Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Mkuu Makandara, hongera kwa hoja zako na majibu uliyo mjibu mwanakijiji. Mimi binafsi naona kwamba wewe ndiye unayeshindwa kufikiri nje ya boksi la udini, kwani kule kuwepo kwa sheria za kiislam tu kuna leta harufu ya mgawanyiko katika jamii. Halafu jua kuwa wakristu enzi za yesu na kabla ya hapo hawakutumia sheria za kiislam, bali walitumia sheria za kikristu za wakati huo, kumbuka uislam ulikuja baada ya ukristu. Sasa kama wakristu waliamua kubadili sheria zao za zamani, na uislam ulipo kuja uliamua kuzi adapt hiyo haifanyi sheria hizo kuwa ni za kiislam tokea mwanzo.
Wakati umefika sasa wa kuwa empower wanawake ili wawe na maamuzi inapofikia maswala ya kuolewa. Halafu kuwawajibisha kinababa ambao wanalenga kuoa wake wengi wakati hawawajibiki kuhusu watoto.
Binafsi ninaimani kuwa sheria za kiislam zinaweza kutafsiriwa na kufanyiwa kazi bila kujenga ukuta wa uislam. Uacheni uislam uendelee kuwepo nchini, sambamba na dini nyingine ili waislam waendelee kuenda sambamba na waumini wa dini nyingine.
Serekali inabidi i focus na mambo kujenga uchumi, kuboresha afya, elimu (hasa wanawake)na kupunguza unemployement.
 
Sikonge,
Kushauri kwangu kwamba Serikali iruhusu Mahakama ya Kadhi iundwe kama N.G.O. ni kwa msingi kwamba ni Waislamu tu wanaokubaliana waende kwa Kadhi, kuhusu mashauri baina yao ambayo siyo ya jinai. Pia mhusika ktk kesi asiporidhika na hukumu atoayo Kadhi, ana uhuru wa kukata rufaa ktk mahakama ya kiraia.

Kwa hiyo suala la kubadilisha dini ili uwe Mkristo na usipelekwe mbele ya Kadhi halipo, kwa vile ni kwa ridhaa ya mshtaki na mshtakiwa kukubaliana kutumia Mahakama ya Kadhi.

Napinga kuingiza Sharia Law ktk Statute Book yetu kama serikali ya J.K. inavyonuia, kwa sababu kunaweza kuwa na sheria yetu inayokinzana na kifungu fulani cha Sharia Law. Itakuwa ni kinyume na Katiba yetu, endapo hiyo sheria yetu itarekebeshwa, eti ili iwiane na Sharia Law. Tanzania haina dini; na Sharia Law au Canon Law haiwezi kuingizwa ktk Sheria za Tanzania.

Kama CCM wanataka kutekeleza Ilani yao ya 2005, basi wafuate ushauri wangu wa kuifanya Mahakama ya Kadhi iundwe na waumini wa Kiislamu kama N.G.O.
 
Last edited:
Wewe Kafiri acha kuwapotosha watu. Ndio maana mimi nawashangaa hawa watu wanaojitahidi eti kukuelewesheni watu wenye chuki kama wewe juu ya kazi za mahkama ya kadhi.

Endeleza chuki zako kwa JK ila ujuwe hakuna Rais wa nchi atakayetoka huko kwenu.[/QUOTE]

Hee yameisha kuwa hayo? twafa!
 
Mjadala huu unakuwa si mzuri tena kwasababu, watu wengine wanaanza kuvunja hata kanuni za uchangiaji katika JF kama kushambuliana kwa lugha zisizopendeza na jazba nyingi.
Ni vema tuchangie tukiwa na nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu.
Wengi hawaelewi kazi na mipaka ya mahakama ya kadhi kiasi kwamba wanaingiwa na hofu kuwa sharia itatumika kama ilivyo Sudan, kitu ambacho si sahihi.
Hata hivyo nadhani serikali ili iweze kupitisha sheria ni kwa njia ya bunge tu, ambalo ndiyo baraza la kutunga sheria. Na wabunge ndiyo wawakilishi wetu, tunaowapenda na kuwaamini, kwahiyo wakati mwingine baadhi ya mambo kutokana na unyeti wake yanahitaji subira kidogo. Naamini hicho ndicho kinachofanyika kwa sasa kwani mjadala huu, kama mtakumbuka, uliligawa bunge katika misingi ya kidini, kitu ambacho ni hatari sana.
Kwahiyo kimsingi serikali imetumia hekima kuliweka kando kwanza kwa manufaa yetu sisi Watanzania na Tanzania yetu.
 
