiandaa, bali iliandaliwa na tume maalum,` alisema na kuongeza: `Mimi pale Jangwani wakati wa kuzindua kampeni, nilikabidhiwa na Mwenyekiti wa Taifa wakati ule mzee wetu Mkapa. Nasisitiza Ilani yetu hutungwa kabla ya mgombea hajajulikana.`

Akizungumzia historia ya sakata la kadhi, Rais Kikwete alisema chanzo chake ni wanasiasa.

`Hivi karibuni naziona dalili zinazoashiria kuwa tusipokuwa waangalifu upendo na mshikamano baina ya Waislam na Wakristo hapa nchini utaharibika.

Kiini cha hali hiyo ni matendo na kelele za baadhi ya wanasiasa na baadhi ya viongozi wa dini wa pande zote mbili kuhusu suala la mahakama ya kadhi.

Chimbuko la kinachoendelea ni bunge na muasisi wake alipokuwa Mbunge wa Temeke, wakati huo Bw. Lyatonga Mrema.` alisema.

Alisema baada ya Bw. Mrema kuliwasilisha Bungeni kama hoja binafsi, Spika alilitafakari kwa hekima.

Alisema hata baada ya Mrema kutoka bungeni, Mbunge kupitia chama chake cha TLP, Bw. Thomas Ngawaiya aliliendeleza.

`Spika wa wakati ule, Pius Msekwa, kwa busara zake akaona kwamba iwapo angeruhusu mjadala juu ya suala hilo bungeni, angebomoa badala ya kujenga. Akaamua kulipeleka kwenye kamati husika ile ya Katiba na sheria iliyokuwa inaongozwa na Athuman Janguo,` alisema.

Rais Kikwete alisema kwa niaba ya Bunge, Kamati ilifanya utafiti wa kina kwa kuzitembelea nchi kadhaa zenye wakristo na waislam ambazo zina mahakama hizo na kujionea jinsi zinavyofanya kazi na kwamba masuala yanayohusu waislam yanashughulikiwa vipi.

Alizitaja nchi hizo kuwa ni Kenya, Uganda na Afrika Kusini.
Alifafanua kwamba nchini Kenya Mahakama ya Kadhi ipo, hasa kwenye maeneo yenye waislam wengi, ilianzishwa enzi za ukoloni na inaendelea.

Alisema Uganda mahakama hiyo ipo kwenye |Katiba lakini haijaanzishwa.

Wakati Afrika kusini hakuna mahakama hiyo, lakini masuala ya waislam yamo katika sheria za nchi.

Alisema baada ya Kamati kwa niaba ya Bunge kukamilisha kazi yake, Spika aliwasilisha taarifa kwa serikali kwa ajili ya kuchukua hatua.

`Lakini na sisi serikali hatuwezi kuchukua suala hili hivi hivi tu, kwa vile tuna chombo chetu cha kujadili, kuhakiki na kutoa maamuzi kwa mambo ya kitaam kama hayo. Kwa hiyo suala hilo tukalikabidhi katika Tume ya kurekebisha sheria,` alisema.

Aliwataka watanzania hasa waumini wa dini za Kikristo na uislam kuwa watulivu ili kusubiri maelekezo na ushauri wa tume ya kurekebisha sheria juu ya suala hilo.

Alisema Tume hiyo itatoa hatima ya suala hilo kabla ya mwezi Februari mwakani.

Rais Kikwete alisema lengo la kuwataka wawe watulivi ni ili kuifanya tume hiyo itoe mapendekezo huru juu ya sakata la mahakama ya kadhi, bila kushinikizwa na upande wowote.

Hata hivyo alisisitiza kwamba uamuzi wowote utakaotolewa na Tume hiyo ni ule utakaokuwa na maslahi kwa taifa zima.

`Nasisitiza hili si jambo langu binafsi, mchakato wake niliukuta na sasa nauacha uendelee,` alisema.

Alisisitiza kwamba hakuna sababu ya watu kutokuwa na subira, kwa vile uamuzi wa suala hilo hautakuwa wa siri, wala wasiweke shinikizo katika hili bali waiache tume iendelee na kazi yake.

