Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Acha kuongopa. Kwanza: Kikatiba si sheria kuapa na Msahafu au Qur-an. Unaweza ukaapa bila ya kutumia kitabu chochote cha dini.
.

kama huna dini unaweza KUAPA kwa kushika katiba!

halafu pia wakuu,sheria za kiislamu zikiingia zitawahusu waislamu wenyewe!mkristo hawezi hukumiwa kwa hizo sheria!

dispute yoyote kati ya mristo na muislamu HAITAKUWA SOLVED KWA HIZI SHERIA ZA KIISLAMU

Let's use common sense jamani
 
Mimi binafsi naipa serikali 10/10 kwa soln iliyokuja nayo,napia nawapa pongezi waislamu kwa kuja na idea ya mirathi kwa mama na watoto.

Bado naamini sheria huwa zinaanzishwa na makundi makundi,watu binafsi ,taasisi za kidini Na Serikali inakuwa kama standardnization Unit kwa kuinyanyambua idea na kuiweka ktk misingi sitahiki.

Kweli Tatizo la mirathi ni tatizo sugu na ambalo lahitaji kutungiwa sheria Standard/grobal na si locally.
Mimi nafikiri kwa serikali kusema kuzitafsiri sheria naamini hakuna maana ya translation ya neno kwa neno bali itachekecha na kupata misingi itakayokubalika.

Mfano. Kama mimi ndiye ningekuwa na pendekeza sheria ya mirathi,wanawake wa pembeni ningalisema hivi-
Mwanamume yeyote anayemtia na kusababisha kupatikana kwa mtoto ni lazima atoe huduma kwa mwanae hadi pale atakapotimiza miaka 18.Na huduma hiyo itaendelea mpaka pale mtoto huyo atakapoishia ktk masomo yake maximum bachala na mwanaume huyu atakuwa analipa pesa hiyo kupitia account itakayofunguliwa kwa kila mwezi ama mbele ya mtendaji wa kijiji na kitongoji na nyaraka hizo zitakuwa zinakabidhiwa mahakamani kila mwezi baada ya malipo.

Mwanamke na mwanamme watagawana nusu kwa nusu mali waliyochuma walipokuwepo pamoja tu.

Mirathi itakwenda kwa yule tu atayetambulishwa na mmliki wa mali hizo.Na kama ikitokea mmiliki hakutaja mrithi wake basi mali zitangawanywa sawa kwa sawa kwa watoto wa mmliki.
 
Mkamap,

Ingekuwa hivyo ingekuwa vizuri. Lakini tatizo ni kuwa ukishaziingiza kwenye mchekecho wa serikali waislam hawatazikubali kama sheria za kiislam. Sheria za kiislam zipo na zipo kwenye msahafu wao. Huo mchekecho unaousema ndo uliofanyika kwenye hizi sheria tulizo nazo. Hizi zina-influence za waislam na influence za wakristo. Waislam wanaziona ni inadequate kwa sababu hziko neno kwa neno na kilichoandikwa kwenye vitabu vyao vya dini.

Sheria ya serikali inaruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja na inaruhusu taraka. Ni aibu kusema hii sheria imetokana na wakristo wakati wakristo wanailalamikia kwa kuvunja ndoa zao!

Huwa kuna mwandishi mmoja, Joseph Mihangwa huwa anaandika sana makala kwenye rai na magezeti mengine mengi. Huyu amefanikiwa kuwashawishi watu wengi hasa waislam kuamini kuwa sheria zetu msingi wake ni ukristo. Madai mengi huwa naona yanafanana sana na maandishi ya Mihangwa.

Lakini ukweli ni kuwa sheria nyingi za kimagharibi msingi wake mkubwa ni sheria za kigiriki na baadaye za kirumi. Huwa kuna makosa ya kuamini kuwa ukristo ndo uliinfluence sheria na taratibu za kirumi. Wanaojua vizuri huwa wanasema ni kinyume chake; yaani ukristo umeathiriwa sana na urumi na uyunani. Na hili liko wazi. Ukristo usingekubalika katika utamaduni wa kigiriki na kirumi uliokuwa umeshajikita kwa miaka maelfu kadhaa bila wenyewe (ukristo) ukristo kujibadili.

Sasa kina Mihangwa wanawadanganya watu eti msingi wa sheria za kimagharibi ni ukristo, kitu ambacho si kweli. Jambo hili huwafanya waislam wengi kulalamika eti sheria zetu ni za kikristo na usekulari ni ukristo. Msingi wa taratibu nyingi za kimaisha nje na ndani ya makanisa ya kikristo umeathiriwa sana na tamaduni na mila za kirumi na kiyunani ambazo ndo zimo katika sheria zetu nyingi.

