kumbe mimi nilifikiri tunasheherekea mahakama kuruhusiwa ....kumbe kuna wenye mawazo tofauti waanafurahia kufikiri serikali itazigharamia.....hilo ni gumu sana...fikiria mara mbili !!
Ni lini serikali imegharamia pesa za kununua kanzu za watumishi kanisani ,kula au mishahara yao????........ pia makanisani kuna mabaraza ya usuluhishi ..hayagharamiwi na serikali...
nadhani watu wanachanganya mambo pengine...hasa kuhusu suala la hospitali za kanisa zinazohudumia wilayani [kama hospitali teule]..au za rufaa kama KCMC ,bugando...meta etc....hasa sehemu ambazo serikali haina hospitali..,[asilimia 40% ya health services].....wale wananchi wanaoishi huko wapo kwenye mipango ya afya ya nchi kwa hiyo lazima serikali ipeleke mgawo dawa..na vifaa ..ambavyo ni mgawo kwa kila wilaya...sasa kama wilaya ina hospitali teule ya misheni mnataka ikose mgawo huo....anayetaka kujenga mahospitali mikoani hajanyimwa!!
kwenye elimu ....serikali inatenga mgawo nafikiri dola 8 kwa elimu ya msingi...na kuongezeka sekondari,vyuo vya ufundi...stadi..,na mikopo ya chuo kikuu.....sasa kwa elimu ya msingi na sekondari serikali imejitosheleza...lakini kuna vyuo vikuu ,ualimu na ufundi vya kanisa ...serikali inatoa rusuku kwa wanafunzi....kupitia vyuo husika.....UTAFANANISHA HUDUMA AINA HIII NA MAHAKAMA YA KADHI!!
kubalini tu kuwa ili mahakama za kadhi ziwe indelevu lazima waumini waingie mifukoni...asiwadanganye mtu ndugu zangu!!!.....wala vijembe vya wenye wivu wakajinyonge hauna nafasi hapa...hakuna cha kuonea wivu!!