Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Katika hili naipongeza serikali it was not fair kuchukua hela za walipa kodi kuhudumia jambo ambalo wengine haliwahusu chamsingi waislam watafute hela zao na kuanzisha mahakama yao bila kuihusisha serikali.Chuo cha Morogoro walipewa bure senti tano hawakutoa wakati kilikiwa ni chuo cha shirika la umma. not fair !!!
 
Kweli hapo mkanganyiko kwani serikali isema kuiweka sheria ya kiislam katika mahakama za inchi ?????????? To me it means hiyo ni tayari mahakama ya kadhi ambayo itakua inasimamiwa na----------------------------???????????

Amwanga,
Serikali ina ittelligency yake ambayo huishauri namna ya kumaliza mambo ki-silencer. Unakumbuka mwaka fulani waislamu walitaka kuwasomea albadri Mkapa na Sumaye? Jamaa waliwaambia wapuuzeni tu hawa jamaa (waislamu) wala msibishane nao. Na kweli waliwapuuza wala hakuna kitu kilichoendelea. Hii ya kusema serikali inta-integrate sheria za kiislamu kwenye sheria za nchi ni namna tu ya kuwapoza hawa waislamu ili mambo yaishe. Hakuna kitu kama hicho maana serikali inajua fika kwa kufanya hivyo wataibua mizozo mingine tena ya kidini. Tuombe uzima tuone kitakachoendelea.
 
Msimamo huo sio sahihi ,hili ni lazima mulielewe kilichopo hapa ni ahadi iliyotolewa na CCM kuwa watawapatia wapiga kura wao madai waliyoyataka ikiwa watawatilia kura sawa na kuahidi utawajengea daraja,utaweka maji bure,nyinyi mnaona sahihi lakini huu ni mtihani mkubwa kwa CCM na ni jambo ambalo linaweza kuwaangusha katika uchaguzi ujao ikiwa wapiga kura hao wataamua kuzipeleka kura zao kwengine japo wasipewe hayo madai yao,kama watazipeleka kura zao Chadema au CUF na kwengineko.
Tatizo wakristu mnalichukulia suala hili kama ushindi katika dini yenu lakini hatari ni pale Waislamu wote watakapoamua kuzipeleka kura zao kule wanakoona ndiko kwenye maslaha na dini yao hapo mtalia kilio cha mbwa mdomo juu ,najua mnadanganyika kuwa wakiristu ni wengi hapa Tz lakini kinyume chake Wakristu ni wachache tena wachache sana ,hilo halina ubishi wala mjadala ,endeleeni kuchochea.

Mwiba,
Tofautisha ahadi za kujenga madaraja, kutoa huduma za maji, kujenga barabara etc. na ahadi ya kuleta mahakama ya kadhi. Walioipigia kura CCM si waislamu peke yao na Wakristo kwa wingi pia. Kwahiyo ahadi hiyo ingekuwa na maana kama ingetolewa Iran na si Tanzania nchi isiyo ya kidini. Unaposema kuwa CCM itaanguka kama waislamu watainyima kura huo ni mtazamo wako wewe na watu wachache wa aina yako. Napenda ufahamu kuwa si waislamu wote wanaoitaka mahakama ya kadhi bali ni baadhi yenu tu hasa wanaume mnaojua fika kuwa mtafaidika nayo huku wanawake wakiteseka na kukosa haki zao kupitia mahakama hiyo. Lifahamu hilo pia.
 