Mila na taratibu za kiyunani na kirumi zilikuwepo miaka mamia kadhaa kabla ya ukristo kuingia. Na kikweli ukiangalia huu usekulari unaozungumziwa hasa ni urumi na uyunani. Tuanzie hapo!!
 
Mimi nilikataa kuwepo kwa mahakama za kadhi kwa sababu za kiufundi na kiutendaji; kwamba wakati mwingine tutamfanya mtu ambaye si mtu wa dini fulani (si mwislam) kulazimika kutoa maamuzi ambayo yataathiri watu wa imani fulani tu.

Kimsingi nitapinga hii integration vile vile kwa sababu za kiufundi au kiutendaji. Itakuwaje pale ambapo sheria ya kiislam inapingana na sheria ya nchi? Ni sheria ipi itaprevail? Kwa mfano; sheria za nchi zinasema mme atarithiwa na mke. Sheria ya kiislam inamgawanyo tofauti. Sasa itakapotokea mtu mmoja kupinga uamzi unaotumia sheria ya kidini itakuwaje? Hatutazifanya hizi sheria zionekane subordinate?

Nakumbuka zamani kwenye sheria ya ardhi, kulikuwa na ruhusa ya kutumia customery law. Lakini nakumbuka movements za wanawake zilisababishwa hiki kipengele cha customery law kwenye ardhi kimeondolewa. Sasa tunataka tu-insert islamic law!

Vipi mahakimu wakristo, watakuwa na uwezo wa kuhukumu kutumia sheria za kiislam? Ninavyojua mgawanyo wa mahakimu kwenye mahakama zetu hauzingatii dini. Sasa mtu akisema mimi hapa nataka nihukumiwe kwa sheria za kiislam, itabidi atafutwe hakimu mwislam? Au itabidi kila mahakama iwe na mahakimu waislam kwa ajili ya kuhukumu kesi za waislam?

Vipi mahakimu watakaohukumu kutumia sheria za kiislam? Kwenye mtaala wa sheria najua kuna specialty ya islamic law. Sasa ikiwa mkristo anataka na akasomea islamic law ataruhusiwa kuhukumu waislam?

Mimi shida yangu, ni pale ambapo kabla ya kuhudumiwa itabidi uwe unaulizwa kwanza dini yako. Hili tunaweza kuliona jambo jepesi tu leo, lakini litatutoa jasho kesho.

Kusema sheria zilizopo ni za kikristo kwa sababu nyingi zilitungwa wakati viongozi ni wakristo ni kutoitendea haki historia yetu. Historia yetu inaonesha kuwa mchakato wote wa kupata uhuru waislam walishiriki sana katika capacity mbali mbali. Hivi tunadhani hawa waislam wao walikuwa mbumbumbu kiasi hicho kwamba waliruhusu nchi yao itungiwe sheria za kikristu? Hili linanisikitisha kidogo, tunaonekana kudharau kila kilichofanyika huko nyuma.
Si ndio maana maswala ya operation yanatakiwa kujadiliwa na wahusika watuambie vipi mfumo huu utafanya kazi? wewe unakataa kwasababu ya operation yake kuwa ngumu au nini? wataalamu watasema itakuwaje ili wahusika (wananchi waislamu) wafurahi maisha yao na dini na nchi yao I have no problem with it "wataalam wizarani wateleza operation yake itakuwaje siyo unaanza kuwa "negative na ku-oppose"
 
Mtoto,
Ningependa kukusahihisha hapo. Wakati wa Yesu, hazikuwa sheria za Kikristo. Hizi sheria ni za kiyahudi na zinatumika mpaka leo. Zinapatikani katika Torati (Torah). Tafadhali, Usipotoshe watu kwa kuongea usichojua.
Mkuu sijui una quote wapi niliposema kuwa hizi ni sheria za Kikristu. Nilichoandika ni kwamba sheria nyingi za Kiislaam zilitumika hata wakati wa Yesu na hakuna mahala popote ktk Biblia, Yesu amepinga sheria hizo zisitumike...hii ni ktk kusherehesha dhana ya kwamba sheria hizi ni za dini ya Kiislaam tu..Nadhani umenielewa..

