juvenile davis
JF-Expert Member
- Apr 13, 2015
- 4,752
- 4,477
Kila binadamu anapitia magumu
Sawa kiongozi.Baada ya kujifunza mambo ya ufalme wa Mungu; Nimegundua vitu vingi sana, na vyeti vyangu naviona vya kawaida sana.
Na ninaelewa kwanini Ma JEWS hupendelea kuwakazania watoto wao kuthamini Elimu ya Mungu kuliko hii tunayofundishwa Mashuleni.
Na ninaelewa kwanini wanaongoza kwa kuwa wagunduzi + wabunifu wakubwa ulimwenguni
Teh teh teh teheeeeeNgoja awashe mshumaa uangukie kwenye cheti. Teh!!
Bulldog,aren't you?Hiyo hali inatokea sana. Na haitakuja kutokea kuisha. Ilishawahi kunitokea aliekuja kunisaidia ni ndugu yangu wa damu. Kila rafiki ninayejaribu kumkopa ananiambia nikakope benki. Baada ya kuwa vizuri nilipunguza marafiki kwa 98%. Sikuona umuhimu wa kuwa na marafiki wa whattsap wakati ukiwa na shida anakukacha.
Aren't me.Bulldog,aren't you?
Okay.. Sorry for asking. Uwe na wakati mwema.Aren't me.
Asante Ndugu kwa kunisahihisha. Lakini kutukana haikufanyi uonekane kuwa una Hekima. Barikiwa sana Ndugu"Kila MTU anaweza kusema "Mungu". Kuna Mungu wengi sana. Muhimu ni kumtambua Mungu wa Kweli ( tena umtambue personally na Jina lake halisi)
Siku ukimtambua, Hakika nakwambia kweli. Jina lake lina Nguvu sana. Na ukimuita Atakuitikia! ( Jeremiah 33:3)"
Rubbish, kuna Mungu mmoja lakini kuna mungu wengi, dont post shit
Nimefurahi sana kusoma comment yako. Namshukuru sana Mungu kwa maisha ya Baba yako na yako pia. Mungu awabariki sana katika jina la YESU.Inaweza kuwa yuko sahihi! Unajua duniani kuna mambo mengi sana mengine ni ya ajabu sana! Baba yangu mkubwa ambaye ni "Role model" wangu kwa masuala ya imani, alifanana na huyu kwa kiasi fulani. Alipenda kusema "kama imempendeza Mungu yeye kupitia mateso,mimi inanihusu nini? " Hakupenda nisikitike kwa yeye kuteseka na magonjwa yasiyopona! Tangu napata akili yeye anaumwa tu, mpaka nafika Sekondari bado anaumwa tu! Lakini ajabu aliamini kuwa kuteseka kule ilikua ni mpango wa Mungu na alishukuru kwa ajili hiyo! Baadae sana nilielewa kwamba utukufu wa Mungu wakati mwingine huja kwa namna za ajabu! Kwamba kuna watu Mungu huwapa mateso ili jambo Fulani liwe!
Ilinichukua miaka mingi kuelewa hili!
Kuna mahali inafika unaona kama dunia haitaki ushirikiano nawe,unaona wote ni kama wamekutenga hakuna anaejali matatizo yako hata wale wa karibu yako hawakuoni.
Unabaki wewe na Mungu wako tu,ni kipindi kigumu kwakila mtu. Tumepita na tunaendelea kupita kwenye changamoto mbalimbali....
Muhimu ni kua karibu na Mungu zaidi na atakuvusha salama.
Yan hizo zote nimeshazipitia siwez kuja kusahau kwenye maisha yangu kabisa nilala chin kwa kulalia nguo zangu na kula mkate kama chakula kwa muda wa wiki nzima. Kuna wakati nilitaman kujiua niliumwa vibaya sana halafu hakuna mtu sio rafik wala ndugu anayekupa ushirikiano wa dhati. Oh MGD sitak kukumbuka kabisa.
Haya matatizo niliyopitia na ninayoendelea kuyapitia katika hii miezi ya karibuni, nimegundua kwamba, kufikwa na matatizo ni tatizo ila kukosa mtu wa kushare nae hayo matatizo (hata wa kumhadithia tu) ni tatizo zaidi!
Ila Mungu ndo kila kitu, i ll never lose hope!
