Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

Juu ya OIC na Mahakama ya Kadhi

CCM naamini imefanya uamuzi mzuri. Uamuzi ambao japo hautawaridhisha watu wote, vile vile hautawaudhi wote.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
nadhani utakumbuka kwamba hata mimi nilipendekeza sana sheria hizi za kiislaam kuingizwa ktk sheria zetu badala ya mahakama ya kadhi na na sababu nilizitoa kwa pande zote mbili..
Ajabu umekuja na maswali ambayo nashindwa kuelewa unachojaribu kujenga hapa..
Kwanza kabisa tulisha sema kwamba Mahakama ya kadhi ni sawa na Civil Court inayo deal na kesi (maswala) za MADAI na siii Criminal cases kama mnavyotaka kuzipamba hoja zenu..
Hivyo maswali yako yote hayana nguvu kama utazingatia ni kitu gani kinachuhusiana zaidi na mahakama ya Kadhi..
Kwa mfano ukiwa una wake zaidi ya mmoja nini haki ya mke wa pili na wa Tatu..Sidhani kama wewe unaweza kunijibu.. na huwezi kumjibu hata Musuguli ambaye kaoa wake zaidi ya mmoja kwa kufuata mila na desturi za kabila lake..
Hapa kama wewe Mkristu swafi, nasema tena SAFI, sheria hii haiwezi kukufiokia kwa sababu utakuwa na mke mmoja tu. Ila hata wale wasiokuwa waislaam maadam wameamua kuona mke wa pili au tatu basi hawa wote waktakuwa na haki zao kwa mume aliyewaoa..Hii ni pamoja na watoto wote waliozaliwa ktk ndoa hizo. Kukataa kuwepo kwa sheria kwa sababu tu mnaona jina Kiislaam ni kutofikiri nje ya box la Udini..Kumbuka hata wale unaowaona sii wakristu wanataka sheria pamoja na kwamba dini au mila zao zinawaruhusu..

Kwa hiyo hofu yako ya hukumu na kufikiria sijui waktakatwa mikono au kupigwa mawe haihusiani pamoja na kwamba hata wakristu wakati wa Yesu walitumia adhabu hizo hizo za waislaam mnazozikataa leo. Kifupi hakuna aya wala sura inayokataza hukumu za kiislaam ambazo zimetumika toka enzi ya Ibrahim, hivyo madai yan kwamba hizi ni hukumu za mahakama za Kiislaam ni uzushi ambao mnashindwa kukubali Ukristu wenu wenyewe..

Kifupi mimi naunga mkono sana fikra hizi na labda shida kubwa itakuja pale ambapo kuna watoto nje ya ndoa.. Hapa ningeishauri serikali kutunga sheria ambayo itawabana wazzazi hasa wa kiume kuchukuwa responsibility ya mzazi pindi mtoto atakapojukana mzazi wake ni nani bila kujali swala la ndoa au laa..

Halafu kulingana na taarifa ya taasisi ya DNA imegundulika kwamba kati ya watoto 10 wanaozaliwa, sita huwa sii wa baba aliyejulishwa.. Hii ikiwa na maana ni asilimia 60 ya watoto hufungiwa baba mzazi (biological father)..Inabidi kila penye mashaka DNA ifanyike mapema kuweza kuepuka mgogoro baadaye..
Nje ya hapo mkuu ningependa sana uelewe kwanza nini mahakama ya kadhi kisha jenga hoja zako zinazohoji kesi au swala linalokutatiza toka mahakama hiyo na sii kuhoji tu mahakama kwa sababu ina jina la Uislaam.

