Joshua Nassari MB.

Joshua Nassari MB.

Bila samahani ndugu yangu, nilishakusamehe kabla hujawaza kuandika post yako!
Ila tu nikukumbushe kuwa, Dr. Slaa na Chdm inaheshimu sana mawazo yako kama shabiki au mwanachama katika kuimarisha chama. Kudhania kuwa raia hana mchango wowote katka uwajibikaji wa viongozi ndiko kulipotufikisha hapa tunapopalalamikia leo.
Nakushauri, acha ushabiki tumia mantiki katika kuhoji mambo! Pole sana kwa kujidharirisha, ila usiumie sana bado una nafasi ya kuonesha kuwa unaakili, uliteleza tu na hukuanguka, kama alivyoteleza Nassari.
Mungu wetu anaita!


Mwee kweli jinga"Majina uumba" ovyo! kada mkubwa wee!!

 
Well said my brother,

Niliandika pia siku ya kwanza kabisa kuwa nasary bado mdogo na ni mchanga sana katika siasa. Pia nilisema kuwa nafasi

Ubunge aliyoyano imemzidi umri na uwezo i mean sio saizi yake.

At least umenena kweli.

Ni kwa watu kama wewe pekee ndio jamii hupata manufaa ya kweli.

Well done my brother.

Nope! mdai haki yeyote! huuitwa majina mbaya! kama vile gaidi, mhaini etc!! apelekwe mahakamani kama kakosea! He is a freedom fighter!!
 
Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Lakini nadhani nchi hii inahitaji watu watakaotibua hali ili watawala wetu wapate akili. Nakumbuka kuna wakati Mh Mbowe alisema inabidi wakati fulani pawe na Civil disobedience, je utasema Mbowe alikosea? Ni kwa sababu utawala uliopo hauwezi usikia vilio vya watu bila kauli kali kama hizi. Kwa nchi yenye demokrasia ya kweli na iliyotulia, na ambayo viongozi wake ni wasikivu kwa matakwa ya raia wake, kauli ya Nassari ingekuwa mbaya sana, lakini si kwa serikali kama yetu, ambayo kwa kutumia jeshi la polisi wanaifichia CCM ukweli wa mauaji wanayoyafanya kwa viongozi na makada wa vyama vya upinzani.

Natamani kauli kama hizi ziwe nyingi ili kuwaamusha wananchi na kuifanya serikali hii izinduke. Msimamo wangu siku zote ni kuwa CCM haindoki kwa lugha laini laini, lazima iambiwe maneno magumu ambayo hata wakiyasikia masikio yawe yawashwe.

Wito kwa Polisi wetu; acheni kufuatilia mambo yasiyo na umuhimu na kujaribu kuyakuuuuuza; kumbuka walivyomkamata Mbowe kule Dar na kumpeleka Arusha, nguvu kubwa inatumika kwa mambo madogo sana. Wao wanajua kuwa pamoja na Nassari kutamka yale maneno, hana uwezo wa kufanya lolote, ama wananchi wa Arusha hawawezi kufanya chochote kwa kauli ile; kwa nini msifanye mambo muhimu kwa nchi hii?

Ndugu, nadhani hujaichunguza kauli ile! Naweza kuamini kuwa alikuwa anaishinikiza serikali, lakini ukweli huu pia hauwezi pingika..."kauli inapinga umoja tulionao, inaamsha chuki ya watanzania wengine dhidi ya wameru, inajenga picha mbaya kwa chama, inakiuka utaifa wetu" Mbowe hakuwa na maana hiyo, civil disobdience ni kama zile zinazotokea Mbeya, wamerusha mawe, watu kugoma, nk. Lakini huku kwa Nasari sio kuikomoa serikali, bali ni kuwakomoa watanzania wengine! Kwanza atakuwa hajashinda vita, ila ameikimbia, na chuki ambayo itaibuka kati ya watz na wameru sio ya kuizima na maji. Ndio maana nilikuja na mawazo hayo, kuimarisha umoja kumshinda adui yetu. Yalikuwa mawazo yangu mimi, sio amri!
Mungu wetu anaita!
 
Bwana RAGE alipanda na bastola Igunga jeshi halikuona,bwana Mkama akatoa kauli nzito za makomando na walikopata mafunzo bila vielelezo polisi wakaishia kusema CDM iwashtaki kwani wao hawajui,leo kijana kasema hli neno wao wamelipandia juu.Ukweli ni kwamba CCM wanawatumia polisi kuwatishia watanzania wasifuate njia ya haki lakini hatuchoki kama GADDAF na wenzake walishindwa na utajili wao wote na nyie magamba mtashinwa tu.Ebu ona kesi za kupinga uchaguzi zlivyo kibao kwa USHINDI WA CDM alafu wanajitetea kutohuska na mauaji wakati mnakataa ushindi wa kweli.POLENI MAGAMBA MAANA HAMNA TENA JIPYA.WATU WANAJUA KUWA MNAWADANGANYA KWA VISINGIZIO VISIVYO NA MASHIKO.NA MKOME KUTUDHARAU WATANZANIA KANA KWAMBA HATUNA MACHO HATUONI!
 
