figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,492
- 54,895
Jengo la PSPF
Ukiacha na Jengo refu kabisa duniani la Burj Khalifa la huko Dubai lenye urefu wa kwenda Juu zaidi ya Mita 828, sasa yanajengwa Majengo mapya Marefu kulipita na yanatazimwa kufunika kabisa Khalifa. Je, Watafanikiwa kuyajenga?
Jengo la TPA
Kwa Upande wa Tanzania, Jengo PSPF COMMERCIAL TOWERS lililopo Dar es salaam ndilo refu. Lina Urefu wa Mita 134 kwenda Juu likifuatiwa na TPA TOWER leenye Urefu wa Mita 134 kwenda Juu pamoja na RITA TOWER leenye Urefu wa Mita 115 kwenda Juu na mengine yanafuata.
Jengo la RITA
Hata hivyo, Zanzibar kunajengwa jengo refu ambalo litapiku haya majengo yote ya Tanganyika ambalo litakuwa na Urefu wa Mita 385 ambalo likikamilika litaitwa Zanzibar Domino Commercial Tower.
Zanzibar Domino Commercial Tower.
Majengo mapya yanayojengwa ni kama ifuatavyo;
1. Oblisco Capitale linalojengwa Nchini Misri lenye Urefu wa Mita 1,000 kwenda Juu
2. Jeddah Tower huko Saudi Arabia lenye urefu wa mita 1,008 kwenda Juu
3. Dubai Creek Tower huko Dubai lenye Urefu wa Mita 1300 kwenda juu
4. Sky Mile Tower huko Tokyo lenye Urefu wa Mita 1700 kwenda Juu
Haya ni moja ya majengo ambayo ni Mega project Duniani.
Pia kuna majengo mengine mengi yanajengwa. Angalia Video hii
Tanzania hatupo nyuma sana