Wakuu,
Baada ya kuwaacha kwa muda narudi tena kuwafahamisha zaidi kwani siwezi kufanya Uvivu kulielimisha Taifa hili pamoja na kwamba tuna tofauti zetu.
Kwanza nitaanza na swala la Katiba..
Inaonyesha wengi hawafahamu jinsi katiba inavyofanya kazi..na wala inatungwa vipi kwa sababu kinachozungumziwa hapa ni hatua baada ya vitendo fulani kufanyika. Maamuzi ya Bunge au serikali yangekiuka Katiba ikiwa tu Bunge litaamua kutumia sheria za Kiislaam kuwalazimishwa watu kuoa zaidi ya Mke mmoja. Au serikali kuweka sheria kuwa Polygamy ni crime (kikristu), ama serikali ingeweka kiwango cha mwisho wa kuoa wake isiwe zaidi ya idadi ya Waislaam..Na hata kuwalazimisha watu kuoa wake kulingana na uwezo na matakwa ya mume (Asili).

Hapo ndipo swala la dini moja lingetumika kuonyesha kuvunjwa kwa Katiba. Lakini maadam kila mmoja wetu ana ruksa ya kufuata dini yake akaoa mke au wake kulingana na imani yake basi maamuzi ya kitendo hicho inapofikia haki za wahusika na hasa wanawake haiwezi kuwa sawa kwa sote. na itakuwaje sawa ikiwa kila mmoja wetu anaruksa tofauti na mwingine.

Mahakama inajenga sheria zake kulingana na Katiba yaani haikiuki Katiba..Katiba imetupa ruksa sote kufuata dini zetu hivyo maamuzi ya mahakama ni lazima yafuate ruksa hizo na sii vinginevyo..Na ktk swala hili tumeona kuwa katiba ipo huru kwa wafuasi wa madhehebu yote kufanya ibada zao(ndoa) kulingana na imani hizo. Na hukumu zetu zitatofautiana kwani ni lazima mahakama ikubali ndoa ya kikristu na haki zake ambazo ndizo zinatumika kisha ikubali ndoa za kiislaam na Kiasili.. Inapofikia swala hili kuwa na matatizo ndipo sheria zilizotoa ruksa kwa wote kuzingatia haki ya pande zote kulingana na imani ya wafuasi wake...

Tumesha kubaliana kwamba mahakama ya kadhi yaifai na hata mimi nimeunga mkono swala hilo kwa sababu sii waislaam wote wanaofuata sheria za Kiislaam lakini kwa wale wanaofuata inatakiwa sheria moja itumike na kila Muislaam anayeingia ktk ndoa hizo afahamu nini hukumu za madai na majukumu anayokabiriwa nayo..Hutaki oa mke mmoja itaepuka madai ya hukumu hizo kama nilivyo fanya mimi.. Nina mke mmoja hivyo hizo sheria haziwezi kuniathiri na wala haina maana mimi nimegeuka kuwa Mkristu kuoa mke mmoja.

Ndio maana nimetoa mfano hapo juu kuhusiana na Mwizi, nilisema waislaam hukata mikono, jamaa zetu wa Asili hukumu ya jizi ni kuua palepale kama wanavyofanywa vibaka Kariakoo ndivyo walivyofanya mababu zetu..pengine huingia vitani kabisa kwa sababu ya wizi tu wa mifugo..Lakini ktk sheria na maamuzi ya matatizo haya tumechukua lililo bora zaidi bila kujali waumini wa dini zote.. Maadam wewe ni mwizi basi haya ndio utakabiriana nayo bila kujali faith yako. Hii ni katika hukumu sii swala la kuingiza sheria Kikatiba kuukubali wizi kulingana na Asili ya Wamasai..Kwi kwi kwi!

Mengineyo yote hujmu mnaongezea na kuzua wenyewe kwa sababu mnashindwa kuangalia nje ya kabati la dini.. Na nimeuliza ikiwa mtu kaoa wake waanne nini haki ya wake wale wengine kisheria mmeshindwa kunijibu kwa sababu dini yenu inawaambia kwamba kuwa na zaidi ya mke mmoja ni Polygamy, hivyo kufikiria nje ya hapo..
 
Last edited:
Mkamap,

Ingekuwa hivyo ingekuwa vizuri. Lakini tatizo ni kuwa ukishaziingiza kwenye mchekecho wa serikali waislam hawatazikubali kama sheria za kiislam. Sheria za kiislam zipo na zipo kwenye msahafu wao. Huo mchekecho unaousema ndo uliofanyika kwenye hizi sheria tulizo nazo. Hizi zina-influence za waislam na influence za wakristo. Waislam wanaziona ni inadequate kwa sababu hziko neno kwa neno na kilichoandikwa kwenye vitabu vyao vya dini.

Sheria ya serikali inaruhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja na inaruhusu taraka. Ni aibu kusema hii sheria imetokana na wakristo wakati wakristo wanailalamikia kwa kuvunja ndoa zao!

