JK awapandisha vyeo majenerali

JK awapandisha vyeo majenerali

Mkuu JokaKuu

Umechokoza swali muhimu sana. Kwa mfano itokee Ndomba anaondoka kwenye utumishi sasa hivi(eg kwa maradhi/death) itamanisha kuwa CoS mpya LAZIMA atoke kati ya Makakala/Ryoba AMA wastaafishwe jeshi kabla ya muda wao AMA ateuliwe mwingine na apewe uGenerali.

Either way. WAMECHEMKA
 
Last edited by a moderator:
Hemed Maronda, ngwendu, gobore, Phillemon Mikael,

..JK akiendelea namna hii itafika mahali tutalazimika kuwa na FIELD MARSHAL ktk jeshi letu.

..sote tunapaswa kuelewa kwamba CHEO/RANK ndiyo inayompa final say mhusika yeyote yule jeshini.

..waliofanya uamuzi kwamba CDF na COS wawe na vyeo vya Jenerali, na Luteni Jenerali, na no other active soldier should have those ranks walikuwa na busara zao.

..je, leo hii ikitokea kwamba Lt.Gen.Ndoma ana-retire au kwa namna moja au nyingine hawezi kuendelea na wadhifa huo, what is going to be the rank of the COS will replaces him??

..Je, JK atalazimika kumteua Makakala au Ryoba kuwa COS kutegemea nani ndiyo senior Lt.Gen?? Je, the incoming COS itabidi awe na cheo cha Jenerali ili aweze kutoa amri kwa Makakala na Ryoba? Au, Makakala na Ryoba wastaafishwe toka jeshini hata kama hawajafikia umri wa kustaafu?

..kwa kweli uamuzi huu wa JK umeniacha na maswali mengi sana.

Ndio maana nikauliza Mh Rais anayo mamlaka ya kupandisha vyeo na kuteua bila ushauri wowote? Tatizo ni Mh Rais tu au na wasaidizi wake kama Mkuu wa Majeshi?
 
Mimi siyo mtaalamu wa majeshi wajuzi naombeni kufahamu kitu kimoja. Tuseme kwa mfano, Luteni Generali Ndoma, kama Chief of staff, ashindwe kuendelea na kazi hiyo kwa sababu moja au nyingine (Mungu epusha mbali), ni nani kati ya Luteni Generali Sylvester Chacha Ryoba na Luteni Generali Charles Lawrance Makakala atachukua hiyo nafasi ya Chief of Staff?

Ni nani senior kati ya Luteni Generali Sylvester Chacha Ryoba na Luteni Generali Charles Lawrance Makakala?
 
MTAZAMO,

..kwa uelewa wangu Raisi anayo mamlaka ya kuchukua au kutochukua ushauri ktk teuzi zake.

..tatizo linaweza kuwa la washauri, raisi, au wote raisi na washauri wake.

..I just hope kwamba teuzi hizi hazitaleta complications huko mbele ya safari ama kwa JK, au raisi atakayemfuatia.

gobore,

..labda Lt.Gen.Ryoba na Makakala wanakaribia kustaafu hivyo hakutakuwa na tatizo lolote lile.

..hopefully, Ndomba, Makakala, na Ryoba, watastaafu kwa wakati mmoja.

EMT,

..it is not automatic kwamba Ryoba au Makakala watakuwa COS ikiwa Ndomba atastaafu.

..seniority baina ya Ryoba na Makakala inategemea ni nani ameteuliwa kabla ya mwenzake.

..lazima barua za uteuzi wao zielekeze suala hilo, au labda kitakachoangaliwa ni nani alikuwa senior kwa mwenzake ktk rank ya Maj.General.

..hili ni tukio ambalo liliwahi kutokea: Twalipo na Musuguri walipandishwa vyeo kuwa Generals siku moja. Sasa Twalipo alikuwa senior kwa Musuguri kwasababu yeye ndiye alitangulia kuvalishwa cheo chake na Mwalimu Nyerere pale Ikulu.

