Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Wakulu wangu mimi naona hii mijadala iishe. Najua we have all said things out of the heat of debate but tusameheane. Tuvunje hizi kambi za sijui ukristo au uislamu. We are all Tanzanians. Mimi binafsi nasema kwa yoyote niliyemkosea au kumvunjia heshima anisamehe. I hope na mimi nita samehewa. For the sake of Tanzania let's end this debate. After all we are the United Republic of Tanzania. Not the Islamic Republic of Tanzania or the Christian Republic of Tanzania.
100% right. hapo umenena mkuu.naongezea pia...kila mtu apewe heshima, utu na haki yake ya kibanadamu, hakuna kundi moja kunyonya kundi lingine la watanzania kwakuwa wako wengi zaidi au kwakuwa wao ni weusi sana na weupe sana, au kwakuwa wao wanaenda kanisani au msikitini nk.
 
Ibada gani hiyo inahusu Mirathi na Ndoa tu? Masuala mengine vipi? Kwa nini msitekeleze maagizo yote ya Mola wenu na Mtume wenu? Kwa nini mchague baadhi tu ya kutekeleza huku sheria nyingine mnazikanyaga?

Unafiki mtupu!
Hizo kidogo maaskofu wameandika na kuvuruga mara nyingi, taratibu tunategemea progressively iwe yote....inshAllah. Hapa ndiyo utaona neema ya muumba wako ikienea!.
Unafiki ni msamiati kwa uislamu ndio hatuna MoU za siri ndugu kila kitu kiko hewani kila mtu anajadili..anapinga halafu anaachia mwenyewe...."you cannot resist the power"
 
Wakuu kwanza sitaki kukubali. Lakini kama ni kweli this is the lowest point of Pinda. I wonder why would he allow the country to have two legal systems. Wakristo nao wakianza kudai mahakama zao nadhani itakuwa ni wapagani tu watakao kwenda kwenye mahakama za kawaida. Ni ujinga mwingine unaotokea waziwazi na unapitishwa na watu wazima wenye akili timamu. Leo itasemwa itashughulikia mambo ya kidini tu, kesho itakuwani mambo yanahusu waumini wa dini ya kiislamu na kesho kutwa itakuwa hata wasio waislamu wanaoathiri mambo ya waislamu. Kimsingi ni kuwa huu ni mwazo wa Sharia law kuingia Tanzania. God forbid.
 
SIASA, SERIKALI NA Mahakama ya Kadhi

Kama ni kweli vyema. Kama sio kweli Waislamu harakati zinaendelea, sote Wakiristo na wasio na dini na wapenda haki tuko nyuma yenu. Maana tunajua mafaniko yenu ni mafanikio yetu pia.

KITENDO cha serikali kutaka kuichanganya hoja ya Kadhi na kazi za kiserikali isiyokuwa na dini ni kitendo cha dharau, kiburi na dhuluma kwa Waislamu.

Ni kitendo kinachoashiria kwamba sasa hivi serikali inafanya kazi zake kwa kuamrishwa na Maaskofu wa Kanisa Katoliki.

Kwa upande mmoja inawaheshimu viongozi fulani wa dini lakini kwa sababu inazojua imeamua kuwa ni kawaida yake kuwadharau viongozi wa dini ya Kiislamu.

Utawezaje kuingiza katika mchakato wa Mahakama ya Kadhi jambo jipya kabisa bila kuwashirikisha viongozi wa Kiislamu na kisha kuwashtukizia tena kwa kukosa heshima, utu na nidhamu kwa kulitangaza jambo lenyewe kwa kupitia bungeni kama vile viongozi hao wadini ni watoto tena wasiokwenda shule na wewe eti ndio unawaingiza darasani kwa mara ya kwanza. Hivi Waislamu wanakubali kudharauliwa kiasi hiki kwa kweli ? Kwanini ? Kwa vishilingi viwili vitatu vinavyoibwa na CCM kutoka kwenye BAJETI ZA UONGO NA KWELI AMBAZO HUANDALIWA ILI CCM ICHOTEWE FEDHA NA MAWAKALA WAKE KATIKA WIZARA NA TAASISI MBALIMBALI NCHINI ?