Tatizo si serikali tatizo ni kwa waislamu wenyewe kuwa wanafiki katika masuala ya dini yao.Ukweli upo palepale kuwa waislam wengi walio katika madaraka ya uongozi uwe wa kidini au serikali ni wanafiki wakubwa na ndio chanzo cha kuwafanya wenzao kuwa duni hata katika imani yao.Angalia jinsi mashujaa wa kikristo walivyokuwa imara katika kutetea mambo yao,serikali kutaka kufuta misamaa ya kodi tuu wakatishia kujitoa sisieeem,serikali kwa kulijua hilo haraka ikarudisha misamaha ya kodi ili wazee wafanye mambo yao, na kweli kama serikali isingerudisha huo ulaji hawa maaskofu wangejitoa na kujiunga chadema au chama chochote makini na sisieem ingekula wa chuya 2010.Ushauri kwa nyie mnaojiita mashehe kabla ya yote acheni unafiki wenu na kuwapumbaza waumini wenzenu kwa kufanya hivyo mnawapotosha,unganeni na jitoeni huko sisieeem na jiungeni katika chama makini,kwani sisiieem inawaletea chakula majumbani kwenu?Nyie vipi?
Huo ni uchochezi kwa kuwa misamaha ya kodi ilihusu waumini wote(wakristo na waislamu). Halafu mbona kinachodaiwa kimetekelezwa na serikali kwani cha muhimu si ni sheria za kiislamu kutambulika na imekubalika hivyo au ni kutaka mashekhe wawe majaji wa mahakama kuu hata hivyo kuna majaji waislamu na wakristo.Tushauri vya msingi na vinavyotekelezeka.
 
Mimi ningeshauri kwa issue sensitive kama hii. Ni bora Kuvunja muuungano na kuiacha znz iendelee na mipango yake ya OIC na mahakama ya KADHI.
 
Mi ninachoshangaa ni mambo mawili, kwanza kwa hawa ndugu zetu wanajiita wkristo kutoonesha kuhisi uchungu wa ndugu zao Waislamu, kwa kuwa dhana ya Waislamu itakuwa kukme hawa wakristo sio wema kwao, sa tukifikia hapo... tujue tunaiingiza nchi katika matatizo makubwa, maana watakachoona waislamu ni wao wajipange wapate haki yao ya kimsingi ya kuabuadu. Wengine wanafikiri haki ya kuabudu kuswali nakuhiji makka, hapana ni pamoja na mambo mengine ya sheria ya kuhukumiwa kwa mujibu wa dini yao, haitawezekana kwa Wakristo kama nao wangekuwa na sheria za kuendesha mambo yao, achana na zile za kanisani!!! Sheria zingine kama walizonazo wailslam... halafu sheia hizo ziingizwe kwenye sheria za watu halafu hata muislamu amuhukumu huyo mkrsto, hawa wakristo watakubali?? au wanashangiria tu bila ya kupima.
Lakini pili naishangaa serikali kwa kulifuta hili kwa vigezo visivyokuwa na mshiko, wanajua madhara yake kwa taifa?? au hii amani wameshaichoka?? hawajifunzi kutoka nchi za wenzetu ambapo vita haviishi... ni kutokana na mambo kama haya ya kudharau hisia za baadhi ya makundi katika jamii na kupendelea za wengine. Sio siri serikali imetaka kuwaridhisha maaskofu na wakristo wengine pale walipokuja juu pale serikali kufikiria kuanzisha mahakama za kadhi, na kudharau hisia za waislamu ambao wao ndo wanaathirika zaidi pindi mahakama hizo zinapokuwa hazipo.

Serikali ilichokiangalia ni kutovunja Katiba yake yenyewe na sio kuangalia waislamu wanasema nini. Wewe unafikiri kuvunja Katiba uliyoapa kuilinda ni jambo dogo?
 
Hivi kila mwislamu aliyepiga kura za ndiyo kwa JK alifanya hivyo kwa kuwa aliahidi uwezekano wa kuwepo kwa mahakama ya Kadhi? Si kulikuwa na ahadi za madaraja, barabara, mabilioni ya JK, nk? Kwa nini waislamu hawaulizi angalau moja ya hilo? Kwani huyo kadhi akija ndio atajenga barabara, madaraja, madarasa, nk?
 
Mimi ningeshauri kwa issue sensitive kama hii. Ni bora Kuvunja muuungano na kuiacha znz iendelee na mipango yake ya OIC na mahakama ya KADHI.

Mahakama ya Kadhi ipo Zanzibar na hakuna mtu aliyewakataza kuendelea nayo. Pole kwa kuteleza kwenye maelezo yako.
 
