Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

  1. Ni kama hadithi ya Hamani na Mordekai ktk kitabu cha Esther. Hamani alichonga mti ili Mordekai atundikwe mwisho wa siku akaishia kutundikwa yeye kwa mti aliouchonga mwenyewe. Kuna wakat maadui hutuwekea mitego mbele yetu ili itunase, lakn ashukuriwe Mungu atuteteaye maana hyo mitego huishia kuwanasa hao hao waliotutegea.
Hakika ndivyo ilivyokuwa Kaka yangu. Haikuwa rahisi hata kidogo..... lakini nilisema Mungu ninayemtumikia atanipigania, atanitetea .....Nakumbuka maneno ya Mchungaji nilipokwenda kumshirikisha changamoto hii..... Aliniambia ..... "Mwanangu Vita hii haitaisha Mpaka umetangazwa Mshindi".... Haikuwa rahisi..... Namrudishia Mungu Sifa na Utukufu..... Amenitetea ..... Amenipigania.... Amenipa Ushindi. Utukufu wake sigusi!!!! .... Utukufu kwa Yehova Pekee.....
 
Hiyo hali inatokea sana. Na haitakuja kutokea kuisha. Ilishawahi kunitokea aliekuja kunisaidia ni ndugu yangu wa damu. Kila rafiki ninayejaribu kumkopa ananiambia nikakope benki. Baada ya kuwa vizuri nilipunguza marafiki kwa 98%. Sikuona umuhimu wa kuwa na marafiki wa whattsap wakati ukiwa na shida anakukacha.
Hata mimi imenitokea aisee, mabest wanakwambia ukakope benki au Vikoba
 
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.

Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)

Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.

Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.

Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.

Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.

Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.

Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.

Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.

Natumia muda kuwaombea maadui

f077592e4c5aa05c1d2e35ac99a56ca1.jpg
Pole sana mkuu! Mungu ni mwema atakutendea. Wala usihangaike tena kufunga safari ndefu hivyo kumtafuta mtu akuwekee mkono mf TB Joshua. Mungu anaweza kumtumia hata mtu yeyote wa hapa hapa ama akakujibu wewe mwenyewe direct. Yesu alitupatanisha na Mungu...so hatuitaji tena kuomba kupitia care of
 
Kwann ukiwa katika hali ngumu watu wansajiweka mbal nawe? na wanajisogeza kwa yule alie vizuri kiuchumi,kimaisha etc..
Binaadam tutaacha lini huu unafki?
Mi nshaapa hakyamama siku mtu anikute nashine mwenye pesa asijisogeze kwangu...Sitaki marafiki
Yaani we learn in a difficult way
 
wewe 98% mimi 99.99% we acha tu nilikuwa natoaga ndugu/rafiki akiwa na shida but now hunichomoi hivihivi unala umekunywa maji, huna sabuni kodi marafiki/ ndugu huwaoni yakiisha wanakupavkadi za michango na kukuweka kwenye kamati nguvu
Umeonaee, mi mwenyewe nimekuwa mgumu sana! Ndugu au rafiki hanichuni hela hivi hivi
 
Umeonaee, mi mwenyewe nimekuwa mgumu sana! Ndugu au rafiki hanichuni hela hivi hivi

iwe issue serious yupo hospital na nihakikishe hama hata kumi ntatoa hata milioni, harusi natoa ntakayopanga sio kunilazimishia ooohh uko kwenye kamati ni laki 3 maisha uko shule uwe una wastani wakuanzia 65+ below hapo situpi ada yangi . hela zangu zilikuwa kwangu zinapita tuu kwenda kwa watu hiyo huruma Mungu nimemuomba aiondoe kabisa! ukipata shida wanakuangalia kama nyanya mbichi shiiiiittt sahivi sicheki na mti hovyo akanichuna bureeew
 
#1Peter 4:19,"So then, those who suffer according to God’s will should commit themselves to their faithful Creator and continue to do Good."
2ad1e0df0d54d3a949bd04106ce9f24b.jpg
 
Mimi mwenyewe napitia changamoto nzito sana na ngumu sana ila najuua IPO siku Mungu ataniinua, kama kukata tamaa, Mara nyingi sana ila kila ninapo muangalia mwanangu na kuona a smile on my son's face napata matumaini na faraja that Mungu atatubariki na kuniwezesha Mimi na mwanangu. I believe Mungu will make a way and GOD will make the impossible become possible
 
Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
Nikweli ni kwa neema tu, tukianza kuhadithia hapa watu watamwaga machozi, na Mwenyezi Mungu humuinua mtu toka mavumbini hata mahali pa juu sanaaaaa, hii ndio hali niliyonayo.

Kuna kipindi mke niyeachana naye kwa talaka mimi nikiwa nje ya nchi alimtukana mama yangu mzazi. Na uanaume wangu wote nililia wiki nzima. Maana tulipo pita na mama yangu mwenyezi Mungu ni shahidi. ..

HUU UZI KWANGU NI KUNIKUMBUSHA UGUMU NILIOPITIA ,maana nashindwa kueleza na nikikubuka nalia kila wakati.

Wengine hauwajawahi kumuona mwanaume akilia kwa nguvu na machozi mengi ndio hali niliyonayo mimi bado kila kukicha. .

AMEN
 
Hustle ninayokumbuka ni ile ya kula mlo mmoja kwa siku tena kwa shida alafu asubuhi ukiamka unasikia jamaa anamtoa demu alie lala nae elfu kumi
Inauma sana bty nashukuru Mungu maisha yanakwenda
 
Kwa mtu ambae hajawahi kupitia hali mojawapo kati ya hizo hawezi kuamini....Ila mimi nilishapitia hata pesa ya pipi kifua haionekani.....Na elimu yangu ya chuo kikuu niliosha magari,niliuza bangi,nilikaba,kinyozi etc....(tena nchi ya watu) Na kanisani sikuwahi kukosa nilimuomba sana Mungu sikuacha hata siku moja.Huwezi kuamini leo hii nakula pipa mpaka mikanda imenitoa sugu..Na niko na nidhamu iliyotukuka ya fedha.Kwa kifupi maisha ni mazuri boss of my own company/business...Even hustlers wish they had a hustle like mine.Respect to all the hustlers out there
 
Mi nakumbuka enzi hizo kila nililofannya lilionekana baya!
Ndugu walinidharau na kunichukia,
Kazi nilikosa,mademu mtaani walinidharau,
Nlipanga chumba nje ya mji kisicho na umeme wala maji
Nililalia mabox na nlikuwa naenda kula ukoko kwa mama ntilie!
Kuna siku nilisubiri usiku nikazunguka nyuma ya choo kuna yale maji yanayotoka bafuni kuna mchicha ulikuwa umestawi hapo niliuchuma nkaingia gheto nikapika nikala!
Ni mengi nkikumbuka nalia!
Pole sana bro.
Dah roho imeniuma aiseee . Mungu yu mwema
 
Sio tu hadi uumwe, wewe ukiwa na kajambo kako tu kanakokufanya uone kama Mungu kakusahau, basi nenda tu ukatembelee wagonjwa.... Health is the most important thing in life
Kuna watu wanatania humu....mtu anasema kamaliza chuo hajapata kazi eti hio nayo ni shida! Ushukuru Mungu umeweza hata kusoma na kupata degree.
 
Back
Top Bottom