Huwa kuna mwandishi mmoja, Joseph Mihangwa huwa anaandika sana makala kwenye rai na magezeti mengine mengi. Huyu amefanikiwa kuwashawishi watu wengi hasa waislam kuamini kuwa sheria zetu msingi wake ni ukristo. Madai mengi huwa naona yanafanana sana na maandishi ya Mihangwa.

Lakini ukweli ni kuwa sheria nyingi za kimagharibi msingi wake mkubwa ni sheria za kigiriki na baadaye za kirumi. Huwa kuna makosa ya kuamini kuwa ukristo ndo uliinfluence sheria na taratibu za kirumi. Wanaojua vizuri huwa wanasema ni kinyume chake; yaani ukristo umeathiriwa sana na urumi na uyunani. Na hili liko wazi. Ukristo usingekubalika katika utamaduni wa kigiriki na kirumi uliokuwa umeshajikita kwa miaka maelfu kadhaa bila wenyewe (ukristo) ukristo kujibadili.

Sasa kina Mihangwa wanawadanganya watu eti msingi wa sheria za kimagharibi ni ukristo, kitu ambacho si kweli. Jambo hili huwafanya waislam wengi kulalamika eti sheria zetu ni za kikristo na usekulari ni ukristo. Msingi wa taratibu nyingi za kimaisha nje na ndani ya makanisa ya kikristo umeathiriwa sana na tamaduni na mila za kirumi na kiyunani ambazo ndo zimo katika sheria zetu nyingi.

Mila na taratibu za kiyunani na kirumi zilikuwepo miaka mamia kadhaa kabla ya ukristo kuingia. Na kikweli ukiangalia huu usekulari unaozungumziwa hasa ni urumi na uyunani. Tuanzie hapo!!

Mkuu
Nakubaliana na wewe kwa asilimia nyingi sana ni kweli watu tusioelewa vizuri Ukristu unatukanganya ,Nakudhani ndivyo sivyo hasa tunapojaribu kuoanisha tamaduni fulani na kuzifanya ndio ukristu.Ni wazi Wayahudi si wakristu pia ni wazi ukristu imeanza baada ya Yesu .Zingine huko nyuma zilikuwa ni sheria za Musa ,Babu ibrahimu n.k

Pia ni wazi suala la urithi ni suala sugu linahitaji sheria na kwa kuwa Serikali ndiyo itaibatiza sheria hiyo itangalia namna nzuri ya kui implement sheria hiyo ambayo itakuwa na tunda bivu kwa wananchi walio wengi.

Na watakao taka kuimplement neno kwa neno mimi nafikiri watakuwa wamepoteza dira.
 
MkamaP,
Mkuuu nilichoandika mimi kinahusiana na Uislaam sio Ukristu. Sheria za Kikristu zilianza na Canon laws ambazo zilitumika ktk nchji zote za magharibi nasi tukaiga na kuzivuta kwetu..Nimeandika huko nyuma vizuri tu ..someni muelewe kwanza mtu kaandika nini kabla hamjaanza kugeuza maneno. Kwani wakati wa Mussa na Ibrahim watu walishikishwa Biblia kuapa?
Kisha basi nani kasema swala la Talaka ni la Kikristu?..mbona talaka zilikuwepo toka enzi za mitume na macheif wetu wasiokuwa ktk historia, nani kasema ni la Kiislaam! jamani mbona mnazoa hoja huku na kule wakati hakuna mtu aliyeleta hoja hizi.
 
Mkandara
swali lako ni logical sana halihitaji kuwa prof kulichungulia jibu.

Mwanawasu !!Pamoja nakusema kwamba watu tunaona ndani ya box Lakini na wewe wenda bado uko ndani ya box lile lile kwanini nasema hivi?

Kwanza nafikiri wewe bado unaona ama una mentality kitendo cha mwanamke kuolewa na mwanamume ni ajira.
Pili bado una mentality kwamba kitendo cha kuchapa SEX ni mwanaume anamtumia mwanamke.
tatu bado una mentality ya kwamba mtoto ni mali ya mwanaume.
Sasa ukichanganya hayo mambo matatu ndio yanakupa taabu sana.
 
Last edited:
Mku soo what? point yako nini hasa.. yaani sheria zisitungwe kwa sababu Tanzania ina dini tatu tofauti..
Ebu nikuulize wewe mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa tumpe sheria gani apate haki yake! waislaam hawana solution na Wakristu pia hawana jibu kwa sababu dini zote hizi hazitambui mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa.. Lakini tukitazama sheria za Asili, hao unaowaita wenye indigenous belief wanayo solution..Kwa nini tusiitumie hukumu yao kumpa haki mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa.. ili hali nchi yetu haina sheria kuzuia watu kufanya kitendo hicho nje ya ndoa..Tuache tu maadam inafuata hukumu ya Kiasili kinyume cha matwakwa ya waislaam na Wakristu!