Kama ni hivyo basi kuanzia sasa waislamu wawe wanalipa kodi kwa Kanisa katoliki na sio kwa serikali maana mwenye sauti ya mwisho kwenye masuala ya nchi hii ni Kanisa katoliki na sio serikali na chama tawala.

Kuna maswali mengi ambayo Ndugu Mwanakijiji yanafaa pia kuulizwa ili tujue serikali inasimama wapi, mabwana zao wanasimama wapi na sisi Waislamu tunasimama wapi. Maswali hayo ni pamoja na:
-Unaweza ukachanganya kweli nyama ya nguruwe, mbwa na ya ng'ombe huku Muislamu akiona na akakubali kula chakula chako ?

-Serikali kwa hiyo kwa kuchanganya mahakama ya dini na ile ya serikali inakubaliana na Wakatoliki kuwa SERIKALI INA DINI SASA ?

-Kwamba viongozi wa CCM si tu ni wanafiki, waongo na wababaishaji ?

1. Viongozi wetu wa dini walishauriwa kabla ya kutangazwa na waziri bungeni?

2. Ni nani kashirikishwa miongoni mwa Waislamu ?

3. Je, wasio na elimu ya dini hapa Tanzania wanajifanya wana akili kuliko masheikh na maimamu wetu ?

4. Kuna Waisalimu walioulizwa kuafiki juu ya mapendekezo hayo ya serikali ?

5. Huu ni uamuzi wa serikali au wa Kanisa Katoliki Tanzania ?

6. CCM inaafiki juu ya kitendo hiki ?

7. Hii ina maana kama masuala ya Waislamu yataamuliwa na Mahakama za serikali kwamba kutakuwa na Jaji Mkuu na Majaji waislamu, mahakimu mfawidhi, mahakimu, waendesha mashtaka, mawakili na mapolisi Waislamu ili kufanikisha kazi za kitengo hicho kipya katika mahakama zetu ?

8. Je tunaweza kukataa sheria hii kibudu kwa waislamu wote kwa pamoja kusema hatukubali Mahakama ya Kadhi iwe ni choo au bafu katika Mahakama ya serikali ?

9. Je, ni lazima tuitegemee serikali kuiendesha Mahakama yetu ya Kadhi. Kwa hasira waliyo nayo Waislamu hatuwezi kupitisha fatwa kwamba kuanzia sasa kila mwenye uwezo achange kuanzia shilingi 100 kwenda juu kwa siku ili kuijaza Mahakama Huru ya Kadhi mapesa na ianze kufanya kazi kwa kupitia misikiti ya mitaa itakayochaguliwa; msikiti mmoja kitarafa , mwingine kiwillaya na mwingine kimkoa na wa juu kabisa kitaifa kwa minajili ya rufaa za mahakama huru ya kadhi ya Kiislamu Tanzannia?

10. Fatwa hiyo ifuatiwe na tamko kwamba Waislamu hawatatambua hukumu yoyote juu ya jambo la Kiislamu itakayoamuliwa na mahakama zisizo na baraka ya Waislamu?

11. Je, tunaweza katika miezi hii mitukufu kwa Waislamu kusomo visomo vya aina yote, kusali sala zote za kumkuribisha zaidi MM kwetu sisi na kuyafanya mambo yetu mepesi ?

12. Je, tunaweza kuiweka mikakati ya Waislamu kupiga kura kwa BLOCKS, kwa maana, Waislamu wakishampitisha mgombea mmoja waislamu wote walazimike kupiga kura ya pamoja kwa mtu huyo ?

13. Je, wakati haujafika wa kuwa na Magavana badala ya wakuu wa mikoa kama vile Marekani au Nigeria ili mikoa yenye waislamu wengi iwe na serikali zao za Kiislamu. Suala sio madaraka mikoani bali uhuru wa KILA MKOA KUJITAWALA WENYEWE KIUTAMADUNI, KIUCHUMI NA KIJAMII.