..pia kuna kipindi Maj Gen Kiwelu alikuwa senior kuliko Maj General Ernest Kiaro. Mzee Mwinyi akampandisha cheo Kiaro kuwa General na kumteua kuwa CDF. Kiwelu akapandishwa cheo kuwa Lt.Gen na kuteuliwa kwa mara ya pili kuwa CSO.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Rais kikwete Huu mfumo wa Jeshi anautoa wapi?

JWTZ at any given time inakuwa na Active General mmoja tu ambaye ni Mkuu wa Majeshi.......

..........na active Lt Gen mmoja tu ambaye ni Chief of Staff.............

As of hawa wawili...Sylvester Riyoba na Charles Makalala.....ambao kabla ndio waliokuwa na seniority na wakapendekezwa mmoja wao awe chief of staff...Lakini badala yake Kikwete ammpandisha cheo Junior wao....Sylvester Ndomba kuwa chief of staff...

Kinachoonekana haPa kikwete...ameamua Kuvunja utaratibu wa kimuundo wa Jeshi kuipeleka kuwa na ma luteni generali watatu Kazini badala ya mmoja........ni mbinu tu ya Rais kuwapooza hawa senior general kwa kitendo chake cha kuwaruka wakati na kumuwekA junior kuwa chief of staff......

Pamoja na kuwa hawa wanastahili kupanda .....upandishaji Huu ni holela kwa kuwa umevuruga mfumo wa Jeshi .........hii inatokea wakati Jeshi bado watu wanashangaa muundo wake wa kuwa na mameja jenerali wawili ...wanamama kwenye kitengo cha utuumishi ambacho Mara zote kimekuwa kikiongozwa na brigedia generali au maj generali....na msaidizi kanali au brigedia .....kitendo cha kuweka maj generals wawili kitengo Kimoja ni matumizi mabaya ya rasilimali watu....

Kwa hakika hakuna tatizo lolote kuwa na active generals kadha wakati mmoja. Kuna nchi nyingi ambazo zinakuwa na 4-star generals wakiwa wamepewa nyadhifa mbalimbali. Kwa mfano, Marekani wanaweza kuwa na Joint Chiefs of Staff majenerali na ma-admiral wakati huo huo viongozi wanaoongoza shughuli za medani sehemu mbalimbali wakawa 4 star generals pia. Mfumo wa majeshi waweza kupangwa na nchi yenyewe inavyoona itafaa vipi. Sidhani kama Baba Ritz hapo kakosea. Anapotoka mengine, and God knows ni mengi mno. Lakini si hili.
 
Tujaribu kuwa waelewa na wepesi wa kupambanua mambo Jeshini kuna Vyeo na Madaraka pia hata Jeshi la Polisi pia kuna Vyeo na Madaraka kwa mfano Ma RPC karibu wote ni Ma Senior Assisstant Commissioners of Police ingawa wapo wenye nafasi Vyeo chini ya hapo ama juu ya hapo.

Kwa Jeshi la Wanainchi tulikuwa na utaratibu wa kuwa na Luteni Jenerali mmoja tu ambae ndiyo anakuwa ni Afisa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi na Meja Jenerali wengi wanakuwa wakuu wa Vitengo sasa inafika wakati una Meja Jenerali Watano na wote wanastahiki kuwapandisha cheo lakini madaraka wanayotakiwa kuyashika iko nafasi moja kimsingi utaangalia vigezo vingi sana mpaka umpate mmoja ambae utmteua na kumpandisha cheo kushika madaraka husika ila hautatenda haki kama wengine wanaostahili kupandishwa cheo hawatapandishwa cheo, nafasi ya kuwalipa stahiki zao kama ipo basi huna haja ya kuwanyima cheo husika ila madaraka yatabaki kwa mtu mmoja ambae umemteuwa kushika madaraka husika.