Rais Kikwete aliwaomba waumini wa madhehebu yote kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kuimarika nchini.

`Ni jambo lililo wazi kuwa amani na utulivu tulionao hapa nchini umetokana kwa kiwango fulani na juhudi zinazofanywa na Kanisa,` alisema

Jana, gazeti moja la kila siku (si Nipashe) lilidai kuwa Rais Kikwete, wakati huo akiwa mgombea, `inawezekana aliliweka suala hilo katika ilani yake ili kuhakikisha kuwa anapata kura nyingi kutoka kwa waumini wa dini ya Kiislamu..`

Rais Kikwete alimweleza Mkuu mpya wa KKKT, Askofu Alex Gehaz Malasusa, kwamba ni matumaini yake kwamba ataendelea kuliimarisha kanisa hilo na kuendeleza mema aliyoachiwa na mtangulizi wake, Askofu Samson Mushemba ambaye amestaafu.

Alisema serikali yake itaendelea kushirikiana na KKKT hasa katika kudumisha huduma za afya na elimu.

Akijibu hutuba hiyo, Akofu Mkuu Malasusa alisema: `Mheshimiwa Rais, suala la kadhi ni gumu sana, ni jambo nyeti ni uamuzi mgumu mno, lakini Kanisa litakuombea katika kipindi hiki.`

Hata hivyo, Askofu Malasusa alitaka umakini uwepo katika suala hilo na kuonya kwamba lisije likawa chanzo cha kufanya Tanzania kuzalisha wakimbizi. Alisisitiza kwamba mifano juu ya maafa ya migogoro ya kidini ipo.


SOURCE: Nipashe

JAMANI INAKUWAJE MKUU WA NCHI ASEME HAUSIKI? INAMAANA KAMA WANAO KAANZISHA KITU KATIKA FAMILIA BABA UTASEMA SIHUSIKI KWASABABU MWANAO ALIANZISHA?
 
Mie sikutegemea Rais kuendesha nchi kwa majungu na kupigana vijembe,tena katika jukwaa la kanisa??au ndio kujibu tuhuma za ufisadi.??nakubaliana na Mhe. Mwandosya kuwa Muungwana ana miaka mingine mitano,watu watamkataa.
 
Hapa Lilifafanuliwa vizuri zaidi

Uhusika wa Rais Kikwete na CCM

"Nathibitisha kwenu kuwa uanzishwaji wa mahakama hii si jambo langu, lilikuwepo kabla yangu na mchakato wake nimeukuta," alisema Rais Kikwete na kuongeza kuwa yeye ameuacha uendelee pale alipoukuta.

Kuhusu uanzishwaji huo kuwepo kenye Ilani ya uchaguzi ya CCM, Rais Kikwete alifafanua kwamba Ilani hiyo ilichofanya ni kutambua mchakato ulikuwepo na kuagiza Serikali yake kuufuatilia.

Alifafanua kuwa katika utaratibu wa utengenezaji wa Ilani wa CCM mgombea hahusiki na kwamba mchakato wa kutengeneza Ilani ya CCM inayotumika hivi sasa, ulianza kabla ya kujulikana kwa mgombea.

Aidha alibainisha kwamba Mwenyekiti wa Kamati ya kutengeneza Ilani ya CCM inayotumika hivi sasa alikuwa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru ambaye si muumini wa dini zinazohusika. Alirudia tena kuwa uamuzi hauta pendelea upande wowote.


SOURCE MAJIRA

Habari zaidi bofya hapa:
 
SIELEWI PIA MUHASHIMIWA RAISI anaposema waliotunga ilani ya ccm ni kina kingunge,mkapa na mangula..ilhal yeye aliposhinda kutetea kiti cha ccm aliahidi mbele ya wanachama na wananchi kuitetea ILANI...haiingii akilini kuanza kuihoji ilani leo ..kama aliona haitekelezeki na haiamini alikuwa na uamuzi mmoja tu KUTOGOMBEA..ANGEAWAACHIA KINA SALIM AU MWANDOSYA AMBAO WANA UWEZO SANA KULIKO YEYE ..ilani ilijulikana kwa wagombea wa ccm wote ..waliisoma ,wakaamini ndio wakaomba nafasi...HOJA YA KUSEMA ILANI HAKUANDAA YEYE NI YA KUWAKAMATA WATU WENYE UWEZO MDOGO WA KUCHAMBUA...