14. Je, wanasheria wetu wanasemaje kuhusu UWEZEKANO WA WAISLAMU KWENDA KUISHTAKI SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KWA KUWANYIMA HAKI YA KUABUDU KWA MUJIBU WA DINI NA VITABU VYAO VITAKATIFU ?
 
Wakuu kwanza sitaki kukubali. Lakini kama ni kweli this is the lowest point of Pinda. I wonder why would he allow the country to have two legal systems. Wakristo nao wakianza kudai mahakama zao nadhani itakuwa ni wapagani tu watakao kwenda kwenye mahakama za kawaida. Ni ujinga mwingine unaotokea waziwazi na unapitishwa na watu wazima wenye akili timamu. Leo itasemwa itashughulikia mambo ya kidini tu, kesho itakuwani mambo yanahusu waumini wa dini ya kiislamu na kesho kutwa itakuwa hata wasio waislamu wanaoathiri mambo ya waislamu. Kimsingi ni kuwa huu ni mwazo wa Sharia law kuingia Tanzania. God forbid.
Neither you nor Pinda can resist peoples justice... afterall who is pinda? what is he?
 
Kimsingi ni kuwa huu ni mwazo wa Sharia law kuingia Tanzania. God forbid.

Hili ulioliongea ni neno la busara.

Huko siku za nyuma hapa JF wakati tunajadili adhabu ya stoning n.k kwa ndugu zetu wasilamu niliwahi kuwapa challenge kama ifuatavyo:

1. Je sharia ni halali kutekelezwa au la?
2. Kama ni halali kwa nini hazifuatwi ipasavyo kila pahali duniani kwa kila aliye msilamu? kitimilifu?moja baada ya nyingine?
3. Iweje watu hawazifuati na bado wanajinadi usilamu?
4. Na kama hawa wanaong'ang'ania kufuata tu sehemu tu ya sharia kuhusu Ndoa na Mirathi, zile nyingine za kukatana mikono mnamwachia nani? Je huku si kumdhihaki aliyeagiza package nzima ya sharia?

Sikupatiwa majibu mujarabu bali ndg 'wanyenyekevu' waliamua kufungulia sewerage kupoteza lengo..lakini nilikwisha wasoma kuwa hawana majibu!

Sasa mindhali serikali imeanza kuzikubali hizi soft laws, tena imekubali kuzi-implement kwa gharama za dola..ni wazi mwanzo wa safari ni hatua..Sisi tusio wasilamu inabidi tufanye mitigative measures maana ndio hivo tunakula matunda ya kuchagua rais weak.
 
ma lawayer waliosign mikataba ya kifisadi almost wote ni wakristo
waliofikishwa mahakamani kwa tuhuma za kifisadi almsot wote wakristo
make up our own conclusion
Kwa sababu wasomi wengi ni wakristu, kwa hiyo possibilities za mtu kuwa katika post fulani serikalini na kwingineko kunakohitaji taaluma inawaangukia wakristu. Mara nyingi utakuta waislamu wanaongoza vilabu vya soka, ngumi, urembo na vinginevyo ambavyo havihitaji taaluma.
 
Mh..haya wajameni huku ndiko tulikofikia..
 
Pongezi zako zimekaa kinafiki zaidi kuliko hali halisi ilivyo...!

Kaka shusha muunkali hatwendi hivyo.
Tatizo hauja mwelewa mwkjj alivyosema.
Binafsi siwapi pongezi sababu maakama yenyewe ni nusu.
Wakulu wawaachie mahakama yao itatue matatizo yao yoote yaani mpaka jinai. Ili kesi zote zilizo maakamani zinazo muhusu mnyenyekevu ziamishiwe kwa kadhi.
Lakini kodi mwananchi isitumike tunapata huduma ktk uwiano sawa lakini tikianza kupata ktk uwiano usio sawa kutokana na tofauti za kidini haitakuwa haki.
Wakristo na waislam wakianzisha mahakama zao waumini wenyewe wagalamie mahitaji yote.
 
Hili ulioliongea ni neno la busara.

