John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...
tapatalk_1512965310147.jpeg

Mambo yalitegemewa kuwa mteremko toka siku nyingi lakini upepo kama kawaida ulibadili mwelekeo, push ups zilianza kurindima jukwaani huku Lubuva akijiandaa kumalizia game.
 
Huyo jamaa hafahi kuwa rais hana hekima wala busara maamuzi yake huwa ni ya kukurupuka sana ameitia sana hasara serikali imekuwa ikilipa fidia mara kwa mara kutokana na maamuzi yake ya hovyo tumeona kwenye ile meli ya samaki tumetakiwa kulipa fidia shilingi bilioni 2 baada ya kushindwa kesi pia huyu jamaa ndiye aliyepeleka pendekezo na kushupalia kuuza nyumba mbali mbali zilizokuwa zinamilikiwa na serikali na yeye mwenyewe akiwa mnufaikaji wakati wa utawala wa serikali ya Mkapa wakati huo Magufuli alikuwa waziri wa nyumba na makazi wamejiuzia na kujichukulia majumba mengi ya serikali kwa bei chee mpaka aibu maeneo mbali mbali nchini mfano Nyumba za Oysterbay,Masaki,Msasani,Chang'ombe,Kurasini,Mikocheni yani wamejiuzia yale amjumba yaliyokuwa kwenye maeneo mazuri yote nchini katika mikoa yote .Hayo tu machache leo mnasema huyu jamaa anafaa kuwa rais hfahi hata kidogo na ikitokea tu CCM wamempitisha huyu jamaa wapinzani wana mengi ya kuzungumza kuhusu huyu jamaa hafahi hata kidogo ni Fisadi sana kwa watu wanaomjua vizuri
Heshima yako mkuu
 
Duh....... ama kweli mda ni Mwalimu mzuri! Huu uzi umenikumbusha mbali.

Kuna waliomo humu JF leo wanazikana posts zao kuhusu huyu bwana walizoandika kwenye huu uzi...kuna wengine wamekuwa vindicated.....kuna wengine wamebadili gia angani..Na of course kuna wengine hata ukisoma mawazo yao miaka kumi iliyopita humu..bado imani zao au fikra zao hazijatetereka!

Anyway akiba ya maneno ni bora kuliko akiba ya pesa!
 
Unafiki wa dikteta uchwara.

MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Dk. John Magufuli, ameeleza masikitiko yake jinsi baadhi ya viongozi wa Jumuiya ya Vijana wa Chama hicho (UVCCM), walivyoshindwa kuenzi misingi ya chama hicho baada ya mwenyekiti wa umoja huo, Sadifa Juma Khamis kutiwa mbaroni na Taasisi za Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

*~*~*~*~*~*~*~*~*~

MONDAY, NOVEMBER 7, 2016
Takukuru yachunguza Sh10 milioni za wabunge CCM


Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola.

Kwa ufupi
Wiki iliyopita, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliibua tuhuma dhidi ya wabunge hao akidai kwamba walipewa fedha hizo ili wapitishe mpango wa maendeleo ya Taifa na muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

By Peter Elias, Mwananchi pelias@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) imeanza kuchunguza tuhuma za wabunge wa CCM kupewa Sh10 milioni kila mmoja ili kupitisha Muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

Wiki iliyopita, Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni (KUB), Freeman Mbowe wakati akiuliza swali kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, aliibua tuhuma dhidi ya wabunge hao akidai kwamba walipewa fedha hizo ili wapitishe mpango wa maendeleo ya Taifa na muswada wa Sheria za Huduma za Habari.

Hata hivyo, swali hilo halikujibiwa na Waziri Mkuu baada ya Naibu Spika, Dk Tulia Ackson kumkingia kifua akidai swali hilo halikuwa la kisera.

Mbowe licha ya kusisitiza kwamba swali hilo ni la kisera kwa sababu masuala ya rushwa na maadili ya viongozi wa umma ni ya kisera, aligonga mwamba.

Suala hilo liliibuka tena kwenye mahojiano kati ya Rais John Magufuli na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, na Rais alisema vyombo vinavyohusika vinalichunguza ili kupata ukweli.


“Ninafahamu kuna kanuni za Bunge na nina uhakika vyombo vya PCCB (Takukuru) vitauliza kupata ushahidi. Tuna vyombo vyetuvinavyoshughulikia rushwa, bahati nzuri sheria sasa imeshapitishwa, sheria namba 3 ya mwaka 2016, watakwenda kuthibitisha huko,” alisema Rais Magufuli wakati akijibu swali la Henry Mhanika ambaye ni Katibu wa Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (Moat).

Akizungumzia suala hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola alisema wameanza kufanya uchunguzi juu ya suala hilo kwa sababu ni jukumu lao na watalifanya kiuhakika.

Alisema: “Kama Rais amesema tunachunguza suala hilo, mnataka mimi niseme nini? Ndiyo,tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chakena tumeanza kazi hiyo. Kama na wewe unaushahidi tuletee tuufanyie kazi.”


Alipoulizwa kama analifanyia kazi suala hilo, Kamishna Mkuu wa Sekretarieti ya Maadili yaViongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda alisema: “Takukuru ndiyo wenye kazi hiyo kwa sasa, watafute uwaulize.”

Hata hivyo, muswada wa habari ulipitishwa na Bunge Jumamosi iliyopita licha ya kupingwa na wadaumbalimbali wa tasnia ya habari na wabunge wa upinzani.