Unafikiri serikali ikichukua sheria za Asili na kuzitumia ktk mahakama zetu za madai watafanya kosa kwa sababu nchi yetu ina dini tatu tofauti.. Mkuu nani wa kum blame hapa ikiwa Waislaam na Wakristu ndio wanaozaa nje ya ndoa, kinyume cha dini zetu...Leo unazivuta dini ktk sheria wakati unajua fika kwamba uloyafanya ni makosa...Mkuu hizi ni hukumu tunzozungumzia sio sheria ya kuzuia watu kufanya wanayoyafanya..

Hata Jizi huwa na sababu ya kuiba, sheria hutungwa kumlinda victim aliyeibiwa na tunatazama uzito wa hukumu kulingana na makosa.. badala ya kukatwa mikono kama Waislaam na watu wa asilia (indigenous) walivyokuwa wakihukumu, tunachukua njia ya kati ya kumfunga Jela ambayo ilitumika zaidi na tawala za Kikristu..Tatizo liko wapi! wote tunakubaliana na maamuzi hayo bila kujali dini zetu zinatuambia hukumu gani itumike..

Mkuu umezidi sasa kulalamika mpaka unaboa. Nilikuwa nimetoa statistics mtu akataka nimthibitishie ndiyo maana nikampa hizo source mbili. Usitafuta malumbano sehemu ambayo haipo. Mtu kaomba nimpe wapi nimepata data nilizo toa on previous post ndiyo nikampa sasa sioni umejisumbua nini kujibu hiyo post.Naona you have taken it upon yourself to make things into what they are not.
 
Mkuu umezidi sasa kulalamika mpaka unaboa. Nilikuwa nimetoa statistics mtu akataka nimthibitishie ndiyo maana nikampa hizo source mbili. Usitafuta malumbano sehemu ambayo haipo. Mtu kaomba nimpe wapi nimepata data nilizo toa on previous post ndiyo nikampa sasa sioni umejisumbua nini kujibu hiyo post.Naona you have taken it upon yourself to make things into what they are not.
Mkuu huyo mtu hakutokea tu na kuanza kutaka statistics.. wewe ndiye uloanzisha swala la nchi kuwa na dini tatu..Kisha basi ukasahau kwamba katika dini zote hizi kuna sheria zinazotumika ktk dhehebu moja na hazitumiki ktk jingine..
Haya maswala ya dini umeyaanza wewe mkuu na tofauti zake umeziasha wewe, wala sina malumbano nawe au mtu yeyote nachofanya mimi ni kukufahamisha wewe pale swala zima la mada hii linapohusika. Sitoki nje ya mada..Yaani kama kuboa mkuu wangu nafanya heshima tu umeniboa longtime!
 
Mkuu huyo mtu hakutokea tu na kuanza kutaka statistics.. wewe ndiye uloanzisha swala la nchi kuwa na dini tatu..Kisha basi ukasahau kwamba katika dini zote hizi kuna sheria zinazotumika ktk dhehebu moja lna hazitumiki ktk jingine..
Haya maswala ya dini umeyaanza wewe mkuu na tofauti zake umeyaanza wewe mkuu wala sina malumbano nachofanya mimi ni kukufahamisha wewe pale swala zima la mada hii linapohusika. Sitoki nje ya mada..

Mkuu yeye alisema kuwa haamini kuwa kuna asilimia kubwa ya Watanzania ambao wana dini indigenous. Ndiyo maana nikamuonyesha hizo data. Hizo data zilikuwa kwa ajili yake sasa wewe ukani nukuu na kusema "So what" kana kwamba data umepewa wewe. Rejea post ambayo huyo mtu kaniuliza hilo swali na nikamjibu utagundua kuwa it has nothing to do with what you said. Jamaa alitaka wapi nimepata hizo data the proportionality za kidini na mimi nikampa plain and simple. Kauliza swali mimi nimemjibu. Kama unalingine sema otherwise sioni kosa la kumuambia mtu wapi nimepata data ambazo nimepost mimi mwenyewe.
 
Mwanafalsafa1,
Labda nikukumbushe...


