Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mkuu Mkandara,

Apo juu naona umeongelea mambo mengi kwa wakati mmoja...

HOja ya mabaraza ya jadi na mahakama ya kadhi...mi sijawahi kusikia katika ukoo wangu tukiitaka serikali itambue UWEPO wa baraza la ukoo, toofauti na hilo la mahakama ya kadhi,

Suala jingine ni kuwa hapa tunajadili hoja...na sio udini manake wengine hawana dini kabisa...kwa hiyo hatuongei kutokana na emotions zozote zile, no hoja kwa hoja

Jingine ni kuwa kama mswada inabidi upelekwe bungeni mkuu, utakwepaje kutumia gharama za serikali kuanzaia kuuandaaa hadi posho za wabunge watakaokaa kuujadili badala ya kujadili mambo mengine? (Hapa simaanishi kuwa hili halifai kujadiliwa)

Kwa hiyo japo sijaauona mswada wenyewe kuwa UNAOMBA FEDHA, ZA KUUENDESHA, akili yangu kidogo inanituma lazima kutakuwa na gharama zitakazobebwa na serikali ikiwa utapita katika mkondo huo!
 
Wazee naona tusi hesabu Vifaranga wakati Mayayi Bado haya jatotolewa.

So tutapigana bure au kuwekeana chuki na kuacha vitu vya msingi kwa sasa wakati hao wana siasa za hiyo Kadhi Court etc aidha wataiondoa kimya kimya au kuileta kwa njia mbadala , so mpaka hapo itakapo letwa naona tusubiri, ingawa kiongozi wetu Mpendwa naona ameshindwa Kujitetea Vizuri na Hiyo Mada ya Kadhi na kimsingizia Mrema, kisa ni kuwasikiliza baadhi ya watu wake wa karibu ambao si washauri wazuri.

sasa kutokana masomo aliyopata au matatizo mengi toka aingie madarakjani , ni vizuri akaachana na marafiki wa uongo, na ajifunze kutokana na makosa ya wale walio mtangulia.
Au awe anaomba ushauri wa kimya kimya kwa watu na kujaribu kuchambua mambo kabla ya kuyawasilisha Mbele ya Umma wa Kijamaa??

Au Jamii yetu ya Wadanganyika/watanzania.

Maana hata hiyo kadhi court yenyewe haijulikani kama itachukua sheria zote za Kiislamu au itakuwa Selective kwa yale mambo wanayo taka baadhi ya watu au baadhi yetu , nayo ni Mirathi na Sheria Ya Ndoa?

Na si ya Ugoni au ya Wizi?

Sasa tusubiri hayo Mapendekezo kama ni Total Islamic Law au Selective na Jinsi itakavyo endeshwa kwa kuchangiwa aidha na Serekali Kuu au Bakwata/Balukta/ Au Baraza la Kuendeleza Kuraani Tanzania na ita muhusu nani na inapotokea Mgongano aidha ya watu inakuwaje (btn Muislamu kwa Muislamu au Muislam na Mtu wa Madhehebu Mengine inakuwaje?
 
Baraza la ukoo ama Asili ni sawa kabisa na mahakama ya jadi isipokuwa tu ina deal na baadhi ya maswala madogo madogo. labda hili neno mahakam ya Kadhi ndio limewashtua lakini ndio kiswahili hicho hakuna neno dogo zaidi na huwa lina deal na ndoa, mirathi na mabo ya familia za kiislaam peke yake. Halivuki nje ya mipaka hiyo kama yalivyo mabaraza yetu na hata hao mabalozi wa nyumba kumi. Muhimu tu ni kwamba uamuzi wao huheshimiwa kisheria na hauwezi kufanya hivyo kama huwezi kuzitambua korti hizi kisheria.
Mwisho hiyo akili yako inavyokutuma ndivyo unavyozidi kupotosha Umma kwani kama ni dhana kwa nini usiiweke hadi pale utakapo kuwa na hakika?.... waislaam hawajaomba fedha wameomba korti zao sasa haya ya gharama yametoka wapi. Kuna muswada unaoweza kuzungumziwa bila gharma za watu kukaa na kuutazama?.. Guys tuwe na subira kidogo kuliko kuzua vitu, Tunaupotosha Umma.
 