Hapa naona umeamua kudanganya waziwazi kabisa. Hakuna mafundisho ya kikristo yanayofundisha watu kupiga wenzao mawe. Kuna wakati Yesu aliulizwa na Wayahudi swali kuhusu mwanamke aliyefumaniwa kwa uzinzi kwamba kwa Sheria za Musa alitakiwa apigwe mawe, kuhusu hilo Yesu alikuwa anasemaje? Walifanya hivyo ili kumtega. Yesu aliwaambia kwamba asiyekuwa na dhambi na awe wa kwanza kumpiga mawe huyo mwanamke! Hapo ndipo walipoanza kuondoka mmoja moja kuanzia mkubwa hadi mdogo bila kumpiga huyo mwanamke kwa mawe huku Yesu akiwa anaandika chini. Alipoinuka Yesu hakuwaona tena hao Wayahudi na alimuuliza mwanamke kuwa wako wapi akasema wameondoka. YESU ALIMWAMBIA WALA YEYE (YESU) HAMHUKUMU. AENDE NA ASITENDE DHAMBI TENA! Hapa mafundisho ya kupiga mawe yako wapi? Yesu mwenyewe alisema kuwa hamhukumu huyo mwanamke ila alimuonya asitende dhambi. Usidanganye watu kuhusu kitu ambacho hakipo kuhusu Wakristo wanaoshika imani yao ambao huwa wanasisitiza msamaha, upendo, huruma na unyenyekevu katika mafundisho yao huku wakikemea dhambi kwa nguvu zote!
 
Acheni kutubabaisha jamani,kwani waislamu ndio nani katika nchi hii mpaka waundiwe chombo ambacho kitapelekea serikali kuingia gharama za kukiendesha? Ni kwa nini lakini serikali inachezea amani kiasi hiki?Kwani katiba ya nchi inasemaje kuhusu hili? Wasitake kutuingiza kwenye matatizo hatutaki isipokuwa kama wakitulazimisha.NASEMA HATUTAKI OIC HATUTAKI MAHAKAMA YA KADHI AU KUIHUSISHA SERIKALI KATIKA MAMBO YA DINI.Dini zibaki dini na mambo yao na serikali ibaki na mambo yake.Au ndio vile ilivyosemwa kuwa haya yote ni fadhira ya Kikwete kwa waislamu?Najisikia kichefuchefu ninapoyasikia haya?
Na Leon Bahati, Dodoma (mwananchi)

SERIKALI imetoa msimamo wake kwamba, Tanzania haitaunda Mahakama ya Kadhi na badala yake itatafsiri sheria za Kiislamu na kuzijumuisha kwenye sheria za nchi, ili zitumike kwenye mahakama za kawaida hapa nchini.

Uamuzi huo wa serikali unatokana na mapendekezo yaliyowasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Tume ya wataalamu waliochambua mapendekezo ya utafiti uliofanywa na Kamati ya Kurekebisha Sheria.

Hata hivyo, uamuzi huo wa serikali ulipingwa vikali na Mbunge wa Kigoma Kusini, Manju Msambya (CCM), ambaye alisisitiza kuwa haoni kosa kwa Waislamu kuundiwa mahakama hiyo.

Msimamo wa serikali ulitolewa bungeni jana na Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe wakati akiwasilisha makadirio na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2009/10.

Hata hivyo, Chikawe alisema mchakato wa kufikia hatua ya kuzijumuisha sheria hizo za Kiislamu kwenye sheria za nchi lazima upate maoni kutoka kwa madhehebu yote ya Kiislamu nchini.

''Hivi sasa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imeanzisha mchakato wa kukusanya mawazo na maoni kutoka kwa viongozi wa madhehebu yote ya dini ya Kiislamu kwa nia ya kuorodhesha misingi ya dini ya Kiislamu, hususan ile inayohusu sheria binafsi kwa madhumuni ya kuihuisha misingi hiyo katika sheria za nchi, kwa kuzingatia sheria ya The Islamic Law Act, sura ya 375 ya mwaka 1964,'' alifafanua Chikawe na kuongeza:

''Kimsingi baada ya viongozi hawa wa dini kukubaliana kuhusu misingi hii, basi Waziri wa Sheria atatoa tamko kuhusu misingi hiyo na baada ya hapo kwa mujibu wa Ibara ya tatu ya sheria hii, matamko haya yatakuwa ni sheria zitakzotambuliwa na mahakama zetu zote hapa nchini.''

Alisema lengo la serikali la kutumia mfumo huo ni kuweka utaratibu utakaolinda haki za waumini wa Kiislamu bila kuathiri misingi ya Katiba ya nchi.

Chikawe alisema utaratibu kama huo umekuwa ukitumika nchini Afrika Kusini ambako kuna waumini wengi wa Kiislamu na imeonyesha mafanikio.

Akichangia hotuba hiyo, Msambya alipinga utaratibu huo wa serikali na kutaka serikali iunde moja kwa moja mahakama za kadhi ili kutatua matatizo yahusuyo waumini wa Kiislamu.