Kina Ritz wanamwona Nassary ni mtu mkubwa sana. Ni waoga hujapata kuona

Mtawala ambaye sera zimemuishia njia ya mwisho ni kutumia rungu na mabavu ya dola ili kupunguza makali ya wapinzani wake. Subiri mengi tutayaona.
 
Mwee kweli jinga"Majina uumba" ovyo! kada mkubwa wee!!


Kweli, ukikosa akili duniani borakufa. Jinalo laumba nini mwenzangu? Mimi mwenzio jinga kweli, wewe?
Ficha upuuzi wako, na si hekima yako "invisible" amenena!
Mungu wetu anaita!
 
I can't believe this. Kwamba Polisi wamemhoji Nassari for 6 hours! Walikuwa wanamhoji kitu gani hasa WASICHOKIJUA????
Hakika HATUNA POLISI NCHI HII! Hivi huyu dogo na MANENO ALIYOTAMKA KUWA ANAWEZA KUMZUIA RAIS WA NCHI JAKAYA KIWETE ASIKANYAGE ARUSHA YANA UKWELI WOWOTE HAPO????Kwa ujinga wa Polisi wetu wanayaona haya maneno kama DEAL na issue nzito ya kupotezea muda!!!!...

Kwa hiyo tunaweza kuhitimisha kwa kusema kuwa KAMA JOSHUA NASSARI NA WAFUASI WA CDM ATAWEZA KUMZUIA KIWETE ASIKANYAGE 'A' TOWN,THEN HATUNA JESHI LA POLISI,HATUNA UWT,HATUNA JWTZ NA KWA MAANA HIYO HATUNA SERIKALI. MAANA YAKE NI NINI??NI WAKTI WA CHADEMA KUCHUKUA NCHI. Pambaf!


Hapa unaona waziwazi kabisa kwamba dola na mashabiki wake wamekuwa kama mfa maji kapata unyasi wa kushikilia. Mh. Nassari kateleza kikawaida kabisa kama ilivyo kwa wanasiasa wetu wengi. Basi tungeshtuka sana enzi zile Mh. Sumaye alipowataka wafanyabiashara wajiunge na CCM wakitaka mambo yao yawaendee safi. Kusema kwamba kauli ya Nassari inatishia amani ya nchi ni unafiki wa hali ya juu na ubabaishaji. Ingekuwa CHADEMA wamesema ndio msimamo wa chama ingekuwa habari nyingine. Nassari anatakiwa kupewa mawaidha na chama chake kuhusu kauli maridhawa za kisiasa; sio kupigiwa kelele zote hizi zisizo na mashiko kwenye media!
 
Ni mkubwa sana kimamlaka, ni mwakilishi wa wanaarumeru wa mashariki wote, pia wengi vijana wameshamfanya kama role model wao, unaweza kufikiria kauli yake imezaa nini kwa watu hao? Hata kama alikuwa na lengo la kuhamasisha mikoa mingine, tafsiri hiyo imo nafsini mwake tu, ni njia ya kitoto na haina mantiki, kwanini asiombe radhi tu aeleweke yaishe! Ndugu we sijui umechambua kwa ujumla upi? Usitumie hisia zako kwake, utaishia kumtukana, au kumpa sifa za kijinga. TUMIA MANTIKI!
Mungu wetu anaita!

asante
 
Bila samahani ndugu yangu, nilishakusamehe kabla hujawaza kuandika post yako!
Ila tu nikukumbushe kuwa, Dr. Slaa na Chdm inaheshimu sana mawazo yako kama shabiki au mwanachama katika kuimarisha chama. Kudhania kuwa raia hana mchango wowote katka uwajibikaji wa viongozi ndiko kulipotufikisha hapa tunapopalalamikia leo.
Nakushauri, acha ushabiki tumia mantiki katika kuhoji mambo! Pole sana kwa kujidharirisha, ila usiumie sana bado una nafasi ya kuonesha kuwa unaakili, uliteleza tu na hukuanguka, kama alivyoteleza Nassari.
Mungu wetu anaita!

jinga kwanini una amini sana kwamba kuna mantiki kwenye hoja zako, na za wengine ni ushabiki ama hisia? Hapa umetumia hoja yenye lengo la kumshushua mwenzako. Pia huo msamaha wako umewai sana kuutoa, aina iyo ya misamaha husukumwa na kiburi tu! Na sijui ni Mungu wetu yupi huyo anaye ita, na anaita mwito gani!
 
jinga kwanini una amini sana kwamba kuna mantiki kwenye hoja zako, na za wengine ni ushabiki ama hisia? Hapa umetumia hoja yenye lengo la kumshushua mwenzako. Pia huo msamaha wako umewai sana kuutoa, aina iyo ya misamaha husukumwa na kiburi tu! Na sijui ni Mungu wetu yupi huyo anaye ita, na anaita mwito gani! Kama ni YAHWE, naomba tuongee nje ya JF.