Sasa sheria za waislamu ziingizwe kwenye katiba ya nchi ina maana hata wasio waislamu wata hukumiwa na sheria hizo hizo? Na Tanzania si tunadai ni secular state sasa sheria za dini zitageuzwaje kuwa sheria za nchi? Na je wakianzisha mahakama ya kiislamu hiyo haitaonekana na upendeleo iwapo itagundulika adhabu za moja wapo ya mahakama(aidha ya nchi au ya kiislamu) ni nzito au nyepesi kuliko ya mahakama nyingine? Kuna ulazima wa waislamu kuwa na mahakama yao wenyewe na wata hakikisha vipi sheria zao hazitaingiliana na sheria za nchi? Tatizo watanzania tuna kimbilia kujiingiza kwenye mambo. Hapa kuna baadhi ya watu watakuja na kusema oh mbona nchi fulani wana mahakama ya serikali na ya kiislamu?! Tusi kimbilie kuingiza vitu ambavyo haviendani na hali yetu kwa ajili ya kuridhisha tu baadhi ya makundi ambao wao kila siku wanaona tu kuwa wanaonewa au wenzao wana pendelewa.
kwanza historia inasema mahakama ya kazi ilikuwepo hapa Tanzania kabla ya na baada tu ya Uhuru, ila ilivunjwa na serikali kwa maoni tofauti yanayotolewa na wanaojua hoja hii...waislamu wamekuwa wakidai mahakama hii kwa muda na CCM walifanya KOSA kuwaahidi waislamu kwamba itarudisha mahakama ya kadhi ambayo mpaka leo ipo kule ZNZ... inasemekana hapa CCM ilikuwa inatafuta KURA, kitu ambacho leo bungeni SPIKA alikanusha na kusema..CCM HAIJAWAAHIDI WAISLAMU KUWAPA MAHAKAMA YA KADHI BALI IMESEMA ITALISHUGHULIKIA KAMA ILIVYOFANYA SASA...this is very contrary to original translation...na hili swali aliuliza PM ila kajibu SPIKA...
suala la mahakama na OIC serikali isipokuwa makini italigawa taifa...I hope CCM knows what they are doing maana hili suala litaleta mazara mabaya kwakuwa waislamu wanaamini serikali imelikataa kwa shinikizo kutoka kwa wakristo...kumbuka suala kama OIC inasemekana wizara ya mambo ya nje ilishajirizisha lakni tamko la maaskofu likabadili kabisa mwelekeo...lazima serikali iwe makini sana kuendelea kujenga mazingira ya kufanya upande mmoja uhisi unakandamizwa ni hatari sana...tujikumbushe madhara ya vita vingi duniani sanasana africa...tizama ushiriki wa viongozi wa dini??? je unatuma ishara gani?? kwani Rwanda hakukuwa na waislamu??? mbona waliohukumiwa wengi ni viongozi wa makanisa???
 
Mimi hoja ninayoishangaa ni hii hoja kuwa sheria za Tanzania ni Canon law. Hivi Bunge letu kwa miaka yote hii halijawahi kutunga sheria na tunatumia canon law mpaka leo?

Hii ni sawa na kusema maandishi yalibuniwa uarabuni hivyo maandishi yote tunayoandika leo ni kiarabu!! Sijui ni wasomi gani hawa wa sheria wanaosema eti kwa kuwa msingi wa sheria nyingi zinazotumika ni canon law, basi leo sheria zetu ni canon law. Hili nitalipinga sana.

Jambo hili linasababisha chuki zinazotokana na hilo tuu. Mtu ukimuuliza katika sheria zetu ni sheria ipi unahisi inakandamiza watu kutokana na dini yao (soma waislam), hakuna mfano wa sheria hizo. Tunapinga hizi sheria zilizotungwa na bunge letu kwa sababu tunaambiwa zina misingi au muundo wake umetokea katika Canon law.

