Julius Nyerere: Katika Uchaguzi wa mwaka 1995, Kamati Kuu ya NEC-CCM ilikata jina la Lowassa kwa hoja

ungemuuliza Sokoine ni kitu gani alifanya Lowassa akaletwa Dar kijiweni mpaka akaombewa msamaha ndio akarudishwa kundini. Nyerere alishamuwekea X huyu mwizi siku nyingi. Japo simuungi au sikumuunga mkono Nyerere kwa mambo mengi lakini hili la kufumbua macho WaTZ wengi kuhusu mfisadi Lowasa namshukuru mno. Ukweli mimi nilikuwa miongoni mwa waliomshabikia sana Lowasa 1995 lakini baada ya Nyerere kumwanika na hapo na yeye mwenyewe Lowasa kuonyesha waziwazi alivyo duuuu
Bado hujasema lowasa alifanya nini?
Mpaka sahz ila unatoa maneno matupu..
Ainisha sokoine alimuhamisha lowasa kwa sababu hii Na hii!

Wote tunajua kuwa Sokoine Dhumuni lake lilikuwa kuwa Rais wa Tanzania na yoyote yule aliyekuwa anaonyesha Dalili za kutaka urais Alimtafutia zongo kama sio kumjengea kamati
 
Huyu alipewa tu ushindi na Mwl.
Hapana mkapa round ya pili alimshinda jk kwa kura chache,,hazifiki hata 50,,nimetoka kuangalia video yake iko TBC,,,mwinyi ndo alitangaza matokeo,tafuta hiyo video nimeshindwa ku copy,mtandao uko very slow
 
We unahisi kwanini Kipind hicho lawama zilienda kwa Nyerere zote watu wakawa wanamsema katumia Vigezo gani kumkataa Lowasa..

Na baadae Team.ya ENL ikahamia kwa JK..
Akashtuka Pia na ndo maaana Inasemekana hata JK alishinda Mwaka 1995 ila Matokeo akapewa Ben na hata Kama unakumbuka Kura hazikutangazwa ila alitangazwa mshindi wa kwnza mpaka wa tatu bila kura zao

View: https://youtu.be/_MrghqPeOHg?si=Ms8uht5RohO0eeOI
 
SHERIA ya PCCB na ya Maadili ya Viongozi inapinga "mitikasi ya kujitafutia maishani," ambayo serikali haiijui.

Ndo maana:

1/ kuonekana na mali kuliko salary scale yako ni reasonable suspicion ya ku justify wewe kuchunguzwa na PCCB
2/ kiongozi anaorodhesha utajiri na umaskini wake siku anaingia, na kila mwaka. Kwa nini?

Huwezi kuwa na dhamana ya kusaini mabilioni ya manunuzi na mikataba ya umma, na kugawa mapande ya nchi kwa wawekezaji halafu tunakuona una ma mabilioni ya mali, ukiulizwa kwenye vikao vya michujo ya chama unasema nina "mitikasi ya kujitafutia maisha." Itaje ! Tuonyeshe ankara za mitikasi yako, sina, mitikasi yangu ni halali ila ni ya juu kwa juu, inafanyika mahotelini na kwenye simu, na ma njiani, hakuna registered business. Ahaaa, kwa hiyo unapata lakini hulipi kodi ya mapato wanayolipa wenzio Kariakoo? Oooh, naonewa! Ohh, nyinyi washamba wa maisha.

Wewe usiyeheshimu sheria ndio mshamba! NI SHERIA.
Wachana na mambo ya salary scale, watu wanawekeza vijimishahara vyao kidogo wanavyopata wanaenda kulima huko vijijini kuanzia heka mbili, wakivuna wanaongeza tena mbili, mwisho wa siku mambo yao yanabadilika wewe unawaza tu kipato kwa "salary scale"

Wengine wapata mshahara, wananunua ndama, wanakaa nae wanamlisha, akikua, wanaongeza mwingine, mwisho wa siku mtu anakuwa na n'gombe wake kadhaa, anaanza kuuza maziwa, na ngombe pia anauza kwa wenye bucha, nyie mnawaza tu "salary scale".

Watu wanafuga vitimoto kwa mtindo huo mambo yanawanyookea, nyie vichwani ni kile kile "salary scale".

Ndio maana mwisho wa siku licha ya kuwaita wezi bado mnashindwa kuwapeleka mahakamani, kwasababu ya dhana hasi mliyojijengea vichwani ya "salary scale" isiyo na ushahidi wowote.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
 
Kumbe hii kasumba ya mwenye pesa kuonekana mwizi imeanza kututafuna miaka mingi sana, kama unaamini mtu ameiba, na ushahidi unao, mpeleke mahakamani, shida iko wapi?!

Lakini kumnyima haki zake kwa madai ya kihisia, kwasababu tu anaonekana ana pesa ni kumuonea. Lowassa amevumilia mengi toka kwenye jamii ya kishamba iliyokuwa nyuma ya fikra zake za mitikasi ya kujitafuta maishani.

- Jamii inayoona umaskini ni sifa, ndio maana utaskia fulani akijiita mimi mtoto wa maskini. Usipokuwa jasiri mtanzania unaweza kuacha kupambania maisha yako kwa kuogopa kuitwa mwizi!.

Ajabu kuanzia miaka hiyo mpaka miaka ya karibuni bado akawa anaitwa fisadi, kumbe tumerithi tabia ya kuhukumu kwa hisia bila udhahidi toka enzi za Nyerere, tukawa bado tunaishi nayo mpaka sasa, hili ni tatizo la jamii ya kitanzania - awe mpinzani au chama tawala.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Upumbavu wako upo dhahiri shahiri kichwani mwako.
 
Back
Top Bottom