Huu ni uzi maalum wa kujifunza kununua bidhaa mbalimbali kutoka alibaba. Natumai wanunuzi wa alibaba mpo huku.

Tunapaswa kujifunza ni yapi ya kuzingatia kwani wengi wetu tumezoea kununua aliexpress.

Na naomba nikiri kuwa alibaba sasa hivi wanauza pia bidhaa moja moja zipo nyingi tu.

Cha msingi ni kutazama minimum order ukiona.minimum order ni 1 ujue hapo utaweza kununua bidhaa hata 1 tu kama tulivyozoea mitandao mingine
Halafu huku bidhaa ni rahis mno kuliko popote pale duniani.

Naomba wenye ujuzi waje watufunze na ambao mshawahi kununua humu hususan bidhaa moja moja

Napenda kujua yafuatayo;-
Gharama za usafirishaji
Mzigo unafika kwa siku ngapi? mapema au unachelewa?
Vipi kuhusu kukatwa kodi ya vitu kama ukinunua tv yako, ama radio kubwa kama subwofer?
Jee wanaruhusu paypal?

Ni hayo tu natumai uzi huu tutajifunza mengi
 
Alibaba imepigwa marufuku USA kwa sababu ya kuuza bidhaa fake...yaani unaagiza bidhaa lakini unaipata ikiwa counterfeit aunchini ya kiwango...labda ununue kupitia Amazon au Ebay...
 
Masoko yanayoamini Kabisa na Shipment yake ni ya haraka Ni Ebay Na Amazon, Hayo masoko Ya Jack Ma ni Poa sana Kwa price ila linapokuja la Genuine Product na Kuship kwa Wakati ni Shidaa
 
Naombeni ushauri payment method nyingine tofauti na paypal...kwasababu paypal account yangu hailink na crdb bank accound yangu!
 
Kupigwa kodi inategemeana na njia uliyotumia!
Fedex,ems,ups,dhl au posta(percel) kwa uzoefu wangu hapa lazima mzigo ufunguliwe na utapigwa kodi 25%income tax+18%vat ya thamani ya pesa uliyonunua kwa kulingana na kiwango cha pesa cha dola siku hiyo.
Kama mzigo ni mdogo chini ya kg 2 hapa nakushauri utumie registered airmail with tracking namba hii ni huduma ya posta na inachukua siku 7-21 kufika,advantage ya hii mzigo haufunguliwi unapewa kama ulivyo na hubugudhiwi na wale watu wa tra pale posta.
Asante.
Kwa mfano nataka nunua dslr camera ya dollar 2000 - 4000, kodi yake inaweza kuwa ngapi
 
Kwa mnaotumia kadi ya NBC ni lazima kadi yako ukaombe wairuhusu kufanya online transaction?Au inakubali tu?
 
Hatimaye nimefungua akaunt equity ahsanteni sana mlionishauri thanks mwlm rct mungu akubariki @Mwl_Rct
 
Najaribu kujisajili paypal inazngua hususan nikijaza tarehe na mwaka wa kuzaliwa sasa sijui nakosea nn wakuu
 
Back
Top Bottom