Msimamo huo sio sahihi ,hili ni lazima mulielewe kilichopo hapa ni ahadi iliyotolewa na CCM kuwa watawapatia wapiga kura wao madai waliyoyataka ikiwa watawatilia kura sawa na kuahidi utawajengea daraja,utaweka maji bure,nyinyi mnaona sahihi lakini huu ni mtihani mkubwa kwa CCM na ni jambo ambalo linaweza kuwaangusha katika uchaguzi ujao ikiwa wapiga kura hao wataamua kuzipeleka kura zao kwengine japo wasipewe hayo madai yao,kama watazipeleka kura zao Chadema au CUF na kwengineko.
Tatizo wakristu mnalichukulia suala hili kama ushindi katika dini yenu lakini hatari ni pale Waislamu wote watakapoamua kuzipeleka kura zao kule wanakoona ndiko kwenye maslaha na dini yao hapo mtalia kilio cha mbwa mdomo juu ,najua mnadanganyika kuwa wakiristu ni wengi hapa Tz lakini kinyume chake Wakristu ni wachache tena wachache sana ,hilo halina ubishi wala mjadala ,endeleeni kuchochea.

Mkuu embu tupe hiyo sensa ilifanyika lini,ya nini tuandikie mate??tupe idadi waislam tupo milioni ngapi na wakristu tupo milioni ngapi?
Huenda wakati wa sensa nilikuwa sipo TZ !
 
Ndugu wana JF, Tanzania ni nchi isiyofuata mfumo wa dini yoyote hivyo kuihusisha serikali katika kuendesha na kusimamia mahakama ya kadhi ni kuvunja katiba ya nchi na kuleta migongano.

Nisaidieni ndugu zangu, hivi waisilamu hawawezi kuendesha mahakama ya kadhi nje ya mfumo rasmi wa serikali? Nikimaanisha kuwa mzigo/gharama za uendeshaji zibebwe na waislamu wenyewe pasipo kugharamiwa wala kusimamiwa na serikali kama zilivyo makakama za kanisa katoriki ambazo uendeshaji wake hauihusishi serikari? Yaani wawe huru kuzianzisha lakini si kwa kulijadili bungeni bali walijadili wao wenyewe misikitini na kwenye vyombo vyao na namna watakavyoendesha pasipo ushiriki wa serikari.


Ni hayo tu
 
kwa kulitazama katika mtizamo wako linawezekana, lakini mazingira ya hapa tanzania ni magumu sana. haiwezekani
 
Wakiamua wanaweza kuziendesha mbona wenzao wakatoliki wanaziendesha? Na ni sawa waziendeshe wenyewe bila kujiweka chini ya serikali kwani mahakama hizo ni ibada, yaani ni sehemu ya swala, sehemu ya kumwabudu Mungu. Kwa nini serikali iingilie mambo ya ibada za watu?

Halafu cha ajabu: mambo ya imani ni mambo yaliyo juu ya utawala wowote wa kibinadamu kwani yanajishughulisha na Mungu mwenyewe. Sasa sijui kwa nini waislamu wanataka kujirudisha nyuma kwa kuyaweka mambo ya imani chini ya himaya ya serikali na vyombo vyake vya dola. Yaani wanataka kujidunisha na kuifanya serikali kwa mambo ya dini kuwa "Bwana Mkubwa" wao. Kwa nini serikali iwaamulie mambo yao ya imani, ya ibada?? Hapa kuna jambo kubwa wanalitafuta hao ndugu zetu.

Makanisa hayawezi kujipeleka na kutaka kujiweka chini ya serikali katika mambo yake ya ibada. Haiwezekani!! Wao wanajitegemea na ni haki wajitegemee kwani mambo ya kumwabudu Mungu ni juu ya wachungaji na maaskofu kuyashughulikia. Mashehe, vipi ninyi? Kuna nini mnatafuta huko seriakalini? Kipi bila serikali hamkiwezi? Mbona mashehe mna nguvu na uwezo tele mmepewa na Allah na mtume wake? kwa nini msijione mko kamili kuwahudumia waamini wenu? Kweli mnaihitaji serikali kwa hayo? Au Msichanganye dini na dola.
 
kwa kulitazama katika mtizamo wako linawezekana, lakini mazingira ya hapa tanzania ni magumu sana. haiwezekani


Hebu fafanua huo ugumu kwa hapa Tanzania ndugu Edson ili tupate kuelewa!
 
