Ni lazima kwanza ufahamu tofauti za mahakama na kazi zake, kisha jenga hoja inayohusiana. Mahakama ya kadhi inalenga ku settle tofauti baina ya waumini wa kiislaam, na Sharia law ni kwa ajili ya Utawala mzima hivyo haichagui mhusika na kwa kuelewa hivyo hawawezi kuomba ujinga huo..
Sheria za kadhi zinalenga waumini wa dini hiyo pekee na hawa wazee waislaam wameweka hoja hii kwa kupima uzito tofauti wa hoja hizi mbili kulingana na nchi yetu.
Inashangaza sana unapouliza swali kuhusu kukatwa mikono mwizi na stoning wakati ukijua wazi hutakubaliana na wazo hilo..Na kama wakiweka utasema sana kuhusu ubaya wa Uislaam hali wezi walikatwa mikono ma stoning zilifanyika toka wakati wa Nuhu..
ma lawayer waliosign mikataba ya kifisadi almost wote ni wakristo
waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za kifisadi almsot wote wakristo
make up our own conclusion
Habari zinazoingia sasa hivi ni kuwa serikali imekubali kuanzishwa kwa mahakama za Kadhi na itazi gharamia
Naona sasa mkuu Game Theory, unakosa point na nidhamu kwenye kuheshimu dini za watu wengine, na hapa JF sio sehemu ya kudhalilisha dini nyingine. Hapa tunatoa arguments pekee. Tafadhali utashi wa mtu kwenye mambo anayoyafanya yasihusishwe na dini. Put respect before each other religion otherwise we can not tolerate this anymore.
Nitajie lawyer hata mmoja muislam aliyehusishwa na kesi za kifisadi
Kwani yule Mnkono ni Muislam?
hebu nipumzishe mie...mnataka sources from Masatu...vyenu mbona huwa hamtoi sources?
au ushasahau kuwa JF ni mabingwa wa exclusives?
Ummy Muya, Mwananchi, Julai 06, 2009.
MASHEIKH zaidi ya 400 jana walikutana kwenye Msikiti wa Mtoro wa jijini Dar es Salaam kuanza maombi maalum kwa siku arobaini mfululizo kumlilia Mungu ili atoe adhabu kwa wote walioshiriki kuwahadaa Waislamu.
Akisoma tamko mbele ya masheikh zaidi ya 400 waliowakilisha jumuiya mbalimbali za Kiislamu, Sheikh Mohamed Issa alisema Waislamu wamekerwa sana na kauli za viongozi wa serikali kuhusu kufuta hoja ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, ikiwemo kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
"Kwa mujibu wa waziri mkuu, Mahakama ya Kadhi italeta kuvunjiku kwa amani, jambo ambalo si kweli kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuvunjika kwa amani katika nchi tulizotaja na badala yake mahakama hizo zimeimarisha umoja, amani na upendo baina ya Waislamu na jamii nyingine," alisema.
"Natoa wito kwa Waislamu wote nchini kuondoa dhuluma hizo kwa mikono yetu wenyewe na njia moja wapo ni katika uchaguzi mkuu wa 2010 kwamba kura zetu zina thamani na ndio nguvu yetu dhidi ya dhuluma zinazofanywa na maadui wa Uislamu," alisema.
Sheikh Issa alisema kauli iliyotolewa bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kuwa Waislamu ni wengi nchini Afrika ya Kusini ni uongo na ukweli ni kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa mwaka 2007, Waislamu ni 772,678 kati ya watu 41,743,459. Alisema hiyo ni sawa na asilimia mbili.
Alisema waziri huyo ameacha kwa makusudi kutumia uzoefu wa nchi zinazofuata utawala wa sheria kama Tanzania na ambazo zina Mahakama za Kadhi na kutoa mfano Ethiopia ambayo alisema suala la Mahakama ya Kadhi lipo katika katiba ya mwaka 1994 kwa mfumo wa mahakama za mwanzo (Shariah) na mahakama za juu (Kadhi).
Wakati nchini Kenya mahakama ya kadhi iko katika kifungu cha 5 cha katiba ya mwanzo ya 1963 na ile ya 1967, nchini Uganda suala hilo limo kwenye katiba ya mwaka 1995 kifungu cha 129 na Gambia kifungu cha 120 (b). Alisema katika katiba ya Zanzibar ya 1997 suala hilo limo katika kifungu cha 100.
