Joshua Nassari MB.

Joshua Nassari MB.

Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Huenda hamkumuelewa Nassari kuhusu "udogo" wake. Amesema yeye ni mdogo, hajafafanua udogo katika umri, umbile au ushawishi. Kwa kauli ya kusema "basi hiyo nchi haipaswi kuwapo", mimi nimemuelewa kwamba alikuwa anazungumzia udogo wa ushawishi!
 
Nassari kakosea na kama ndivyo wote tunakubaliana hivyo basi hana budi kuwajibika kwa makosa yake kwa kukiri kwa maandishi amekosa kisha turuhusu utaratibu mwingine uendele, hata tukisema maneno billion mia ya kujaribu kumdis credit Dogo bado haitoshi kumhukumu kwamba mtazamo wake ni mfupi. Hivyo basi tukubali kosa lime kwisha tendeka kilicho baki ni kusonga mbele katika kulijenga taifa...!
 
Hakuna chembe ya mantiki hapo hata kidogo ndugu yangu! Amefanya kosa then analeta mzaha. CHE GUEVARA alikufa akiwa na miaka 38, ndani ya muda huo mfupi akawaadabisha mabepari wakubwa kama Marekani.
Kwanza ni kujidharirisha mwenyewe, anajifananisha na mtoto asiyejua jema na baya, hali lukuki ya wana-arumeru wana tumaini naye? Anataka waamini wamekosea kumchagua?
1. Akiri kuteleza ulimi, na kuomba radhi, ni jambo la kawaida sana, sisi kama watz tuko tayari kumsamehe, na ajipange upya, tuko nyuma yake.
2. Chadema itoe tamko la kulaani, na kutoa karipio kwa maneno hayo. Na sio kuishia kusema "hayo sio maneno ya chadema", kwani ametoa nani na wapi?
3. Asipokubaliana na yote hayo, basi chdma kama chama makini, kisisite kumuwajibisha. Lakini sitegemei kufikia huko!
Mungu wetu anaita?

Nakubaliana na wewe kwa kiasi fulani. Lakini nadhani nchi hii inahitaji watu watakaotibua hali ili watawala wetu wapate akili. Nakumbuka kuna wakati Mh Mbowe alisema inabidi wakati fulani pawe na Civil disobedience, je utasema Mbowe alikosea? Ni kwa sababu utawala uliopo hauwezi usikia vilio vya watu bila kauli kali kama hizi. Kwa nchi yenye demokrasia ya kweli na iliyotulia, na ambayo viongozi wake ni wasikivu kwa matakwa ya raia wake, kauli ya Nassari ingekuwa mbaya sana, lakini si kwa serikali kama yetu, ambayo kwa kutumia jeshi la polisi wanaifichia CCM ukweli wa mauaji wanayoyafanya kwa viongozi na makada wa vyama vya upinzani.

Natamani kauli kama hizi ziwe nyingi ili kuwaamusha wananchi na kuifanya serikali hii izinduke. Msimamo wangu siku zote ni kuwa CCM haindoki kwa lugha laini laini, lazima iambiwe maneno magumu ambayo hata wakiyasikia masikio yawe yawashwe.

Wito kwa Polisi wetu; acheni kufuatilia mambo yasiyo na umuhimu na kujaribu kuyakuuuuuza; kumbuka walivyomkamata Mbowe kule Dar na kumpeleka Arusha, nguvu kubwa inatumika kwa mambo madogo sana. Wao wanajua kuwa pamoja na Nassari kutamka yale maneno, hana uwezo wa kufanya lolote, ama wananchi wa Arusha hawawezi kufanya chochote kwa kauli ile; kwa nini msifanye mambo muhimu kwa nchi hii?
 
Msemo wa mgema akisifiwa TEMBO hulitia maji, dalili zaonyesha CDM wamelewa misifa HIVYO wamefikia kuongea pasipo tafiti wala busara. Imefikia hatua viongozi kutoa matamko tofauti wakiwa majukwaani. Moja kwa moja UONGOZI WA KITIMU NDANI HIKI CHAMA HAUPO.

Imethibitika katika mkutano wa UNGA LTD, mbunge Nasari katoa tamko la UBAGUZI na kuthibitika hiki chama ni cha Kanda ya Kaskazini tu, wengine ni abiria.

