Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Asee asikwambie Mtu kuna watu tumepitia mengi mpaka ukihadhia mtazani ni maigizo yani mtu na degree yake anapata tabu anachakaa na kua kama ndorobo.

Nimepitia changamoto mpaka nikahisi dunia imeamua kunivalia bukta bila boksa.
Aaaa ata sitaki tena kukumbuka nilikotokea kwani kuna kipindi nilitaman nisahau lakini inashindikane usiombe ukutwe sikia tu kwa wenzako.
 
Kuna watu wanatania humu....mtu anasema kamaliza chuo hajapata kazi eti hio nayo ni shida! Ushukuru Mungu umeweza hata kusoma na kupata degree.
Ujue binadamu tunaamini material things ndo zinafanya maisha yetu yawe kamilifu. Yes pesa na Vitu vingine ni vya muhimu, but kuna Vitu vya muhimu zaidi tunavi-overlook sana ie Health, Peace of Mind, Love (family, relatives, friends). Hivi vitu ukivikosa hata pesa unaweza iona haina thamani

Kwa vile tunaamka asubuhi tukiwa wazima wa afya, basi tunachukulia like it's something ordinary, nothing special with it... kumbe every single day is such a huge blessing to us. Kwa vile una routine yako ie unaamka, kazini then home basi kuna muda unaona kabisa like your life is boring, nothing is exciting. Ila siku ukiamka you can't move your legs, au macho hayaoni, au mikono haifunction tena au kufukuzwa kazi/biashara kufa, ndo unaona like ile boring routine yako ni kitu cha thamani sana kwako.

We should learn to be grateful. Kila siku sisi ni watu wa kuomba tu, Mungu naomba this, naomba that. Hakuna siku mtu unasema Mungu Ahsante kwa A, B, C. Mungu katupa vitu vingi sana, ila ikitokea tu kuna kitu tunakihitaji sana, and Mungu hajatupa kwa muda huo tunaotaka Sisi, basi ndo kulalamikia tu, tunasahau yale yote tuliyopewa bila hata kumuomba. Sio kama ndo turidhike na maisha, tutafute tu zaidi but tusijistress sana juu ya tusivyonayo hadi tukakufuru. Tuwe watu wa shukrani
 
Smart
 
Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?
Hiyp mbona kawaida tu. Kibaya zaidi ukute na jirani yako anapenda kupiga ule wimbo wa......UMEFULIA..... We, unatamani kuua mtu.
 
Ujue binadamu tunaamini material things ndo zinafanya maisha yetu yawe kamilifu. Yes pesa na Vitu vingine ni vya muhimu, but kuna Vitu vya muhimu zaidi tunavi-overlook sana ie Health, Peace of Mind, Love (family, relatives, friends). Hivi vitu ukivikosa hata pesa unaweza iona haina thamani

Kwa vile tunaamka asubuhi tukiwa wazima wa afya, basi tunachukulia like it's something ordinary, nothing special with it... kumbe every single day is such a huge blessing to us. Kwa vile una routine yako ie unaamka, kazini then home basi kuna muda unaona kabisa like your life is boring, nothing is exciting. Ila siku ukiamka you can't move your legs, au macho hayaoni, au mikono haifunction tena au kufukuzwa kazi/biashara kufa, ndo unaona like ile boring routine yako ni kitu cha thamani sana kwako.

We should learn to be grateful. Kila siku sisi ni watu wa kuomba tu, Mungu naomba this, naomba that. Hakuna siku mtu unasema Mungu Ahsante kwa A, B, C. Mungu katupa vitu vingi sana, ila ikitokea tu kuna kitu tunakihitaji sana, and Mungu hajatupa kwa muda huo tunaotaka Sisi, basi ndo kulalamikia tu, tunasahau yale yote tuliyopewa bila hata kumuomba. Sio kama ndo turidhike na maisha, tutafute tu zaidi but tusijistress sana juu ya tusivyonayo hadi tukakufuru. Tuwe watu wa shukrani
Yebo! Tuwe watu wa shukrani. Amina kwa statement hiyo.....
 
Watoto wa Bakhresa, Mengi au Mo dewje ktk maisha yao yote kuanzia wakiwa tumboni mwa mama yao hawatokaa wajue maisha magumu ni kitu gani au waje wapitie maisha magumu! Na sis tutafute hela kwa bidii watoto wetu wasije kupitia njia tulizo pitia tujitume tuachane na siasa
Ugumu wa maisha sio kukosa fedh tu hiyo ni sehemu ndogo sana ya ugumu wa maisha na hili ndilo tatizo la wengi hutafuta pesa wakidhani watatatua changamoto zao lakini huishia kufa kwa mawazo