Hivi sasa watu wamejenga utaratibu usio rasm wakumbeza Mheshimiwa Raisi kila anapofanya uteuzi mara oohooo hakuzingatia sifa za wateuliwa mara aliowateua hawana elimu stahiki mara amewateua waislam watupu mara ameteua marafiki zake tuu hii imejijenga kuwa tabia miongoni mwetu tena ni tabia mbaya ambayo haina mfano.

Mimi namfahamu sana Luteni Jenerali Makakala mpaka famillia yake karibu yote iliyopo Kijiji cha Ndengere na Mbamba Bay ila miaka ya karibuni Luteni Jenerali huyu amejiunga na Dhehebu la KILOKOLE sasa angeweza kuwa Afisa Mnadhimu Mkuu kabla ya Luteni Jenerali Ndomba ambao wote hawa wanatoka Mkoa wa Ruvuma tena hapo mwanzo walikuwa wanatoka Wilaya moja ya Mbinga kabla ya kutenganishwa na kuwa na Wilaya ya Nyasa ambako Makakala ndiko anakotoka.

Hivyo basi Ulokole wa Makakala ndiyo umempunguzia saifa ya ziada kumbuka Jeshini kuna kitengo cha Ujasusi cha Jeshi[Military Intelligence Unit] ambacho kina kazi ya ziada ya kuwachunguza Maofisa wa Jeshi mienendo yao ya kila siku na kuripoti moja kwa moja kwa Mkuu wa Majeshi hivyo tusilaumu kila uteuzi maana vigezo vingine vinavyotumika ni vigumu kuvitambua. Jeshi ni Taasisi nyeti ambayo inafanya mambo yake kwa utaratibu na tamaduni zinazoeleweka.

Jeshi siyo Chama cha siasa vinginevyo tungekuwa hatuishi kwa amani hapa angalia mifano ya Nchi kama Mali kila siku Jeshi ni kupindua tu Serikali halali ni kwa sababu hawana utaratibu tusilaumu hovyo hovyo!

Kwahiyo mtu kuwa mlokole kunampunguzia sifa ya kuwa kiongozi sio? Mi nilifikiri nchi yetu haibagui watu kwa imani zao! Yaani Tz walokole wameshaanza kubaguliwa siyo? Kazi mnayo!
 
Kwahiyo mtu kuwa mlokole kunampunguzia sifa ya kuwa kiongozi sio? Mi nilifikiri nchi yetu haibagui watu kwa imani zao! Yaani Tz walokole wameshaanza kubaguliwa siyo? Kazi mnayo!

Mkuu wangu licha mimi binafsi kuheshimu imani za watu wengine lakini napenda kusema ukweli kwamba Watanzania wengi wanatumbukia ktk Ulokole kutokana na matatizo ya maisha yanayosababishwa na matatizo ya kiafya na pesa! Ni kuchanganyikiwa kwa aina fulani. Na hii ni kwa dini zote mbili kubwa hapa ambazo ni Ukristo na Uislamu. Na hawa ndiyo wamekua chanzo cha udini wa kijinga ktk nchi yetu.
 
Haya wee si kila jambo lafaa kujibiwa....
 
MTAZAMO,

..kwa uelewa wangu Raisi anayo mamlaka ya kuchukua au kutochukua ushauri ktk teuzi zake.

..tatizo linaweza kuwa la washauri, raisi, au wote raisi na washauri wake.

..I just hope kwamba teuzi hizi hazitaleta complications huko mbele ya safari ama kwa JK, au raisi atakayemfuatia.

gobore,

..labda Lt.Gen.Ryoba na Makakala wanakaribia kustaafu hivyo hakutakuwa na tatizo lolote lile.

..hopefully, Ndomba, Makakala, na Ryoba, watastaafu kwa wakati mmoja.

EMT,

..it is not automatic kwamba Ryoba au Makakala watakuwa COS ikiwa Ndomba atastaafu.

..seniority baina ya Ryoba na Makakala inategemea ni nani ameteuliwa kabla ya mwenzake.