UTARATIBU WA KUANDAA ILANI NDANI YA CHAMA UNAJULIKANA ...ILANI YA MWAKA 1985..ALIYOIPOKEA MZEE MWINYI..ILIANDALIWA NA MWALIMU NA KINGUNGE,NA MWAKAWAGO[?}..hapo hatukumsikia mzee mwinyi akilalama kuwa ilani hakuandaa yeye ..alijitahidi alivyoweza ...ilipofika ILANI ya 1990...akaandaa mwenyewe..ILANI ya mwaka 1995 aliyoipokea mkapa aliandaa mzee mwinyi ,KINGUNGE...ET al..mkapa hakulalama..alatekeleza na mwaka 2000 akaandaa yake...

kwa hivyo ni UTOTO muhashimiwa saaana kuanza leo kulia oooh kuikana ILANI YA CCM..maana ukiikana sehemu tu ya ilani ni kama kuikana ilani yoote ...hivyo ina maana uliingia madarakani kutetea usichokiamini na ukijua HAUNAUWEZO ...mnaaza kuona namna ..people are not serious!!!!

he has been reduced to ZERO...and now here comes THE REALLY MUUNGWANA!!!!
 
SIELEWI PIA MUHASHIMIWA RAISI anaposema waliotunga ilani ya ccm ni kina kingunge,mkapa na mangula..ilhal yeye aliposhinda kutetea kiti cha ccm aliahidi mbele ya wanachama na wananchi kuitetea ILANI...haiingii akilini kuanza kuihoji ilani leo ..kama aliona haitekelezeki na haiamini alikuwa na uamuzi mmoja tu KUTOGOMBEA..ANGEAWAACHIA KINA SALIM AU MWANDOSYA AMBAO WANA UWEZO SANA KULIKO YEYE ..ilani ilijulikana kwa wagombea wa ccm wote ..waliisoma ,wakaamini ndio wakaomba nafasi...HOJA YA KUSEMA ILANI HAKUANDAA YEYE NI YA KUWAKAMATA WATU WENYE UWEZO MDOGO WA KUCHAMBUA...

UTARATIBU WA KUANDAA ILANI NDANI YA CHAMA UNAJULIKANA ...ILANI YA MWAKA 1985..ALIYOIPOKEA MZEE MWINYI..ILIANDALIWA NA MWALIMU NA KINGUNGE,NA MWAKAWAGO[?}..hapo hatukumsikia mzee mwinyi akilalama kuwa ilani hakuandaa yeye ..alijitahidi alivyoweza ...ilipofika ILANI ya 1990...akaandaa mwenyewe..ILANI ya mwaka 1995 aliyoipokea mkapa aliandaa mzee mwinyi ,KINGUNGE...ET al..mkapa hakulalama..alatekeleza na mwaka 2000 akaandaa yake...

kwa hivyo ni UTOTO muhashimiwa saaana kuanza leo kulia oooh kuikana ILANI YA CCM..maana ukiikana sehemu tu ya ilani ni kama kuikana ilani yoote ...hivyo ina maana uliingia madarakani kutetea usichokiamini na ukijua HAUNAUWEZO ...mnaaza kuona namna ..people are not serious!!!!

he has been reduced to ZERO...and now here comes THE REALLY MUUNGWANA!!!!
Kwa maelezo haya nikijitokeza hadharani leo kusema Muungwana ni Msanii na muhuni,Je nitafunguliwa mashataka ya uchochozi
 
Kama ningekuwa karibu na rais ningemshauri kitu kimoja tu, kwamba kuna information sio lazima kuzi-release to the public. Pamoja na kwamba ni za ukweli...

