Mzee Kigogo
JF-Expert Member
- Jun 3, 2018
- 10,500
- 17,557
Watu kama hawa huwa wachache sana! Hawamung’unyi manenoUzuri wa Jenerali huwa hakwepeshi wala kuremba
Watu kama hawa huwa wachache sana! Hawamung’unyi manenoUzuri wa Jenerali huwa hakwepeshi wala kuremba
Unatambua kuwa 1995 Ulimwengu alikuwa katika timu ya kampeni ya Mkapa? Kwamba alizunguka naye nchi nzima?for 15 yrs now he has been critic to Big Ben kila aandikapo makala ama platform....Lakini kweli apart from his ups n down against Mkapa anakuwaje na 80% negative on Mkapa
Mimi Mzee Mkapa namkubali kwa yote lkn kubwa haswa ni kulea vyama vya upinzani ,maana kaanza madaraka na upinzaniUnatambua kuwa 1995 Ulimwengu alikuwa katika timu ya kampeni ya Mkapa? Kwamba alizunguka naye nchi nzima?
Rais Mkapa hawakupika hasa baada ya ile hoja kwamba Jenerali si Raia wa Tanzania.
Mkapa alijua ni Raia, kwa bahati mbaya 'intelligence ' walimshauri afanye fyongo na akakubali fyongo.
Kwa upande mwingine, Jenerali anajaribu kubadili mitazamo ya watu kuhusu marehemu.
Tumezoea kuwasifu marehemu hata watu kama akina Nkurunziza wenye '' mapipa ya damu' mikononi
Kwasasa tubadilike, watu waelezwe wasifu wao kama walivyotenda wakiwa hai. Jenerali anamuongelea Mkapa kama alivyomfahamu, hizi habari za sugarcoat si zama zake. Tumechoka kusifu hata wasiostahili kisa wametangulia.
Kwangu mimi bado narudia, kiongozi wa kitaifa ni Nyerere. Huyu alisimama kama baba wa Taifa hata baada ya kustaafu. Hawa waliofuata baada ya kuondoka Ikulu wamebaki kuwa makada wakereketwa bila faida kwa Taifa
Eti Rais Mwinyi anataka katiba ibadilishwe kisa mtoto wake ashinde Urais Zanzibar, halafu ipo siku kizazi kitatakiwa kiongelea mema yake na kufumbia macho uozo kama huo.!!! Hapana tutasema tu wakati ukifika
JK hasemi kwasababu kuna watu wana masilahi na chama. Ipo siku tutazungumzia ukimya wake
Kwa ufupi, mtu aelezwe kama alivyofanya wakati akiwa hai! halafu matendo na kauli zake zitapimwa na busara za wanaosoma au kusikiliza habari zake. Big up Jenerali
Unajua historia yao....Hawa waligombana personally ....na wanajua walichogombea!Uzuri wa Jenerali huwa hakwepeshi wala kuremba
Kweli kabisa!....Ulimwengu mengine snazidisha! Mkapa aliimarisha Sana Utawala Bora...kubwa kabisa alianzisha Taasisi za kuendesha nchi!Nimesikiliza mpaka mwisho wa mahojiano na Jenerali amejibu kile alichoulizwa hasa kuhusu maoni yake.Hayo ni maoni yake na nakumbuka kuwa kwa kipindi chote cha utawala wake hakuwahi kufanya mahojiano ya mwandishi wa habari mzawa.
Mimi binafsi kuna mazuri ambayo alifanya na mojawapo ni kujenga mifumo ya kiserikali,hii TRA tunayoiona leo,kisomo kwa watoto waliokosa nafasi (MEMKWA) na alimudu kudhibiti inflation kwa miaka yote kumi.
Pia aliweza kutoa pesa kwenye mifuko ya watu binafsi na kuirudisha serikalini kimya kimya (Enzi za Mwinyi pesa ilikuwa mifukoni mwa watu tena wengeine kwa ujanja ujanza).Ukiondoa ujeuri wa Kimakua naona alijitahidi sana kulijenga Taifa.Mengineyo alishatubu kwenye kitabu chake.
Kwani uwongo?Aliwaita wanahabari wa Tanzania ni makanjanja.
Ulimwengu is being harsh unnecessary.
Ukweli mtupu bila kupindisha.
Hivi Generali anaiva na nani?
Jakaya aliiva naye siku chache sana za mwanzonimwanzoni mwa utawala wake.
Labda JPM anaiva nae.
MakanjanjaMkapa hakuwahi kufanya mahojiano na mwandishi mzawa? Alikuwa anawadharau waandishi wa nchini kiasi hicho?
NotedUmewahi kupata msukosuko wowote na wenye Mamlaka au unaongea tu! chukulia mfano mtu kama LISU aliyotendewa kisha akiulizwa habari ya watawala wa leo ajibu vzr..... kuepuka haya watu tuishi kwa kuheshimiana bila kujali vyeo
Nimemsikia jenerali kwa makini sana,na hakuna asiyejua kuwa hawa jamaa walikuwa marafiki na walikuwa karibu sana na hatimae waligombana sana,na sinde waryoba alifanya juhudi kubwa sana kuwasuluhisha,lakini haikuwezekana na mpaka anakufa henerali na mkapa hawaongei jabusa na zaidi ya mara 2 kwa macho yangu nimewaona wakukwepana,walipokuwa wanakaribua ana kwa ana.jambo kubwa ni kwamba kwa dunia hii,kusameheana ni wajibu muhimu wa binadamu,nsiposameheana Mungu atawasamehe nyie vipi,pili kwa mila za kiafrika mwenzio akifariki na hapo ndipo mwisho wa ugomvi wenu.huyu jenerali ni mgonjwa maana hataki kusamehe na ugonjwa huo ndio utakaomponza,akumbuke kuna watu pia amewakosea sana,je na wao wamuwekee nongwa na kumchukia kama anavyomchukua mkapa?,jibu analo yeye twaha ulimwenguDuh!
Naona Jenerali Ulimwengu na marehemu Rais Mkapa walikuwa hawapikiki chungu kimoja!
Jenerali inaonekana bado ana hasira za kunyang'anywa uraia na kunyimwa uwaziri wa habari na utangazaji!
Hakuna binadamu asie na kasoro .. mtu akifa tunatoa sifa njema, tunaondoa vinyongo banaa
Shida iko wapi? Kwani Ulimwengu hana haki ya kutoa maoni yake hata kama hayafurahishi baadhi ya watu?Huyu mbwa sana linaongea utopolo tupu
Enzi hizo mimi na wewe tunajificha kichaka cha pamoja kwenye kombolela....Ilikuwa rahaaaaaaMimi pia,yaani sijui naona aje. Kitu pekee positive nakiona ni alivyowapatanisha kina Mwai Kibaki na Raila. Hapa nchini sio au kwa vile alitawala tukiwa ma teenagers ?