Huko siku za nyuma hapa JF wakati tunajadili adhabu ya stoning n.k kwa ndugu zetu wasilamu niliwahi kuwapa challenge kama ifuatavyo:

1. Je sharia ni halali kutekelezwa au la?
2. Kama ni halali kwa nini hazifuatwi ipasavyo kila pahali duniani kwa kila aliye msilamu? kitimilifu?moja baada ya nyingine?
3. Iweje watu hawazifuati na bado wanajinadi usilamu?
4. Na kama hawa wanaong'ang'ania kufuata tu sehemu tu ya sharia kuhusu Ndoa na Mirathi, zile nyingine za kukatana mikono mnamwachia nani? Je huku si kumdhihaki aliyeagiza package nzima ya sharia?

Sikupatiwa majibu mujarabu bali ndg 'wanyenyekevu' waliamua kufungulia sewerage kupoteza lengo..lakini nilikwisha wasoma kuwa hawana majibu!

Sasa mindhali serikali imeanza kuzikubali hizi soft laws, tena imekubali kuzi-implement kwa gharama za dola..ni wazi mwanzo wa safari ni hatua..Sisi tusio wasilamu inabidi tufanye mitigative measures maana ndio hivo tunakula matunda ya kuchagua rais weak.
Ninesema maelezo mengi uanyoandika ni vichekesho vitupu.. sasa kama Waioslaam wataomba Sharia law itumike upo huru kuikubali?..

Ni lazima kwanza ufahamu tofauti za mahakama na kazi zake, kisha jenga hoja inayohusiana. Mahakama ya kadhi inalenga ku settle tofauti baina ya waumini wa kiislaam, na Sharia law ni kwa ajili ya Utawala mzima hivyo haichagui mhusika na kwa kuelewa hivyo hawawezi kuomba ujinga huo..
Sheria za kadhi zinalenga waumini wa dini hiyo pekee na hawa wazee waislaam wameweka hoja hii kwa kupima uzito tofauti wa hoja hizi mbili kulingana na nchi yetu.
Inashangaza sana unapouliza swali kuhusu kukatwa mikono mwizi na stoning wakati ukijua wazi hutakubaliana na wazo hilo..Na kama wakiweka utasema sana kuhusu ubaya wa Uislaam hali wezi walikatwa mikono ma stoning zilifanyika toka wakati wa Nuhu..
Kweli kuna tofauti kubwa kati ya Uislaam na Ukristu, kwani kwenu mtu anaweza kuua akaenda kwa Padre kuungama akasamehewa hapa duniani na akhera lakini sii Waislaam ni lazima ufikishwe kwenye sheria(mahakamani). Ajabu wakristu mnalikubali mahakama ya jinai ambayo haipo ktk dini yenu..
Hivyo swali linakurudia wewe.. Kwanini mnakataa nusu sheria, msikatae kitu kizima?..
 
Last edited:
Kaka shusha muunkali hatwendi hivyo.
Tatizo hauja mwelewa mwkjj alivyosema.
Binafsi siwapi pongezi sababu maakama yenyewe ni nusu.
Wakulu wawaachie mahakama yao itatue matatizo yao yoote yaani mpaka jinai. Ili kesi zote zilizo maakamani zinazo muhusu mnyenyekevu ziamishiwe kwa kadhi.
Lakini kodi mwananchi isitumike tunapata huduma ktk uwiano sawa lakini tikianza kupata ktk uwiano usio sawa kutokana na tofauti za kidini haitakuwa haki.
Wakristo na waislam wakianzisha mahakama zao waumini wenyewe wagalamie mahitaji yote.
Ongera kwa kumuelewa!
 