Nyie endeleeni kuchokonoa na kujiona wababe ikiwa Raisi amelipuliwa kibao na ana ulinzi wa kila kona itakuwa nyie hohe hahe mnaosubili hesabu kutoka kwa pope.

Unafikiri kwa akili finyu kama hii unayo onyesha JF mtapewa Kadhi. Ninyi kama mnasujudu kadhi, nendeni mkaishi kwa mnao waabudu, Waarabu.
 
kwa kulitazama katika mtizamo wako linawezekana, lakini mazingira ya hapa tanzania ni magumu sana. haiwezekani
Naamini yawezekana. Kwani kinachohitajika katika mahakama hizo ni nini? Sanasana ni personel - wataalamu wa sheria za mirathi na ndoa ambao lazima wawe waislamu (kwani kesi ni ibada). Mashehe wote ni wataalamu wa sheria za ndoa na mirathi. Na uzuri mashehe ni wengi kwani kila msikiti kuna shehe. Wakiungana mashehe wa misikiti ya karibu na kufanya mahakama hawawezi kushindwa kuwasaidia waamini wao.

Gharama za kesi hizo zilipwe na wahusika wa kesi. Isitoshe wana vyanzo vingi vya mapato ikiwa ni pamoja na misaada kutoka ng'ambo.

Halafu kama ni mashehe ndiyo mahakimu, sioni kama watahitaji gharama kubwa kwani mashehe watakuwa wanatimiza kazi hiyo kama sehemu ya wajibu wao wa kiibada na wa kiuongozi kwa watu wao. Hivyo hawatahitaji mshahara wa pekee kama hakimu wa uraiani au serikalini. Kuamua kesi za mirathi na ndoa ni sehemu ya wajibu wao kama mashehe (maimamu na ustadhi).
 
kwa kulitazama katika mtizamo wako linawezekana, lakini mazingira ya hapa tanzania ni magumu sana. haiwezekani

Hebu fafanua huo ugumu kwa hapa Tanzania ndugu Edson ili tupate kuelewa!

nafikiri ugumu upo kwenye
1. ku execute hizo kesi zao, kwa kawaida mtu akihukumiwa, geshi la polishi/magereza wanakuwepo ili kumpeleka gerezani au kukata kiganja (somalia)nk sasa kwao itakuwaje? je mtu akiona upepo unaelekea kubaya akaenda kubatizwa kwa kakobe pale watafanyeje? ile hukumu itakuwa na uzito tena? nk
2. ndoa nyingi ni za mseto waislamu wameoa na kuolewa na wakristo hawa watahusika vipi na hizo mahakama?
3. Je mahakama za juu za nchi zinauwezo wa kubatilisha hukumu ya mahakama ya kadhi? mf. inavunja sheria za nchi au inavunja haki za binadamu? (wengi wanasema mahakama ya kadhi huwa inawanyima haki wanawake na watoto) then what will be next? maandamano?
nk nk
 
Hii mahakama ya kadhi nduguzanguni ni yetu Waislam, Wakristo kinawauma nini?
 
Jamani suala hilo lipelekwe kwa umakini yasije yakatukuta yanayotokea nchi zenye mivutano ya kidiniiiiiiiiiiiiiiiii

Na kweli migongano ilishaanza. Kuna wakatoliki ambao nao walikwishaanza kudai Mahakama yao nayo iwe accomodated kwenye syytem iwapo ya waislamu ingekubaliwa. Nilisoma makala moja yenye hoja kama ya mwaka jana:
Source: (Tanzania Daima 31 Agosti 2008): Bonyeza hapa: (Makala -Mahakama za dini zijadiliwe kwa kina)
-----------