Au kama kuna Mtu ana hiyo Paper au Dodoso la hiyo Kadhi Court basi iwekwe hapa tuweze kuijadili.
 
Mrema, Mtikila, JK wooote hawa ni wanasiasa na midomo yao sometimes haina break (simaanishi wasiwe responsible)...mimi naona cha msingi hasa ni kutafuta maandishi ya hiyo Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2005 ilisema nini hasa kuhusu Mahakama ya Kadhi...yaani word for word. Tutajua iwapo ilani ilisema Serikali ya CCM italeta mahakama ya kathi (katika mazingira yoyote) au Itafanya uchunguzi na kuamua uwezekano wa kuwepo mahakama ya kathi. Kama walisema tu watafanya uchunguzi then ndio sasa wanafanya na tume itakamilisha ripoti yake February kama JK alivyoaahidi (kwa maana nyingine wanatekeleza Ilani yao kwa wapiga kura). Kwa hiyo kabla ya kuanza kusema Mrema alisema au JK alisema na Mtikila hakusema kama wahuni wanapiga umbea mtaani. Mwenye Ilani ya CCM atuwekee hapa ili tujue kama ni JK na CCM ndio waliochemsha tumkome giladi hapa hapa forum.
 
Baraza la ukoo ama Asili ni sawa kabisa na mahakama ya jadi isipokuwa tu ina deal na baadhi ya maswala madogo madogo. labda hili neno mahakam ya Kadhi ndio limewashtua lakini ndio kiswahili hicho hakuna neno dogo zaidi na huwa lina deal na ndoa, mirathi na mabo ya familia za kiislaam peke yake. Halivuki nje ya mipaka hiyo kama yalivyo mabaraza yetu na hata hao mabalozi wa nyumba kumi. Muhimu tu ni kwamba uamuzi wao huheshimiwa kisheria na hauwezi kufanya hivyo kama huwezi kuzitambua korti hizi kisheria.
Mwisho hiyo akili yako inavyokutuma ndivyo unavyozidi kupotosha Umma kwani kama ni dhana kwa nini usiiweke hadi pale utakapo kuwa na hakika?.... waislaam hawajaomba fedha wameomba korti zao sasa haya ya gharama yametoka wapi. Kuna muswada unaoweza kuzungumziwa bila gharma za watu kukaa na kuutazama?.. Guys tuwe na subira kidogo kuliko kuzua vitu, Tunaupotosha Umma.

Mkuu Mkandara, heshima mbele tena,

Dhana kama dhana huwa zinajadiliwa mkuu, labda mimi sielewi, lakini nijuavyo dhana zipo na zinajadiliwa! Watu hawasubiri hadi wawe na uhakika nazo ndipo wazijadili, la msingi hapa ni kusema kuwa hii dhana ni halali au potofu/inakosa mashiko....

Apo pengine, mkuu, hizo gharama atazibeba nani mkuu kama unakubaliana na mimi kuwa zitakuwepo?

Na unaposema tunaupotosha umma, nadhani kuna haja ya kuwa makini kidogo mkuu, maana naona ni hitimisho ambalo PIA lingesubiri kidogo.
 
Mwisho hiyo akili yako inavyokutuma ndivyo unavyozidi kupotosha Umma kwani kama ni dhana kwa nini usiiweke hadi pale utakapo kuwa na hakika?.... waislaam hawajaomba fedha wameomba korti zao sasa haya ya gharama yametoka wapi. Kuna muswada unaoweza kuzungumziwa bila gharma za watu kukaa na kuutazama?.. Guys tuwe na subira kidogo kuliko kuzua vitu, Tunaupotosha Umma.


Bob

Nimekueelewa unavyosema tuwe na subira lakini nashindwa kukuelewa kabisa unaposema (on red notes). Wataombaje korti ambayo itakuwa part ya judicial system ya nchi halafu wakati huo huo wawe wanajitegemea...!!! Nani atayefanya kazi ya kusimamia maamuzi ya hiyo mahakama iwapo kama sio serikali ya watanzania wote kupitia walinda sheria zetu...sorry mkuu kwa mtazamo wako huo naona hii hoja wala haisimami.

