John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Hana Nguvu za kisiasa ndani ya CCM na wala hana sifa zozote kuwapita wenzake ndani ya CCM kama Lowassa, Membe, Sitta, Mwakyembe, Mwandosya, Wassira, Mwigulu, Nchimbi.
Ila sifa moja ya kiCCM ya msingi anayo, ambayo ni Ufisadi. Magufuli ni Fisadi mzuri sana.
Lakini pia ni mnafiki mkubwa, kwani ni juzi tu alimkana Sitta na kudai hana mpango wa Urais kabisa!!
Hapo kwenye bold unamaana huyu huyu nchemba madelu? Kama ni yeye hapana aisee, ni bora Hitler afufuke aje kututawala lakini sio huyo.
 
Kiukweli namkubali Magufuli, najua nikimpigia kura, kura yangu haitapotea bure, all the best Mkuu. All in all Mungu ndiye anajua ni nani atakuwa Rais wa nchi hii, so wote tuombe ili Mungu atuchagulie Rais atakayetuongoza
Acha ujinga ndugu yangu. Mungu ametupa AKILI ya kuweza kutambua na HAKI ya kuamua kile tunachokitaka. Mungu hatuchagulii viongozi bali ni sisi tunaochagua.

Na kama Mwenyezi Mungu angekuwa anatuchagulia viongozi nina uhakika kamwe 2015 asinge mchagua mtu yoyote kutoka CCM.
Kwanini? CCM ndio mfumo unaopalilia Rushwa, Ukandamizaji, Hila, Mauaji, Uonevu na kila ubaya ndani ya nchi yetu kwa sasa.
 
Waziri wa ujenzi bwana John Pombe Magufuli kaamua kuaanika wazi kuwa sasa anautamani urais wa Tanzania.

Kasema hayo huku akitanabaisha kuwa iwapo atakidhi vigezo vya katiba mpya.

Source: Nipashe

..................Kesha ona kunoga maana alitamka kwamba hata U waziri alionao anajionea shida tu... alishawahi kusema yeye alichoomba ni Ubunge sio uwaziri...
 
Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...
So Do I!!
 
Hapo kwenye bold unamaana huyu huyu nchemba madelu? Kama ni yeye hapana aisee, ni bora Hitler afufuke aje kututawala lakini sio huyo.

andate ndio huyo huyo Madelu Mwigulu Nchemba ninaye mzungumzia.
Kuna wanaCCM wenzake wanasema anafaa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM kwa kuwa ataweza kupambana na CHADEMA!!!
 
Last edited by a moderator:
Mbona Mhe.Samwel Sitta aliposema katika kambi ya wanaoutaka urais naye yumo hivyo watamchagua mmoja wao katika kundi hilo alikataa na kusema hakuwa hata na ndoto ya Urais? Kiongozi mnafiki na anayeamua mambo kwa kushawishiwa hawezi kupata kura yangu kwani bila maono huwezi kuongoza taifa. Tamaa gani ya urais ambayo haikuwepo mwezi uliopita lakini sasa anayo?

alisema hana ndoto,hakusema hautamani...na kwa style aliyosema kuwa anautamani urahisi inaonyesha kuwa hajali kama anakua rais au la,kwake siyo deal kubwa.
 
Jamaa anafaa kwa sasa Tanzania inahitaji kiongozi mwemye sifa km zake.
 
Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...

You are totally wrong. Jamaa huyo ni mjanja sana na ana mbinu kali sana za kuteka akili za watu lakini ni fisadi tu kama magamba wenzake. Anzia kwenye kuuza nyumba za serikali halafu umalizie na zile bilions za shilingi zaidi ya 200 ambazo report ya CAG imezianika kwamba hazina maelezo wizarani kwake na yeye mwenyewe akashindwa kuzitolea ufafanuzi kule bungeni. Zaidi ya hayo kama kila siku anamsifia Mr. Fastjet kwa kufanya safari nyingi za nje ya nchi yeye mwenyewe akipewa kiti si atasafiri kuzidi huyo?? Mabadiliko ni muhimu
 
Waziri wa ujenzi bwana John Pombe Magufuli kaamua kuaanika wazi kuwa sasa anautamani urais wa Tanzania.

Kasema hayo huku akitanabaisha kuwa iwapo atakidhi vigezo vya katiba mpya.

Source: Nipashe

mbona Magufuli mwenyewe kasema hajawahi kusema haya? isije ikawa huyu bwana anamwekea baba wa watu maneno mdomoni
 
no thanks.... huna busara ktk maamuz na jazba zisizo na msingi!!!! nadhan FFU watafanya kazi sana huyu jamaa akiwa rais maana hana uvumilivu kabisa!!!

...Tumekuwa na Rais "mwenye hizo unazoziita busara" na "uvumilivu" kwa miaka mingi, huu ni wakati wa watu wa aina ya Magufuli ili waionyooshe kwanza hii nchi....
 
tunasubiri kauri yake rasmi ni jembe tutamuunga mkono
 
You are totally wrong. Jamaa huyo ni mjanja sana na ana mbinu kali sana za kuteka akili za watu lakini ni fisadi tu kama magamba wenzake. Anzia kwenye kuuza nyumba za serikali halafu umalizie na zile bilions za shilingi zaidi ya 200 ambazo report ya CAG imezianika kwamba hazina maelezo wizarani kwake na yeye mwenyewe akashindwa kuzitolea ufafanuzi kule bungeni. Zaidi ya hayo kama kila siku anamsifia Mr. Fastjet kwa kufanya safari nyingi za nje ya nchi yeye mwenyewe akipewa kiti si atasafiri kuzidi huyo?? Mabadiliko ni muhimu

Na wewe acha siasa za maji taka kauza nyumba za serikali unaweza kutupa ushahidi wa kina ikiwa ni pamoja na kutaja namba za nyumba zilizouzwa na ziliuzwa sh ngapi,magufuli anafaa acha maneno mbofumbofu.
 
Akiwa waziri tu aliuza nyumba za serikali. Tukimpa uraisi si atauza hadi nyumba zetu?!!!!
 
kumbe unapenda waongeaji!! kwa taarifa yako magufuli.....hapendwi ndani ya ccm EITHER.....JK na Pinda wanamuogopa na hakuna mwana CCM ndani ya CC atakayempitisha

kingine mkuu Magufuli siyo injinia.......by his age he will never be!!!! ni mkemia

Magufuli msanii tu bana, kajimilikisha nyumba za NHC...na muoga mno!!
 
Back
Top Bottom