Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Amen sis. It is well with my soul, huu wimbo umekuwa ukitupa matumaini makubwa mnoo. His life is a living testimony

Me nina wimbo huu, kuna mwingine wa Tenzi pia unaitwa "Nipitapo Majaribu"

1. Nipitapo majaribu katikati ya miiba
Ninatosheka kwa kuwa, Unanifikiri

×××Unanifikiri mimi, waniwaza sana
Nahitaji kitu gani, wewe wanitosha

2. Masumbufu ya dunia, yasongayo moyo wangu
Mwisho yananikumbusha, unanifikiri

3. Shida zija au zisije, maisha bora au ya shida
Mwisho yananikumbusha, unanifikiri

Na kuna ule Liseme - Sarah K. Afu Nikimaliza namsikiliza Joel Osteen- Having the right perspective Aaah ni nitalia wee, Nikimaliza hapo nakuwa na hiyo amani daah, nacheka tu

Wimbo wa marehem mama yangu, alifafiki mwaka 1994 ila bado nmuona akiimba bado
Joel osteen alinibariki sana mwaka 2013 na somo la "get over it"
 
Ujue binadamu tunaamini material things ndo zinafanya maisha yetu yawe kamilifu. Yes pesa na Vitu vingine ni vya muhimu, but kuna Vitu vya muhimu zaidi tunavi-overlook sana ie Health, Peace of Mind, Love (family, relatives, friends). Hivi vitu ukivikosa hata pesa unaweza iona haina thamani

Kwa vile tunaamka asubuhi tukiwa wazima wa afya, basi tunachukulia like it's something ordinary, nothing special with it... kumbe every single day is such a huge blessing to us. Kwa vile una routine yako ie unaamka, kazini then home basi kuna muda unaona kabisa like your life is boring, nothing is exciting. Ila siku ukiamka you can't move your legs, au macho hayaoni, au mikono haifunction tena au kufukuzwa kazi/biashara kufa, ndo unaona like ile boring routine yako ni kitu cha thamani sana kwako.

We should learn to be grateful. Kila siku sisi ni watu wa kuomba tu, Mungu naomba this, naomba that. Hakuna siku mtu unasema Mungu Ahsante kwa A, B, C. Mungu katupa vitu vingi sana, ila ikitokea tu kuna kitu tunakihitaji sana, and Mungu hajatupa kwa muda huo tunaotaka Sisi, basi ndo kulalamikia tu, tunasahau yale yote tuliyopewa bila hata kumuomba. Sio kama ndo turidhike na maisha, tutafute tu zaidi but tusijistress sana juu ya tusivyonayo hadi tukakufuru. Tuwe watu wa shukrani
Watu wote tungekuwa kama wewe nadhani cheating isingekuwepo kabisaa coz kila mtu ana hofu ya Mungu.

BTW huu uzi unaonyesha ni kiasi gani Mungu anatupigania, eti shukrani yetu kwake tukishafanikiwa ni kuzini kwa kwenda mbele, kaishakuwezesha kifedha sasa wanakukoma, ni kunyanyasana coz mwenzio hana, duuuh!!
 
Wimbo wa marehem mama yangu, alifafiki mwaka 1994 ila bado nmuona akiimba bado
Joel osteen alinibariki sana mwaka 2013 na somo la "get over it"
Pole Sana Mdada.
 
Take heart my brother.!!! Jesus Christ is aware of your situation.

Binafsi, hali hiyo iliwahi kunipata na nilikuwa na rafiki mmoja kwenye mtandao wa kijamii.

Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nasali nimepiga magoti kitandani. Baada ya kusali , nikafungua simu, nikaona meseji " xxxx do you have a bank account number? " ... nikamshukuru sana Mungu. Huyu mtu sikumuomba pesa . Akatuma 500USD. Baada ya mwezi tena akatuma 1000USD. Hatujawahi kuongea kwenye simu. Kila nikimpigia simu anakuwa anani avoid. Ni mtu wa Mungu sana. ( Binafsi namuona kama malaika )

Duuh...Mungu wako ni mkuu sana
Usiache kuzipita njia zake mana katika meseji zako ninabarikiwa mnooo na tena nimemuomba Mungu msamaha kwamba kumbe mimi sina matatizo makubwa ni tamaa za kibinadamu zinanifanya nimlaumu Mungu kwa kukosa baadhi ya vitu!!!
Ubarikiwe ulieanzisha uzi huu
 
Wimbo wa marehem mama yangu, alifafiki mwaka 1994 ila bado nmuona akiimba bado
Joel osteen alinibariki sana mwaka 2013 na somo la "get over it"
Uuuh pole sana mpenzi, be a grateful daughter always and Mshukuru Mungu kwa ajili ya maisha ya mama, hata kama alikuacha akiwa bado mdogo sana. Kuna watu hawajawahi kuwaona mama zao kabisa, au mama zao wapo lakini waliwakataa. Sisi tuliofanikiwa kuwaona na kutunzwa nao, basi Tumshukuru Mungu kwa neema hiyo.
 