WAKATI mijadala kuhusu kuanzishwa kwa mahakama za kidini, unaoongozwa na mjadala wa kuundwa kwa Mahakama ya kadhi, inapamba moto, nadhani ni wakati muafaka wa kukaa chini na kutafakari kwa kina na kuyasoma kwa makini mawazo yote yanayowasilishwa.
Kwa njia hiyo tutajikuta tumefika mahala tunajua mahitaji ya wengi katika jambo hili. Baada ya hapo kitakachobaki ni kutathmini uwezo wa kufanyia kazi yaliyopendekezwa. Naamini wataalamu wa uchumi, sheria na wengine watatusaidia kwa hilo la mwisho.
Wasiwasi wangu ni kutokuwa na uhakika na idadi ya wanaoelewa vizuri miundo ya mahakama za madhehebu yetu.
Ingawa kinachozungumziwa kwa undani ya Mahakama ya Kadhi, lakini tufahamu kuwa kimsingi kinachojadiliwa hapa ni mahakama za kidini.
Kwa kuwa mimi napata nafasi kusoma sheria za dhehebu langu (Kanisa Katoliki). Leo ni nafasi yangu kueleza ninachokiona ndani ya sheria hizo.
Lengo ni kuwasilisha maelezo ya muundo wa mahakama za kanisa langu, ili tunapotamka Mahakama ya dini tutarajie nini kutoka kwa Wakatoliki.
Kueleza muundo sidhani kuwa ni kitendo cha kujiunga na moja ya kambi zilizogawanyika wakati wa mjadala.
Hata nikihofu kutogawanyika haitasaidia maana sina uwezo wa kujadili lolote zaidi ya ukatoliki. Hivyo mengi ninayoeleza ni ya ukatoliki.
Mahakama ni neno la Kiswahili linaloeleweka kama chombo cha kusimamia haki. Kuelewa mahakama za Kanisa Katoliki ni vizuri kudadisi kwanza muundo wa utawala wa kanisa hilo.
Pia ni muhimu kujua baadhi ya sheria zinatumika katika kanisa hilo.
Nahofu mazoea yanaweza kufanya utawala wa kanisa na tawala za nchi kama yetu, ambayo huongozwa kwa kutenganisha mihimili mitatu ya mamlaka, kuanza kuchanganya mambo.
Kanisa Katoliki ni tofauti. Ni kawaida kukuta mtawala ndiye anatunga sheria au kushiriki vikao vya kutunga sheria na vilevile aweza kuwa ni jaji au yumo katika jopo la majaji (tribunal) wa kesi.
Kanisa lina sheria nyingi. Hapa yatosha kutambulisha zile zijulikanazo kwa jina la Canon Laws.
Hizi zimeorodheshwa kwa namba kuanzia ya kwanza hadi ya 1752. Sheria hizi zaweza kupatikana kwenye maduka ya vitabu na maktaba za Kanisa Katoliki.
Imekuwa ni juhudi ya Kanisa kutafsiri sheria hizi kwa lugha ya Kiswahili kama ilivyotokea mwaka 1995 kwenye matoleo ya gazeti la Kiongozi.
Muhtasari wa muundo wa kanisa duniani umeelezwa kuanzia Can. 330 hadi Can. 571. Kuhusu muundo huo, humu yatasimuliwa machache.
Iwapo tutapiga hatua kuhitaji mengi ya kitaalamu basi Kanisa limesheheni wataalamu waliobobea kwenye sheria za Kanisa.
Kanisa Katoliki linaongozwa na Papa, akiwa na makao yake kwenye nchi iitwayo Vatican City.
Papa ndiye mkuu wa Kanisa Katoliki hapa duniani (Can. 331 na Can. 335). Anaendesha kanisa kwa kupitia chombo kiitwacho Roman Curia kinachoelezwa kwenye Can. 360.
Kuona zaidi muundo wa uongozi wa Kanisa Katoliki duniani, yapaswa kupitia Can. 330 hadi Can. 563.
Sheria hizi zina maelezo kuhusu Papa (Can. 330-335), Kadinali (Can. 349-359), Askofu (Can. 375-430), Askofu wa kanda (Can. 435-438), Parokia (Can. 515-552), Baraza la Maaskofu (Can. 447-459), Balozi wa Papa (Can. 362-367), Mikutano ya maaskofu au sinodi (Can. 342-348) na mengineyo.
