Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Hapa nina maanisha kufilisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku. kutengwa na ndugu. kukosa kazi muda mrefu, Kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba./mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.

Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uwongo
Kudharauliwa na mambo kama hayo na je?

Uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?

Unauliza kama kuna mtanzania keshawahi kupitia maisha magumu??
 
nimepitia wakat mgumu sana mwaka jana. masomo yangu hayakwenda salama. jkt sikwenda nkaja kuona jina baadae biashara zangu hazikwenda baada ya KUOKOKA NA KUMUEKA MUNGU KAMA MKOMBOZI WA MAISHA YANGU NOW NAKULA BATA NA FURAHA TELE. BINADAMU wabaya sana now naishi kiimani na kwa bahati nziri wabaya wangu nawatambua hata alienifanyia yote mwaka jna ni mke wa ...... wangu. IMANI NA MUNGU ndo msingi wa maisha. kama ni jambo baya litatokea mbelen naliona kama zuri pia naliona maisha yangu yamekua ya furaha sana na yote nlopoteza mwaka jana yanaanza kuja pole pole hap natanga niongeze jitihada zaidi nijiweke karibu na Mungu pia niache Dhambi maana ndo zinazoninyima amani
 
uwezi kula MUWA BILA KUKUTANA NA FUNDO hebu angalia wa Libya leo wa Siyria leo hawakua vile walikua namaisha ya raha amani upendo nk hiyo ndio dunia na Maisha
Naukumbuka huo wimbo....wa kitambo sana.
Hauwezi kula muwaaaa....bila kukuta fundo
 
ndio hata maandiki yanasema kuwa kuna mapito, kuna misalaba. ili ukitoka huko uje utoe ushuhuda kwa wengine wamjue Mungu.
 
Watoto wa Bakhresa, Mengi au Mo dewje ktk maisha yao yote kuanzia wakiwa tumboni mwa mama yao hawatokaa wajue maisha magumu ni kitu gani au waje wapitie maisha magumu! Na sis tutafute hela kwa bidii watoto wetu wasije kupitia njia tulizo pitia tujitume tuachane na siasa
 
Kuna mahali inafika unaona kama dunia haitaki ushirikiano nawe,unaona wote ni kama wamekutenga hakuna anaejali matatizo yako hata wale wa karibu yako hawakuoni.

Unabaki wewe na Mungu wako tu,ni kipindi kigumu kwakila mtu. Tumepita na tunaendelea kupita kwenye changamoto mbalimbali....

Muhimu ni kua karibu na mungu zaidi na atakuvusha salama.
Ukichomoka hapo unakuwa dhahabu
 
ndio hata maandiki yanasema kuwa kuna mapito, kuna misalaba. ili ukitoka huko uje utoe ushuhuda kwa wengine wamjue Mungu.
Ukitoka huko unakua dhahabu..
na ndio maana ya KUTOKA
 
Watoto wa Bakhresa, Mengi au Mo dewje ktk maisha yao yote kuanzia wakiwa tumboni mwa mama yao hawatokaa wajue maisha magumu ni kitu gani au waje wapitie maisha magumu! Na sis tutafute hela kwa bidii watoto wetu wasije kupitia njia tulizo pitia tujitume tuachane na siasa
Wana magumu ya aina yao
Maradhi...
Vifo..vifo kwa matajiri huwa vinawauma sana.
Ndoa...zina misukosuko
 
Hapa nina maanisha kufilisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku. kutengwa na ndugu. kukosa kazi muda mrefu, Kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba./mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.

Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uwongo
Kudharauliwa na mambo kama hayo na je?

Uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?

Haya mambo yapo.... Nikikumbuka niliyopitia ..... Nazidi Kumshukuru Mungu kwani nimekuwa jasiri zaidi, nimejifunza mengi.... Nimejifunza pia katika maisha kuna kupata na kukosa, nimejifunza marafiki wa kweli ni wepi, Nimejifunza kuwa mtu wa shukurani na sio kulaumu laumu, nimejifunza kuangalia maisha in a very positive way haijalishi napitia lipi..... There is HOPE always..... Nimejifunza kuwa katika hali kama hiyo ni Mungu pekee ndio rafiki wa kweli na msaada wa karibu. All is well. Maisha yanasonga vema kabisa sasa.
 
Ndugu, ni vigumu sana kuelewa ninayopitia. Na kile ninachopata baada ya maombi.

Bila kufanya hivi , tayari ningekuwa nimeishajinyonga zamani au kufa.

Last week nilipata attack nikiwa bafuni naoga, nilianguka ghafla...damu zilitoka nyingi sana... ( nakumbuka , mchana yake kuna mtu alinitamkia atanifanya kitu kibaya - jioni nikapatwa na hali hii)
ecc23a8c060db886933b6764fb298519.jpg


Ni watu wachache sana wakianguka bafuni kama nilivyoanguka wanapona. Mara nyingi huwa wanapata stroke au kufa.
Nimenusurika kufa mara nyingi sana Ndugu. Huwezi kunielewa kwa kusoma hapa.

Kutokana na maelezo yako, unavita kubwa katika ulimwengu wa roho, na vita vyako hutashinda kwa nguvu za kimwili. unahitaji maombi maalum ya ukombozi, ndio umeokoka lakini kuna vifungo utakuwa umefungwa kwavyo na inahitaji maombi maalum na ufunuo kwaajili ya kuvi deseable, inaonekana umekuwa ukiomba mara zote bila kujua specific nini cha kuombea, umekuwa ukiomba kwa ajili ya kupata kazi, lakini shida sio katika kupata kazi.

Ni kosa kubwa sana katika maombi kuomba bila target, au kulenga wrong target. kama inashindikana kabisa ni vizuri kuwa na mfungo wa utakaso na maombi katika Roho. ROMANS 8:26-28. MATTHEW 17:21. Ina bidi ufanye mfungo wa maombi kuomba Roho mtakatifu akufunulie ( akuonyeshe) wapi palipo na tatizo ili uweze ku deal direct na chanzo.

Kaa chini tafakari, angalia historia ya maisha yako, ya wazazi wako. kuna mahali palifanyika agano fulani la kiroho? Je kuna jambo wewe ulowahi lifanya ambalo linaweza kuwa sababu ya milango kufungwa? jaribu kuangalia hata yale madogo ambayo unaona ni irrelevant. Fanya sala ya toba ya ukombozi ( special deliverance) na kama kuna mahali kwa namna moja au nyingine unahisi ulifanya jambo ambalo lilimuumiza mtu sana, katengeneze nae, machozi ya mtu ni mabaya sana.
 
Kwann ukiwa katika hali ngumu watu wansajiweka mbal nawe? na wanajisogeza kwa yule alie vizuri kiuchumi,kimaisha etc..
Binaadam tutaacha lini huu unafki?
Mi nshaapa hakyamama siku mtu anikute nashine mwenye pesa asijisogeze kwangu...Sitaki marafiki
Ni kweli sisi binadamu ni watu wa ajabu sana ,yani wakati ukiwa na shida wanakimbia kabisa,unabaki mpweke bila hata msaada lakini mambo yakianza kunyooka wanaanza kujisogeza.
Binadamu ni viumbe wa ajabu sana.
 
Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.

Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)

Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.

Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.

Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.

Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.

Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.

Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.

Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.

Natumia muda kuwaombea maadui

f077592e4c5aa05c1d2e35ac99a56ca1.jpg
Nina IMANI utafanikiwa ili iwe funso kwa wengine....
DHAHABU lazima ipite motoni
Shukran
 
Back
Top Bottom