Quote:​



Mkuu hizo nchi wewe unazosema zilianza na sheria za kidini ni kwa sababu wananchi wake walikuwa overwhelmingly wa dini fulani. Ndiyo maana unakuta nchi kama Saudi Araba inaongozwa kwa sharia kwa sababu karibia wananchi wote ni Waislamu na nchi si secular bali inadini. Tanzania Waislamu 35% na Wakristo 30% kwa maana hiyo hakuna dini ambayo ina an overwhelmingly the majority. Kabla ya kulinganisha Tanzania na nchi zingine tabua kwanza hali za nchi hizo zilivyo tofauti na kwetu. Tusipende kufanya kila kitu simply because nchi fulani nao walifanya.

Na alivyojibu yeye ama niseme kilichofuatia
Mkuu MwanaFalsafa1.
Hizi takwimu za idadi ya waislamu na wakristo umezipata wapi ?.Sensa zote zilizowahi kufanyika Tanzania hazijawahi kuwa na kipengele cha kuonyesha idadi ya watu kwakuangalia dini !.Umesema idadi ya waislamu ni 35% na wakristo 30%.mkuu unataka kutuaminisha kwamba Tanzania ina karibu ya watu 35% wasiokuwa na dini au wanaoabudu dini za jadi ?.tafadhali naomba ufafanuzi.
 
Mwanafalsafa1,
Labda nikukumbushe...


Quote:


Mkuu hizo nchi wewe unazosema zilianza na sheria za kidini ni kwa sababu wananchi wake walikuwa overwhelmingly wa dini fulani. Ndiyo maana unakuta nchi kama Saudi Araba inaongozwa kwa sharia kwa sababu karibia wananchi wote ni Waislamu na nchi si secular bali inadini. Tanzania Waislamu 35% na Wakristo 30% kwa maana hiyo hakuna dini ambayo ina an overwhelmingly the majority. Kabla ya kulinganisha Tanzania na nchi zingine tabua kwanza hali za nchi hizo zilivyo tofauti na kwetu. Tusipende kufanya kila kitu simply because nchi fulani nao walifanya.




Mkuu MwanaFalsafa1.
Hizi takwimu za idadi ya waislamu na wakristo umezipata wapi ?.Sensa zote zilizowahi kufanyika Tanzania hazijawahi kuwa na kipengele cha kuonyesha idadi ya watu kwakuangalia dini !.Umesema idadi ya waislamu ni 35% na wakristo 30%.mkuu unataka kutuaminisha kwamba Tanzania ina karibu ya watu 35% wasiokuwa na dini au wanaoabudu dini za jadi ?.tafadhali naomba ufafanuzi.

Swali lake lilikuwa sensa hiyo nimezitoa wapi kwa sababu kwa madai yake Tanzania haifanyi sensa ya idadi ya watu wa dini fulani. Sasa nimemjibu hizo data nimezitoa wapi. Sasa wewe umeona kosa liko wapi? Si kaomba nithibitishe hizo tkwimu? Ndiyo nimempa sasa. Wewe ulicho fanya ni kuprove tu my point which is kaomba wape nimetoa takwimu na nimempa.
 
Hapana mkuu soma vizuri nilicho quote hapo juu. Wewe ndiye umeanza na hizo figure (maelezo mekundu) kisha yeye akaomba ufafanuzi.. ndipo ulipoweka ufafanuzi ukurasa uliofuata.
Mkuu hivi ukikubali utapoteza kitu gani...hapa tunazungumza hoja inayohusiana na serikali kukataa mahakama ya kadhi badala yake kuchukua sheria za Kiislaam na kuzitumia pale ipaswapo.
 
Hapana mkuu soma vizuri nilicho quote hapo juu. Wewe ndiye umeanbza na hizo figure kisha yeye akaomba ufafanuzi.. ndipo ulipoweka ufafanuzi ukurasa uliofuata.

Eh sasa tatizo liko wapi? Kwani mimi nimesema nini? Ndiyo mimi ndiyo nimetoa hizo takwimu. Yeye akaomba mimi nifafanue kwa hiyo mimi nikampa hizo statistics. Yeye alikuwa anasema hajawahi kusikia takwimu ziki chukuliwa za dini ya mtu. Mimi ndiyo nikamuonyesha wapi nimepata. Sasa sema wewe mkuu tatizo liko wapi? Kuwa nimethibitisha takwimu nilizo pata mwenyewe? Sasa napo kutoa takwimu utasema ni udini nao? Mkuu umekosa hoja. Sema basi mkuu tatizo likuwapi kwa kumuambia takwimu nimezipataje? Tell me what is wrong with what or how I answered him/her.
 
Alaaah! sasa imekuwa tatizo liko wapi?.. sii wewe uliyeandika hapo juu kuwa natafuta malumbano ambayo wewe hukuyaanzisha!
 
Alaaah! sasa imekuwa tatizo liko wapi?.. sii wewe uliyeandika hapo juu kuwa natafuta malumbano ambayo wewe hukuyaanzisha!