 
YeboYebo,
Duh mjomba hata sijui nikujibu vipi maanake nakumbuka kuna mtu aliwahi niuliza Huyu JK anaweka sheria ya elimu ya shule za msingi kuwa bure nani atagharamia walimu na gharama za Private schools?...
Kifupi, mjomba weka hapa hiyo dossier tuitazame kisha tujadili....maswala ya gharama nimechoka nayo hata iwe kodi yako, mambo mangapi tunalipa kodi zetu kwa kugharamia wakimbizi, vita Uganda na sijui kuikomboa Africa isiwe deal lakini hili mnamchambua kama kuku wakati walaji sio nyie...
Fanya subira...ama nipe suluhisho la maswala niliyouliza.Sijaona mtu akisema kitu kuhusiana na maswali yangu isipokuwa tunazidi kubishana na kutoia hukumu tukitazama the cover of the the book.
Bakwata wameiunda serikali yeyewe mbali kabisa na matakwa ya waislaam wengi, gharama zake mnazipokea na hali waislaam wenyewe hawataki kuwekwa ktk kapu hili. haya nambieni hiyo Bakwata mbona haija utokomeza Ukristu ama kutugawanya.
 
Mkandara
Jamani UZALENDO UKO WAPI?

Mahakama zenyewe za kawaida hazitoshi kwa sababu uchumi wa nchi ni tata hizo PESA za kuanzisha Kadhi zitoke wapi?

Harufu kingine mnasahau kuwa mfano mie ni muislamu ikatokea mitafaruku ktk ndoa ambayo naona kabisa kadhi itaniazibu huoni ninaweza kuikana DINI ya kiislamu ili isihukumu kesi yangu au ndiyo maana mnaitafutia msemeno wa sheria?

Pia nimekuambia BAJETI YA TZ Zaidi ya 40% inategemea wahisani na wahisani hawa walio wengi hawako tayari kuona dau lao linahudumia KADHI tena wanaona ni kheri iliyo je ya mfisadi kuzifisadi pesa zao kuliko kwa pesa zao kuhudumia Kadhi.

ASIyefanya kazi asile ajira kwa mtindo huu harafu tutegemee uchumi kupaa mwendo wa rocket duuuuuuuu.

Acheni kumbabaisha RAis kwa kumshinikiza kwa vitu vya imani ,mnambabaisha wee mpaka ametereza akasema hiyo ni hoja ya MREMA Wa TLP Lakini imo ndani ya ilani ya CCM .

Tuweni wazalendo na NCHI YETU tuijengeni kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo.

Tanzania Masikini mno tena ya mwisho duniani pamoja na maliasili ya kutosha tuliyonayo badala ya KUTOKOMEZA nchi umasikini na ukiisha wala mahakama nyingi zitakosa waharifu UMASIKINI NDIO UNASABABISHA HADI KUFIKIRIA MAHAKAMA YA MIRATHI wewe ukiwa na ukwasi wa kutosha utafikiria kwenda kuhangaika na mahakama kweli?? kwa ajiri ya mirathi mbona ULAYA sijawahi kusikia watu wakigombea mirathi na kama ipo ni very rear.TAFUTENI UKWASI WENU SIO WA MIRATHI huu ndio unasababisha umasiki yani leo mtanzania akipata tatizo kitu cha kwanza kufikiri nani ndugu anazo anisaidie badala ya kufikiri kutatua tatizo,ama mwenye nazo akiumwa WATANZANIA wananza kushangiria na kusoma sheria jinsi ya kukwapua mali zake kwa njia ya mirathi 'NANI KATUROGA' .NDOA ni UTASHI wala si swala lakulazimishana,kama nimegoma kumpa mwezangu wa ndoa raha kitandani huwezi kunilazimisha kwa kuniundia mahakama badala yake ushauri tu unahitajika

MAHAKAMA ya kadhi kuwepo kisheria si sababu tu ya tofauti ya kidini ninaipinga bali ITS ILLOGICAL
 
katika siku ambazo jk ameongea UTUMBO ni leo.....sikumuelewa kabisa nadhani ana tatizo ..

1.it was untimely kuongelea ile ishu pale ..wana philosophy kwa kuchambua maneno yake pale watabaki na maswali mengi kuliko majibu...

2.JE UJUMBE WA RAIS KWA MAASKOFU NI UPI..KWAMBA HOJA YA KADHI HAKUIAZISHA YEYE MUISLAMU BALI NI MKRISTO AGUSTINO L MREMA??

