Jenerali Ulimwengu afunguka kuhusu Rais Mkapa

Jenerali Ulimwengu afunguka kuhusu Rais Mkapa

Mwaka 2010 kwenye kugombea urais zanzibar, kura za maoni aliongoza Amani Karume akifuatia na Dr . Bilal.
Sasa 2015, utaratibu wa CCM wanaachiana umalize miaka 10, cha kushangaza Amani karume kachukua fomu na Dr. Bilal akachukua fomu.
Kipindi hicho Mkapa ndio mwenyekiti wa chama
Kufika kwenye vikao vya NEC , wajumbe wanajua wanaenda kupiga kura, Mkapa akamwambia Dr. Bilal toa jina lako .
Macho makavu kabisa.
Dr.Bilal akaondoa jina lake kwa unyonge sana.
Mtu mwingine ambaye hataudhulia msiba huu ni Dr. Bilal
Kikwete ndio kumuonea huruma kuja kumpa umakamu urais JMT baadae.
Dah huyu mzee alikuwa mtata sana, kumbe Bilal na upole wake huko Idodomiya aliambiwa atoe jina upesi hivo.
Mimi nilikuwa simjui kivile siku ametukana mapumbavu na malofa nikajua kumbe ni mtata hvo
 
Dah huyu mzee alikuwa mtata sana, kumbe Bilal na upole wake huko Idodomiya aliambiwa atoe jina upesi hivo.
Mimi nilikuwa simjui kivile siku ametukana mapumbavu na malofa nikajua kumbe ni mtata hvo
Niendelee kukupa visa vya Mkapa au niishie hapa
 
Endelea kudadavua zaidi visa vyake bwana
Mwaka 2015 kwenye mkutano wa NEC kumchagua raisi wa awamu ya tano , mwenyekiti wa chama ni rais kikwete.
Kabla ya kikao imeshajulikana Lowassa kakatwa na majina ni JPM, Membe, January, Migiro na Amina.
Sasa kikwete ameingia tu ukumbini wameanza kuimba, tuna imani na lowassa oya oya oya ...... badala ya kusema Kikwete.
Hali ya ukumbini ilikuwa imechafuka kabisa.
Mkapa akamuomba kikwete aseme neno kidogo.
Mkapa akapewa ruhusa
Mkapa akawaomba wajumbe wakae kwanza
Wajumbe wakaa
Mkapa akawauliza kama kuna mtu anayepinga Lowassa kukatwa asimame kwa miguu yake.
Kama kuna mtu hakubaliani na maamuzi ya Amiri jeshi mkuu, rais w JMT na mwenyekiti wa CCM asimame kwa miguu yake.
Hakuna aliyesimama na ndio utulivu ukarudi.
Chezea kusimama hadharani kumpinga Amiri Jeshi mkuu.
 
Mwaka 2010 kwenye kugombea urais zanzibar, kura za maoni aliongoza Amani Karume akifuatia na Dr . Bilal.
Sasa 2015, utaratibu wa CCM wanaachiana umalize miaka 10, cha kushangaza Amani karume kachukua fomu na Dr. Bilal akachukua fomu.
Kipindi hicho Mkapa ndio mwenyekiti wa chama
Kufika kwenye vikao vya NEC , wajumbe wanajua wanaenda kupiga kura, Mkapa akamwambia Dr. Bilal toa jina lako .
Macho makavu kabisa.
Dr.Bilal akaondoa jina lake kwa unyonge sana.
Mtu mwingine ambaye hataudhulia msiba huu ni Dr. Bilal
Kikwete ndio kumuonea huruma kuja kumpa umakamu urais JMT baadae.
Heeeewwh kumbe huyu marehemu n katili hivi duuuuh
 
Kuna mazuri BWM alifanya lakini kuna mengi mabaya ambayo yameliingizia taifa hasara kubwa. Tatizo lake kubwa ni kujilimbikizia mali, Je, alikuwa hana nyumba SA? Kama alikuwa nayo kwa nini? Je, Hakuchukua kiwanda kusini mwa Tanzania na kuwa mali yake? Kama alichukua ni kwa nini? Je, hivyo alivyochukua alikuwa navyo kabla ya kuwa rais? Kama ni ndiyo kwa nini alivipata alipokuwa rais?
 