Jana usiku (Tar.5 Julai) nilikuwa nikitazama TV, Channel 10, kipindi kinachoitwa Arrisaalah. Kabla ya mzungumzaji kuendelea na mada yake aliongea kwa kifupi kuhusu Mahakama ya Kadhi. Alisema ya kuwa kulikuwa na kikao kilishofanywa na Mhe. Pinda, Mhe. Chikawe, Mhe.Lukuvi na Wah. Masheikh zaidi ya 20. Matokeo ya kikao hicho ni kuwa Serikali imeridhia uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Lakini, masuala vipi Mahakama hiyo itaendeshwa, na nani watakuwa Makadhi, na pia kuhusu malipo/mishahara kwa hao Makadhi bado haijaamuliwa. Haya yatatafutiwa ufumbuzi katika vikao vitakavyokuwa vikiendelea kufanyika kati ya Serikali na Kamati itakayoundwa na Mhe. Mufti. Ndio habari hiyo niliyoisikia.
Mimi binafsi, sioni haja ya kuwazuia waislamu wasifanye tendo la ibada, kwani itakuwa ni kuwaindilia katika uhuru wao wa dini. Lakini, Serikali ya Tanzania isijihusishe kwa lolote, kwani Serikali haina Dini. Mhe. Mufti aunde tu kamati yake, na waanze utekelezaji hakuna mtu wa kuwazuia watu katika ibada zao. Serikali isijihusishe na mambo haya, isiingilie kamati itakayoundwa, na pia kamati hiyo isiingilie Serikali, labda tu kama itaonekana kuna uvunjaji wa sheria fulani fulani za nchi.
 
Kwa kuongezea tu nataka mfahamu kwamba wewe kama Mkristu ukiwa Saudia au kokote kule kwenye mahakama ya Kadhi, they will never touch kesi yako ya madai kama Urithi na kadhalika haiwahusu...lakini usiibe ukafikiri pia utatoka..
 
Ummy Muya, Mwananchi,
Julai 06, 2009.

MASHEIKH zaidi ya 400 jana walikutana kwenye Msikiti wa Mtoro wa jijini Dar es Salaam kuanza maombi maalum kwa siku arobaini mfululizo kumlilia Mungu ili atoe adhabu kwa wote walioshiriki kuwahadaa Waislamu.

Akisoma tamko mbele ya masheikh zaidi ya 400 waliowakilisha jumuiya mbalimbali za Kiislamu, Sheikh Mohamed Issa alisema Waislamu wamekerwa sana na kauli za viongozi wa serikali kuhusu kufuta hoja ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, ikiwemo kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

"Kwa mujibu wa waziri mkuu, Mahakama ya Kadhi italeta kuvunjiku kwa amani, jambo ambalo si kweli kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuvunjika kwa amani katika nchi tulizotaja na badala yake mahakama hizo zimeimarisha umoja, amani na upendo baina ya Waislamu na jamii nyingine," alisema.

"Natoa wito kwa Waislamu wote nchini kuondoa dhuluma hizo kwa mikono yetu wenyewe na njia moja wapo ni katika uchaguzi mkuu wa 2010 kwamba kura zetu zina thamani na ndio nguvu yetu dhidi ya dhuluma zinazofanywa na maadui wa Uislamu," alisema.

Sheikh Issa alisema kauli iliyotolewa bungeni na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kuwa Waislamu ni wengi nchini Afrika ya Kusini ni uongo na ukweli ni kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa mwaka 2007, Waislamu ni 772,678 kati ya watu 41,743,459. Alisema hiyo ni sawa na asilimia mbili.

Alisema waziri huyo ameacha kwa makusudi kutumia uzoefu wa nchi zinazofuata utawala wa sheria kama Tanzania na ambazo zina Mahakama za Kadhi na kutoa mfano Ethiopia ambayo alisema suala la Mahakama ya Kadhi lipo katika katiba ya mwaka 1994 kwa mfumo wa mahakama za mwanzo (Shariah) na mahakama za juu (Kadhi).

Wakati nchini Kenya mahakama ya kadhi iko katika kifungu cha 5 cha katiba ya mwanzo ya 1963 na ile ya 1967, nchini Uganda suala hilo limo kwenye katiba ya mwaka 1995 kifungu cha 129 na Gambia kifungu cha 120 (b). Alisema katika katiba ya Zanzibar ya 1997 suala hilo limo katika kifungu cha 100.

Sheikh Issa alisema kwa kuwa CCM imewahadaa Waislamu kwa kutumia ulaghai na ujanja wa maneno katika ilani yao ya uchaguzi ya 2005, wanalaani kitendo hicho.