Vilevile, Msambya alitaka Tanzania ijiunge na Jumuiya ya Uislamu Duniani (OIC), kwa kile alichoeleza, nchi itafaidika kwa mambo mengi kama ilivyo Uganda na Msumbiji.

Katika hatua nyingine, Msambya alilishutumu Kanisa Katoliki nchini kwa kutoa waraka ambao unawafundisha waumini wake kuhusu namna ya kuchagua viongozi bora.

Waraka huo wa Kanisa Katoliki ulikuwa unawaasa waumini wake wasiwachague viongozi ambao wana tabia ya kubadilika badilika kama kinyonga.

Msambya ambaye hakutaja moja kwa moja dhehebu la dini lililotoa waraka, alisema unapingana na kanuni kwamba watu wasichanganye dini na siasa.

Akizungumza kwa jazba, Msambya alisema alichukizwa na kitendo cha waziri ambaye hakumtaja, kwamba alipoulizwa na waandishi wa habari kuhusiana na waraka huo, aliusifu akisema ni mzuri kwa sababu ni moja ya elimu ya kupiga kura.

Hoja ya kuwepo kwa Mahakama ya Kadhi ilianzishwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu lakini ilizimwa, kisha ikafufuliwa tena miaka mitatu iliyopita na kuwagawa wanasiasa na wananchi katika makundi mawili. Wako waliounga mkono na wengine waliipinga kwa maelezo kwamba itasababisha vurugu na mgawanyiko katika jamii.

Maswali:
- Kwa kuingiza baadhi ya sheria za dini ya Kiislamu katika sheria za nchi kunaondoa haja ya kuwepo mahakama ya kadhi? Yaani, mahakama za kawaida zitumikee kufanya kazi ya mahakama za Kadhi?

- Je, mahakama za kawaida za nchi zinapotoa hukumu kwa mujibu wa kufuata sheria za Kiislamu je Muislamu analazimika kutii hukumu hizo kana kwamba ni za mahakama ya kidini?

- Je adhabu zitakazotolewa kwa mtu anayevunja sheria hizo mpya zitaendana na adhabu zinazotolewa kama ingekuwa ni mahakama ya Kiislamu?

- Kwa vile sheria hizo zitaingizwa kwenye sheria za kawaida za nchi, je zitawahusu vipi wananchi wengine? Kama zitawekwa kwa ajili ya waislamu tu je hicho si kinyume na Katiba ambapo mamlaka ya nchi inapitisha sheria za kibaguzi (moja za wananchi wote na nyingine za waislamu tu)?

- Kwanini serikali isiamue kuweka mazingira ambapo Mahakama ya Kadhi inaundwa na Waislamu wenyewe kwa misingi ambayo wao wanaikubali na pale ambapo kunahitajika msaada wa serikali basi ijulikane ni kwa vipi na kwa namna gani?
 
Acheni kutubabaisha jamani,kwani waislamu ndio nani katika nchi hii mpaka waundiwe chombo ambacho kitapelekea serikali kuingia gharama za kukiendesha? Ni kwa nini lakini serikali inachezea amani kiasi hiki?Kwani katiba ya nchi inasemaje kuhusu hili? Wasitake kutuingiza kwenye matatizo hatutaki isipokuwa kama wakitulazimisha.NASEMA HATUTAKI OIC HATUTAKI MAHAKAMA YA KADHI AU KUIHUSISHA SERIKALI KATIKA MAMBO YA DINI.Dini zibaki dini na mambo yao na serikali ibaki na mambo yake.Au ndio vile ilivyosemwa kuwa haya yote ni fadhira ya Kikwete kwa waislamu?Najisikia kichefuchefu ninapoyasikia haya?

Wewe hujui usemalo.

Unjwa kuna mahakama ya Biashara, Mahkama ya Kazi n.k.

Je serikali inapoingia gharama kuziendesha ina maana watu wote ni wafanya kazi au wafanya biashara?.

Maoni yako yamejaa chuki mno lakini yanadhihirisha upeo wako ulivyokuwa duni.