3.ALIPOSEMA HOJA IMETUMIWA NA WANASIASA KWA MTAJI WA KISIASA ..ANA MAANA CCM WALIINGIZA KWENYE ILANI YAO ILI KUPATA KURA ZA WAISLAMU TU...KWA HIYO INA MAANA ILANI YA UCHAGUZI WA CCM NI YA UWONGO?? KWA MAANA YA KULENGA MAKUNDI MBALI MBALI KIMAHITAJI KWENYE ILANI ILI KUTOA AHADI ZA UWONGO KUPATIA KURA??

4.KAMA HOJA NI YA MREMA ...KWANI MREMA NDIO ALIYEANDAA ILANI YA CCM??

Ninachoweza kuona ni kuwa rais anatoa majibu mepesi kwenye hoja nzito na sasa AMEDHAMIRIA KU DIVERT ATTENTION YA WANANCHI KUTOKA KWENYE KUMDAI AHADI YA KADHI KUPELEKA MGONGANO KATI YA WAISLAMU NA MTIKILA NA MREMA ...WAKATI INGETAKIWA WAISLAMU WAMBANE YEYE ..WAKATI MUDA UNASOGEA ITAFIKA MWAKA 2010 ..AMBAPO CCM WATAAMUA KUIONDOA AHADI HII KWENYE ILANI..KWANI KIUKWELI HAITAWEZEKANA...NDIO MAANA AKASIMAMA MBELE YA MAASKOFU KUTUBU.KUWA HATAFANYA KINYEMELA[KUSILIMISHA NCHI]

kimsingi rais analeta siasa ...na kwa bahati mbaya waislamu watabaki wanawalaumu wakristo kama kikwazo cha kadhi badala ya kuilaumu CCM kwa kuwaghilibu kura zao kwa ahadi isisyotekelezeka..

Mikael,
You have gone too far, punguza jazba then rephrase your comments.
pole sana.
 
Nitavunjika mbavu pale Mrema akisema mimi niliposema hilo la Mahakama ya kadhi nilikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi...sasa sipo huko hebu nendeni mkamuulize James Mbatia wa NCCR.

Tafadhali mwenye maandishi ya Ilani ya CCM 2005 atuwekee hapa.
 
Nitavunjika mbavu pale Mrema akisema mimi niliposema hilo la Mahakama ya kadhi nilikuwa Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi...sasa sipo huko hebu nendeni mkamuulize James Mbatia wa NCCR.

Tafadhali mwenye maandishi ya Ilani ya CCM 2005 atuwekee hapa.

I love it, imebidi nicheke sana!
 
Mimi kwa mtazamo wangu nadhani turudi katika mstari mmoja kabla hatujaendelea kuchangia na kujibizana.
Kuna mtu yeyote ambaye anaweza kututundikia kazi lengwa za mahakama ya kadhi? na inatakiwa iwe na mfumo gani? na Je mipaka yake ni ipi?
Vinginevyo tutaogelea kama tuko bahari kuu pasi na kufika nchi kavu.
 
Mkandara
Jamani UZALENDO UKO WAPI?????

Acheni kumbabaisha RAis kwa kumshinikiza kwa vitu vya imani ,mnambabaisha wee mpaka ametereza akasema hiyo ni hoja ya MREMA Wa TLP Lakini imo ndani ya ilani ya CCM .

Ama kweli ukipenda chongo huita kengeza?

Hapo kababaishwa? mpaka kateleza..

Vipi alipo zunguka nchi nzima akiimba kwa nguvu zote kuombea kura 2005 napo alishinikizwa? alibabaishwa? aliteleza?? ama ndo hivo mzee wa ku cut toka kwa mrema na Kupaste CCM (kwikwi.. eti hoja ya Mrema?? duuu!!!)

Hili ni tatizo la Raisi wetu, Inabidi washauri wake wafanye kazi ya Ziada kumsaidia kuongea yasiyo na utata mbele ya umma! Naona haka ka ugonjwa?/katabia? kake ka kuongea mambo yanayo kinzana ama yanayo leta maswali zaidi ya majibu kana zidi kukua!
 
Habari hiyo kwenye Dailynews..

We shall consider national interest

DAILY NEWS Reporter
Daily News; Monday,November 12, 2007 @00:02


PRESIDENT Jakaya Kikwete has urged the people to be patient as the government deals with the question to either establish the Kadhi or Islamic Sharia law court in Tanzania or not.