Ugumu wa maisha unaongelewa hapa ni kukosa furaha na amani kwa sababu mbalimbali maisha siyo magumu kama mtu atakuwa na furaha na amani ktk maisha hata kama kwa siku anakula mara moja hivyo furaha na amani na utulivu wa ndani haununuliwi kwa pesa hivyo kinachowasumbua wengi sio kukosa pesa ila kukosa amani na furaha ya kweli
 
Kwa mtu ambae hajawahi kupitia hali mojawapo kati ya hizo hawezi kuamini....Ila mimi nilishapitia hata pesa ya pipi kifua haionekani.....Na elimu yangu ya chuo kikuu niliosha magari,niliuza bangi,nilikaba,kinyozi etc....(tena nchi ya watu) Na kanisani sikuwahi kukosa nilimuomba sana Mungu sikuacha hata siku moja.Huwezi kuamini leo hii nakula pipa mpaka mikanda imenitoa sugu..Na niko na nidhamu iliyotukuka ya fedha.Kwa kifupi maisha ni mazuri boss of my own company/business...Even hustlers wish they had a hustle like mine.Respect to all the hustlers out there
Umesahau kutuambia kitu kimoja bado unakwenda kanisani na bado unamtegemea Mungu ama baada ya kupata hayo ukaona kanisa linakupotezea muda
 
Unakua huna hela kiasi kwamba hata ukikwea daladala na kumuona konda ana mihela ile unatamani kumnyang'anya.

Enzi za chuo hii ilintokea sana maana safari ya kutoka Udsm hadi Mabibo kwa miguu si ya kitoto, halaf ukifika hostel wachanganya Maji na sukari unakandamiza kitu cha mkate. Umasikin ni kitu cha kulaani sana jaman
Hiyo ni natural force towards success, itumie.
 
Hapa nina maanisha kufirisika/kufulia kukosa uhakika wakupata angalau chai kwa siku kutengwa na ndugu. Kukosa kazi muda mrefu, kuugua na watu kukutenga, kukosa kodi ya nyumba/mahali pa kulala, kusingiziwa kwamba hutafuti kazi au kusemwa umelogwa ndugu kusema una laana.Kukatishwa tamaa kwamba Mungu kakuacha,kwamba unasali uongo
kudharauliwa na mambo kama hayo.

Je uliweza vipi kuchomoka katika hali hiyo?

Ashakum si matusi.

haya uyasemayo yapo na yamewakumba baadhi ila nachelea kutoa maelezo kwa kuwa wewe si mtu halisi ni mtu hewa, na kama ndivyo basi hata haya uliyoyaandika ni hewa.

vitu hewa havihitaji mchango halisi. labda tuwasubiri watu hewa wenzio wachangie.

ahsante
 
Nashukuru kwa ukomavu wako
 
Nilichojifunza hizo nyakati huwa haziishi, na hakuna maisha ambayo yatakua hayana changamoto sema zitatofautiana tu.
Hali kama hizo zimeniimarisha sana, hata nikipata tatizo kubwa, si panic, najipa moyo tu, kama niliweza kumudu matatizo makubwa na Mungu akanivusha, hata hili lililopo mbele yangu litapita.

Hauna kazi, unadaiwa kodi, mbaya zaidi mwenye nyumba mnaishi nae nyumba moja na un afamilia. Hiyo hali unaweza kutamani uyeyuke. Hapo haujaambiwa wife kajifungua katikati ya hiyo hali! Lakini mara zote, Mungu ni mwema sana.
Acha tu mkuu, ulivyo-comment kama unaniona vile mkuu wangu. Maisha yanahitaji uvumilivu sana.
 
Huu uzi umenikumbusha mbali sana!! Usiombe ukafiwa na wazazi ukiwa mdogo alafu uishi na ndugu mwenye roho mbaya na hana huruma! anaweza kukutolea maneno ambayo hayawezi kufutika ktk ubongo wako! sitasahau nikiwa kidato cha pili niliomba ada kabla sijapewa niliambiwa maneno haya(wengine wazae wengine walee) niliumia sana siku ile nililia siku zima,anyway nawashukuru walinisomesha kwa masimango ila nimetoka huko kwa nguvu za Mungu,na sasa ninaishi kwa amani na furaha nikwa na familia yangu na watoto wangu.
Yupo dogo mmoja rafiki yangu alipata matatizo nikamsaidia pa kuishi ... hadi sasa hajanisaau.
 
Dah.. We acha tu, umasikini usikie tu.. Unajua inafika hatua kwa wale wenye familia inapoteza hata kujiamini kama baba.. Lakini hata maelewano pia yanapungua ndani ya nyumba.. Unajihisi mnyonge na kukata tamaa..
Ukweli ni kwamba Maisha yana changamoto nyingi sana.. Wanasema shida huleta akili.. Kuna wakati utafika na utasahau yote!
 