CCM naamini haikukurupuka ilifanya tathmini na ikaona kama Yes inawezekana waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi (kumbuka mahakama hii ilikuwepo tangu enzi za ukoloni lakini ikaondolewa na serikali ya awamu ya kwanza). Waka iweka kwenye ilani yao ya uchaguzi.

Walivyokuwa wanataka kuifanyia kazi..wazee wa Kanisa wakasikia. Wakapiga mkwara mzito wakisaidiwa na wawakilishi wao kule bungeni. Serikali ikatishwa kutazamwa upya uhusiano wake na kanisa kama uko mashakani iwapo itathubutu kuanzisha mahkama hiyo.

Kama walivyorudia tena kwenye sakata la kufutwa kwa misamaha ya kodi..serikali yetu ilifyata mkia. Na ilikuonyesha kama ni tiifu kwa kanisa imechagua kipindi hiki ambacho joto limepanda na kuzidi kuweka msumari wa moto kwenye kidonda.

Ah waislamu kwani wana nini cha kutisha? wao hawana Jeshi kama lile la uokovu (Salvation Army), hawana mkakati wa kutoa elimu kwa wapiga kura na inshort sio tishio kwa uwepo wa serikali hii. Kiufupi wingi wao ni kama mapovu tu. They can be dealt and trated kama inavyodhaniwa ndivyo.

Tanzania tunapanda mahusiano mabaya mno..tunajenga chuki mbaya kati yetu raia. Mimi kwetu ni Tanga, Wallahi sikuwa ninajuwa kama kuna udini mpaka nilipotoka nje ya mkoa ule. Nimekaa na kuishi na Wakristo kama ndugu, tumesoma na kulala pamoja kwenye nyumba zao na zetu. Na kwa sisi watu waTanga nina ndugu kibao waksrito.

Waswahili wanasema kuwa na tembea uyaone..kweli nieyaona. Yaani kuna mijitu na kukosa kwa haya imekuwa milafi, mibaguzi inataka kuhodhi kila kitu. Yote haya najuwa yamepandikizwa na mtu mmoja. Ee Mungu ee zidi kumhalikisha chokochoko huyu. Ametuletea taabu mno Tanzania yetu.

Yaani Mtanzania kwenye nchi yako unajiona ni mtumwa. Laa Haula. Sallaale.

Kingwele.
 
Acheni kutubabaisha jamani,kwani waislamu ndio nani katika nchi hii mpaka waundiwe chombo ambacho kitapelekea serikali kuingia gharama za kukiendesha? Ni kwa nini lakini serikali inachezea amani kiasi hiki?Kwani katiba ya nchi inasemaje kuhusu hili? Wasitake kutuingiza kwenye matatizo hatutaki isipokuwa kama wakitulazimisha.NASEMA HATUTAKI OIC HATUTAKI MAHAKAMA YA KADHI AU KUIHUSISHA SERIKALI KATIKA MAMBO YA DINI.Dini zibaki dini na mambo yao na serikali ibaki na mambo yake.Au ndio vile ilivyosemwa kuwa haya yote ni fadhira ya Kikwete kwa waislamu?Najisikia kichefuchefu ninapoyasikia haya?

Hapo nilipo highlight kwa rangi nyekundu andika "CCM"
 
Kuna mengi yameandikwa lakini ningependa kusema kuwa Mahakama ya Kadhwi tanzania itakuwa ni Civil court kwa ajili ya waislam hususan kwa civil cases yaani kesi za madai tu

Ukiangalia kiundani mahakama hizi zitashughulikia kesi za Ndoa, talaka na mirathi tu ambayo itafuata taratibu za kiislamu.

Sasa nikiangalia sheria hizi na ndoa ,talaka na miradhi za kiislamu kuzichanganya katika sheria za nchi pamoja na kuwa itakuwa kuvunja katiba ya nchi lakini pia itakuwa ni kuongeza confusion katika katiba ya nchi.

Sasa tunapotaka lumbana tuangalie katika nyanja ya mahakama ya Kadhwi katika civil cases hususan ndoa, miradhi na talaka.
 
