Jenerali kaonyesha immaturity kubwa kwenye hii Interview.
Mkapa alijenga taasisi Imara nyingi tu za nchi yetu
Alidhibiti mfumuko wa bei.
Alipandisha kipato cha mtanzania kutoka dola 170 kwa mtu hadi 500 kwa mtu kwa mwaka
Alijenga Taasisi imara, TCU, NHIF, NSSF, TANROADS, LOANSBOARD.
Alikuwa na Programmes za maendeleo kama vile MKUKUTA, Mkakati wa kuondoa umasikini Tanzania, MMEM Mpango wa Elimu ya Msingi, MEMKWA, MKURABITA
Ni Mkapa ndiye aliyewaita wenye magazeti ya Mwananchi na The Citizens waje wawekeze Tanzania
Ni Mkapa ndiye aliyeanzisha TV ya Taifa (TBC1)
Ni Mkapa ndiye aliyetujengea uwanja bora kabisa na wa kisasa wa mpira hapa Dar
Pia alikuwa Jasiri kukiri makosa na kurekebisha, Serikali yake ilipounda Bodi ya Parole na kuweka wakiristo watupu, alikuwa wa kwanza kuona tatizo na immediately kuamua kuivunja na kuiunda upya.
Mitihani ya kidato cha nne ilipovuja kama njugu mwaka 1998, Aliifuta mitihani na kuleta mingine.
Waislamu walipolalamika kuwa hawajanufaika ipasavyo na matunda ya uhuru katika elimu, aliwapa majengo ya Tanesco wajenge chuo chao lakini wakati huohuo pia akabalance kwa kuwarudishia makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Nyerere
Sasa Jenerali Ulimwengu asilete chuki zake binafsi kwenye msiba wa mzee wetu.
Na kabla ya kuwa rais, Benjamin Mkapa alifanya kazi nzuri sana kama waziri wa. mambo ya nje kipindi cha Vita vya Kagera na pia alifanya kazi nzuri sana kwenye ukombozi wa kusini mwa Afrika
Mzee Mkapa katutoa mbali, Jenerali akae na chuki zake lakini tunayo rekodi nzuri ya kutukuka ya mzee wetu