Hahaha hapo safi basi. Kama umekubali hamna malumbano ina maana mjadala umeisha. Sasa kutokana na post yako hapo juu umekubali kuwa hamna tatizo wala malumbano so let's move on. Kukiwa na ishu yoyote nyingine we niambie tu mkuu tuta jadiliana.
 
Date: 7/1/2009

Mahakama ya Kadhi yakoroga Waislamu, Wanasiasa


Na Waandishi Wetu


SIKU moja baada ya serikali kutoa msimamo wake wa kutounda Mahakama ya Kadhi na badala yake kuzijumuisha Sheria za Kiislamu kwenye sheria za nchi, baadhi ya Waislamu na Wanasiasa wamekuja juu na kudai kuwa imeshindwa (serikali) kutekeleza ahadi iliyotoa wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005.

Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kidini, wanasiasa na wasomi waliambia gazeti hili jana kwamba, uamuzi huo wa serikali unakwenda kinyume na kilichomo katika ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo ina kipengele kinachoruhusu kuanzishwa kwa mahakama hiyo.

Juzi Waziri wa Sheria na Katiba, Mathia Chikawe aliliambia Bunge Tanzania haitaunda Mahakama ya Kadhi badala yake sheria za Kiislamu zitaingizwa katika sheria za nchi ili zitumike katika mahakama ya kawaida.

Katibu wa Kamati ya Kutetea Mali za Waislamu Tanzania, Sheikh Khalifa Khamisi alisema kamati hiyo inatarajia kupinga hatua ya serikali kufuta ombi la kuanzishwa Mahakama ya Kadhi na kutoa tamko lake rasmi Jumapili hii.

Sheikh Khamisi aliliambia gazeti hili jana kuwa, hoja ya serikali kwamba yenyewe haina dini ndiyo maana imeamua kupinga hatua hiyo, siyo sahihi.

"Serikali imesema kuwa haina dini, kwa nini basi iwazuie Waislamu kuanzisha mahakama ambayo wanaitambua kwa mujibu wa imani ya dini yao?"alihoji Sheikh Khamisi na kuongeza:

"Tena mambo haya wanafanyiwa Waislamu tu na sio dini nyingine hasa baada ya maaskofu kutishia kujitoa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kufutiwa misamaha ya kodi," alisema Khamisi.

Alisema kamati yake inaipinga vikali kauli hiyo ya serikali iliyotolewa juzi bungeni na Waziri wa Sheria wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2009/10.

"Serikali inawaogopa sana maaskofu na kuwadidimiza Waislamu hata pale wanapokuwa na haki sawa na wengine na imekuwa ikiwapuuza na kuwasahau," alisema.

Alidai kuwa wameziona taasisi kadhaa za dini ya kikristo zikifanyabiashara kwa kivuli cha kutoa huduma za kiroho, lakini serikali imekaa kimya tena.

“ Tena baadhi ya makanisa yanafanya mambo kinyume na taratibu za nchi, serikali imeshindwa kuyakemea, lakini wanaliona hili la Waislamu ambao wanyonge kuwa halifai," alisema Sheikh.

Alisisitiza kuwa suala la kuwapo kwa Mahakama ya Kadhi ni haki ya Waislamu kama ilivyo katika nchi nyingine ambazo wamepewa uhuru kamili wa kuabudu wanachoamini.

Nalo Baraza kuu la Waislamu Tanzania, (Bakwata) limesema litatoa tamko rasmi kuhusu kauli ya serikali kufuta mpango wa kurudisha mahakama hiyo.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Suleiman Lolila aliliambia gazeti hili ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es Salaam jana kwamba, tamko hilo litatolewa baada ya Mufti Mkuu, Sheikh Issa bin Shaaban Simba kukutana na baraza la Masheikh, ili kujadili suala hilo.

“Tamko rasmi la Bakwata kuhusu kufutwa kwa mpango wa kurudisha Mahakama ya Kadhi litatolewa na Mufti kesho (leo) saa nne asubuhi baada ya kukutana na Baraza la Masheikh,” alisema Sheikh Lolila.

Sheikh Lolila alisema kuwa, Baraza la Masheikh wa mkoa wa Lindi limemteua, Sheikh Mohammed Said Mushangani kuwa kaimu Sheikh wa Mkoa wa Lindi ili kuziba pengo la Marehemu Sheikh Gorogosi aliyefariki kwa ajali ya gari hivi karibuni mkoani humo.

Kwa mujibu wa Sheikh Lolila, Sheikh Mushangani atashika wadhifa huo hadi uchaguzi utakapokamilika mwezi Agosti.

