Joshua Nassari MB.

Joshua Nassari MB.

Naanza kudoubt uwezo wa huyu kijana umbile la mtu haligawi nchi bali maneno ya mtu.Mimi naona bora anyamaze mambo ya poe kwanza.Mbowe mwambie afyate mdomo huyu kijana.

Nimeipenda hii Mzinga,
Nafikiri ifike wakati sisi wananchi tujijengee uwezo wa kuchambua mchele na chuya,si ksbb ni M'chadema tu basi ndo tushabikie hata u'tumbo.
Dogo apunguze speed,shauri yake.
 
Watu wetu wameuawa na wahuni wa ccm, na bado vitisho vinaendelea kutolewa dhidi ya wanachama wa chadema.
Hivi katika haya bado hatujaelewa kwanini Nassari amedhiriki kutamka?
Na kama watu wa kaskazini wataendelea kuuawa na ccm, watu wa kaskazini bila hata ya kuishirikisha chadema tutatoa tamko rasmi kuhusu watu wetu.
 
Imesha rekebishwa na kiongozi wa juu kabisa wa CDM sasa mnataka tukamuombe baba mwanaasha a.k.a Gamba aje aturekebishie?
 
Ngoja niweke wazi kabisa; sina tatizo na kauli ya 'kujitenga'. Ni kauli ya kisiasa na imeshawahi kutolewa mara nyingi na watu wa Kigoma, watu wa Mtwara/Lindi, na hata watu wa Pemba.Binafsi hilo halinisumbui sana. Na mtu yeyote anajua aliitoa kauli hiyo kwa maana ya kuweka point ya utani ndio maana alisema "kama Sudan". Haina maana nzito ya kihivyo kwani na wengine wameshatoa kauli kama hizo.

Lakini huwezi kutoa kauli yenye kumtishia Rais na ukabakia hivihivi. Mtagundua kwamba kauli zenye kutishia maisha au usalama wa kiongozi yeyote wa umma huwa hatuzivumilii hapa kwa sababu moja kubwa - siyo watu wote wana akili zilizotulia na huwezi kujua nani akisikia anasukumwa vipi.

Nassari ni kiongozi maarufu sana sasa hivi na ameshinda kwa kishindo kikubwa sana. Kule Arusha ana mvuto mkubwa sana na ni mvuto wa watu kukesha na kumlinda hadi dakika ya mwisho. Chuki dhidi ya CCM ni chuki ya kweli (real hate) na siyo watu wote wanaweza kudumu kwenye chuki hiyo na wakiacha kwenye mambo ya kisiasa tu. Sasa, mbunge maarufu, tena kijana anaposimama na kusema anaweza kumpiga mkwara rais asikanyage Arusha siyo jambo dogo kwa sababu siyo wasikilizaji wake wote wanamuona 'mdogo hivyo'. Nassari ana ushawishi na anamvuto.

Labda watu wengi hawajui historia. Martin Luther King hakuwa na cheo chochote cha kisiasa zaidi ya kuwa mhamasishi mwanaharakati. Lakini mauaji yake yalisababisha miji ya Wamarekani kuingia katika machafuko makali sana. Ni kwa sababu watu walijua ameuawa na mikono ya watu wenye nguvu. Hata Nassari pamoja na "udogo" wake wote hakuna mtu Arusha atapenda anatendewa vibaya au kuonewa na wapo watu wanaoweza kufanya lolote kwa ajili ya utii wao. Nadhani watu wengi wameshasahu kuwa mauaji ya Arusha ya 2011 kwa kiasi kikubwa yalisababishwa na polisi kutumia nguvu dhidi ya watu ambao waliona wanaonewa.

Sasa mbunge anaposimama na kutoa kauli ambayo vyombo vya usalama vinaiona ni ya vitisho dhidi ya Rais ni kutokuwa makini kudhania tu ni jambo dogo. Alichotakiwa kusema Nassari ni hiyo kauli yake ya kwanza tu kuwa hakumaanisha ubaya wowote na kama mtu yeyote amekwazwa anaomba radhi. Lakini siyo kusema kuwa ati yeye ni mtu mdogo na asingeweza kugawa nchi; well hilil ni zaidi ya kugawa nchi. Hivi akisema kuwa Rais asikanyage na Kikwete akaamua kukanyaga na mwehu mmoja akaamua kufanya kitu kibaya kwa msafara wa rais watu watamlaumu mwehu kwa vile ni mwehu siyo? Lakini, yule mwehu ukimuuliza atasema "rais wetu" alitoa amri Kikwete asikanyage Arusha na akakanyaga!