Wachambuzi mbalimbali wamezungumzia tuhuma hizo kwamba zimelichafua Bunge na kuhatarisha uhuru wa chombo hicho, ambacho kina dhamana kubwa ya kutunga sheria zinazoongoza Taifa hili.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Faraja Kristomus alisema tuhuma hizo ni nzito kwa chombo cha kutunga sheria na kwamba siyo mara ya kwanza kutolewa kwa tuhuma za rushwa kwa wabunge.

Alisema tuhuma hizo zinaibua maswali mengi ikiwamo hamu ya wananchi kutaka kujua kama kweli wabunge walipokea Sh10 milioni, na kama ndiyo jumla ya fedha zilizotolewa ni kiasi gani na fedha hizo ni za nani kati ya CCM au Serikali.

“Inabidi Bunge lichunguze na kutoa majibu kuhusu suala hili, nashindwa kusema moja kwa moja kwamba muswada huo umepita kwa sababu ya rushwa hiyo, lakini safari hii wabunge wa CCM wameonekana kuungana sana ukilinganisha na mabunge yaliyotangulia,” alisema.

Alisisitiza kwamba uongozi wa Bunge usilifumbie macho suala hilo hata kama liliulizwa nje ya kanuni kwa sababu linatoa picha kwamba wabunge wote ni wala rushwa na hilo litafanya sheria hiyo isipokelewe na wananchi kama sheria halali.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha (Rucu), Gaudence Mpangala alisema Takukuru inatakiwa kuzifanyia kazi tuhuma hizo kwa sababu ni rushwa kama yalivyo matukio mengine ya rushwa.

Alisema endapo itabainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli, wananchi watakosa imani na Bunge lao kwa sababu litakuwa limeshindwa kutumia uhuru wake katika kufanya maamuzi yenye manufaa kwa Taifa.


“Tusubiri tu taarifa ya vyombo vinavyofanya uchunguzi, hapo ndiyo tutapata ukweli wote.Inawezekana pia zikawa ni siasa ndani ya Bunge,lakini uchunguzi ni muhimu kwa sababu lisemwalolipo,” alisisitiza Profesa Mpangala.
 
Uzuri humu hata miaka 10 thread utaikuta kama uliandika pumba utazisoma tena, nilichogundua kuna watu wana misimamo na wengi vigeu geu ila MTU mmoja nimemkubali anamsimamo sana hata kama anachokisimamia ni pumba lakini humtoi


CC: Lizaboni
 
Kulingana na hali inavyokwenda jamaa hataachia madaraka. Unajua nini jamaa anachokifanya ni kujenga syndicate ambayo kila pale atakapoleta agenda yake anahakikisha mfumo wake unamlea. Kwamfano timu ya juu kabisa ya maamuzi yote kaiteua yeye au mtu ambaye amemuweka yeye. Kwa maana ileile anahakikisha maeneo yote ya maamuzi ndani ya kikundi chake anayashikia yeye na hakika hakuna maamuzi zaidi yake yeye. Na kaamua kushika hata matawi yote bila haya anaweka watu wanaomtii yeye tu kwa maslahi yake yeye.

Haya maneno mtayakumbuka siku moja. Mwisho wa siku ile kamati ya kuchinja majina itaondolewa kabla ya mwaka wa uchaguzi, maamuzi ya nani awe yatatolewa na kikosi maalum na huenda watakuwa wawakilishi wa hizi taasisi mfano wazazi, vijana nakadhalika. Ipo siku kamati zitakaa zitaona hakuna haja ya kufanya mabadiliko na watapeleka muswada if hiyo ni hypotheis sahihi. au njia ya pili kamati itakata kila mmoja na kumbakisha kijana yule. Unajua kwa msioona mbali mnachukulia poa tu. lakini maneno yanamimba ipo siku yakizaa mtanikumbuka. Nimeanza mikakati ya kuwa na makazi nje ya nyumbani kwangu. Nimeoa ubakini ili ikifikia ule wakati nisiwe mmoja wa kunyamazishwa kwakua najua ukwel waja.

Wakuu naota tu lakini ipo siku yaja. Sina hakika naongelea timu ya mpira au naungelea nini lakini litakuwa tukio kubwa la kihistoria katika nyika yetu kutokea.

Nangu mahwelu
Bora umemalizia kuwa unaota.
 
Wanabodi hivi kwa waziri kama maghufuri amedanganya umma wa watanzania kwamba flai ova zinajengwa na suala hili kaongea karibu kila bajeti yake anapowasilisha.sasa je waziri kama huyu na bado nae anataka uraisi wakati wizara imemshinda je! Tunampa adhabu gani kwenye msimu huu wa uchaguzi?

Fly over bado huamini Kama zinajengwa?

Wenye akili hawaweki Akiba ya Chupi wanaweka akiba ya Maneno, ona Sasa umeumbuka!
 
Huyu mzee Nyambibo (87) nadhani atakuwa alishakufa kwa kumpa huyo mzee kichwa
Kama hajafa R.I.P. in advance kudaadeki
 
Uzuri humu hata miaka 10 thread utaikuta kama uliandika pumba utazisoma tena, nilichogundua kuna watu wana misimamo na wengi vigeu geu ila MTU mmoja nimemkubali anamsimamo sana hata kama anachokisimamia ni pumba lakini humtoi


CC: Lizaboni

Hata huyo hana msimamo ni swala la mda tuu. Wewe WaTanzania huwajui. Unawasikia tuu!

Waliodeki barabara Lowassa apite (Read Msukuma) ndo hao hao leo wanafagia barabara JPM apite! Na Lowassa wamemchinjia baharini...

It is just a matter of time! Trust nobody. Respect All.
 
Back
Top Bottom