Nimeshaandika huko nyuma, hata Canon law haina misingi katika ukristo. Misingi ya canon law ni Urumi na Uyunani. Kuna wakristo wengi hawaitambui canon law. Kwa hiyo badala ya kusema kirahisi tu kuwa sheria zetu ni Canon law, ni vema tukajua hiyo Canon law ni nini na imetokea wapi. Msingi wa ukristo uko katika biblia hasa agano jipya. Hilo agano la kale sheria zake ni zile zile za kiislam. Kwa kweli sheria za kikristo hasa na za kiislam misingi yake inafanana (uyahudi).

Sheria hizi zinazotumika, misingi yake hasa au mizizi yake hasa si ukristo kwani sheria za kikristo hazitofautiani sana na za kiislam.

Hizi sheria za kirumi na kiyunani ambazo jamii nyingi zimezipitia na kuzi-adopt kwa mazingira yao ni kosa kubwa kuziita sheria za kikristo au kuziita canon law. Kuna ukweli wa kihistoria ambao hatuwezi kuupinga. Lakini kusema eti sheria zetu ni Canon law ni uongo kimuundo na kimaana.
 
Mimi, ambaye nimetokea katika jamii yenye waislam wengi, nimeshuhudia na nina mifano mingi ya waislam waliokataa maamuzi (hasa ya mirathi) kutumia sheria za kiislam. Wengi hukimbilia mahakamani kupinga mgawanyo unaofanyika kufuata sheria za kiislam. Sasa ajabu ya hapa jf eti hizo sheria ambazo waislam wanazikataa huko mitaani, eti zinatakiwa imma faima. Najua Mashekhe wengi huchukia pale mgawanyo wa urithi uliotolewa kwa misingi ya kidini unapopingwa mahakamani na mahakama kutengua na kutumia sheria za nchi. Swali langu ni kuwa hivi wanaopinga huwa si ni waislam?? Sasa hao hao ndo tunawasemea eti wanataka mambo yao yaamuliwe kwa mujibu wa sheria zao!!

Kuna kitu zaidi kinatakiwa. Si haya mambo ya mirathi na kesi za madai kama wengi wanavyotaka tuamini. Vinginevyo, tungekusanya takwimu za ni waislam wangapi wamekataa migawanyo ya urithi inayotumia sheria za kidini, wala tusingefikiria hata kuzileta sheria hizo. Ikiwa wanaikataa hiyo migawanyo, tunataka tuipe nguvu za kidola ili wasikatae?? Haya yana reflect zaidi sentiments za mashekhe kuliko waislam wenyewe!

Si suala la madai tu, hapa kuna zaidi. Vinginevyo tungeona hoja zenye nguvu. Badala ya hizi za kuwa tunatumia canon law ndo maana waislam wanataka sheria zao!!
 
Last edited:
Najua hii mambo inaweza kuleta kizungumkuti kikubwa sana. Anyway, Serikali imefanya kwa manufaa yake na nchi.
 
Nchi yetu ni secular, hivyo uamuzi huu wa sasa wa kufutwa uundaji wa Mahakama za kidini za Kadhi ni sahihi... Waumini bado wanaweza kupeleka mambo yao/ matatizo yao binafsi kwa viongozi wao wa kidini.
 
sasa mbona sijaona meaningful arguments za against ku incorporate Sharia laws kwenye sheria zetu?

naona watu wana bishana tuuu
 
Msimamo huo sio sahihi ,hili ni lazima mulielewe kilichopo hapa ni ahadi iliyotolewa na CCM kuwa watawapatia wapiga kura wao madai waliyoyataka ikiwa watawatilia kura sawa na kuahidi utawajengea daraja,utaweka maji bure,nyinyi mnaona sahihi lakini huu ni mtihani mkubwa kwa CCM na ni jambo ambalo linaweza kuwaangusha katika uchaguzi ujao ikiwa wapiga kura hao wataamua kuzipeleka kura zao kwengine japo wasipewe hayo madai yao,kama watazipeleka kura zao Chadema au CUF na kwengineko.
Tatizo wakristu mnalichukulia suala hili kama ushindi katika dini yenu lakini hatari ni pale Waislamu wote watakapoamua kuzipeleka kura zao kule wanakoona ndiko kwenye maslaha na dini yao hapo mtalia kilio cha mbwa mdomo juu ,najua mnadanganyika kuwa wakiristu ni wengi hapa Tz lakini kinyume chake Wakristu ni wachache tena wachache sana ,hilo halina ubishi wala mjadala ,endeleeni kuchochea.
 