Heeeewwh kumbe huyu marehemu n katili hivi duuuuh
Soma hii screenshot article
20200725_110706.jpg
 
Watanzania wanapenda watu wanafiki wanaomwaga tu sifa kwa watawala pasipo kutoa ukosoaji wowote..

Mkapa pia atakumbukwa kwa kusimamia utawala uliokubuhu kwa ufisadi. Wakati wa utawala wake ndio zilipozuka kashfa nyingi sana kuwahi kutokea katika historia ya nchi hii.

Pia alijitwalia kinyemela mgodi wa makaa kule Kiwira kwa kutumia cheo chake kama rais na pia fedha zilizotokana na mauzo ya mashirika ya umma hazijulikani zilipoenda bila kusahau alivyomwaga damu za watu wasio na hatia kule Pemba.

Bahati mbaya sana amekufa bila kupelekwa mbele ya sheria kujibu hizi tuhuma lkn, inshallah, huko alikoenda bado atatakiwa kuyajibu hayo kwani Mungu ndio jaji wa ukweli hivyo kukwepa haki hapa hukumsaidii sana.
 
Hayo ni "comment" binafsi na jinsi alivyomuona. Tusimlaumu kwa hilo.

Ofcourse ni comment binafsi iliyojaa chuki na visasi.

Lakini haisaidii, maana tunamheshimu mzee wetu alitujengea taasisi tunazonufaika nazo kama nchi.

Jenerali atulie tu, tunatambua mchango wake kwenye tasnia ya habari lakini hana impact yoyote kwa Taifa kama aliyokuwa nayo mkapa.

Zipo sheria nyingi na Tassisi nyingi nchi hii zina Signature ya Mkapa tunanufaika nazo na tutaendelea kunufaika nazo.

Who is Jenerali compared na Mkapa mtu aliyetuletea mifumo kama vile VAT, NSSF, Mkukuta, Mkurabita, MMEM, MEMKWA, TAMISEMI, Uwanja wa Taifa, TANROADS NHIF na mingine mingi?

Chuki na visasi ni dalili ya udhaifu
 
Jenerali kaonyesha immaturity kubwa kwenye hii Interview.


Mkapa kipindi cha utawala wake Alidhibiti mfumuko wa bei, hata nauli ya daladala ilibaki shilingi 150 kwa muda mrefu sana kwenye utawala wake

Alipandisha kipato cha mtanzania kutoka dola 170 kwa mtu hadi 500 kwa mtu kwa mwaka.

Alijenga Taasisi imara, TCU, NHIF, NSSF, TANROADS, LOANSBOARD.

Alikuwa na Programmes za maendeleo kama vile MKUKUTA, Mkakati wa kuondoa umasikini Tanzania, MMEM Mpango wa Elimu ya Msingi, MEMKWA, MKURABITA

Ni Mkapa ndiye aliyewaita wenye magazeti ya Mwananchi na The Citizens waje wawekeze Tanzania

Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha TV ya Taifa (TBC1)

Ni Mkapa ndiye aliyetujengea uwanja bora kabisa na wa kisasa wa mpira hapa Dar

Pia alikuwa Jasiri kukiri makosa na kurekebisha, Serikali yake ilipounda Bodi ya Parole na kuweka wakiristo watupu, alikuwa wa kwanza kuona tatizo na immediately kuamua kuivunja na kuiunda upya.

Mitihani ya kidato cha nne ilipovuja kama njugu mwaka 1998, Aliifuta mitihani na kuleta mingine.

Waislamu walipolalamika kuwa hawajanufaika ipasavyo na matunda ya uhuru katika elimu, aliwapa majengo ya Tanesco wajenge chuo chao lakini wakati huohuo pia akabalance kwa kuwarudishia makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Nyerere

Sasa Jenerali Ulimwengu asilete chuki zake binafsi kwenye msiba wa mzee wetu.

