Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,520
- 34,510
Alisema! na akaeleza jinsi alivyosaidia mpango wa ''HIPC' na alivyoweza kuongeza akiba ya nchi kutoka mwezi hadi mitano.Ila ulimwengu angetaja mazuri ya mkapa badala ya kudwel on the negatives only!
Jenerali alitendea haki maoni yake kwa kueleza pande zote.
Tuache unafiki wa kusema mAzuri tu, hata mabaya yasemwe.
Tunataka viongozi watambue hilo kwamba, siku wakiondoka tutawaeleza kwa abcd zao
Mbona Nyerere anapimwa na kuelezwa kwa mazuri na mabaya yake kila siku na hatusikii kelele.
Mwisho wa siku Nyerere anabaki kuwa Nyerere kama baba wa Taifa na 'statesman''
Ni statesman kwasababu aliutumia Urais wake vizuri, akiwa Ikulu na alipostaafu.
Hivi nani hakumbuki 1995 Nyerere aliposimama hadharani Jangwani na kukemea unyanyasaji wa Wapinzani!
Baada yake waliofuata wakiondoka Ikulu wanakuwa makada wa vyama kwa masilahi yao huku tukiwaita viongozi wastaafu wa kitaifa. Si kweli, hawa ni viongozi wastaafu Ikulu ambao ni makada kindaki ndaki wa CCM kwa masilahi yao na familia zao. Ukiwasikia wanasema ni kama yale ya Mwinyi ya kubadili katiba!
Rasimu ya Warioba ilipigwa chini, na hawa wastaafu walikaa kimyaaa!
Mkapa aliandika alitamani Tume huru akijificha nyuma ya kitabu. Hilo tusiseme!
Na kwamba eti kuna siku tutasahau Mwinyi kudai katiba ibadilishwe!