HUna lolote lile zaidi ya focus ya Uchaguzi wa 2015. Jk anajua makalala siyo mtu wa kuingilika na mambo yasio leta haki ndo maana akamruka kiaina. Na huyo Chacha naye ni Mlokole? Teuzi za kisiasa hizi hakuna la ziada.Tujaribu kuwa waelewa na wepesi wa kupambanua mambo Jeshini kuna Vyeo na Madaraka pia hata Jeshi la Polisi pia kuna Vyeo na Madaraka kwa mfano Ma RPC karibu wote ni Ma Senior Assisstant Commissioners of Police ingawa wapo wenye nafasi Vyeo chini ya hapo ama juu ya hapo. Kwa Jeshi la Wanainchi tulikuwa na utaratibu wa kuwa na Luteni Jenerali mmoja tu ambae ndiyo anakuwa ni Afisa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi na Meja Jenerali wengi wanakuwa wakuu wa Vitengo sasa inafika wakati una Meja Jenerali Watano na wote wanastahiki kuwapandisha cheo lakini madaraka wanayotakiwa kuyashika iko nafasi moja kimsingi utaangalia vigezo vingi sana mpaka umpate mmoja ambae utmteua na kumpandisha cheo kushika madaraka husika ila hautatenda haki kama wengine wanaostahili kupandishwa cheo hawatapandishwa cheo,nafasi ya kuwalipa stahiki zao kama ipo basi huna haja ya kuwanyima cheo husika ila madaraka yatabaki kwa mtu mmoja ambae umemteuwa kushika madaraka husika. Hivi sasa watu wamejenga utaratibu usio rasm wakumbeza Mheshimiwa Raisi kila anapofanya uteuzi mara oohooo hakuzingatia sifa za wateuliwa mara aliowateua hawana elimu stahiki mara amewateua waislam watupu mara ameteua marafiki zake tuu hii imejijenga kuwa tabia miongoni mwetu tena ni tabia mbaya ambayo haina mfano. Mimi namfahamu sana Luteni Jenerali Makakala mpaka famillia yake karibu yote iliyopo Kijiji cha Ndengere na Mbamba Bay ila miaka ya karibuni Luteni Jenerali huyu amejiunga na Dhehebu la KILOKOLE sasa angeweza kuwa Afisa Mnadhimu Mkuu kabla ya Luteni Jenerali Ndomba ambao wote hawa wanatoka Mkoa wa Ruvuma tena hapo mwanzo walikuwa wanatoka Wilaya moja ya Mbinga kabla ya kutenganishwa na kuwa na Wilaya ya Nyasa ambako Makakala ndiko anakotoka. Hivyo basi Ulokole wa Makakala ndiyo umempunguzia saifa ya ziada kumbuka Jeshini kuna kitengo cha Ujasusi cha Jeshi[Military Intelligence Unit] ambacho kina kazi ya ziada ya kuwachunguza Maofisa wa Jeshi mienendo yao ya kila siku na kuripoti moja kwa moja kwa Mkuu wa Majeshi hivyo tusilaumu kila uteuzi maana vigezo vingine vinavyotumika ni vigumu kuvitambua. Jeshi ni Taasisi nyeti ambayo inafanya mambo yake kwa utaratibu na tamaduni zinazoeleweka. Jeshi siyo Chama cha siasa vinginevyo tungekuwa hatuishi kwa amani hapa angalia mifano ya Nchi kama Mali kila siku Jeshi ni kupindua tu Serikali halali ni kwa sababu hawana utaratibu tusilaumu hovyo hovyo!