John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

hizi ndo tunaitaga steriotype...mwisho mtakuja na "toka lini mhaya akawa raisi".
Mh ameshaukana uhaya na Jina la Kato wa kwa mzee machalila,, jirani yao Telemoni uhuru platform linaeleaa
 
Magufuli (na wengine wachache CCM) anaweza kua Rais mzuri pale tu atakapopitishwa kwa kura za wanaCCM wengi bila ya kushikwa mkono na kakikundi cha watu fulani fulani au kupata huruma ya M/kiti...hapo atakua na "wide mandate" ya "kufanya" yale ambayo Magufuli tumezoea anafanya...otherwise Marais wote wa CCM watategemea a combination ya Dhaifu pamoja na kikundi fulani kitakachomfanya Rais ajaye wa CCM awe dhaifu mwingine (labda atokee kichaa atakayepiga sarakasi na kuwageuka wote waliomuweka kwenye kiti)....
Comment safi
 
Jembe la kazi,sasa ni ulimwengu wa wanasayansi,baba mtakatifu frances wa kanisa katoriki ni mkemia,ni furaha mkemia mwingine kuhisiwa urais tanzania .-na mapungufu yake kama mwanadamu yeyote ,but kwa huyu jpm,ntapanga foleni kupiga kura yangu.
Ulipanga?
 
To be realistic, huyu anakurupuka katika maamuzi! Anakuwa driven na hisia na si reasoning! Dikteita mkubwa hafai! Anatoa maamuzi kwenye jukwaa watu wamsikie. Sawa na Mrema enzi zake. Kweli nchi hii na vichaa wa siasa!
Daah!Ndiyo shida ya watu kutokusoma comments za wenzao!Kumbe haya yote yalikuwa kweli?Daah! Sasa nimeamini kweli jiwe kawa rais kwa bahati mbaya.
 
Nchi inataka rais aina ya magufuli kwa sasa,dikteta halafu mtendaji,huyu kwa Tanzania ya sasa anafaa sana aje kurudisha nchi kwenye mstari,wasiwasi wangu jeshi litampindua tu,kwa sababu jeshini kuna ufisadi kiwango cha kutisha
Duh
 
Nchi inataka rais aina ya magufuli kwa sasa,dikteta halafu mtendaji,huyu kwa Tanzania ya sasa anafaa sana aje kurudisha nchi kwenye mstari,wasiwasi wangu jeshi litampindua tu,kwa sababu jeshini kuna ufisadi kiwango cha kutisha
Geshi liko mfukoni
Safu ya juu ni WA NYUMBANI
 
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos', muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong'ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

"Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani, mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri," alisema Dk. Magufuli.

"Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo&[HASHTAG]#8230[/HASHTAG];na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana," alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa &[HASHTAG]#8211[/HASHTAG];CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.

Chanzo: Nipashe

==============
UPDATE (1):

Tarehe 18, Feb 2015: Kwa mujibu wa magazeti ya leo; Magufuli katangaza nia kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano
Kwahiyo mkuu aliongopa aliposema hautaki urais na kaupata kwa bahati mbaya tu kwani alikuwa akijaribisha tuu!

Uongo wa sampuli hii tayari ni disqualification.
 
......Ni Mafuta yanayobaki kwenye magamba ya Korosho yanavyoweza kutumika kutengeneza Chemical za kuulia wadudu waharibio mazao mashambani, ameifanyia PHD yake huko South Africa.
Hii phd ya utomvu mbona ina maelezo mengi ya tofauti tofauti? Huo utomvu wa maganda ya korosho una kazi gani aliyoigunduwa?Kuna wanaosema umeme, wengine mnasema dawa za kuulia wadudu shambani. Kipi ni kipi?Ndo maana wakampoteza Ben Saanane, maana hamna kitu inaeleweka hapa.
 
Back
Top Bottom