Acheni kutubabaisha jamani,kwani waislamu ndio nani katika nchi hii mpaka waundiwe chombo ambacho kitapelekea serikali kuingia gharama za kukiendesha? Ni kwa nini lakini serikali inachezea amani kiasi hiki?Kwani katiba ya nchi inasemaje kuhusu hili? Wasitake kutuingiza kwenye matatizo hatutaki isipokuwa kama wakitulazimisha.NASEMA HATUTAKI OIC HATUTAKI MAHAKAMA YA KADHI AU KUIHUSISHA SERIKALI KATIKA MAMBO YA DINI.Dini zibaki dini na mambo yao na serikali ibaki na mambo yake.Au ndio vile ilivyosemwa kuwa haya yote ni fadhira ya Kikwete kwa waislamu?Najisikia kichefuchefu ninapoyasikia haya?
.

Hapo muungwana naona imekupuruchuka.

Labda nikuulize kidogo. Mbona kuna balozi wa VATICAN huko Tanzania? je huyo balozi anamwakilisha nani? na yupo kwa maslahi ya nani?

Mind you Vatican ni kajisehemu ndani ya Italy kama ilivyo Zanzibar katika Tanzania.
 
Hii mada tulisha ijadili nakumbuka zamani. Lakini mimi bado nawauliza ndugu zangu waislam, "hivi ni kweli kwamba sheria na mahakama zilizopo hazitoi hukumu mkaridhika mpaka muwe na sheria zenu pamoja na mahakama?" Mimi naona hapa haya ni mawazo ya watu wachache (viongozi) wa madhehebu ya kiislam kutaka kuwaburuza wenzao.

Ni juzi tu mmeona wenzenu wamekatwa vikanyagio na viganja bado mnang'ang'ana na sheria zenu, tumieni akili hizo hela mnazopata kutoka uarabuni zitawatokea puani. Mnaingia mikataba ya kishenzi na waarabu eti mtaanzisha sheria za kiislam nchini bila hata ya kuwauliza waumini wenu.

Angalia unafiki wa viongozi wa kiislam, mzee mwinyi alipopigwa kofi walifurahi eti mzee mwinyi alikosea kuwaambia watumie kondom la sivyo ukimwi utawamaliza. Ndo hizo sheria nzuri za kiislam mnazo taka zinazo ruhusu muumini wa kiislam kumpiga kofi rais mstaafu halafu mashehe hawa hawa wanafurahi.......?

Nawashauri, dini bila elimu itawamaliza.......msitake kutumaliza na sisi.
 
.

Hapo muungwana naona imekupuruchuka.

Labda nikuulize kidogo. Mbona kuna balozi wa VATICAN huko Tanzania? je huyo balozi anamwakilisha nani? na yupo kwa maslahi ya nani?

Mind you Vatican ni kajisehemu ndani ya Italy kama ilivyo Zanzibar katika Tanzania.

mambo ya vatican kuwepo hapa ni sawa na ubalozi wa iran kuwepo hapa bongo. Uliwahi kusikia vatican inaitaka serikali ya Tanzania kuweka mahakama ya wakristu (wakatoliki)?

Kama waislam wana haja ya mahakama hizo si waanzishe? nani kawa kataza? Tunachopinga ni kutumia pesa ya serikali (ya wananchi wasio waislam) kuendesha mahakama ya waislam.

Mbona wakristu wanatatua migogoro yao ya mambo ya ndoa n.k. wenyewe? Na yanayo shindikana yanaenda mahakama za kawaida?
 
i do support kutokuwa na mahakama ya kadhi na kutojiunga na OIC. Za kazi gani while this country haifuati misingi ya dini yoyote. We should respect that principle which made live peaceful until today
 
hizi mahakama za kadhi jamani tuachane nazo na biashara ya kuziingiza kwe sheria nayo sidhan ka ni wazo zuri..ninaloshauri hapa ni kwamba sheria zilizopo za nchi zisizoangalia dini wala kabila ndo ziendelee..wanaotaka kutawaliwa na sheria za kiislam wajameni ruksa mtu kwenda akaish iran..
Tanzania hatuwezi kuanza ku-accomodate kila matakwa ya kila dini..maana huu ni mwanzo tu..mtasikia wakristo nao wataleta zao..budhists nao watadai zao na rastafarians as well..kwahiyo ni muhimu yote haya yangeangaliwa kwa kina kabla ya kutolea maamuzi..kikwete aimarishe uchumi...mambo ya ma-kadhi na nin ni kuogopa kukosa kura za waislamu tu hana lolote..jenga uchumi maisha ya watu yawe bora..achana na kujitafutia regitimacy kwe mambo ya kipumbavu ambayo yanaweza kugawa umma..
 
mambo ya vatican kuwepo hapa ni sawa na ubalozi wa iran kuwepo hapa bongo. Uliwahi kusikia vatican inaitaka serikali ya Tanzania kuweka mahakama ya wakristu (wakatoliki)?