Watu wote tungekuwa kama wewe nadhani cheating isingekuwepo kabisaa coz kila mtu ana hofu ya Mungu.

BTW huu uzi unaonyesha ni kiasi gani Mungu anatupigania, eti shukrani yetu kwake tukishafanikiwa ni kuzini kwa kwenda mbele, kaishakuwezesha kifedha sasa wanakukoma, ni kunyanyasana coz mwenzio hana, duuuh!!
Mmh binadamu tuna mambo, wewe acha tu. Yani mwingine kila siku anaomba kitu fulani ili tu awakomeshe wengine. Do you think wewe ambaye Mungu amekuinua sana kimafanikio, ni mjanja sana au una akili sana kuliko wengine? Sijui kwa nini tunakuwa na mioyo ya viburi na kujisifu. Kila kitu ni kwa neema tu, kuna watu wanavyomtukuza Mungu maishani mwako but still unashangaa wanastruggle na maisha bila kukata tamaa, wewe mwenzangu na mie ambaye hata kumkumbuka Mungu ni shida eti unajiona ni bora zaidi yao kisa umefanikiwa sana. Aisee kila kitu ni kwa neema, me naonaga sistahili chochote kabisa
 
Mi kuanzia nikiwa mdogo nimepita maisha ya changamoto. Kuna wakati unaweza kulaumu family uliyozaliwa lakini haisaidii chochote.

You cant imagine family ya watu 6 baba, mama na watoto 4 wanaishi kwenye chumba kimoja for almost ten years.

Na kuna kipindi nakumbuka tuliishi na mama for almost 3 years bila baba, acha kabisa aisee masuala ya kula ugali na maharage ya mama ntilie wiki nzima ilikuwa kawaida sana halafu fikiria hapo tupo watoto na mama tu. Achana na mambo ya kula mlo mmoja kwa siku maana ilikuwa kama kawaida.

But here i am, kwa hali ile ya udogoni ya changamoto za maisha nilikuwa nikijituma sana kwenye elimu na haikunitupa mkono japo pia mazingira ya kusoma yalikuwa magumu maana ilikuwa mwendo wa koroboi mpaka natia mguu Chuo Kikuu na nafanya safari ya kwanza kuja Dar.

Hivi sasa nimeshamaliza elimu yangu lakini bado changamoto nakumbana nazo tena kubwa lakini sijafa moyo maana hakuna kigeni si kushinda wala kulala njaa zote nna uzoefu nazo na wala siogopi tena.

Ila kikubwa tu ni kwamba mimi ni mtu nisiyekufa moyo wala kukata tamaa kwa sababu tangu nimalize chuo hadi sasa nimekutana na nnaendelea kukutana na changamoto kubwa mno mno na nikifikiria nilipotoka na maisha niliyoishi ingekuwa ni kukata tamaa nisingefika hapa nilipo japo bado changamoto hazijaisha lakini kadri mda unvooenda mbele "the tough gets going"

Namshukuru tu Mungu kwa mentality na busara aliyonipa maana imekuwa silaha yangu moja kubwa sana kuweza kusurvive mpaka sasa na bado jamii inayonizunguka wananiona mi ni mtu mwenye maisha yangu ya furaha japo ukweli upo moyoni mwangu.
 
Mimi bado napita changamoto,kuna wakati natamani mshumaa wangu uzime nipumzike,ila yote kheri,maana wote tunapita na yote yatupatayo tutayaacha,
 
Mimi bado napita changamoto,kuna wakati natamani mshumaa wangu uzime nipumzike,ila yote kheri,maana wote tunapita na yote yatupatayo tutayaacha,
Mungu akutie Nguvu Kaka...
Jipe Moyo Mkuu.
 