Naam... Tupo pamoja, ninachotaka kuongezea hapo kwenye context yako... Ni juu ya vionjo namaanisha yale maarifa yatakayotuwezesha kwenye maombi yetu.... Moja wapo ni Kufanga, huu mwili ukishashiba ni tatizooo ni lazima tuunyime chakula kwanza ili tuwe karibu zaidi na MFALME WA WAFALME.... jamani Mungu yupo na anajibu ikiwa tutaomba sawasawa,,Ni kweli mtumishi shemkunde ukijaribu kusoma katika matthew 26:36, na 26: 42 .inaonyesha ni jinsi gani Yesu alivyo kuwa kwenye wakati mgumu, alishindwa kabisa, alikuwa anajua nini kilicho mbele yake, Alijua nini uchungu wa majaribu ndo maana kwenye Matthew 26:41 akasema Kesheni mwombe msije ingia majaribuni. Akasema kuwa mara nyingi roho ya mwanadamu inaweza kuvumilia katika majaribu, lakini mwili katika hali ya kibinadamu ni vigumu sana kuvumila majaribu " roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu".
mkuujamani ila kuna matatizo mengine unaweza kusema ni laana....kuna wakati nakumbuka amri ya pili ...kutoka 20:1...nawapatiliza wana maovu ya baba zao....
nikikumbka tangu nikiwa mtoto sikulelewa na mama ameniacha nikiwa na 5yrs....baba hakuwahi kuoa tena akawa ananipeleka kwa marafiki zake niliishi zaidi ya miji mitano badae akanichukua tukawa tunaishi mm na yeye ila sasa mlevi balaa
siku moja alikwata kixhwani na mpenzi wake nikawa namhudumia nikashindwa kwenda shule..yani acheni tu jamani...t
Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.
Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
Yupo Mungu... Yupo Mfalme.... Hakika atakujibu tu.......Hayo yote uliyoyaandika , ndio nayapitia sasa. Tena yamekuwa kwa muda mrefu sana.
Ilifika mahala nikaenda SCOAN Nigeria kwa PTB Joshua kwa njia ya bara bara ( nilitumia siku 76 kufika)
Nimekuwa kiroho sana. But matatizo yapo pale pale. Na yanazidi kuongezeka mpaka kukimbiwa na watu wa karibu kabisa, uliowasomesha na kuwainua juu.
Wakwe kukuona kama mwehu, mke kukuona hufai , na kuudharau Wokovu wako.
Mara waseme sitaki Kazi, na kwamba nachagua Kazi. Wakwe wanamsisitiza mke wangu aachane na Mimi kuwa nampotezea muda, sina Kazi.
Nakuwa karibu sana na Mungu kila mara. Na ninafunga na kuomba kila mara.
Hii ni sehemu ambayo naitumia kusali mchana na Usiku..., asubuhi mchana jioni.
Usiku kabla ya saa 6 , Then saa 7-8 , na saa 9-10.
Nimetandaza vyeti vyangu vyote kuanzia chini hadi Postgraduate, na mahitaji ya watu wengine.
Natumia muda kuwaombea maadui
![]()
Word!! Hapa umenikumbusha jambo lililoifedhehesha nafsi yangu sana sana... Kuna kipindi nilipitia hali ngumu sana, sikuwa na mtu wa kushare naye hata ideas kutokana na nature ya watu walionizunguka. Akatokea mtu aliyehisi kuwa nina tatizo linalonisumbua. Alionekana kutaka kunisaidia kisaikolojia maana nilikuwa kama mtu niliyechoka sana, sura ilipoteza nuru na nikaonekana kuwa mnyonge kila mara. Katika kunihoji nikaona nimweleze huenda nitapata relief moyoni... Kumbe alikuwa chui katika vazi la kondoo....alizidi kunichinjia kwenye maji... Akanizidishia matatizo... Poor Patience...
Uliyoandika hapa Kwangu Mimi binafsi ni 25% ya yaliyonikuta ila nikikuhadithia hizo 75% zilizobaki unaweza ukalia mwaka mzima ila sina cha kumpa Mwenyezi Mungu kwani ALINIPIGANIA mno na KUJIKABIDHI Kwake hadi kuweza KUYASHINDA yote na sasa kuwa BINADAMU katika Watu. Ni story ndefu sana ila niliyoyapitia nadhani sina hata haja ya kwenda kufanya Kozi ya UKOMANDOO kwani NIMESHAFUZU kupitia haya MAPITO na labda nikienda huko nikafundishwe tu KUTEGA na KUTEGUA MABOMU ila kwingine kote TRAINERS wangu watashangaa kama siyo kustaajabu.
Usife moyo mpendwa.... Nami pia bosi wangu kuna mambo alikuwa akinifanyia kuhakikisha naondolewa Kazini.... hakika sikukata Tamaa.... Nilimwamini Mungu na kuzidi kufanya Kazi kwa bidii.... Nilimshirikisha Mchungaji changamoto hiyo... Hakika Mungu si mwanadamu.... shimo alilotamani nidumbukie..... Tumbua Tumbua imempitia.... Amedumbukia katika lile lile shimo alilochimba mwenyewe..... Hakika mwanadamu hawezi kuziba riziki ya mtu....na kwa wenye vyeo.... wakumbuke ni dhamana tuu.... Mwisho wa ubaya Aibu....