Kama waislam wana haja ya mahakama hizo si waanzishe? nani kawa kataza? Tunachopinga ni kutumia pesa ya serikali (ya wananchi wasio waislam) kuendesha mahakama ya waislam.

Mbona wakristu wanatatua migogoro yao ya mambo ya ndoa n.k. wenyewe? Na yanayo shindikana yanaenda mahakama za kawaida?

na mkishamaliza wote wenye dini kuomba mahakama zenu, nasi tusio na dini pamoja na wale wenye dini za jadi (ambazo ndo asili yetu, ukristo na uislam uliletwa na wazungu na waarabu respectively) tutaomba mahakama zetu za kukubaliwa masuala yetu ya kipagani/kikafir na ya jadi.
naona hapa ufundi ni kushindanisha dini bora na kutokujiamani tu.
kuna mtu mwenye data za kuonyesha ni ndoa ngapi zinavunjika, watoto wangapi wanadhurumiwa nk, nk. tunaacha kuangalia matatizo ya malaria, umasikini na ujinga tunakaa na colonised minds zetu. miafrika bwana argghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh
 
MASWALI MAGUMU KWA WAISLAM WENZANGU
1- kutokuwapo kwa mahakama za kadhi na nchi kutoingia IOC mumepungukiwa nini hasa???
2- hamuoni kuwa uwapo wa mahakama 2- kwa wakati mmoja ambazo kisheria zinatakiwa zifuatile mienendo ya waislamu itakuwa ni taabu na wakati mgumu kwenu waislamu??
3- je ni kweli mahakama zilizopo haziwatendei haki kama waislamu??...maana matatizo yote katika jamii yanaamulika na maakama zetu kwa sheria zilizopo...kuanzia hiyo mirathi mpaka hizo ndoa na haki za watoto...ndioo...si marehemu kuandika wosia na kukabidhi mahala panapoeleweka kisheria..na ukasomwa siku atapofariki..
4- je ni kweli tunataka kujiunga IOC ili TUPEWE MISAADA???....HUO sio umasikini wa fikira??
NAOMBA MAJIBU SAHIHI KWAA MASWALI HAYA MAGUMU
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji,
nadhani utakumbuka kwamba hata mimi nilipendekeza sana sheria hizi za kiislaam kuingizwa ktk sheria zetu badala ya mahakama ya kadhi na na sababu nilizitoa kwa pande zote mbili..
Ajabu umekuja na maswali ambayo nashindwa kuelewa unachojaribu kujenga hapa..
Kwanza kabisa tulisha sema kwamba Mahakama ya kadhi ni sawa na Civil Court inayo deal na kesi (maswala) za MADAI na siii Criminal cases kama mnavyotaka kuzipamba hoja zenu..
Hivyo maswali yako yote hayana nguvu kama utazingatia ni kitu gani kinachuhusiana zaidi na mahakama ya Kadhi..
Kwa mfano ukiwa una wake zaidi ya mmoja nini haki ya mke wa pili na wa Tatu..Sidhani kama wewe unaweza kunijibu.. na huwezi kumjibu hata Musuguli ambaye kaoa wake zaidi ya mmoja kwa kufuata mila na desturi za kabila lake..
Hapa kama wewe Mkristu swafi, nasema tena SAFI, sheria hii haiwezi kukufiokia kwa sababu utakuwa na mke mmoja tu. Ila hata wale wasiokuwa waislaam maadam wameamua kuona mke wa pili au tatu basi hawa wote waktakuwa na haki zao kwa mume aliyewaoa..Hii ni pamoja na watoto wote waliozaliwa ktk ndoa hizo. Kukataa kuwepo kwa sheria kwa sababu tu mnaona jina Kiislaam ni kutofikiri nje ya box la Udini..Kumbuka hata wale unaowaona sii wakristu wanataka sheria pamoja na kwamba dini au mila zao zinawaruhusu..