Lakini ningependa kuwa upande wake kama binadamu,,, kwa kuwa ingekuwa ni jambo rahisi sana kwa Rais Mkiristo kulielezea hili, lakini ni jambo gumu kidogo kwa President ambaye ni Muislamu na hili ndilo lililomkuta Rais wetu.
 
Kikwete ajitoa suala la Mahakama ya Kadhi

* Asema iliandaliwa na Mkapa, Mangula, Kingunge

na Agnes Yamo

RAIS Jakaya Kikwete, jana kwa mara ya kwanza alilizungumzia hadharani suala linalozidi kushamiri katika mijadala ya kijamii, la uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi, na kueleza kuwa hakuhusika kuliweka katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Ndugu zangu napenda mtambue kuwa, mgombea urais ahusiki na uandaaji wa Ilani, wala ahusishwi… nawasihi tu tuwe watulivu na tuiache kamati ifanye kazi yake, ni watu wenye busara, naamini hawatafanya maamuzi mabaya,” alisema.

Rais Kikwete aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akizungumza katika Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Alex Malasusa, katika Kanisa Kuu la Azania Front, Dar es Salaam.

Katika hotuba yake, Rais Kikwete alisema ameamua kulizungumza suala hilo kwa sababu ameziona dalili zinazoashiria kuwa “tusipokuwa waangalifu, upendo na mshikamano baina ya Waislamu na Wakristo hapa nchini utaharibika” kutokana na mjadala kuhusu Mahakama ya Kadhi.

Lakini aliwasihi Watanzania kuwa na subira kwa sababu suala hilo, ambalo mjadala wake unashika kasi, hatma yake itajulikana Februari mwakani, Tume ya Kurekebisha Sheria, itakapotoa ripoti yake.

Hata hivyo, Rais Kikwete alionekana kuwatupia lawama wanasiasa kuwa ndio wanaochochea suala hilo kutokana na manufaa yao binafsi.

Alisema kuwa kiini cha mjadala kuhusu Mahakama ya Kadhi ni wanasiasa.

“Chimbuko la kinachosemwa sasa kuhusu Mahakama ya Kadhi ni bungeni, na muasisi wa hoja hii ni Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema alipokuwa Mbunge wa Temeke.

“Bwana Mrema alikuja na hoja ya binafsi bungeni ya kutaka kuundwa kwa Mahakama ya Kadhi nchini,” alisema Rais Kikwete na kubainisha kuwa hoja hiyo iliungwa mkono na aliyekuwa Mbunge wa Bagamoyo wakati huo, marehemu Baruti Rajabu.

Alisema kuwa baadaye ikafuatiwa kwa nguvu na hoja binafsi ya aliyekuwa Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia TLP, Thomas Ngawaiya.

Alisema kwa busara za Spika wa kipindi hicho, Pius Msekwa, akisaidiwa na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni, Frederick Sumaye, ambaye alikuwa Waziri Mkuu, alikataa hoja hiyo kujadiliwa bungeni moja kwa moja kutokana na kile alichokitaja kuwa ni unyeti wake, na kuamua kuipeleka katika Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, ambako kamati hiyo iliongozwa na wenyeviti wawili tofauti, Arcado Ntagazwa ambaye alipoteuliwa kuwa waziri, nafasi hiyo ilishikwa na Athumani Janguo.

Alisema baada ya kamati hiyo kukamilisha utafiti na kukabidhi ripoti kwa Spika, aliikabidhi serikalini ambako inafanyiwa kazi ili kutoa ushauri upasao.

“Serikali imekabidhi Tume ya Kurekebisha Sheria kulifanyia kazi jambo hilo na kushauri ipasavyo. Tume inaendelea na kazi yake ya utafiti wa kina na kwa taarifa nilizonazo, huenda mwezi Februari mwakani watamaliza kazi yao ya utafiti na kuwa na lolote la kushauri,” alisema Kikwete.

Aliwahakikishia Watanzania kuwa serikali haitafanya uamuzi ambao hauna maslahi kwa nchi na wala jambo hilo halitaamuliwa kinyemela.