Watanzania tutumie vichwa vyetu tufikiri kwa makini, CDM ni kwa ajili wa KANDA MOJA!!!!

Kuna matukio mengi yanayoonyesha CDM hawana utashi wa kuongoza TZ, kwani walianza kutoutaka muungano, na sasa wanataka kujitenga. tuwahurumie ndugu zetu toka kanda ya Ziwa, Kusini Nyanda za Juu waliovutwa na upepo wa msimu wa CDM pasipo kujua undani wa wamiliki wa CDM; ambao ni Mbowe & Mtei Co.

Najua wafuasi wa CDM toka kanda husika mtasema sana kwa vile nimewagundua ujanja unaotumia kutaka kutugawa watanzania kwa misingi ya ukanda.

Kwa mtazamo huo wako, hapo ndipo unapo gundua uogaa na uchanga wa siasa ulio gubikwa na unywaji wa juice ya maji ya bendera ya jembe na nyundo.... hili linatosha kuonyesha jinsi gani mabadiliko kwa CCM ni sawa na mtu kukalia mafiga ya moto... lazima muogope....!
 
Kumbe ni kweli Chadema mnataka kujitenga...

CDM itajitenga vipi wakati wimbi la mageuzi sio la Arusha tena. Nenda Bukoba, mpaka Songea; anzia Musoma mpaka Tunduma, kote huko CDM inapaa kwa kasi, sasa CDM itajitengaje? Tumia akili ndogo tu. Lililo wazi ni kuwa CCM bye bye
 
[h=3][/h]
POLISI mkoani Arusha jana lilimhoji Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari kwa zaidi ya saa saba baada ya kujisalimisha katika Kituo Kikuu cha jeshi hilo.

Nassari ambaye anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi dhidi ya Serikali katika mkutano wa hadhara wa Chadema uliofanyika Mei 5, mwaka huu katika Uwanja cha NMC, alishikiliwa kituoni hapo kuanzia 6:12 mchana hadi saa 12 jioni kisha kuruhusiwa kuondoka na kutakiwa kuripoti kituoni hapo leo.

Alifika hapo akiwa na Wakili wake, Arbert Msando bila ya kuwakuta viongozi wa jeshi hilo hivyo wakaamua kuondoka.

Lakini nusu sasa baadaye, Naibu Kamishna, Isaya Mungulu na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akilimali Mpwapwa walifika na kuwataka viongozi wa Chadema, waliokuwa kituoni hapo kuwasiliana na Nassari ili arejee.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema aliyekuwapo aliwasiliana na Nassari ambaye alirejea saa 7:20 akiwa na Wakili Msando na alichukuliwa na Kamanda Mpwapwa ambaye alimwelekeza kuelekea Ofisi ya Mkuu wa
Upelelezi Mkoa (RCO) kwa mahojiano.

Baada ya kumfikisha Mbunge huyo katika ofisi za mahojiano, Kamanda Mpwapwa alisema kulingana na uzito wa shauri lake atalazimika kutafuta watu wa kumwekea dhamana mara baada ya kuhojiwa.

“Hapa yupo mikononi mwa polisi, atahojiwa na baadaye atapewa dhamana,” alisema Mpwapwa.

Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Msangi kutoka Makao Makuu ya Idaya ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (CID), ndiye alikuwa akiongoza kikosi maalumu kilichokuwa kikimhoji Nassari.

Msangi ambaye ameteuliwa hivi karibuni kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa mpya wa Simiyu, alikuwa akisaidiana na Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Hamisi Warioba kutoka ofisi ya upelelezi Mkoa wa Arusha.

ASP Warioba ndiye aliyewahoji watuhumiwa wengine, John Heche na Ally Bananga juzi kwa zaidi ya saa tisa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 2:00 usiku, walipoachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurejea jana asubuhi.

Awali, Nassari alieleza alikuwa hana taarifa za kuitwa polisi kwa shtaka lolote bali, mara baada ya mkutano huo wa Mei 5, alipokea ujumbe wa simu kutoka Ofisa Upelelezi Mkoa wa Arusha, Faustine Mafwere kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa Arusha, Thobias Andengenye alikuwa anamtafuta ili waagane baada ya kuhamishiwa makao makuu.

