Kwa wengi tulionunua viwanja halali pembezoni mwa Barabara, tumeona jinsi nyumba zetu zikipigwa X. Tulipofuatiria, tukaambiwa ni sehemu ya barabara. Nani aliyeandaa hiyo ramani? mbona nasi tulipewa viwanja ambavyo viliuzwa na wizara hiyohiyo ya ardhi? Hakuna aliyejibu maswali yetu, tulipofungua kesi mahakamani, kabla hukumu hazijatolewa, usiku wa manane, buldoza na mgambo wapo nje kubomoa nyumba zetu. Magufuli hakujali kama kulikuwa na watoto wamelala au wagonjwa, alivunja nyumba zetu wanyonge. Magufuli huyu anayetumia nguvu nyingi kuliko akili wala sheria, aliuza nyumba za serikali Oyster bay kwa bei ya kutupa. Nasema huyu baba akiupata Urais, masikini hatuna chetu, bora nikalale kwenye mahema nje kuliko ndani ya nchi ninayolipia kodi