Sheikh Issa alisema kwa kuwa CCM imewahadaa Waislamu kwa kutumia ulaghai na ujanja wa maneno katika ilani yao ya uchaguzi ya 2005, wanalaani kitendo hicho.
Hata hivyo, kifungu namba 108 cha ilani ya CCM ya mwaka 2005 hakitoi ahadi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi bali kinaeleza kuwa suala hilo litashughulikiwa na kutolewa ufumbuzi. Chikawe aliliambia Bunge kuwa serikali imeamua kuingiza baadhi ya sheria za Kiislamu kwenye sheria za nchi badala ya kuanzisha mahakama hiyo.
"Tunalaani ulaghai huu wa kisiasa wa CCM na tunaahidi kutolaghaiwa tena na tunadhamiria kuipa CCM adhabu inayostahili na wote wanaowafanyia Waislamu kejeli katika uchaguzi ujao 2010," alisema.
"Sababu tunayo, nia tunayo na uwezo wa kufanya tunao na siku zote Allah (SW) amewaahidi waumini ushindi," alisema.
Alisema kwa kuwa serikali ya CCM imeonyesha dharau kubwa kwa Waislamu watafanya maombi hayo maalum, yanayojulikana kama Qunut, katika misikiti yote nchini kumuomba Mungu awaadhibu wale wote waliofikia maamuzi ya kuzikijeli sheria zake kwa kutaka zichanganywe na kanuni za binadamu.
"Tunaitaka serikali ibadili msimamo wake haraka iwezekanavyo la sivyo tutaandaa maandamano ya amani nchini nzima kudai haki yetu na kwa kuanzia maandamano hayo ya tutafanya Ijumaa sambamba na kongamano kubwa litakalojumuisha misikiti, jumuiya na taasisi mbalimbali za kiislamu za Dar es Salaam na mikoa jirani," alisema.
Aliongeza kusema: "Kusudio la serikali kutumia sheria iitwayo 'Islamic law (restatement) Act 1964 (Re 2002) ambayo waziri anatakiwa kutangaza katika gazeti la serikali mara kwa mara, ni jaribio la ukarabati wa sheria za Allah (SW) jambo ambalo Uislamu na Waislamu hawakubaliani nalo kamwe."
Nitajie lawyer hata mmoja muislam aliyehusishwa na kesi za kifisadi
Kwani yule Mnkono ni Muislam?
hebu nipumzishe mie...mnataka sources from Masatu...vyenu mbona huwa hamtoi sources?
au ushasahau kuwa JF ni mabingwa wa exclusives?
No two countries are the same. Sisi si Kenya, Ethiopia au Afrika ya Kusini. Si kila wafanyalo wao linatufaa sisi. Kwa mfano, Afrika ya Kusini ina lugha zaidi ya moja ya kitaifa. Sasa na sisi tuamue Kisukuma na Kichaga navyo viwe lugha za taifa? Afrika ya Kusini hawana Waziri Mkuu. Sasa na sisi tumfutilie mbali Mizengo Pinda? Kenya wana wagombea binafsi lakini sisi hatuna.
Kumwomba Mungu amwadhibu mwanadamu mwenzio ni inverse religion. Kumtakia mabaya mwezio ni kutompenda, na hicho ni kinyume cha sheria za Mungu! Sasa mkiombea Tanzania mabaya na ikapata mafuriko makubwa mtafurahi?
Kama mnaombea CCM mabaya mbona zaidi ya nusu ya CCM yenyewe ni Waislamu?
Nadhani umeshajibiwa kuwa mambo ya wataaluma ndg zetu mliegemea kwenye madrasa..sasa huko taaluma za uanasheria, utabibu etc zitapatikana wapi?..teh teh teh..
Waambie jamaa zako nao wafute ujinga kwanza ili wakae karibu na 'jikoni'..