Na kabla ya kuwa rais, Benjamin Mkapa alifanya kazi nzuri sana kama waziri wa. mambo ya nje kipindi cha Vita vya Kagera na pia alifanya kazi nzuri sana kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika

Mzee Mkapa katutoa mbali, Jenerali akae na chuki zake lakini tunayo rekodi nzuri ya kutukuka ya mzee wetu
Munapotoa mazuri yake msisahau na mabaya yake.

Kwakuongezea ndio rais wa kwanza ktk taifa hili kuuza mashirika ya umma aka kubinafsisha,na ndie ktk utawala wake kulitokea mauwaji yakutisha mwembe chai 1998,kisha Zanzibar 2001,ana uzuri wowote acheni kumsifu mtu anapokufa,utawala wa ben ulikuwa wahali ngumu sana kwa raia wakipato chachini.afadhali ya huu mara 90 unaweza ukamwaga hata bamia sehemu zenye wateja ukapata mlo wako wasiku.na ndio maana jk akaingia na sera ya maisha bora kwa kila mtanzania baada yakuona maisha magumu kwa raia.80% ya viongozi kama sio 90% wizi walijifunza ktk utawala huu.
 
nyie wapemba acheni kulia lia,kwani mkapa alikuwa rais wa Zanzibar ? ,kosa ni lenu ,kwani rais wenu alikua na kazi gani ?
Huko Pemba watu walizikwa wangali hai,wanawezaje kumsifu huyu bhana kuba?
 
Nimemsikiliza nukta kwa nukta, na lazima nikiri kwamba alichosema Jenerali ni ukweli mtupu!!

Ni kweli Mkapa kuna mazuri aliyofanya lakini sidhani kama mazuri hayo yanaweza kufuta uuzaji holela wa mashirika ya umma!

Ni kama alivyosema Ulimwengu kwamba alifanya kazi nzuri ya kuongea na mashirika ya fedha, lakini lau kama Ulimwengu angerudia upya kumbukumbu zake, angekumbuka alichofanya Mkapa sio kuzungumza na mashirika ya fedha bali kutekeleza kwa ufanisi matakwa ya mashirika ya fedha ambayo pia ni kweli yameisaidia sana Tanzania!

Katika hili, bila shaka Ulimwengu anazungumzia the so-called Heavily Indebted Poorest Countries (HIPC) Initiative ambayo ndiyo ilizaa MKUKUTA, TASAF na programming kadhaa zinazoendelea hadi sasa nchini ikiwa ni pamoja na Shule za Kata, MMES, MEMKWA, Ujenzi wa Hospitals n.k.

Through HIPC Initiative, Mkapa alifanya almost everything Mabeberu walichotaka hadi akafikia kushutumiwa nchini lakini at the end, matunda yake yalionekana!

Kuhusu Media, ni kweli Mkapa hakuwa rafiki wa media, na alikuwa anawakejeli sana wana habari wa TZ! Nakumbuka siku amemsifia Riz Khan wa CNN wazi wazi huku akidai "hawa ndio waandishi" badala ya hawa "Vilaza" wa Bongo!!!

Makala ya Jenerali Ulimwengi ya "Akina Jefferson na Magazeti" ilikuwa ni ama makala yake ya mwisho, au ya pili kutoka mwisho kabla hajapigwa ban kwa hoja kwamba hakuwa Mtanzania!!!

Makala ya "Akina Jefferson na Magazeti" ilikuwa inaelezea ni namna BM alivyokuwa anakandamiza media na kutotaka kukosolewa!
 
Hivi Generali anaiva na nani?
Jakaya aliiva naye siku chache sana za mwanzonimwanzoni mwa utawala wake.
Labda JPM anaiva nae.
Viongozi wengi hawampendi Kwa sababu anasema ukweli hapindishi maneno ili kumfurahisha mtu kwani viongozi wetu wanapenda kuambiwa yale wanayopenda kusikia.
 
Hivi kwa nini mtu akitoa maoni yake, kwa upeo wake, watu badala ya kuchambua hoja wanakimbilia kusema immaturity na chuki?

Jenerali is probably the most mature journalist in Tanzania right now.

Daktari mzungu akisema mgonjwa huyu ana Caancer mbaya na atakufa mara nyingi humwamini lakini Daktari wa kiswahili akisema hivyo wote humwona sio mzalendo
 
Back
Top Bottom