JK awapandisha vyeo majenerali

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780

Na Mwandishi Wetu, Dar na Rufiji

Posted Jumanne,Decemba4 2012 saa 22:59 PM

KWA UFUPI

Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inaeleza kuwa maofisa wakuu waliopandishwa cheo ni Meja Jenerali, Sylvester Chacha Ryoba ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Luteni Jenerali.

RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu.

Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inaeleza kuwa maofisa wakuu waliopandishwa cheo ni Meja Jenerali, Sylvester Chacha Ryoba ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Luteni Jenerali.

Mwingine ni Meja Jenerali, Charles Lawrance Makakala ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi.

Rais Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewapongeza wakuu hao.

Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kufanya ziara ya siku moja mjini Rufiji, licha ya mambo mengine atahutubia mkutano wa hadhara mjini Ikwiriri.

Akizungumza jana kwenye Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alisema Rais Kikwete atapokelewa mpakani mwa wilaya ya Kilwa na Rufiji, eneo la Malendego.

Rwegasira alisema wananchi wa Rufiji wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo atakapoingia wilayani hapa ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mwaka 2010.

Hata hivyo, Rwegasira aliwataka madiwani kuwajulisha wananchi kushiriki kumpokea.

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,880
9,832
Yeye atapandishwa cheo lini kutoka kwenye uluteni kanali wake ambao hata hivyo huwa hapendi kuutumia zaidi ya udaktari wa kuchakachuliwa na kupewa?

Mkuu yeye alishatoka huko jeshini.

Hongereni sana Lt. Gen. Ryoba na Lt. Gen. Makakala. Naona tunazidi kusonga mbele. Huko nyuma jeshini kulikuwa kwa kawaida kuna Four-Star General (CDF) mmoja na Three-Star General mmoja (CoS) lakini sasa naona tuna Four Star General mmoja na three star generals watatu mmoja akiwa ni CoS. Tuendako huenda tukapata general of the army (five-star general) na hivyo four-star generals kuwa wengi pia.
 
Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,228
7,890
Rais kikwete Huu mfumo wa Jeshi anautoa wapi?

JWTZ at any given time inakuwa na Active General mmoja tu ambaye ni Mkuu wa Majeshi.......

..........na active Lt Gen mmoja tu ambaye ni Chief of Staff.............

As of hawa wawili...Sylvester Riyoba na Charles Makalala.....ambao kabla ndio waliokuwa na seniority na wakapendekezwa mmoja wao awe chief of staff...Lakini badala yake Kikwete ammpandisha cheo Junior wao....Sylvester Ndomba kuwa chief of staff...

Kinachoonekana haPa kikwete...ameamua Kuvunja utaratibu wa kimuundo wa Jeshi kuipeleka kuwa na ma luteni generali watatu Kazini badala ya mmoja........ni mbinu tu ya Rais kuwapooza hawa senior general kwa kitendo chake cha kuwaruka wakati na kumuwekA junior kuwa chief of staff......

Pamoja na kuwa hawa wanastahili kupanda .....upandishaji Huu ni holela kwa kuwa umevuruga mfumo wa Jeshi .........hii inatokea wakati Jeshi bado watu wanashangaa muundo wake wa kuwa na mameja jenerali wawili ...wanamama kwenye kitengo cha utuumishi ambacho Mara zote kimekuwa kikiongozwa na brigedia generali au maj generali....na msaidizi kanali au brigedia .....kitendo cha kuweka maj generals wawili kitengo Kimoja ni matumizi mabaya ya rasilimali watu....
 
Kaka Huu ni mwendelezo wa uteuzi za kijikosha.....hawa wawili ndio walikuwa maj generals senior kuliko wote....active Jeshini .....kiutaratibu mmoja wao lazima alikuwa awe chief of staff...na likely ilikuwa awe Makalala...kwa kuwa mbinu ya kawaida ya kumuhamishia senior Riyoba ikulu ...ofisi ya PM...pia ni option pale ambapo unataka kumkwepesha kuwa CoS kwa wakati husika.
kitendo cha Ndomba kurushwa...na kuwaruka hawa...kilileta minongono...miongoni mwa majenerali na senior commenders........naona Mkuu anajikosha at the expense ya kuvuruga utamaduni...ni udhaifu Huu
 
Atukilia

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
642
203
Ndio maana baadhi yetu tunapendekeza kwenye katiba mpya madaraka ya Rais yapunguzwe.