Mimi bado napita changamoto,kuna wakati natamani mshumaa wangu uzime nipumzike,ila yote kheri,maana wote tunapita na yote yatupatayo tutayaacha,
Mshumaa kuzima ni jambo la heri kwa mdhambi anayetubu sasa ukapumzika ukiwa na dhambi ni hasara kubwa kikubwa nakushauri uwe una soma biblia ili ikuongoze kutubu kila wakati na mwishowe ukipumzika ktk haki ya kristo itakuwa jambo jema maana utaishi milele
 
The pursuit of happiness ya Will Smith itafute au Life ya Eddie Murphy. Kila Mtu anapitia.ila usiombe kupita Jela.
 
Nimepitia changamoto nyingi lakini za kawaida,changamoto za mwaka jana siwezi kusahau kwenye maisha yangu especially mwezi wa nane..shule masters ilikuwa inanitesa halafu shule yenyewe ya scholarship shirika moja kubwa hapa bongo nikimaliza wananichukua,mjomba yangu kipenzi anafariki ghafla mbele yangu akiwa kaniita kwake kijijini namaliza msiba mzee anaumwa mpaka nilikuwa nalia mwenyewe hospital huku Gf wangu ananiambia tubreak up kisa mimi soma soma sitaki kutafuta kazi.angalau sijaumia sana kwenye hili la Gf sababu kwenye uhusiano naingia nusu nikaja kugundua kumbe kapata kiajira cha kujishikiza analipwa laki 3 nikaacha nae.nashukuru shule imeisha nina job nzuri mzee alirudi poa hila kumbukumbu ya uncle inanitesa na kila siku namuombea kwa Mungu huko alipo
 
Umeshaona utukufu, endelea kushukuru na kutia moyo wengine.
Mimi bado napita changamoto,kuna wakati natamani mshumaa wangu uzime nipumzike,ila yote kheri,maana wote tunapita na yote yatupatayo tutayaacha,
hata yona (yunus) na nabii yeremia waliwahi kujinyoosha chini ili roho itoke. Kufa hufi na cha moto ndo mapito yetu. Kuwa na tumaini tu.
 
Umeshaona utukufu, endelea kushukuru na kutia moyo wengine.

hata yona (yunus) na nabii yeremia waliwahi kujinyoosha chini ili roho itoke. Kufa hufi na cha moto ndo mapito yetu. Kuwa na tumaini tu.

Ahsante mkuu Mungu akutie nguvu na akutangulie kwenye yote yenye heri kwenye maisha yako...Mungu yu pamoja nasi wanasema hili binadamu ukamilike lazima upitie changamoto kwenye maisha
 
Hakika ndivyo ilivyokuwa Kaka yangu. Haikuwa rahisi hata kidogo..... lakini nilisema Mungu ninayemtumikia atanipigania, atanitetea .....Nakumbuka maneno ya Mchungaji nilipokwenda kumshirikisha changamoto hii..... Aliniambia ..... "Mwanangu Vita hii haitaisha Mpaka umetangazwa Mshindi".... Haikuwa rahisi..... Namrudishia Mungu Sifa na Utukufu..... Amenitetea ..... Amenipigania.... Amenipa Ushindi. Utukufu wake sigusi!!!! .... Utukufu kwa Yehova Pekee.....
Mswee, Daaaah! Nimependa huo ujumbe "VITA HII HAITAISHA MPAKA NIMETANGAZWA MSHINDI" Bonge moja la meseji ambayo kwa watu makini tunazidi inatujaza tumaini kubwa mnoo.
 
Umesahau kutuambia kitu kimoja bado unakwenda kanisani na bado unamtegemea Mungu ama baada ya kupata hayo ukaona kanisa linakupotezea muda
Swali zuri sana Mkuu
Sijawahi kuacha kwenda kanisani kutubu dhambi zangu maana kwa namna moja au nyingine huwa tunamkosea Mungu pasipo kutambua, pamoja na kuwaombea ndugu/familia/marafiki zangu wote kwani Mungu ni mwingi wa rehema na haishiwi rehema na uwezo wa kusamehe ni mwenye huruma sana kwa waja wake na wote wenye Imani,Pili Sijawahi kuacha kutoa sadaka na fungu la kumi,Tatu na Mwisho nimefunga ndoa ya kikristo na wanangu wawili wamebatizwa kanisani.
 
Aisee kuna mdau nimemtumia ataweka hapa mmoja kila mtu achambue
 
Back
Top Bottom