Msimamo huo sio sahihi ,hili ni lazima mulielewe kilichopo hapa ni ahadi iliyotolewa na CCM...
Kwenye ilani yao CCM hawakuahidi kuwapatia, bali kuangalia uawezekano wa kuwapatia...
 
Mchukia Mafisadi,

Mimi si mgeni humu. Wakristo wenye kutazama hoja pande zote tunawajua. Augustine Moshi Hayumo. Hao wasio na chuki tunawaambia kwamba tujuane na tukubali kujuana ndio amani itadumu. Lakini ikiwa na la Muislam ni Udini la Mkristo ni hekima, hatufiki.

Fanya utafiti kidogo tu humu JF; kwenye teuzi za viongozi uone ni zipi zinaitwa zina udini. Leo hii waislam wangeanzisha hicho mnachokiita Elimu kwa wapiga kura mngesemaje.

Any way kile kipindi cha akina Mzee Daudi Mwakawago cha kuficha Uislam wao kilishapita. Rugambwa na Nyerere si sawa na Pengo na Mkapa. Hakuna siri tena hata mtu akijitia anatumia lugha ya mafumbo. Fumbo mfumbie mjinga.

Tumejiandaa kwa lolote kwa wale wenye chuki na Uislam kama Augustine Moshi na Philemon Mikel.

Nchi hii yetu sote!

Ohhh Tanzania hakuna udini? Yako wapi sasa wakati watu wamejiandaa kwa lolote lile! Huku wakiandika hivi

Nungunungu said:
Wewe Kafiri acha kuwapotosha watu. Ndio maana mimi nawashangaa hawa watu wanaojitahidi eti kukuelewesheni watu wenye chuki kama wewe juu ya kazi za mahkama ya kadhi.

Endeleza chuki zako kwa JK ila ujuwe hakuna Rais wa nchi atakayetoka huko kwenu.
 
Sasa tumefikia hapa ....

Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM


Na Ummy Muya


BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kutokana na serikali kutupilia mbali ombi la kunzisha Mahakama ya Kadhi, Waislamu hawataipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

Katika taarifa yake, Bakwata ilifikia hatua ya kusema Waislamu wasimchague Rais Jakaya Kikwete iwapo atasimamishwa na CCM kugombea urais, ikiwa ni pamoja na wabunge na madiwani watakaosimamishwa na chama hicho tawala kutokana na kitendo cha serikali kutupilia mbali hoja ya Mahakama ya Kadhi.

Kauli hiyo imetolewa jana wakati Mufti Issa bin Shaaban Simba alipokuwa akitoa tamko kupinga uamuzi wa serikali kutaka kutumia sheria za dini ya Kiislamu katika mahakama za kawaida badala ya kuanzisha Mahakama ya Kadhi, kitu ambacho alisema anaamini kitawanyima haki Waislamu.

Alisema serikali imedhihirisha kuwa inaendeshwa na Wakristo na si kweli kama serikali haina dini na akamtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe kubatilisha kauli hiyo kwa kuwa inamchafua Rais Jakaya Kikwete mbele ya umma wa Waislamu.

Waziri ametuthibitishia kama Rais Kikwete alikuwa akitulaghai ili tumpigie kura kwa kigezo kuwa suala hilo litashughulikiwa na kupatiwa ufumbuzi na sio kuchanganywa kama ilivyokuwa mwaka 1970 katika Sheria ya Ndoa na kuwanyima haki Waislamu,alisema.

Alisema kwa muda mrefu sana Waislamu wamekuwa kimya wakitumia hekima na busara kudai haki zao, lakini katika hatua hii ambayo serikali imefikia hawapo tayari kuendelea kudhalilishwa na kuwa kitendo hicho ni dhalimu.