Zipo sheria zingine hutolewa na gazeti la Vatican (The official gazette of the Holy See), linalojulikana kama Acta Apostolicae Sedis (AAS). AAS huchapishwa kwa lugha ya Kilatini, ambalo ni jambo la kawaida ndani ya Vatican na hutoka mara 12 kwa mwaka.
Katika Kanisani Katoliki haujatajwa wadhifa unaotumia neno Mkuu kwamba mamlaka yake yanaathiri Tanzania nzima. Zipo taasisi neno hili liko hivyo. Huko tunakuta nyadhifa kama, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu, Mnadhimu MKkuu, Mdhibiti Mkuu.
Sina ufahamu mzuri atajwapo Askofu Mkuu wa nje ya ukatoliki kwamba Ukuu ule unaenea mpaka wapi.
Hivyo na kwa ndugu zetu Waislam anapotajwa Sheikh Mkuu au Kadhi Mkuu. Nina ujuzi tu na mazingira ya dhehebu langu. Natumaini uhakika kwingine unapatikana kwa waumini wa madhehebu hayo.
Hata hivyo, ndani ya Ukatoliki kuna wadhifa wa Askofu Mkuu (Archbishop).
Ni yule aliyepewa mamlaka au kazi fulani. Kazi hiyo yaweza kuwa kuongoza Jimbo lenye hadhi ya Jimbo Kuu (Archdiocese) au idara (taasisi) mojawapo ya kanisa.
Hapa nchini wapo sita ambapo watano wanaongoza majimbo yenye hadhi ya Jimbo Kuu ambayo ni Mwanza, Tabora, Songea, Arusha na Dar es Salaam na mmoja ni Balozi wa Vatican hapa nchini.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza ni Mhashamu Anthony Mayala wakati Muadhama Polycarp Kadinali Pengo yeye ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Askofu Mkuu Joseph Chenoz ndiye balozi wa Vatican hapa nchini. Nje ya Tanzania twaweza kumtaja Askofu Mkuu Celestino Migliore yeye ni mwakilishi wa Vatican katika Umoja wa Mataifa.
Masuala yaliyoorodheshwa kwenye Can. 435-438 ni aina ya majukumu mengine ya Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu.
Wakati anatimiza hayo hujulikana kama Metropolitan au Askofu wa Kanda (Tafsiri yangu).
Eneo la mamlaka haya huitwa Ecclesiastical province) au Kanda (Tafsiri yangu). Majimbo yaliyo ndani ya kanda hii huitwa suffragan dioceses.
Jumla yako 15 na matatu kati ya hayo ni Zanzibar, Musoma na Tunduru-Masasi. Kwa jina jingine huitwa suffragan Bishop.
Hata hivyo, Can. 435(3) inatueleza kuwa huyu Askofu wa Kanda (Metropolitan) hana mamlaka ya utawala katika majimbo yale (suffragan dioceses).
Urefu wa maelezo ya Askofu Mkuu ni kuepuka utata unaoweza kujitokeza kwa kujaribu kufananisha kilichomo kwenye dhehebu moja na jingine.
Tunapojadili jambo hili ni vizuri kuondoa aina zote za utata.
Ni vizuri kuendelea kujua neno Askofu (Bishop) ndani ya Kanisa Katoliki. Wako wa aina tofauti na majukumu yao hutofautiana wakati mwingine.
Wanaelezwa kuanzia Can. 375 hadi Can. 430. Wengi nchini ni wale wenye madaraka ya kuongoza majimbo na wanaitwa Askofu wa Jimbo Can. 376.
Wote wale 15 wa zile suffragan dioceses na wale watano wa Majimbo Makuu wako katika kundi hili. Sheria zinazoeleza usawa wao ni Can. 381-402.
Mfano wote wana haki ya kuwa na Askofu Msaidizi (Auxilliary Bishop) kama ilivyo sasa kwa Jimbo Kuu la Dae es Salaam Can. 403(1).