Hata hivyo, kifungu namba 108 cha ilani ya CCM ya mwaka 2005 hakitoi ahadi ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi bali kinaeleza kuwa suala hilo litashughulikiwa na kutolewa ufumbuzi. Chikawe aliliambia Bunge kuwa serikali imeamua kuingiza baadhi ya sheria za Kiislamu kwenye sheria za nchi badala ya kuanzisha mahakama hiyo.

"Tunalaani ulaghai huu wa kisiasa wa CCM na tunaahidi kutolaghaiwa tena na tunadhamiria kuipa CCM adhabu inayostahili na wote wanaowafanyia Waislamu kejeli katika uchaguzi ujao 2010," alisema.

"Sababu tunayo, nia tunayo na uwezo wa kufanya tunao na siku zote Allah (SW) amewaahidi waumini ushindi," alisema.

Alisema kwa kuwa serikali ya CCM imeonyesha dharau kubwa kwa Waislamu watafanya maombi hayo maalum, yanayojulikana kama Qunut, katika misikiti yote nchini kumuomba Mungu awaadhibu wale wote waliofikia maamuzi ya kuzikijeli sheria zake kwa kutaka zichanganywe na kanuni za binadamu.

"Tunaitaka serikali ibadili msimamo wake haraka iwezekanavyo la sivyo tutaandaa maandamano ya amani nchini nzima kudai haki yetu na kwa kuanzia maandamano hayo ya tutafanya Ijumaa sambamba na kongamano kubwa litakalojumuisha misikiti, jumuiya na taasisi mbalimbali za kiislamu za Dar es Salaam na mikoa jirani," alisema.

Aliongeza kusema: "Kusudio la serikali kutumia sheria iitwayo 'Islamic law (restatement) Act 1964 (Re 2002) ambayo waziri anatakiwa kutangaza katika gazeti la serikali mara kwa mara, ni jaribio la ukarabati wa sheria za Allah (SW) jambo ambalo Uislamu na Waislamu hawakubaliani nalo kamwe."
 
No two countries are the same. Sisi si Kenya, Ethiopia au Afrika ya Kusini. Si kila wafanyalo wao linatufaa sisi. Kwa mfano, Afrika ya Kusini ina lugha zaidi ya moja ya kitaifa. Sasa na sisi tuamue Kisukuma na Kichaga navyo viwe lugha za taifa? Afrika ya Kusini hawana Waziri Mkuu. Sasa na sisi tumfutilie mbali Mizengo Pinda? Kenya wana wagombea binafsi lakini sisi hatuna.

Kumwomba Mungu amwadhibu mwanadamu mwenzio ni inverse religion. Kumtakia mabaya mwezio ni kutompenda, na hicho ni kinyume cha sheria za Mungu! Sasa mkiombea Tanzania mabaya na ikapata mafuriko makubwa mtafurahi?

Kama mnaombea CCM mabaya mbona zaidi ya nusu ya CCM yenyewe ni Waislamu?
 
Ninesema maelezo mengi uanyoandika ni vichekesho vitupu.. sasa kama Waioslaam wataomba Sharia law itumike upo huru kuikubali?..

Tuende taratibu..

Hivi hayo ulioandika hapo juu ni nini kama sio utumbo wa grade A? Halafu wasio wasilamu wanawezaje kuomba sharia law? as far as i can see wewe ni zoba na kichwa chako kimejaa matope na miugali iliyooza.
 
Ni lazima kwanza ufahamu tofauti za mahakama na kazi zake, kisha jenga hoja inayohusiana. Mahakama ya kadhi inalenga ku settle tofauti baina ya waumini wa kiislaam, na Sharia law ni kwa ajili ya Utawala mzima hivyo haichagui mhusika na kwa kuelewa hivyo hawawezi kuomba ujinga huo..

Lahaula lakwata!

Kwa hiyo sharia ya mnyaaaazi mngu wa kisilamu leo umekuwa ujinga? Ndo maana humu ndani hatutakaa tuelewane maana humu kuna watu wanakufuru mungu wao allah huku wakijiita wasilamu. Yaani kila kitu ni shaghalabaghala tu..
 