Mufti alisema wamekuwa wakiiomba Mahakama ya Kadhi kwa zaidi ya miaka 20 na hivyo hawezi kuendelea kuwa kimya na kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kuwa mahakama hiyo ni haki yao.

Alisema kauli ya Waziri Chikawe imedhihirisha kuwa serikali ina wenyewe na Waislamu wamewekwa katika tabaka la pili pamoja na Rais Jakaya Kikwete kuwatuliza kwa ahadi kuwa watalipatia ufumbuzi suala hilo.

Natoa wito kwa Masheikh wote nchini na Waislamu wa madhehebu yote kupinga vikali kauli iliyotolewa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe na kwamba Waislamu waige mfano wa Waislamu wa Afrika Kusini,alisema Mufti na kuhoji:

Kwa nini iwe Afrika ya Kusini na isiwe Zanzibar, Uganda na Kenya ambazo zipo ndani ya Afrika Mashariki? Kwa niaba ya Waislamu nasema serikali haikututendea haki na imetuchukiza sana,alisema.

Alisema lengo la kuomba mahakama hiyo ni kuhakikisha Waislamu wanashughulikia masuala yao ya ndoa na mirathi na si vinginevyo, hivyo waziri asipotoshe jamii kwa kutumia mifano ambayo haiko sahihi.

Mahakama hii haitawakata wezi mikono kwa kuwa nchi hii ina katiba na sheria na sisi tutazirudisha kesi zote za jinai mikononi mwa serikali. Sifahamu hiyo kamati ambayo waziri alisema alikuwa amekaa na kutoa tamko hilo ilikuwa na watu gani,alihoji.

Aliongeza kuwa kutokana na mapungufu hayo waziri arudi tena na kukutana na masheikh ili apate muongozo wa nini Waislamu wanahitaji na sio kuzungumza bila kuwa na usahihi wa kile anachosema.

Wakizungumza na waandishi wa habari baada ya tamko la Bakwata, masheikh walikuwa na mitazamo tofauti. Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Salum Mussa alisema wapo baadhi ya Waislamu ambao watakubali kutokana na ufinyu wao wa elimu ya dini.

Mussa alisema haoni sababu ya serikali kufanya njia ya mkato katika suala hilo kwani Waislamu wanahitaji Mahakama ya Kadhi kama ilivyo kwa wafanyabiashara ambao wana mahakama yao.

Hukumu inayotolewa katika Mahakama ya Kadhi ni ibada kwa mujibu wa mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) hivyo ni lazima kwa atakayetoa hukumu hiyo awe Muislamu na si vinginevyo,alisema.

Namshanga waziri anapotaka sheria hizi zitumiwe katika mahakama za kawaida. Aliona wapi John akawa imamu,alihoji sheikh huyo wa mkoa wa Dar es Salaam.

Naye katibu wa Bakwata wilayani Ilala, Sheikh Issa Ausi alisema historia iko wazi. Waasisi na wanaharakati ambao waliitoa Tanganyika mikononi mwa wakoloni walikuwa Waislamu, na akahoji sababu za serikali kuwa mstari wa mbele kuwafunga midomo leo.

Bakwata imezinduka sasa Waislamu wote tumeungana katika kupigania haki zetu na kutetea maslahi yetu na serikali itambue kuwa Bakwata iko hai hao Wakristo walikuwa wapi wakati sisi tukipigania uhuru,alihoji.

Wakati huohuo, Sheikh Salum Rwambo alisema anawashangaa wabunge Waislamu ambao baadhi ni mahajat na malhaj wanakaa kimya na kushindwa kutetea hoja za msingi na kudai kuwa huo sasa ndio mwisho wao wa kuwaita masheikh na kutaka waombewe dua ili wasipate wepesi katika kampeni zao.

Sheikh Rwambo pia alimsifia mbunge wa Nzega Lucas Selelii kwamba ni miongoni mwa wabunge katika Bunge hilo wanaozungumza ukweli na kwa kujiamini tofauti na wengine ambao wanaenda kukaa bila kufanya kazi zilizowapeleka.