..lazima barua za uteuzi wao zielekeze suala hilo, au labda kitakachoangaliwa ni nani alikuwa senior kwa mwenzake ktk rank ya Maj.General.

..hili ni tukio ambalo liliwahi kutokea: Twalipo na Musuguri walipandishwa vyeo kuwa Generals siku moja. Sasa Twalipo alikuwa senior kwa Musuguri kwasababu yeye ndiye alitangulia kuvalishwa cheo chake na Mwalimu Nyerere pale Ikulu.

..pia kuna kipindi Maj Gen Kiwelu alikuwa senior kuliko Maj General Ernest Kiaro. Mzee Mwinyi akampandisha cheo Kiaro kuwa General na kumteua kuwa CDF. Kiwelu akapandishwa cheo kuwa Lt.Gen na kuteuliwa kwa mara ya pili kuwa CSO.

Mkuu uko sawa. Hakuna shida yoyote kwenye kuteua ama kupandisha vyeo. Kupandishwa cheo kunategemea vitu vingi sana siyo kwamba wewe ni senior basi utaendelea kuwa senior weeeeee!Jeshi ni taasisi sensitive sana na suala la vyeo ni sensitive pia.
 
Kwa hakika hakuna tatizo lolote kuwa na active generals kadha wakati mmoja. Kuna nchi nyingi ambazo zinakuwa na 4-star generals wakiwa wamepewa nyadhifa mbalimbali. Kwa mfano, Marekani wanaweza kuwa na Joint Chiefs of Staff majenerali na ma-admiral wakati huo huo viongozi wanaoongoza shughuli za medani sehemu mbalimbali wakawa 4 star generals pia. Mfumo wa majeshi waweza kupangwa na nchi yenyewe inavyoona itafaa vipi. Sidhani kama Baba Ritz hapo kakosea. Anapotoka mengine, and God knows ni mengi mno. Lakini si hili.

Kaka kwenye Tasnia ya kijeshi....idadi ya majenerali inategemea zaidi...na ukubwa wa Jeshi ....usilinganishe Tanzania na marekani ....kule wana active combat soldiers more than one million ....wana operations kila continent ....achilia special operations ......wao hata wakiwa na four star generals 50 ni halali..........ndio maana wao Mkuu wa Majeshi anaitwa Chairman of Joint Generals staff.

Nchi maskini Kama zetu ...ratio yetu ni Askari 5000 kwa brigedia Generals mmoja....Askari 5000 ni divisheni....kwa hapa kuna divisheni zaidi ya tano...na kila moja imomgozwa na brigedia jenerali....mameja jenerali wengi wanakuwa Makao makuu kuongoza Idara kubwa..or wings,...ie personnel ,uhandisi na ugavi,Jeshi la maji,Jeshi la nchi kavu,Anga,Upelelezi,Idara ya utendaji vita or war department .,military medical serv,..mipango ,reserve force na militia,uhakiki etc..na hasa mikakati...idadi nyingine ya brigedia generals ambao hawaongozi divisheni...huwa manaiibu kwenye hivi major wings....na juu yao anakuwapo chief of staff...mmoja ambaye is more or less prime minister ...anaxhughulika na utendaji wa kila Siku ....then CDF...
 
Viongozi wengi walio JKT ndio sasa hivi Wanalishikila JWTZ na WENGI wa JWTZ hawafurahii UAMUZI huo
Mfano MKUU WA MAJESHI ni wa JKT - ALisha kuwa MKUU wa KIKOSI MAKUYUNI ARUSHA
Afisa Utawala NDOMBA -- JKT Wanadai kuwa hawana MAFUNZO kama walio JWTZ waliyonayo; MASELULE walipokuwa JKT walikuwa wanahepa MAFUNZO MENGI TU na kulikuwa hakuna MSISITISO kwao