Ilitokea hivyo kwa Jimbo la Rulenge kwa Askofu Msaidizi Hayati Askofu Christopher Mwoleka (1969) na kwa Jimbo la Bukoba kwa Askofu Msaidizi Placidus Gervasius Nkalanga (1961-1969).
Tuone sasa madaraka ya Maaskofu majimboni mwao kwenye maeneo ya utawala (executive), kutunga sheria (legislative) na kutoa hukumu (judicial).
Ninanukuu Can. 391(1): ..It is for the diocesan Bishop to govern the particular Church entrusted to him with legislative, executive and judicial power according to the norm of the law.
Pia ninanukuu Can. 391(2): .. The Bishop exercises legislative power himself. He exercises executive power either personally or through Vicars general or episcopal Vicars, in accordance with the law.
He exercises judicial power either personally or through a judicial Vicar and judges according to the norm of the law.
Ifuatayo ni tafsiri yangu kwa hizi mbili. Ya kwanza inaeleza madaraka yake Askofu ndani ya jimbo lake.
Madaraka hayo ni kutunga sheria, kutawala na kuhukumu kwa kufuata taratibu za sheria.
Inayofuata ni jinsi anavyotimiza madaraka hayo ama yeye mwenyewe au kutumia wasaidizi wake na kama ni hukumu basi yeye mwenyewe au kutumia majaji wanaotambuliwa na sheria za kanisa.
Sheria inaeleza jinsi Askofu wa jimbo huyu kuwa ni jaji wa kwanza wa mahakama ya kanisa kama inavyoeleza Can.
1419 (1). Ukisoma Can. 1421(1). Waweza kuridhika kuwa Askofu wa jimbo anatakiwa aweke majaji ambao wamepitia madaraja kama upadre.
Pia Baraza la Maaskofu linaweza kuruhusu mkatoliki wa kawaida (laity) kuwa mmoja wa majaji - Can. 1421(2).
Hata hivyo, majaji wanatakiwa wathibitike kuwa na elimu nzuri ya sheria za kanisa Can. 1421(3).
Hadi hapa tumeona ngazi ya awali ya Mahakama ya kanisa ambayo ni kwa jimboni kwa Askofu (suffragan Bishop). Ni muhimu kujua kuwa kwa ruhusa toka Vatican maaskofu kadhaa wanaweza kukubaliana kuwa ngazi hii ifanyike sehemu moja kama inavyoelezwa kwenye Can. 1423 (1).
Zaidi kuhusu ngazi hiyo ni vyema kupitia Can. 1419-1437.
Baada ya hapo Can. 1628 inaruhusu rufani kwenda ngazi ya juu ambayo hapa ni The tribunal of second instance au ngazi ya pili (Tafsiri yangu). Ngazi hii inaelezwa kwenye Can. 1438-1441.
Baada ya ngazi ya pil bado rufani yawezekana (Can. 1628). Rufani baada ya hapa inabidi ipelekwe Vatican Can. 1442-1445.
Ni muhimu kusisitiza kuwa Papa ndiye Jaji Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani kama inavyoelezwa kwenye Can. 1442.
Zaidi ya hapo, hakuna rufani kama inavyosisitizwa kwenye Can. 333(3).
Hata hivyo, adhabu na mwenendo wa mahakama za kanisa ni somo refu.
Hapa inatosha kueleza adhabu nyingi zinapatikana Can. 1311-1399.
Wakati mwenendo wa Mahakama ya Kanisa unapatikana kwenye Can. 1400-1752.
Sikueleza mtiririko unaoanzia Parokiani ambako ni kanisa lenye linaloongozwa na Padri mwenye wadhifa wa Paroko.
Mashauri ya huko yanalenga kusuluhisha zaidi na hivyo ni jambo la kawaida kusikia Baraza la Usuluhishi kwa ngazi hii.
Iwapo usuluhishi haukuwa wa mafanikio basi shauri ndipo linapata nguvu ya kuwasilishwa kwenye ile ngazi ya kwanza ya mahakama.