Ndugu, msamaha wangu wala sio wa kiburi hata kidogo, ni kutoka moyoni japo najua amenikosea, siwezi kumlaumu!
Nimesema tutumie mantiki ya mambo, ila sio ushabiki na hisia, mimi na kwa wengine! Sidhan kama kuna mantiki yoyote katika matusi, au kumuhukumu mtu kisa tu hajasema kile unachokifurahia. Tukosoane ila kwa hoja, na si vinginevyo.

Kweli..."MUNGU WETU ANAITA" LAZIMA TUITIKE KATIKA UMOJA NA KUTHUBUTU.
Labda ni Yahwe.... Lakini nachojua ni Mungu wetu aliye hai! Nitajitahid kukutafuta, nivumilie tafadhali!
Ukishabikia siasa, kubali kuanguka na kunyanyuka, imo!
Mungu wetu anaita sasa!
 
nchi iitweje?tanga,kilimanjaro,arusha manyara,mara mwanza na kagera du bonge la nchi.
hata kagame haoni ndani kwa maendeleo.
kama zanzibar wanataka nchi yao sijui itakuwaje na hawa wakitaka hii nchi.\

yaani ni full amerika.
 
Kigarama,unafahamu maana ya verbatim?Huoni mjadala ungekuwa vyema baina yetu kama ungeweka hayo maneno kama alivyoyasema?
jmushi1 naujua sana lakini nashangaa tangu lini tumeanza kudaiana ushahidi wa neno kwa neno badala ya kujadiliana kwa hoja?
 
Last edited by a moderator:
Ndugu, msamaha wangu wala sio wa kiburi hata kidogo, ni kutoka moyoni japo najua amenikosea, siwezi kumlaumu!
Nimesema tutumie mantiki ya mambo, ila sio ushabiki na hisia, mimi na kwa wengine! Sidhan kama kuna mantiki yoyote katika matusi, au kumuhukumu mtu kisa tu hajasema kile unachokifurahia. Tukosoane ila kwa hoja, na si vinginevyo.

Kweli..."MUNGU WETU ANAITA" LAZIMA TUITIKE KATIKA UMOJA NA KUTHUBUTU.
Labda ni Yahwe.... Lakini nachojua ni Mungu wetu aliye hai! Nitajitahid kukutafuta, nivumilie tafadhali!
Ukishabikia siasa, kubali kuanguka na kunyanyuka, imo!
Mungu wetu anaita sasa!

hotuba ya Nassari pale NMC ililenga kulaani mauaji ya mwenyekiti wa CDM Usariver, ambayo hayaja shughulikiwa ipasavyo. Kuna wabunge wa CDM walicharangwa mapanga, na jeshi la polisi lipo kimya. Nassari alitishia kujitenga au kumpiga raisi marufuku, lakini uchambuzi wako wenye "MANTIKI" na wengine wengi mnachambua kama kwamba tayari ameshatoa tamko rasmi la huko kujitenga! Alisema KAMA, polisi wasipo shughulika kuwapata wauaji na kuwachukulia hatua.... Labda hatuna "MANTIKI", tunaongozwa na hisia na ushabiki, lakini nashawishika kuamini kwamba Nassari alisukumwa na mauaji ambayo yana sura ya visasi vya kisiasa na ubutu wa polisi kufanya kazi yao kutoa kauli tunazotumia kumhukumu. Ndo maana naomba tuangalie context kabla ya kufanya hitimisho la uchambuzi wa maneno.
Mimi ni mfuasi na muumini wa Mungu aliye hai, na jina langu hapo juu ni halisi, and I gave you my number. Sina unafiki, na siyo mwanachama wa CDM, lakini naijua haki na ntasimama kwenye haki tu.
 
:baby:Kamanda Nasari songa mbele usirudi nyuma wala kutishwa nao hao polisiCCM
 
jmushi1 naujua sana lakini nashangaa tangu lini tumeanza kudaiana ushahidi wa neno kwa neno badala ya kujadiliana kwa hoja?
Kigarama, sasa utajadili hoja ya "Mtu kasema kitu" halafu kitu hicho alikichosema mtu huyo hukiwezi wazi kwenye mjadala?Utakuwa unajadili kitu gani sasa?
 
Nyota ya Nassari kama kionozi kijana wa kuwakilisha vijana wa leo imeingia dosari kubwa.
Siwezi kumuweka Nassari katika kundi moja na Zitto intellectually ni kama mbingu na nchi.

Mwanasiasa anapoongea juu ya kujitenga kimsingi huo ni uhaini. Anapopata upport toka kwa wanachama wake hii inamwongeze matatizo na kuonyesha kuwa anacho propagate may come to reality.

Na hapo ndio hatua kali zisizoeleweka zaweza kuchukuliwa kwa mtu huyu na watu wakisha poteza maisha katika sakata kama hili utetezi wa utoto , kama ilivyo kwa Lulu unakuwa hauna maana sana.
 
Back
Top Bottom