Alisema suala la Mahakama ya Kadhi si lake binafsi, na kuwa lilikuwepo kabla yake na mchakato wake ameukuta.

Aidha, alisema mchakato wa suala hilo haukuanza na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005, kama wengi wanavyodai na kuwa Ilani hiyo ya uchaguzi imeutambua mchakato huo kujipa dhima ya kuuendeleza ili kujaribu kutafuta ufumbuzi.

Akikanusha kuhusika kwake kuliweka suala hilo katika Ilani, alisema kuwa mchakato wa kuandika Ilani huanza kabla ya uteuzi wa mgombea urais.

“Ilani ilitayarishwa chini ya uongozi wa Mwenyekiti, Mheshimiwa Benjamin Mkapa (ambaye naye alikuwepo kwenye ibada hiyo), Katibu Mkuu, Philip Mangula na Mwenyekiti wa Kamati, Mheshimiwa Kingunge Ngombale Mwiru. Ilani iko hivi ili kumbana mgombea asijipendelee kuweka mambo mepesi ambayo ataweza kuyatekeleza,” alisema.

Kwa upande wake, katika salamu zake, Askofu mteule Alex Malasusa, alikemea tabia ya baadhi ya viongozi kuzungumzia masuala ya imani kwa lengo la kujitafutia umaarufu.

“Mambo yahusuyo imani yasizungumzwe kisiasa, na viongozi wanaopenda kupata umaarufu kupitia imani waache mara moja,” alisema Askofu Malasusa.

Akizungumzia suala la migogoro inayolikumba kanisa, Askofu Malasusa alisema kila mara anamuomba Mungu kuwezesha katika uongozi wake kuwe na mshikamano na amani miongoni mwa waumini na viongozi wa kanisa hilo.

“Naomba msamaha kwa wale wote waliokwazwa au kuumizwa katika migogoro iliyotokea katika kanisa letu, na nawaomba waliofungua kesi kuzifuta mara moja, ninatubu kwa ajili ya wote… watusamehe na tuanze upya,” alisema kwa masikitiko.

Awali, kanisa lilitoa zawadi ya gari, ng’ombe wa maziwa pamoja na fedha taslimu sh milioni 2.5, ikiwa ni shukrani kwa uongozi mzuri kwa Mkuu wa Kanisa mstaafu, Askofu Dk. Samson Mushemba, ambaye aliongoza kanisa hilo kwa miaka 15.

Akizungumza baada ya kupokea zawadi hizo, Dk. Mushemba alisema kanisa linapaswa kuwafundisha wananchi mbinu bora za kuinua maisha yao.

Kikwete ajitoa suala la Mahakama ya Kadhi
 
SIELEWI PIA MUHASHIMIWA RAISI anaposema waliotunga ilani ya ccm ni kina kingunge,mkapa na mangula

Tatizo ni kwamba umenukuu ya mbele yaliyotangulia ukayaacha.

Alichotangulia kusema ni kuwa suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi si lake binafsi bali la chama na ilani hakuiandika yeye.

Hivyo kama atatekeleza hilo atakuwa akitekeleza ilani ya chama chake. Hakuna mahala alipotamka,au kumaanisha, kuikana Ilani ya chama chake.

Kwa kifupi alikuwa anawajibu wale wanaotaka kumuhusisha yeye binafsi kama Rais Muislam na suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi.
 
Tatizo ni kwamba umenukuu ya mbele yaliyotangulia ukayaacha.

Alichotangulia kusema ni kuwa suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi si lake binafsi bali la chama na ilani hakuiandika yeye.

Hivyo kama atatekeleza hilo atakuwa akitekeleza ilani ya chama chake. Hakuna mahala alipotamka,au kumaanisha, kuikana Ilani ya chama chake.

Kwa kifupi alikuwa anawajibu wale wanaotaka kumuhusisha yeye binafsi kama Rais Muislam na suala la kuanzishwa mahakama ya kadhi.

Nungunungu,


Hapo ndipo watu wanataka kuchukulia advantage wakidhani, siasa mchezo mchafu bwana!!!
 
Back
Top Bottom