Kwa hiyo hofu yako ya hukumu na kufikiria sijui waktakatwa mikono au kupigwa mawe haihusiani pamoja na kwamba hata wakristu wakati wa Yesu walitumia adhabu hizo hizo za waislaam mnazozikataa leo. Kifupi hakuna aya wala sura inayokataza hukumu za kiislaam ambazo zimetumika toka enzi ya Ibrahim, hivyo madai yan kwamba hizi ni hukumu za mahakama za Kiislaam ni uzushi ambao mnashindwa kukubali Ukristu wenu wenyewe..

Kifupi mimi naunga mkono sana fikra hizi na labda shida kubwa itakuja pale ambapo kuna watoto nje ya ndoa.. Hapa ningeishauri serikali kutunga sheria ambayo itawabana wazzazi hasa wa kiume kuchukuwa responsibility ya mzazi pindi mtoto atakapojukana mzazi wake ni nani bila kujali swala la ndoa au laa..

Halafu kulingana na taarifa ya taasisi ya DNA imegundulika kwamba kati ya watoto 10 wanaozaliwa, sita huwa sii wa baba aliyejulishwa.. Hii ikiwa na maana ni asilimia 60 ya watoto hufungiwa baba mzazi (biological father)..Inabidi kila penye mashaka DNA ifanyike mapema kuweza kuepuka mgogoro baadaye..
Nje ya hapo mkuu ningependa sana uelewe kwanza nini mahakama ya kadhi kisha jenga hoja zako zinazohoji kesi au swala linalokutatiza toka mahakama hiyo na sii kuhoji tu mahakama kwa sababu ina jina la Uislaam.

Ukiona dini fulani inataka 'favour' ujue kuna jambo limefichika. Na hakika 'reading the signs of the time' si Mahakama ya Kadhi tu bali huo utakuwa mlango wa kuingiza taratibutaratibu sheria zingine za Kiislamu kwenye katiba.

Cha muhimu ni kwamba hakuna anayewakataza Waislamu kuwa na Mahakama ya Kadhi na kuiendesha kwa jinsi wanavyoona inawafaa wao wenyewe kama wanavyofanya waumini wa dini nyingine.

Lakini kuifanya hiyo iwe sehemu ya Katiba na halafu kufanya hivyo ndiyo iwe nchi kuwajali Waislamu, mimi naona ni kwenda mbali mno. Kwa kweli mimi sioni tatizo liko wapi! Waislamu wawe na Mahakama za Kadhi. Lakini Katiba ya nchi iendelee kutoa uhuru wa kuabudu wa waumini wa dini zote bila upendeleo.
 
na mkishamaliza wote wenye dini kuomba mahakama zenu, nasi tusio na dini pamoja na wale wenye dini za jadi (ambazo ndo asili yetu, ukristo na uislam uliletwa na wazungu na waarabu respectively) tutaomba mahakama zetu za kukubaliwa masuala yetu ya kipagani/kikafir na ya jadi.
naona hapa ufundi ni kushindanisha dini bora na kutokujiamani tu.
kuna mtu mwenye data za kuonyesha ni ndoa ngapi zinavunjika, watoto wangapi wanadhurumiwa nk, nk. tunaacha kuangalia matatizo ya malaria, umasikini na ujinga tunakaa na colonised minds zetu. miafrika bwana argghhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh

Ulivyosema ni sawa kwamba tunaacha mambo ya msingi.....lakini hapa ndipo wametufikisha akina nyerere na wengine waliotangulia, je tufanyeje? inabidi kukabiliana na hali jinsi ilivyo. huwezi kuishia kusema miafrika ndivyo tulivyo, then what next? na mabadiriko lazima tuyatafute sisi wenyewe.

Kweli tumerithishwa dini zisizo zetu lakini hapa ndipo tulipo hatuwezi kurudi nyuma kuanza kusali kwenye miti mikubwa kama wahindi (wahindu) wanaoabudu mto Ganga kuwa ndo mungu wao!!

Ukichinja ng'ombe india nadhani unapata hukumu ya kifo (sina hakika) lakini ng'ombe ambaye dar es salaam ni kitoweo cha kila siku hapa ni mungu wa watu....sasa sijui sisi dini zetu za asili zilikuwaje make mimi hata sizijui.