“Kwa sasa tuko kwenye uchaguzi ambao utakamilika mwezi Agosti, hapo ndipo Lindi watakuwa na Sheikh wao rasmi,” alisema Lolila.

Wakati huo huo aliyekuwa Mwenyekiti wa Bakwata, Sheikh Khamis Mataka alisema kauli ya serikali kuizima hoja ya Mahakama ya Kadhi ina mapungufu mengi na kwamba, wanaisubiri katika mkutano ambao iliahidi kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu kujadiliana kuhusu jambo hilo.

"Tunafanya busara sana kuisubiri serikali kwa kuwa imeahidi kukutana na viongozi wa dini ya kiislamu. Ndipo sisi wanazuoni tutakapotoa hoja zetu na kuweka wazi mapungufu ya maamuzi hayo ya kuifuta mahakama,"alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Baraza Kuu, Jumuiya na Taasisi zote za Kiislamu Tanzania, Ramadhani Sanze alisema wameisikia kauli hiyo ya serikali kupitia kwa waziri wake ya Sheria na katiba, Mathias Chikawe.

Alifahamisha kuwa masheikh wanafanya mkutano wa siku mbili kujadili suala hilo na kwamba, watatoa tamko lao Ijumaa wiki hii.

Alisema hawana haja ya kuyafanya mambo hayo kuwa marefu, isipokuwa serikali itaona ni nini Waislamu wanahitaji kifanyike kwa mujibu wa imani ya dini yao na kuridhika nacho.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwaomba radhi Watanzania kutokana na kutotekeleza moja ya vipengele vya Ilani ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambayo inaeleza kuwa itaruhusu kuwepo na Mahakama ya Kadhi nchini.

Profesa Lipumba aliliambia gazeti hili jana kuwa moja ya vipengele katika Ilani ya CCM ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ilikuwa ni pamoja na kuruhusu kuwepo kwa mahakama hiyo; hivyo kitendo cha serikali kushindwa kutekeleza ahadi hiyo, rais Kikwete anatakiwa awajibike kwa kuwaomba radhi Watanzania waliompigia kura.

"Ni jambo ambalo lipo wazi kabisa, kwa sababu ilani ya uchaguzi inajadiliwa na kupitishwa na chama, hivyo kutokana na hili serikali imeonyesha ni jinsi gani ilivyowadanganya Watanzania. Huu ni 'usanii' kabisa wanaonyesha kuwa hawako makini katika masuala mazito kama hili," alisema Lipumba na kuongeza:

"Wananchi humchagua mtu kutokana na sera zake, hivyo wapo watu walioichagua CCM kwa sababu tu katika kampeni zao walisema watatekeleza suala la Mahakama ya Kadhi".

Katika hotuba yake juzi Chikawe alisema mchakato wa kufikia hatua ya kuzijumuisha sheria hizo za Kiislamu kwenye sheria za nchi lazima upate maoni kutoka kwa madhehebu yote ya Kiislamu nchini.

Naye Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Samwel Ruhuza alilieleza gazeti hili jana kuwa Ilani ya CCM katika uchaguzi wa mwaka 2005, ilisema itashughulikia kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi kama moja ya ajenda kubwa za kuwashawishi wapiga kura.

"Hoja hii ilitumiwa na CCM mwaka 2005 na iliungwa mkono na mmoja wa maaskofu wa Kanisa Katoliki ambaye alitamka kuwa Rais Kikwete ni chaguo la Mungu, hivyo watu wengi walimchagua" alisema Ruhuza na kuongeza:

"Siyo kwamba tunalazimisha kuwepo kwa Kadhi Mkuu, lakini kama suala la Mahakama ya Kadhi lilitumiwa katika ilani ya uchaguzi, basi litekelezwe".

Hoja ya kuwepo kwa mahakama ya kadhi ilianzishwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu lakini ilizimwa, baada ya miaka mitatu iliyopita sakata hilo lilifufuliwa tena na kuwagawa wanasiasa na wananchi katika makundi mawili (wanaounga mkono na wanaopinga).

Wako waliounga mkono na wengine waliipinga kwa maelezo kwamba itasababisha vurugu na mgawanyiko katika jamii.

Imeandikwa na Ummy Muya, Hussein Issa, Elias Msuya na Fidelis Butahe Mwananchi Gazeti
 
Habari ndio hiyo, Mahakama ya Kadhi yapigwa mweleka na Serikali leo 07/01/09.
 
Hapa nafikiri Serikali imefanya jambo la maana la kuziingiza hizo sheria za kadhi ndani ya sheria za nchi.
 
Back
Top Bottom