Nnugu.....Hizo ni habari za kijiweni sio Hali halisi ...mfumo wa sasa hakuna toffauti Kati ya JKT na JW.....toffauti inaonekana nje...Lakini ndani....ni kitu Kimoja .........Zamani wakati JKT Inanza Enzi ya kina Kaswende na Gama labda.....
fanya zoezi dogo ...Angalia mabega ya Askari wa JKT,...kuna nembo ya JW.
jkt ni kama wing ya JW Kama navy au airwing...ila wao malengo Yao ni kuzalisha Mali na kuandaa vijana kwa ajili ya ajira kwenye Majeshi na usalama na Malezi...ya vijana kwa mujibu wa sheria
 
Oh YEAH SASA HIVI NI KITU KIMOJA; Lakini Wakati ULE LA; Sasa VIONGOZI wanaochaguliwa SASA walikuwepo WAKATI ULE... Kwahiyo KUNA MAFUNZO waliyoyahepa... MENGI TU... Lakini Sasa wanaVYEO VIKUBWA JWTZ
 
Oh YEAH SASA HIVI NI KITU KIMOJA; Lakini Wakati ULE LA; Sasa VIONGOZI wanaochaguliwa SASA walikuwepo WAKATI ULE... Kwahiyo KUNA MAFUNZO waliyoyahepa... MENGI TU... Lakini Sasa wanaVYEO VIKUBWA JWTZ

Kwa kifupi kwa sasa maafisa wote wa JKT Wamepata mafunzo yao Tanzania Millitary Academy....kinachofanyika ni kuwa kutokana na mafunzo ya fani unakuta wataalamu kama wa kilimo,mifugo na sekta nyingine za uzalishaji baada ya kumaliza mafunzo JWTZ basi kituo chao cha kazi wanapangiwa JKT........
JKT Pia wana chuo cha kuwafundisha mafunzo ya ziada maafisa...ili waweze kuwa Walezi wazuri Na wazalishaji mali......lakini ikitokea mafunzo ya ziada ambayo kila baada ya kipindi fulani yanamlazimu ofisa kufanya ili apande cheo au kwa ajili ya utimamu basi .....maafisa hao huenda tena kwenye vyuo vya kijeshi [jwtz].........
Na pia wakati wowote wanaweza kuhamishwa kurudishwa JW.
 
Napenda kuwashukuru wote mliochangia hii mada , binafsi ni ELIMU tosha kwangu, nilikuwa sijui muundo wa jeshi la Tanzania ikoje. shukrani kwa kuniongezea knowledge ...nimesoma comments zote za wachangiaji kuongeza wigo wa kuelewa haya mambo.
 
Karibu
 
Kwa kifupi kwa sasa maafisa wote wa JKT Wamepata mafunzo yao Tanzania Millitary Academy....kinachofanyika ni kuwa kutokana na mafunzo ya fani unakuta wataalamu kama wa kilimo,mifugo na sekta nyingine za uzalishaji baada ya kumaliza mafunzo JWTZ basi kituo chao cha kazi wanapangiwa JKT........
JKT Pia wana chuo cha kuwafundisha mafunzo ya ziada maafisa...ili waweze kuwa Walezi wazuri Na wazalishaji mali......lakini ikitokea mafunzo ya ziada ambayo kila baada ya kipindi fulani yanamlazimu ofisa kufanya ili apande cheo au kwa ajili ya utimamu basi .....maafisa hao huenda tena kwenye vyuo vya kijeshi [jwtz].........
Na pia wakati wowote wanaweza kuhamishwa kurudishwa JW.

Ngongo

Yeah kwa SASA... Lakini HAWA VIONGOZI waliopo MADARAKANI wa JKT hawakupitia hayo MAFUNZO ya Wa JWTZ; Then walikuwa wanayakimbia na kuruka hayo MAJUKUMU
 
napenda kuwashukuru wote mliochangia hii mada , binafsi ni elimu tosha kwangu, nilikuwa sijui muundo wa jeshi la tanzania ikoje. Shukrani kwa kuniongezea knowledge ...nimesoma comments zote za wachangiaji kuongeza wigo wa kuelewa haya mambo.

selule au mjongoji?
 
Back
Top Bottom