Dini hata ukiiga angalia mambo ya maendeleo kijamii, kiafya, kiuchumi n.k. sasa hawa wenzetu wanadhani kuswali tu....basi mambo yamekwisha....hapana. Hawana tofauti na wezi wa DECI.
 
Sasa wewe unataka kufanya nini? KAA ANGALIA TU! Hakuna tatizo lolote kwa Waislamu kuwa na Mahakama yao. Kuna vitu ambavyo Waislamu wanataka vishughulikiwe na Mahakama ya Kadhi kama Mirathi, ndoa nk. Sheria kama hizi haviwezi kuwasumbua waumini wa dini zengine. Nchi nyingi tu zilizoendelea zimeanza na sheria za kidini.

kwenye sheria za dini mirathi inawapa nguvu wanaume, wakati serikali inajaribu kuwainua wanawake, wanawake hawaruhusiwi madaraka kwenye vyombo vya dini uoni kwamba hii itakuwa inaenda kinyume na juhudi za serikali za kuwashirikisha wanawake...
ni mwanamke gani mwenye akili atakubali ndoa yake iwe kwenye mahakama ambayo aimpi haki....
mwanamke yeyote atakupeleka kwa serikali mkaachane labda wale ambao uwelewa wao ni mdogo

wakati nchi za middle east zinaangaika kuwa modern TZ inaangaika kurudi nyuma lo
hata hao iran, saudia, kuwait et al wana modernise sheria zao

sheria za kidini ni za kinyume

kuoa wake wengi inaruhusiwa, huo ni ukandamizaji wa wanawake moja kwa moja, sheria za dini zote including za kikristu zinakandamiza wanawake hasa hasa kwenye uongozi, eit mwanamke haruhusiwi kuwa padri au shekh
 
Ulivyosema ni sawa kwamba tunaacha mambo ya msingi.....lakini hapa ndipo wametufikisha akina nyerere na wengine waliotangulia, je tufanyeje? inabidi kukabiliana na hali jinsi ilivyo. huwezi kuishia kusema miafrika ndivyo tulivyo, then what next? na mabadiriko lazima tuyatafute sisi wenyewe.

Kweli tumerithishwa dini zisizo zetu lakini hapa ndipo tulipo hatuwezi kurudi nyuma kuanza kusali kwenye miti mikubwa kama wahindi (wahindu) wanaoabudu mto Ganga kuwa ndo mungu wao!!

Ukichinja ng'ombe india nadhani unapata hukumu ya kifo (sina hakika) lakini ng'ombe ambaye dar es salaam ni kitoweo cha kila siku hapa ni mungu wa watu....sasa sijui sisi dini zetu za asili zilikuwaje make mimi hata sizijui.

Dini hata ukiiga angalia mambo ya maendeleo kijamii, kiafya, kiuchumi n.k. sasa hawa wenzetu wanadhani kuswali tu....basi mambo yamekwisha....hapana. Hawana tofauti na wezi wa DECI.

Baadhi ya mambo ambayo dini zenu zilikuwa zikiyafanya ni mfano mtemi akifa, anazikwa na vijana wakiwa hai, watoto mapacha walikuwa wakiuliwa mara tu baada ya kuzaliwa na pia nyoka, vichaka, mawe makubwa nk vilikuwa vikiabudiwa!
 
naaaaaaaaaaaaaam umenipa-ta. tutavidai navyo viwekwe kwenye katiba. na please naomba usiniingilie kwenye uhuru wangu wa kuabudu. zamani tulikua na hii haki lakini baada ya kuingia waarabu, wazungu na JKN haki zetu zikachukuliwa. tumekaa kimya kwa zaidi ya miaka 200, nasi wenzetu wakishafanikiwa tunadai za kwetu. ilitusaidia sana maana haya mambo ya mashoga, wasagaji, walawiti na wabakaji hawakuwepo. tunataka kuirudisha jamii yetu kwenye uafrika wetu kamili
 
afadhali kama wametupilia mbali swala la mahakama ya kadhi na sioni umuhimu wa kuweka sheria za kiislamu kwenye sheria za nchi hambo kwa mtazamo wangu lina utata mkubwa, kwa sababu watanzania sio wote walio waislam
 
Back
Top Bottom