Mr Kikwete, who was the Guest of Honour at the consecration of the new Head of the Evangelical Lutheran Church of Tanzania (ELCT), Bishop Alex Gehaz Malasusa (47), at the Azania Front Cathedral in Dar es Salaam yesterday, said the Kadhi Court issue if not handled carefully, threatened to divide Tanzanians.

“If not properly handled, the Kadhi Court question is likely to disrupt peace and harmony that the country has enjoyed for centuries to the envy of many other countries,

” said the president. But whatever decision is finally taken, the government will be guided by the need to uphold the national interest.

Tanzania has enjoyed peace and tranquillity by being unwaveringly a secular state.

The president said the issue was first taken to the National Assembly as a private motion by Mr Augustine Mrema when he was MP for Temeke on the Tanzania Labour Party (TLP) ticket, for what the opposition MP thought was high tide political popularity.

It was for the second time brought up as a private motion by Mr Thomas Ngawaiya, then TLP Moshi Rural MP.

The Speaker decided that the motion be discussed first by the Constitutional and Legal Committee then chaired by Mr Arcado Ntagazwa.

The committee recommended that the matter be dealt with by the Law Reform Commission.

The Commission will submit its report in February next year and its recommendations will be made public, the president said but the decision by the government, will take into consideration the public interest, the president emphasised.

In speeches later, outgoing ELCT Head, Dr Bishop Mushemba and Bishop Malasusa thanked the president for shedding light on a subject that exercised the minds of many people.

Bishop Thomas from the Great Lakes Diocese of Michigan, USA, who led the colourful service, said the role of the church was to preach the gospel, tell the truth (even if it hurts) to the authorities on issues of development of the economy, corruption and education.

He also said the church in Tanzania and Africa in general, should also tell the West--Europe and America-- about the importance of family values and speak out against moral decadence, homosexuality and corruption.

Bishop Malasusa took over the pastoral staff from Dr Bishop Mushemba who led the church in Tanzania for 15 years and weathered a lift of its own over the Mwanga versus Same Diocese issue, which threatened to divide the congregation.

Invited guests came from the Geneva-based World Council of Churches (WCC), Lutheran World Federation, Bishops from Rwanda, Malawi, Zambia, South Africa, USA, Canada, Germany and Sweden.

From home there were representatives from Tanzania Supreme Council of Muslims (BAKWATA), the Tanzania Episcopal Conference (TEC) and other Christian denominations.

Present also were retired President Benjamin Mkapa, a Catholic and Premier Edward Lowassa
.
Source link:Daily News.

SteveD.
 
Sio tatizo la Rais ila ni tatizo la sisi watu weusi kama alizunguka nchi nzima akiombea kura mbona hamukuhukumu kwenye kisadaku cha kura?

Kwa data zilizopo waisilamu hawavuki 32% ya watanzania wote kulikoni RWABUGIRI?

ALA!! wakati huo hamukusikia HILO LA KADHI leo ndio tunatoka usingizini??
Nasema tunamchanganya Rais kuanzia wa KRISTU kukubali kwenu wakati ule anapigia debe na mkampa kura nyingi leo hii mnageuka ni CONTRADICTIONS zisizo na msingi U -TURN ya namna hii hakuna maendeleo.

Waislamu nao wanashinikiza vitu visivyotekelezeka kwani kuanzisha mahakama ya urithi chini ya sheria kwa nchi masikini kama ile si sahihi na maana vitu vilivyojikita ktk UTASHI
. BADALA Ya kushinikiza tusongeshe gurudumu la maendeleo na hatimaye kila mmoja awe na maisha swafi sie tunang'ang'ania kwanza mahakama wakati hata mirathi hiyo yenyewe HATUNA

USIPOANA YA MUSA HAKIKA UTAONA YA ..............,

Leteni mijadala ya UTAIFA kujenga nchi yenu tufanyeni kazi kuijenga nchi .MASIKINI NCHI ILE watu wake sijui nini kimewapata .nchi tajiri watu wake choka mbaya wakiulizwa kulikoni eti RAis hana sera za kujenga TAifa .Rais atakuletea aje maisha bora bila ya kufanya kazi.