Chanzo: Mwananchi Date::7/2/2009
 
Msimamo huo sio sahihi ,hili ni lazima mulielewe kilichopo hapa ni ahadi iliyotolewa na CCM kuwa watawapatia wapiga kura wao madai waliyoyataka ikiwa watawatilia kura sawa na kuahidi utawajengea daraja,utaweka maji bure,nyinyi mnaona sahihi lakini huu ni mtihani mkubwa kwa CCM na ni jambo ambalo linaweza kuwaangusha katika uchaguzi ujao ikiwa wapiga kura hao wataamua kuzipeleka kura zao kwengine japo wasipewe hayo madai yao,kama watazipeleka kura zao Chadema au CUF na kwengineko.
Tatizo wakristu mnalichukulia suala hili kama ushindi katika dini yenu lakini hatari ni pale Waislamu wote watakapoamua kuzipeleka kura zao kule wanakoona ndiko kwenye maslaha na dini yao hapo mtalia kilio cha mbwa mdomo juu ,najua mnadanganyika kuwa wakiristu ni wengi hapa Tz lakini kinyume chake Wakristu ni wachache tena wachache sana ,hilo halina ubishi wala mjadala ,endeleeni kuchochea.

Umefanya sensa ya waislamu wenye sifa ya kupiga kura ni wangapi na wakristo wenye sifa hizo wangapi? Usipende kujifariji bure toa data!
 
Kwenye ilani yao CCM hawakuahidi kuwapatia, bali kuangalia uawezekano wa kuwapatia...

Good analysis! Halafu ilani sio katiba isiyoweza kufanyiwa marekebisho. Hata katiba yenyewe hufanyiwa marekebisho. Halafu sijajua waislamu ni nani aliyewakataza kuanzisha mahakama ya Kadhi nje ya mfumo wa kiserikali. Kwani Bakwata imeanzishwa na sheria ipi? Kupata misaada ya OIC mpaka nchi isilimishwe kwanza! Kama hawataki kutupa misaada waache, we can do without them. Wakatoe misaada Darfur, ambako weo wenyewe ni sehemu ya tatizo, na kwingineko watakakoona inafaa.
 
Tatizo wakristu mnalichukulia suala hili kama ushindi katika dini yenu lakini hatari ni pale Waislamu wote watakapoamua kuzipeleka kura zao kule wanakoona ndiko kwenye maslaha na dini yao hapo mtalia kilio cha mbwa mdomo juu ,najua mnadanganyika kuwa wakiristu ni wengi hapa Tz lakini kinyume chake Wakristu ni wachache tena wachache sana ,hilo halina ubishi wala mjadala ,endeleeni kuchochea



Acha utahira wewe chizi tena mshezi, kwa taarifa yako hapa hatishiki mtu wala nini.
Kilio mtalia na mtaendelea kulia ninyi, shika adabu yako, unalopoka sana wewe, haijalishi tuko wachache kiasi gani kama ni noma na iwe noma, ebooooooooo
 
Hapa naona ni kutishana nyau tu. Hakuna dini hata moja yenye uwezo wa kuwaambia waumini wake wamchague nani. Hata kama hiyo dini itasema bado suala la uamzi unabaki kwa mtu mmoja mmoja. Kama hizi dini zingekuwa na nguvu na ushawishi kiasi hicho hawa wafuasi wa dini hizi wangeacha dhambi.

Haya maneno eti serikali imewaogopa wakristo ndo maana imerudisha misamaha ya kodi ni maneno yenye lengo la kuitekenya serikali ili ikasirike. Viongozi wa kikristo au wa kiislam wote wameshindwa kuwashawishi waumini wao kuacha dhambi, wataweza kuwalazimisha wachague mtu wasiyemtaka?

Hizi ni mbinu dhaifu za kuiforce serikali kuact the way you want kwa kuwaambia wanamuogopa yule unayetaka wamshughulikie. It is a cheap rant!
 
Hizo ndizo fikra za wabongo. Bado kuna watu wanaamini kuna siku tutaendelea. Labda tutakuwa na utajiri wa dini na madhehebu mengi.

Disgusting!
 
swalikwa the so called GREAT THINKERS

where are te so called arguments kwa nini its wrong ku incorporate sharia laws kwenye sheria za kawaida
 
Back
Top Bottom