Kuna mmoja hawezi kukutupa wala kukususa, anaitwa MUNGU. Ukiona umebanwa sana na huna suluhisho, kimbilia kwake, kila kitu kinawezekana.
Ni kwa nini ukimbilie kwake wakati una shida? Kwani hupaswi kumkimbilia wakati wa furaha yako kumpa sifa na shukrani? Ukimkumbuka wakati wa furaha naye atakukumbuka wakati wa dhiki. Kinyume chake ni ile unapata dhiki unaomba unaona kimyaaa...unaanza kulalama na kukata tamaa eti Mungu umeniacha.
 
TOFAUTI YA MIPANGO YA MUNGU NA MAISHA YA KIBINADAMU.
Habari za leo. Nataka leo upate kile ambacho nimekipata Na naamini kitakusaidia katika safari ya maisha humu duniani. Binadamu tumekuwa tukiumizwa sana Na binadamu wenzetu, magonjwa, shida, umaskini nk .Kwa wenye malezi ya kidini tunaamini msada Mkubwa ni Mungu. Wengine tunafunga tukisali ili kikombe (shida) zituepuke lakini tunafikia kipindi tunakata tamaa yote kwa sababu tuna moyo wa kibinadamu. Lakini nataka nikwambie Kila kitu katika maisha kinafanyika kwa sababu. Yesu alipo teswa aliumia sana akasema ikiwezekana kikombe huku kiniepuke lakini Mungu alikuwa Na makusudi yake Unajua siku ya Tatu baada ya kifo chake nini kilitokea. Yusufu mwana wa Yakobo "mwanzo 37- 47" kasome, kwa ufupi aliuzwa Na ndugu zake wa dam. akafanywa mtumwa, akawekwa gerezani lakini kwa kuwa kila kitu kinifanyika kwa sababu Mungu Alimpa kipaji cha kutafsiri ndoto. ( japo unapitia magumu Tumia kipaji au nafasi uliyonayo kumtukuza Mungu) Biblia inasema Yusufu alimtafsiria ndoto mfalme Farao. Na Farao akamtoa gerezani Na kumfanya mkuu katika ufalme wake ( Mwanzo 41:37-43)
FUNZO: Ukijikuta umeumbwa binadamu Mapito ( magonjwa, umaskini, manyanyaso ya ndugu, dharau nk) Hutokea kwa Sababu amini amani yako iko mbeleni usimlaumu Mungu Bali mshukuru( Rejea Ayubu) Mungu tunaye Mwamini ni wa Ushindi siku zote. Yesu aliteswa lakini siku ya Tatu alifufuka Na amekaa mkono wa kuume wa Mungu baba. Ayubu aliugua na Mali zake kuisha mwisho wake ni Neema. Yusufu aliuzwa kama mtumwa mwisho wake ni mkuu Na akawa msaada hata kwa waliomuuza. Ukishajiuliza kwanini isiwezekane katika jaribu lako?
JIPE MOYO WA USHUJAA MAPITO UNAYOPITIA MWISHO WAKE NI NEEMA. USIKATE TAMAA KAA KARIBU NA MUNGU.
Naamini umeifurahia makala hii niliyoiandaa Mimi mwenyewe Paul David Kilango (PDK) si mbaya ukiacha Comment yako kwa maboresho. Mungu akubariki
13 mins · Privacy: Public
 
The Meek, pamoja na upendo wako wa dhati kwa Mungu, una tatizo. Umeelemewa. Spiritual approach haikutoshi. Kuanguka kwako bafuni wala hakuhusiani na vita ya kiroho. Uko depressed. Unaweza kubisha lakini kila unapofunguka unaonyesha dalili za mtu mwenye msongo mkali. Una mkanganyo wa identity, wa lengo la kuishi na mambo mengi. Una potential kubwa sana, lakini usipoangalia inaweza kufukiwa kabla hujaifaidia dunia. Huyo YAHWYE akuwezeshe tu maana pamoja na persecution nyingi alikuwa anafanya kazi na kumtunza mama yake aliyekuwa mjane na kugharamia shughuli zake za kimisionari.
Yaani ni kama umeona nilichowaza kuhusu huyu The Meek!

He is in depression! Maisha na maandiko yamemchanganya!

Anahitaji kumpata mtu ambaye atamwelekeza vizuri habari za Kimungu na kumpa maarifa sahihi ya maisha.
 
Kwa kweli ktk umri wangu mdogo huu nimepitia matatizo magumu mno yasiyotatulika kwa fedha ila kwa uwezo wa Mungu pekee
Miaka ya hivi karibuni hadi sasa nimekuwa nikipitia severe psychological torture na tatizo zaidi ni kukosa walau mtu wa ku share nae ila kwa kumtegemea Mungu pekee naamini atanitetea
Unaweza kushare issue yako hata humu JF...wapo watakao kuponda ila kuna watakaokupatia ushauri wa maana pia. Hata hivyo umefanya vema kumtegemea Mungu kwani kumtegemea Mungu kuna faida!
 
Back
Top Bottom