Hii ni sababu moja ambayo inanifanya miye nisiwe shabiki sana ya hoja ya 'uongozi bora ni ujana' kwani tayari tumeshaona mengi yasiyo ya lazima ambayo vijana wameyafanya na kuthibitisha ukosefu mkubwa wa hekima na utulivu unaotokana na busara. Siyo lazima useme kila kinachoingia kichwani hata kama unaamini ni sahiihi. Kuna vingine unaweza kuvisema ila kwa namna tofauti. Hili huwezi kufundishwa shuleni au chuoni!

Ni matumaini yangu Polisi hawatoliendeleza hili na Nassari atakuwa amegundua (sidhani kwa sababu arrogance ya madaraka nayo nimbaya sana!) makosa yake. Sitaki ajisikie ameonewa bali ajue genuinely hakupaswa kutoa kauli hiyo na ni unfortunate. Kwa mfano Lema angekuwa makini na kauli zake wala asingevuliwa Ubunge! HEKIMA, HEKIMA, HEKIMA!!

Mwanakijiji umesema vema, lakini kauli yako ya mwisho ya kukubali hukumu ya Lema kuwa si sahihi umefuta maneno yako yote ya hekima uliyoyasema.
 
ile kauli ya dogo janja isiporekebishwa mapema itaicost sana cdm,dogo janja ningemuona km mweledi sana angeomba radhi,n it was spoken unintentionally.

Mbona magamba walishawahi kusema hamna hata siku moja Rais atatokea Kaskazini kuna mtu alikanusha? sembuse CDM ttamko la Nassary limekanushwa na mbowe pambaf zao
 
sikutegemea kama Nasari ambaye tulimwamini hivi ayafanye haya..ni aibu kwake na wanachadema wenye akili timamu

Hapo kwenye RED mkuu panawakilisha ujumbe wa maana sana...ni ukweli usiopingika kuwa wana'chadema wasio na akili timamu tu ndo wanaoweza ku'support ujinga huu.
 
Wewe sio mdogo tena, Umeshapakwa mafuta kuwa mwakilishi wa wameru mashariki wote, Chochote utakachofanya kwa sasa ni msimamo wa jimbo lako chini ya mwavuli wa CHADEMA, kwa hiyo nakuomba umwombe MUNGU akuongezee hekima zaidi, kama mfalme Suleman, Kwa kuwa ameshakupa nguvu kama DAUDI, sasa hivi kwa mkono wa MUNGU unao uwezo wa kumuua GOLIATHI, Kwa hiyo jitahidi usimdhuru SAULI kwa kuwa ni Mpakwa mafuta wa Mungu hata kama anakusudia kumwacha.

Well said ndugu! Hana udogo wa kiumri, umbo wa mamlaka, asijitetee kitoto, anajidharirisha na kuwatusi wanaarumeru kwa kumchagua!
Jambo rahisi kabisa, "aombe radhi tu". Tutamuelewa. Kwani nani hajui kuteleza, ni jambo la kawaida. Ila namna anavyotaka kujifanya mjuzi, anajiharibia sana! Ni bora kutukanwa na wajinga 1000, kuliko kuzomewa na mwenye hekima 1. Asivimbishwe kichwa na wanaomshangilia kwa hisia, mapenzi, mkumbo,nk hali mantiki patupu!
Mungu wetu anaita!
 
Ushabiki na mapenzi yanayoleta upofu ni mufilisi kwa Great thinker,
kama kweli hajakosea kwa nyie mnaotoa povu kumtetea Nassar kwanini Mbowe alisimama na kurekebisha kauli ya nassar? kama Nasar hakukosea inamaa ni Mbowe ni Policcm .udogo upi alionao huyo Nassar yani kisa anaitwa dogo janja ndo mdogo? yeye ni kijana tegemeo la wananch wa meru na alishinda kwa kishindo na kuweza kuwahamasisha watu kulinda kura zao huu ni ushawish wa hali ya juu na sio wa mtoto au mtu mdogo.
kwa kauli yake ya kumtisha Raisi si ya kupuuzwa hata kidogo, chukulia kama hapa kwenye JF great thinker wasomi na wenye uwezo wa kupembua mambo wanaona yuko sahihi je hao walioko ungalimited matejo usa na kwengine wamechoshwa na ccm hawajui hatma yao na kesho yao then wanapata kauli kama hiyo ambayo kwao wanahisi chadema ndio mkombozi wao,impact yake itakua either kumzomea Raisi au kupiga mawe msafara wa Raisi.