Jana usiku (Tar.5 Julai) nilikuwa nikitazama TV, Channel 10, kipindi kinachoitwa Arrisaalah. Kabla ya mzungumzaji kuendelea na mada yake aliongea kwa kifupi kuhusu Mahakama ya Kadhi. Alisema ya kuwa kulikuwa na kikao kilishofanywa na Mhe. Pinda, Mhe. Chikawe, Mhe.Lukuvi na Wah. Masheikh zaidi ya 20. Matokeo ya kikao hicho ni kuwa Serikali imeridhia uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Lakini, masuala vipi Mahakama hiyo itaendeshwa, na nani watakuwa Makadhi, na pia kuhusu malipo/mishahara kwa hao Makadhi bado haijaamuliwa. Haya yatatafutiwa ufumbuzi katika vikao vitakavyokuwa vikiendelea kufanyika kati ya Serikali na Kamati itakayoundwa na Mhe. Mufti. Ndio habari hiyo niliyoisikia.
Mimi binafsi, sioni haja ya kuwazuia waislamu wasifanye tendo la ibada, kwani itakuwa ni kuwaindilia katika uhuru wao wa dini. Lakini, Serikali ya Tanzania isijihusishe kwa lolote, kwani Serikali haina Dini. Mhe. Mufti aunde tu kamati yake, na waanze utekelezaji hakuna mtu wa kuwazuia watu katika ibada zao. Serikali isijihusishe na mambo haya, isiingilie kamati itakayoundwa, na pia kamati hiyo isiingilie Serikali, labda tu kama itaonekana kuna uvunjaji wa sheria fulani fulani za nchi.

mahakama ya kadhi sidhani kama ina maana yoyote kwa kuwa haki imekuwa ikitendeka kwa watu wote waislamu na dini nyingine kwa mambo yale yatakayofanywa na hiyo mahakama sheria ya ndoa,1971 iko wazi kwa dini zote katika talaka na pia mgawanyo wa mali ndo maana hata akina BIHAWA MOHAMED, walifanikiwa katika kesi zao na itakuwa vp kila dini ikitaka mhakama yake? ila kadri ya JALA marriage act,1971 will prevail in any matter
 
Jana usiku (Tar.5 Julai) nilikuwa nikitazama TV, Channel 10, kipindi kinachoitwa Arrisaalah. Kabla ya mzungumzaji kuendelea na mada yake aliongea kwa kifupi kuhusu Mahakama ya Kadhi. Alisema ya kuwa kulikuwa na kikao kilishofanywa na Mhe. Pinda, Mhe. Chikawe, Mhe.Lukuvi na Wah. Masheikh zaidi ya 20. Matokeo ya kikao hicho ni kuwa Serikali imeridhia uanzishwaji wa Mahakama ya Kadhi.
Lakini, masuala vipi Mahakama hiyo itaendeshwa, na nani watakuwa Makadhi, na pia kuhusu malipo/mishahara kwa hao Makadhi bado haijaamuliwa. Haya yatatafutiwa ufumbuzi katika vikao vitakavyokuwa vikiendelea kufanyika kati ya Serikali na Kamati itakayoundwa na Mhe. Mufti. Ndio habari hiyo niliyoisikia.
Mimi binafsi, sioni haja ya kuwazuia waislamu wasifanye tendo la ibada, kwani itakuwa ni kuwaindilia katika uhuru wao wa dini. Lakini, Serikali ya Tanzania isijihusishe kwa lolote, kwani Serikali haina Dini. Mhe. Mufti aunde tu kamati yake, na waanze utekelezaji hakuna mtu wa kuwazuia watu katika ibada zao. Serikali isijihusishe na mambo haya, isiingilie kamati itakayoundwa, na pia kamati hiyo isiingilie Serikali, labda tu kama itaonekana kuna uvunjaji wa sheria fulani fulani za nchi.

Fiction?
U-turn policy?
No Government under the sun can tolerate the kind of embarrassment, can the Tanzanian Government do?
 
Back
Top Bottom