Tumaini Makene
JF-Expert Member
- Jan 6, 2012
- 2,650
- 6,085
Nasari aliwakilisha kile ambacho viongozi wa Chadema hukisema hasa wanapokuwa wenyewe tu. Kwa hiyo kile alichosema Nasari ni kile hasa Chadema wanaplan kwa nchi yetu nzuri Tanzania.
.
"WASIOSOMA NI CHAKULA CHA WASOMI".
Kadakabikile
Unalipatia hili suala mwelekeo unaoutaka wewe na watu wengine wanaofanana na mawazo kama yako. Msimamo wa CHADEMA katika suala hili uko wazi tangu siku ya kwanza pale pale NMC.
Usiingize maneno yasiyokuwepo kwenye vinywa vya viongozi wa CHADEMA ambao wamedhihirisha pasi na shaka nia na dhamira zao katika kupigania maslahi (haki) ya Watanzania wote, wakiunganisha kila nguvu ya Mtanzania yeyote, wa mahali popote, aliye tayari kujiunga na siasa za vuguvugu kusaka mabadiliko na uhuru wa kweli, hasa mabadiliko ya kiutawala na kimfumo.