Nasary kwa hili umekosea na pima akili yako wewe sio mtu mdogo thats y uko kwenye bunge kuwakilisha wananchi.
 
uwezo wa nassary mb. Unatia mashaka na hasa masilahi ya taifa. Ajiulize. Wakongwe wa siasa kama dr slaa walishawahi kutamka maneno hayo? Si kwamba hawawezi bali ni hekima. Ajifunze kuwa na adabu.
 
Dogo lazima apime nini cha kusema na ambacho sio cha kusema Chadema lazima ijitofautishe na ccm, kwa kuwa na watu makini wasiolewa sifa na kuanza kuongea hivyo hata hivyo bado inatakiwa kuwalea vijana kama nassari na Heche kwa kuwafundisha maadili ya public speaking ili kuepusha watu kuichukulia chadema kama chama cha watu wakorofi
 
Hakuna lolote hapo propaganda za magamba siku hizi hazizai matunda,watu wameelimika wanajua mbaya wao ni CCM tu.
 
Mheshimiwa sn futa kauli yako,mbele ya vyombo vya habari.TAFAKARI KWA KINA KAULI ZAKO.Utashusha heshima yako na heshima chama.
 
tatizo la msingi kwenye hii habari ni kuwa nje ya "context" kwa makusudi. Nassari amesema maneno mengi lakini watu wana"donoa" maneno machache ili kuharibu maana halisi ya alichosema. Kwa mfano hapa unashupalia yeye kusema ni mdogo tu, lakini pia amesema ilikua kauli ya kuhamasisha mikoa mingine. Pia udogo aliosemea siyo umri, ni cheo chake cha ubunge katika chama chake cdm. Tukitaka kutendea maneno haki, tuyachambue kwa ujumla wake, (katika context) tuache "udonoaji"

Ni mkubwa sana kimamlaka, ni mwakilishi wa wanaarumeru wa mashariki wote, pia wengi vijana wameshamfanya kama role model wao, unaweza kufikiria kauli yake imezaa nini kwa watu hao? Hata kama alikuwa na lengo la kuhamasisha mikoa mingine, tafsiri hiyo imo nafsini mwake tu, ni njia ya kitoto na haina mantiki, kwanini asiombe radhi tu aeleweke yaishe! Ndugu we sijui umechambua kwa ujumla upi? Usitumie hisia zako kwake, utaishia kumtukana, au kumpa sifa za kijinga. TUMIA MANTIKI!
Mungu wetu anaita!
 
Mhe Nasari nataka utambue kuwa Chadema ni chama cha kitaifa, pia utambue kuwa pamoja na udogo wako wapo watu wengi ambao wanasikiliza na kufuata kila unachotamka. Maneno ya juzi licha ya kumuudhu mwenyekiti wa Taifa pia yameleta adhari kwa chama kwani wapo wengi wapenzi na wanachama ambao wameona kuwa ni kauli ya kibaguzi. pili ni vyema ukakaa chini ukapanga namna ya kujenga chama ili tuweze kukitoa chama hapa kilipo na kukipeleka mbele. kama akina mbowe wangelewa sifa baada ya kuwa wabunge na kusahau kujenga chama leo chadema wasingekuwa na mafanikio walionayo leo. So dogo tulia acha kuiga mambo fanya yale tuliokutuma bungeni na jenga chama kwa lugha ya kuwavutia hata wapizani wetu.
 
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Kwahiyo unataka kusemaje........
 
Hapo kwenye RED mkuu panawakilisha ujumbe wa maana sana...ni ukweli usiopingika kuwa wana'chadema wasio na akili timamu tu ndo wanaoweza ku'support ujinga huu.
mambo madogo tu hayo nyie..........dogo anajifunza kidogo kidogo.......unaweza kuwa carried away na jazba wakati mwingine.

wapiga domo hapa ndo wamepata kitu cha kuongelea
Mnaikumbuka kesi ya Uhaini Zanzibar?
hukumu ilikuwaje?
 
