Ujenzi Mradi wa Umeme Bwawa la Julius Nyerere wafikia 74%, Kamati ya Nishati na Madini yaridhishwa

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
2 Bwawa.JPG
Ujenzi wa mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere umefikia 74%, hatua ambayo imebainishwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini iliyofanya ziara katika mradi huo Oktoba 15, 2022.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Stella Manyanya amesema hiyo ni hatua kubwa ukilinganisha na 67% ilivyokuwa awali na kulipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kusimamia vema mradi huo na kumekuwepo na mabadiliko ya wazi yanayoonekana.

Ameongeza kuwa mradi huo ambao utazalisha Megawati 2115 ni tumaini kubwa kwa Watanzania

“Tunampongeza Rais Samia kwa kuendeleza mradi huu kwa kuwa kuna wakati tulikuwa na hofu kuwa unaendaje hasa kipindi ambacho Mawaziri walikuwa wakipokezana. Kamati imeridhishwa na kasi ya ujenzi unaotekelezwa na mkandarasi ambaye pia malipo yake yamelipwa na hatudai,” amesema Manyanya.

Mradi huo ambao utagharimu Tsh. Trilioni 6.5 pindi utakapokamilika na hivyo kuimarisha hali ya upatikanaji wa umeme bora na uhakika kwenye gridi ya Taifa.
3 Bwawa.JPG

Kwa upande wake Naibu Mkurugenzi Mtendaji-Usambazaji, Mhandisi Athanasius Nangali amesema: “Vifaa kwa ajili ya ujenzi wa mradi vimeshawasili ikiwemo Transfoma 29 za njia moja zenye ukubwa wa 92.2 MVA ambazo zitatumika kwenye kituo cha kupoza umeme kutoka kampuni ya ABB. Kati ya Transfoma hizo, 27 ndizo zinatakiwa na 2 ni za akiba.”

Kamati hiyo ilitembelea eneo linakojengwa tuta kuu la kuhifadhi maji “main Dam” ambalo lina sehemu kuu tatu yaani upande wa kushoto, kulia na kati na urefu wa mita 1025 na kimo cha mita 190 kutoka usawa wa bahari.

Eneo lingine walilotembelea ni jengo la mitambo “power house” ambapo itasimikwa mitambo 9 yenye uwezo wa kufua umeme wa Megawati 235 kwa kila moja, pia walifanikiwa kuona hatua zinazoendelea eneo zilikosimikwa Transfoma ambazo zitatumika kwenye kituo cha kupooza umeme kabla ya kusafirishwa kuingia kwenye gridi.
4 Bwawa.JPG
 
Sawa ngoja tusubiri ila Kasi imepungua sna tofauti na kipind Cha hayati dkt magufuli
 
Watanzania wenzangu hebu nisaidieni kuelewa kitu hapa!!

Mwaka 2021 ilifikikia 37% sasa tupo 2022 ,=74%. Then tunaambiwa mpaka 2024 ndiyo likamilike!! Sasa hii iko vp ndugu wadau?
Kimahesabu imebaki 26% likamilike, Swali moja kubwa linashangaza kwanini ndani ya mwaka mmoja unajisifu kazi imefanyika kwa 37% alafu 26% iliyobakia igharimu muda wa miaka miwili yani mpaka 2024???
 
Back
Top Bottom