“Mimi nimeshangaa leo kusoma katika vyombo vya habari kuwa nasakwa na polisi na ndiyo sababu nimekuja kwani awali, nilijua rafiki yangu Andengenye anataka tuagane na nilipanga siku nyingine,” alisema Nassari.

Nassari pamoja na viongozi wengine wa Chadema wanatuhumiwa kutoa kauli mbalimbali za uchochezi ikiwamo, kutishia kujitangazia uhuru wa
Arusha na kanda ya ziwa kama polisi haitawakamata waliohusika na mauaji ya mwenyekiti wa chama hicho Kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo.

Pia alimtuhumu mtoto wa Rais, Ridhiwan Kikwete kushinikiza uteuzi wa baadhi ya viongozi serikalini.

Bananga ambaye pamoja na Heche pia walikuwa wakisubiri kuhojiwa zaidi jana alisema juzi aliulizwa juu ya kauli zao kwenye mkutano huo, dhidi ya Rais Kikwete na mtoto wake Ridhiwan. Huku Heche akisema kwamba aliulizwa juu kauli za Nassari katika mkutano huo.



CHANZO - Mwananchi
 
Mkuu Mungii, wewe ni mojawapo ya watu ninao waheshimu sana katika jukaa hili ila unaanza kunipa wasiwasi.
1. Kwamba hukubaliana na kauli ya 'Dogo Janja' na pia "pumba" za MMK nikujikanganya maana hoja ya msingi ya Mzee Mwanakijiji inapinga kauli ambayo unasema hukubaliana nayo.

2. Hizi tabia za kutenganisha chama na viongozi wake ni tabia za CCM, " chama ni kizuri ila viongozi ndo wabovu" na si Chadema. NASARI NI KIONGOZI NA KIONGOZI NI TASWIRA. Anabeba sura ya taasisi/watu anaowaogoza na Nasari anapaswa kuwa hivyo. Kujaribu kumtenganisha Nasari na Chadema unakosea

3. Kinachobishaniwa hapa si sababu zilizomplekea Nasari kusema aliyo yasema. Kinacho jadiliwa/bishaniwa nikwamba Nasari alikosa hekima kueleza alichokikusudia. Moja ya Sifa kuu za kiongozi ni kuwa na hekima/busara. Kwa lugha nyepesi uwezo wa kutambua kitu gani unapaswa kufanya/kusemea na kwa wakati gani. Wakati huo uwe wa furaha au huzuni, sherehe au majonzi. Maranyingi uwezo wa kiongozi unajidhihilisha katika kutatua matatizo kwenye complex situations.

4. Ni utamaduni humu janvini kwa wanajanvi hukubaliana na kupongeza ama kupinga hoja za wenzao. Katika kuonyesha kuikubali hoja wengine hutumia "LIKE" na wengine hueleza hisia zao kwa kuandika na umekuwa ukifanya ama kufanyiwa hivyo karibia kila siko. Nadhani hauko sahihi kumbwambia mwenzio anajikomba kwa Mwanakijiji.

5. Hii tabia ya kulinganisha uovu kwa uovu sio nzuri na bora tukaizika.

6. Ninaanza kupata hisia kuwa baadhi ya vijana wa kasikazini wamenasa kwenye mtego wa CCM. Mtego wa kutumia ukanda/ukabila kuigawa CDM. Kuweni makini makini tena makini. Siku mkianza kujiona zaidi wanaarusha kuliko wanachadema, huo ndo utakuwa mwanzo wa kudidimia kwa harakati hizi ambazo sote ni wadau.


MKUU MUNGI MIMI NA WEWE TU WAPENZI WA CHADEMA LAKINI USIPENDE KUWA MPENZI KIPOFU

Nyie mtaendelea kulumbana kuhusu Nassari wakati wenzenu wako busy wanaiba mali za umma,mkikurupuka toka kwenye malumbano trivio haya mtakuta mabilioni yamevunwa kama mlivyofanywa kwa babu wa Loliondo.

DON'T SAY I DID'NT WARN YOU, au mmewasahau CCM nyie?
 