Wakati fulani nadhani kijana yuko sahihi sana, nchi inatafunywa eti kanda kati, mashariki, kusini kabisa (Mbeya na Iringa) magharibi wanabweteka na CCM, yuko sahihi kutoa mawazo yake. Alichofanya shujaa huyu kinyume na wewe ni kusema anachodhani kifanyike, wewe ni uoga unakusumbua. Inafikia wakati unafikiri tugawanye nchi kwa faida ya kila kundi; Kama Kanda ya ziwa, Kaskazini wamechoka kuibiwa na nyinyi bado mnafurahi kuibiwa kwa faida ya wote si tuachane kwa mtiririko huo? anakosa gani sasa kusema mawazo yake???

Kwa mwenye akili kama kasikazin na kanda ya ziwa, kijana alimanisha tunachoka kusubiri watu ambao hawaji huku nchi inaisha kwa wizi wa kila siku. tunachoka kusubiri TABORA waamuke, Tunachoka kusubiri Pwani, Mtwara na Lindi, Ruvuma, Dodoma tumechoka; Inawezekana tunasubiri mtu mfu aamke, tutasubiri mpaka tufe!!!

Kama nchi ni moja mbona wenzetu mko kimya na wizi huu, mtasababisha tufe masikini nchi nzima eti tunawasubiri muamke, huenda mmelizika sasa tunafanyaje? ni haki yenu kulizika lakini ni haki yetu kusema endeleni na sisi tuendeleee kivyetu. au kuna ubaya???

Tunaipenda TZ moja lakini kwa usaliti huu, Tabora, Pwani, Dodoma, Ruvuma, Mtwara, Lindi, pengine na Dar TUMECHOKA, amkeni kelele ziishe la sivyo kijana kasema tu moja ya option.
 
Kitu kinachoniacha hoi mimi ni kuwa kama kauli ya Mh. Nassari inaweza kugawa nchi basi tuna kila sababu ya kuamini kuwa tayari nchi ilishaanza kuelekea huko na Mh. Nassari anataka kumalizia tu. Nadhani pamoja na ukweli uliopo kuwa kauli ya Mh. Nassari ilikuwa na harufu ya uchochezi, kama ilivyonukuliwa kauli ya Dr. Slaa huko nyuma kuwa nchi haitatawalika, lakini kitu ambacho kitafanya nchi yetu kugawanyika au kutotawalika wala haitakuwa kauli za namna hiyo bali wizi na ufisadi unaoendeshwa na kuratibiwa na genge la wajanja ambao serikali inashindwa kuwachukulia hatua.

Kama waziri mkuu wa nchi hii alisema kuwa mafisadi wakichukuliwa hatua nchi itayumba, basi hiyo hali ya mafisadi kuogopwa ndiyo cha kuogopa zaidi kuliko kauli ya Nassari au ya Dr. Slaa. Watu wanao'capitalize' kauli ya Mh. Nassari wanataka kutufanya kuwa hatuna akili kiasi kuwa kinachosemwa na kila mwanasiasa kitakuwa hivyo eti tu kwa sababu wana ushawishi. Ukweli ni kuwa jambo ambalo wananchi watakubaliana nalo hasa baada ya kusemwa na mwanasiasa kitakuwa kile ambacho wao wanaliamini na wanalitaka. Wananchi siyo roboti ya kuendeshwa na wanasiasa kama watu wengine wanavyotaka kutuaminisha.
 
Mdomo wa Nasari ni mtamu kwa masikio yetu aliyetusemea mawazo yetu (sisi watu wa kanda tajwa); Unadhani maneno ya nassari ni yake pekeee!! umekosea sana; unadhani maneno ya nassari yanaweza kuua taifa haraka zaidi kuliko wizi na matumizi mabaya ya madaraka ya CCM? umekosea sana, Tunachotaka sisi nchi moja ambayo kila mtu anafaidika kihalali, kama haiwezekani basi sio mbaya ziwe mbili ambazo kila upande unafurahia unachoamini; Mafisadi ndo wametufikisha hapo, jee CCM na Serikali yake imewahoji wangapi na imechukua hatua gani??? AIBUUUUUUUUUUUUUUUUUU
 
Ila nassari kaniudhi sana kauli yake inaweza ikakicost chama kwa wanaccm kuibebea bango hiyo kauli kwamba ndo mpango wa Chadema kwenye kampeni 2015. Mimi ni mwanaArumeru na nilikupa kura yangu ila umeniudhi sana. Siku nyingine fikiri kabla ya kuongea.
 
Back
Top Bottom