Hii Tanzania mkinipa mie urais nitawachapa viboko nikileta hoja yangu ya kuendeleza nchi ukaipinga lazima uwe na njia mbadala vinginevyo na kuchana viboko just kidding!!!
 
bandugu bapenzi, turudini kwenye ufisadi, hapa wanataka ku-play devide and rule vita ionekane ni ya wakristo kwa waislamu, mwizi anaondoka kiulaini, mkiguta , ndio kama yule jamaa wa rada alivyo potea.
na wevi wenyewe ni hao hao wakristo kwa waislamu , hata iwe kwa majina not active na hizo dini.
 
Labda wanasheria mnisaidie hapa. Kama tatizo ni kutambulika kisheria kwa hukumu za kidini, hivi hakuna kipengele chochote cha sheria zilizopo kinachowapa waislamu uhuru wa kutatua migogoro mbalimbali kidini, na kwamba hukumu zake zinakubalika kisheria mradi zisiwe kiyume na katiba ya nchi? Kama hakipo basi kiwekwe kipengele hicho ambacho kitawawezesha kuanzisha mahakama hiyo kama mojawapo ya taasisi zake, ielezwe inashughulikia kesi zipi,na utaratibu wa rufaa uwekwe, na itajwe kwamba waislamu wenyewe watagharamia mahakama hiyo kama wanavyogharamia taasisi zao nyingine. Mimi nilidhani utaratibu wa kutatua migogoro kwa taratibu za kidini upo nchini, na asiyeridhika na utaratibu wa kidini anafungua kesi rasmi mahakamani.

Waislamu ni watu huru, waanzishe mahakama hiyo kama sehemu ya kuwawezesha kufuata imani yao (ndivyo ninavyoelewa), kama suala ni kutambulika kisheria, basi itungwe sheria ya kutambua hukumu za mahakama hiyo kwa muktadha wa nchi isiyo na dini, yaani bila kuathiri wale wasio na dini hiyo, na utaratibu wa kukata rufaa.

Changamoto ninayoiona hapa ya kuwa na mahakama ya kidini katika nchi isiyo na dini ni uamuzi wa sheria ipi iko juu ya nyingine. Kimantiki, katiba ya nchi iko juu ya sheria zote. Kwa nchi za kiislamu kama Irani hilo sio tatizo kwa sababu katiba yao ni ya kiislamu, kwa hiyo kauli ya Ayatollah ni ya mwisho. Lakini hapa kwetu kwa mfano, mahakama ya kadhi ikitoa hukumu fulani halafu ikatokea mhusika mmoja wapo hakuridhika na akakata rufaa labda mahakama kuu (ambayo si ya kidini), nayo ikatengua hukumu ya mahakama ya kadhi, je hii si itakuwa sawa na kukashifu Uislamu? Kimantiki, ni kutumia sheria ya binadamu kutengua hukumu iliyotolewa kwa kutumia sheria ya Mungu, na hii ni kufuru. Na hapo hakuna amani tena. Kwa hiyo hao wanaopendekeza kuwapo kwa mahakama hii, walete rasimu ya sheria hiyo tuijadili, na waturidhishe jinsi watakavyoshughulikia mkanganyiko huu.
 
Kwanini kuna tatizo gani iwapo Mwizi kama JK, EL watakatwa mikono? Watu kama hao wanaoibia Taifa pesa hawafai kuwapeleka jela kwa sababu wanaliongezea taifa hasara.

................

Wakatoliki wanaoamini kuwa ndoa haiwezikutenganisha, wanaweza kuwa na mahakama yao pia. Nchi lazima iwe na flavor.

Nakubaliana na wewe kuwa wahalifu wanastahili adhabu, lakini kusema uwakate mikono kwa sababu kuwapeleka gerezani ni mzigo, ni wazi pia kuwa hata wakiwa kwenye jamii huku wamekatwa mikono mzigo uko palepale, la maana zaidi ni kuwapeleka mahali ambapo watatumikishwa ili kulinufaisha taifa.

Wakatoliki wakristo, wanatakiwa kufuata ya kaisari na ya mungu, haya ni mawili tofauti. Mahakama moja tu inatosha, hakuna haja ya mahakama ya kadhi ni kuleta confusion kwenye jamii. Ilituwe secular Tanzania, ni vema kuimarisha utaratibu wa sasa.
 
Back
Top Bottom