Hayo ndiyo maelezo kidogo kuhusu Muundo wa Mahakama ndani ya kanisa Katoliki. Maoni yangu ni kwamba mjadala uliopo uende sambamba na kuanza kuelimishana undani wa Mahakama hizi za dini.
Tukifanya hivyo tumepiga hatua kwenye safari ya kujiridhisha kwamba tunajua tunalolijadili.
Mimi ni mmoja wa waumini wa kawaida na si mtaalamu wa sheria za Kanisa. Itakapobidi wataalamu wajitokeze ili kujibu zaidi maswali yanayojitokeza.
Kwa mfano; Je, ni nani tumpe wajibu wa kuhudumia maaskofu wote nchini kama majaji wa mwanzo wa Mahakama za Kanisa letu? Je, uwezo ni upi? Je walipwe mishahara kwa kiwango gani? Na ni nani mwenye wajibu wa makazi yao? Tuzidi kujiuliza.
Tumeona mahitaji ya utaalamu wa sheria za Kanisa.
Je, ni nani tumkabidhi jukumu la kusomesha wataalamu wa kanisa katika vyuo na viwango vinavyokubalika na Kanisa Katoliki?
Tumeona kuwa Jaji Mkuu wa Mahakama ya Kanisa Katoliki ni Papa (Can. 1442). Tunapofikiria kukidhi mahitaji ya wakuu wa mahakama hizo basi ndani ya ukatoliki tumfikirie huyo.
Hivyo tujipange kukidhi mahitaji yake na wenzake mahakama za madhehebu mengine popote walipo duniani.
Ni dhahiri kwamba kuwauliza mahitaji yao ni sehemu ya mchakato wa kuunda mahakama hizo.
Vatican City ni nchi inayojitegemea (Sovereign State), ikiongozwa na ni Papa huyo huyo.
Mahakama za dini zikiingizwa ndani ya katiba basi majaji wake pia wanaingia kwenye katiba hiyo.
Papa kama jaji mkuu wa wakatoliki anakuwa ameingia ndani ya katiba. Kiongozi wa Jamhuri ya Vatican City anakuwa ameingia ndani ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Maoni yangu, kujiandaa kukubali mahakama hizo ni kujiandaa kukubali matokeo yake kama haya.
Kwamba ndani ya katiba yetu tunajikuta tunataja marais zaidi ya wale wanaoongoza nchi yetu.
Je, nani awajibike kwa suala la ulinzi wa majaji na hadi Jaji Mkuu wa mahakama za dini?
Tumeandaa ulinzi gani kwa majaji wakuu ambao baadhi ni wakuu wa nchi duniani kama alivyo Papa?
Je, ni nani achukue jukumu la usafiri wa majaji wakuu, achilia mbali majaji wengine? Je, tuna uwezo wa kukidhi mahitaji ya usafiri kwa Jaji Mkuu wa Kanisa Katoliki na wengine wa aina hiyo?
Je, tunafikiri vipi haja ya kuwa na warsha, semina kwa majaji kubadilishana mawazo. Kwamba vikiitishwa basi dunia ishuhudie Papa akiongeza safari za kuja Tanzania kukutana na majaji wenzake wa mahakama za dini. Hatuwezi kutegemea kwamba atatuma mwakilishi siku zote.
--------
 
Mimi naona ziwekwe kiuwazi faida za mahakama ya kadhi, labda itapunguza kutoelewa umuhimu wa kitengo hicho muhimu.
 
First of all i see "no reason" why a devout Muslim, provided he or she was "acting voluntarily and without coercion", should not choose to submit a family dispute to a Muslim cleric

A Muslim, devout or otherwise, is certainly free to submit a family dispute to a Muslim cleric. Who is preventing it? Start such courts if they do not exist.

You complain that Christians are able to take family disputes to their religious leaders. Instead of complaining and waiting for the government to start a court for you, go ahead and do it yourselves.
 
Back
Top Bottom