Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa - Dubai lapambwa kwa picha za Bendera ya Tanzania

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Jengo refu zaidi Duniani la Burj Khalifa pale Dubai muda huu limenakshiwa kwa Bendera ya Tanzania mwanzo mpaka mwisho lote. Dunia nzima sasa inatazama maajabu haya kwenye Jengo hilo refu zaidi Duniani huku Utalii wa Taifa letu ukizidi kutangazwa.

Yote hii ni matunda ya ziara ya siku 3 ya Rais Samia Suluhu Hassan Dubai na heshima inayopewa Taifa letu baada ya ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio makubwa sana ya Kiuchumi na Uwekezaji.

Hiyo ni pamoja na mafanikio mengine makubwa ya ziara hiyo ambayo ni Kusainiwa kwa Hati 36 za Makubaliano ya Ushirikiano kwenye sekta mbalimbali yenye thamani ya Shilingi Trilioni 17.1 ambayo itatoa ajira 204,575 kwa Watanzania. Ziara ya Rais Samia Dubai imetulipa kwelikweli. Kazi Iendelee.

Bwanku M Bwanku
bwanku55@gmail.com

burji.jpg



IMG-20220228-WA0003.jpg


IMG-20220228-WA0002.jpg
 
Ana kimuhemuhe tu juzi kati tu Ronaldo aliwekwa hapo siku ya birthday yake. Hamna maajabu kuwekwa bendera ya Tanzania wakati rais yupo huko.
Maajabu yapo sababu watu wa mataifa mengine kuifahamu Tz ni jambo zuri. Ni kama bango la tangazo.
 
Back
Top Bottom