Habari ya KAULI ya NASSARI kijana mdogo asiyemiliki hata mgambo kumi, ni kukwepa majukumu na mambo ya msingi yanayotukabiri... tunataka Kusikia Nini hatima ya TANESCO,ATCL,EPA,KAGODA,DOWANS,...NK , Nini Hatima ya MAIGE na TWIGA wetu na MENGINE mengi yanayofanana na HAYA.
 
We pia pata moja kwa bili yangu
Ronald- stop barking on him, he is soso right! Watakaomshambulia hawajajua maana yake!
Si wanasema hicho Chama Ni cha wakrist Tena Wa kaskazini. Huo ndio msimamo basi wakawaabie wajitenge(najua haitawezekana)
Wala si nia ya Chadema!
Ikibidi hivyo na mimi nitajitoa.
My take.
Ujanja Wa Ccm ulipoishia ndipo smartness ya Chadema inaanzia.
Asante (Dogo janja)
Janja kwel kweli!
Ukiniona unanidai kinywaji!
 
jmushi1 Verbatim? Tangu lini tukaanza kudaiana ushahidi wa namna hiyo?Hebu tujadili hoja hapa.Kama Nassari alikuwa sahihi ni kwa nini Mbowe alimkanusha on the spot??
Kigarama,unafahamu maana ya verbatim?Huoni mjadala ungekuwa vyema baina yetu kama ungeweka hayo maneno kama alivyoyasema?
 
Last edited by a moderator:
Watanzania si wapumbavu kiasi hichu, kumsikiliza mtu mmoja na kufanya maamuzi, na wala Mh. Nasari hana uwezo wowote kushindana na dora, wananchi wanasikiliza wanatafakari na mwisho wanafanya maamuzi. Serikali itambue hilo na polisi walijue hilo, hatutarajii kumsikiliza mtuu kwa jambo la kipuuuzi hivyo kukusanya watu zaidi ya 1000 wakakusikiliza ujue unajambo la msingi na si uchochezi! Mahakama, polisi muda wa kutetea maovu umekwisha umebaki tu muda wa kuadhibu mafisadi only.
work up my people, our country has been destroyed, where shall we get it once again?:baby::baby:
 
Nadhani Nassari sasa anona jinsi alivyo na nguvu katika jamii, ili suala bado linajadiliwa tu!!

Dogo jirekebishe, wewe una nguvu kubwa sana kwenye jamii tambua hilo kwanza halafu zingatia kuwa ulimi ni kiungo kidogo kinachoweza kuleta balaa katika jamii yetu!!

Kisiasa kuwa chonjo na kauli pia magamba yanatufuatilia nyendo zetu!!
 
Mwenyekiti wa CDM ambaye ndiye kiongozi wajuu kabisa wa chama kapinga vikali kauli za Huyo dogo Nassari sasa nashindwa kuwaelewa watu wanaounga mkono kauli ya Nassari,kwa maana nyingine wanampinga mwenyekiti wa CDM!Sitakosea nikiwaita washabiki uchwara wa CDM wanaokwenda kama ng'ombe kufuata miluzi ya mchungaji (Mchungaji wa ng'ombe)
 
We pia pata moja kwa bili yangu
Ronald- stop barking on him, he is soso right! Watakaomshambulia hawajajua maana yake!
Si wanasema hicho Chama Ni cha wakrist Tena Wa kaskazini. Huo ndio msimamo basi wakawaabie wajitenge(najua haitawezekana)
Wala si nia ya Chadema!
Ikibidi hivyo na mimi nitajitoa.
My take.
Ujanja Wa Ccm ulipoishia ndipo smartness ya Chadema inaanzia.
Asante (Dogo janja)
Janja kwel kweli!
Ukiniona unanidai kinywaji!
 
Nimeipenda sana hii Comrade umetoa elimu ya juu sana,nchi tushaiweka mikononi mwetu sasa taratiiibu kuelekea Ikulu cha msingi tusiache majeruhi wengi sana

Ni kweli kabisa kwenye ndoto ukiwa umelala mchana linawezekana kabisa hata kuchukua serikali ya dunia
 
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr


Mwanakijiji...no more to add on top of this.
 
Back
Top Bottom