My point hizi, hakuna relationship kati ya lawyer kuwa mkristo na matendo yake na miiko ya au imani ya KIKRISTO yenyewe. Hakuna sehemu ya vitabu vya KIKRISTO palipoandikwa kuwa lawyer MKRISTO amtetee fisadi au kiongozi wa serikali au kampuni yeyote ile muumini wa dini ya KIKRISTO afanye ufisadi, hakuna, hakuna. Huu ni utashi na tabia ya mtu mwenyewe. Labda nikuulize na wewe kwenye hayo au haya matukio ya UGAIDI,amabapo wafanyaji au watuhumiwa wakubwa ni waislamu. Je waislamu wanaelekezwa kwenye imani yao kuwa wao ndio pekee wafanye vitendo vya kigaidi ikiwa ni pamoja na kujitoa mhanga kwenye hadhara ya watu na kuua mamia na maelfu ya watu. The point is tabia ya mtu au kikundi cha watu isiwekwe au ku-draw its legitimacy kwenye imani ya dini zao.
kama ni kweli serikali imeridhia mahakama ya kadhi basi mwelekeo wa serikali yetu na watendaji wake sio mzuri
Serikari kama serikali ikiamua na kutangaza kitu ni vizuri ikawa na msimamamo kuhusu ilichokiamua.tumeona bungu likiondoa misaada ya kodi kwa mashirika ya dini,kelele zikapigwa na serikari ikasalimu amri na kurejesha misaada iyo.
Leo hii serikali inatangaza kuwa hapatakua na mahakama ya kadhi baada ya kelele inakubali,je tutafika wapi?
Kwa mtazamo wangu mimi,serikali isiwe inatangaza mambo bila kua na utafiti wa kina kama jambo ilo litakubalika kwenye jamii au la.Na ikitokea wameamua kutangaza basi wasimamie walichokitangaza kwani kwa mtindo huu serikali itakuja kua na wakati mgumu pale ikitangaza jambo la muhimu sana na wananchi wakalipinga kwani tumegundua kua watu wakipinga serikali inabadilika .ni hayo tu kwa leo.
kama ni kweli serikali imeridhia mahakama ya kadhi basi mwelekeo wa serikali yetu na watendaji wake sio mzuri
Serikari kama serikali ikiamua na kutangaza kitu ni vizuri ikawa na msimamamo kuhusu ilichokiamua.tumeona bungu likiondoa misaada ya kodi kwa mashirika ya dini,kelele zikapigwa na serikari ikasalimu amri na kurejesha misaada iyo.
Leo hii serikali inatangaza kuwa hapatakua na mahakama ya kadhi baada ya kelele inakubali,je tutafika wapi?
Kwa mtazamo wangu mimi,serikali isiwe inatangaza mambo bila kua na utafiti wa kina kama jambo ilo litakubalika kwenye jamii au la.Na ikitokea wameamua kutangaza basi wasimamie walichokitangaza kwani kwa mtindo huu serikali itakuja kua na wakati mgumu pale ikitangaza jambo la muhimu sana na wananchi wakalipinga kwani tumegundua kua watu wakipinga serikali inabadilika .ni hayo tu kwa leo.
Wewe kama nani hasa useme kwamba mahakama halitufai? kama augustino mkatoliki au kama nani? nduguNo two countries are the same. Sisi si Kenya, Ethiopia au Afrika ya Kusini. Si kila wafanyalo wao linatufaa sisi. Kwa mfano, Afrika ya Kusini ina lugha zaidi ya moja ya kitaifa. Sasa na sisi tuamue Kisukuma na Kichaga navyo viwe lugha za taifa? Afrika ya Kusini hawana Waziri Mkuu. Sasa na sisi tumfutilie mbali Mizengo Pinda? Kenya wana wagombea binafsi lakini sisi hatuna.
Kumwomba Mungu amwadhibu mwanadamu mwenzio ni inverse religion. Kumtakia mabaya mwezio ni kutompenda, na hicho ni kinyume cha sheria za Mungu! Sasa mkiombea Tanzania mabaya na ikapata mafuriko makubwa mtafurahi?
Kama mnaombea CCM mabaya mbona zaidi ya nusu ya CCM yenyewe ni Waislamu?
Of course mwelekeo wa serikali utakuwa mbaya...kwa sababu kidogo walichokiomba waislam wamekipata sasa nyinyi hilo hamlipendi
Hivi waislam wanefanya MoU kama kanisa mngesemaje maana hili roho inataka kuwatoka!