Ilipaswa kuwa na muundo unaotaka wawepo hao maluteni jenerali na sio tu watu wanapandishwa vyeo kwa kuwaangalia, sasa mmoja ameshatoka jeshini (sina hakika kama kitengo cha maafa ni sehemu ya jeshi) halafu anapandishwa cheo!

Zaidi zaidi ni kupata mafao ya uleteni general ukistaafu na ni gharama kwa walipa kodi. Hata hivyo kwa utaratibu wa Jeshi Ndomba ni senior kwa hawa aliwatangulia kupata hiki cheo!
 
MKALIKENYA

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
1,196
484
Mkuu yeye alishatoka huko jeshini.

Hongereni sana Lt. Gen. Ryoba na Lt. Gen. Makakala. Naona tunazidi kusonga mbele. Huko nyuma jeshini kulikuwa kwa kawaida kuna Four-Star General (CDF) mmoja na Three-Star General mmoja (CoS) lakini sasa naona tuna Four Star General mmoja na three star generals watatu mmoja akiwa ni CoS. Tuendako huenda tukapata general of the army (five-star general) na hivyo four-star generals kuwa wengi pia.

Hayo ma FOUR and FIVE star kwangu si kitu kama yule mama wa MALAWI hatuwezi kumshikisha adabu asubuhi na mapema.
 
Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
43,203
25,648
Kaka Huu ni mwendelezo wa uteuzi za kijikosha.....hawa wawili ndio walikuwa maj generals senior kuliko wote....active Jeshini .....kiutaratibu mmoja wao lazima alikuwa awe chief of staff...na likely ilikuwa awe Makalala...kwa kuwa mbinu ya kawaida ya kumuhamishia senior Riyoba ikulu ...ofisi ya PM...pia ni option pale ambapo unataka kumkwepesha kuwa CoS kwa wakati husika.
kitendo cha Ndomba kurushwa...na kuwaruka hawa...kilileta minongono...miongoni mwa majenerali na senior commenders........naona Mkuu anajikosha at the expense ya kuvuruga utamaduni...ni udhaifu Huu

Mkuu kwani wewe ulitaka JK afanyaje?
 
Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
5,065
2,424
Rais kikwete Huu mfumo wa Jeshi anautoa wapi?

JWTZ at any given time inakuwa na Active General mmoja tu ambaye ni Mkuu wa Majeshi.......

..........na active Lt Gen mmoja tu ambaye ni Chief of Staff.............

As of hawa wawili...Sylvester Riyoba na Charles Makalala.....ambao kabla ndio waliokuwa na seniority na wakapendekezwa mmoja wao awe chief of staff...Lakini badala yake Kikwete ammpandisha cheo Junior wao....Sylvester Ndomba kuwa chief of staff...

Kinachoonekana haPa kikwete...ameamua Kuvunja utaratibu wa kimuundo wa Jeshi kuipeleka kuwa na ma luteni generali watatu Kazini badala ya mmoja........ni mbinu tu ya Rais kuwapooza hawa senior general kwa kitendo chake cha kuwaruka wakati na kumuwekA junior kuwa chief of staff......

Pamoja na kuwa hawa wanastahili kupanda .....upandishaji Huu ni holela kwa kuwa umevuruga mfumo wa Jeshi .........hii inatokea wakati Jeshi bado watu wanashangaa muundo wake wa kuwa na mameja jenerali wawili ...wanamama kwenye kitengo cha utuumishi ambacho Mara zote kimekuwa kikiongozwa na brigedia generali au maj generali....na msaidizi kanali au brigedia .....kitendo cha kuweka maj generals wawili kitengo Kimoja ni matumizi mabaya ya rasilimali watu....

Mkuu unazungumza utamaduni lakini sio muundo wa jeshi. Generali ni cheo cha kijeshi na sio madaraka. Mkuu wa jeshi ni madaraka. Hivyo kunaweza kuwepo kwa mageneral watatu.

Na luteni general ni cheo vilevile na sio madaraka ya kuwa chiefu of staff. Kwa Tanzania hata major general anaweza kuwa chief of staff.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom