Kama wewe umeona gharama tu, basi kwa taarifa tu, waislamu, kuhusiana na mazungumzo yetu hapa, maana waislamu wa Tanzania, wakishikama tu na mafundisho ya Qur-ani na Sunna za Mtume Muhammad (S.A.W) wanaweza kuendesha sio hizi mahakama tu za kadhi, bali nchi yetu nzima, tena kwa uadilifu, haki, usawa na heshima. Lijue hilo na usiwe brain-wash na hawa wanaotandaza hofu na utawala wao wa vyombo vya uongo.
Wewe unajibana mwenyewe hapa. Kuwa waislamu waendeshe wenyewe hizi mahakama bila ya serikali kuidhinisha sio kujitenga na kuigawa nchi huko?? yaani waislamu na wasiokuwa waislamu. Na hili pia waislamu wanaliweza, unayo habari hiyo? Lakini je una maana kwako wewe ndio busara hiyo?
Ni wasiokuwa waislamu ambao hapa wanaonyesha kiburi na kutojali. Watanzania msiwe kama watu na serikali zisizo huru za magharibi. Au nanyi mmetiwa mikononi na Uzayuni. Wakistro wa Tanzania, mmelala??? wakati hata hao wenzenu wa magharibi wanaamka. Hebu angalia unavyoishi na huyo jirani yako hapo Manzese au Temeke, na hali ya kuwa dini zenu mbali mbali, sio ubinadamu huo?
Ulimwengu unabadilika, na Mahakama ya kadhi, kama independent body kudili na masuala ambayo purely ni ya kidini ni muhimu hata kwa hao waislamu ambao kutokana na ufinyu wao wa ilmu ya dini, au uhadaa wa dunia hawalioni hili. Waislamu hawaombi hili kwa wasiokuwa wasiokuwa waislamu bali ni haki yetu. Au ndio mmeshatiwa pomu mnapenda kuona waislamu loose control, sio busara ni upumbavu huo.
Nato hoja