Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Je, umeshawahi pitia maisha magumu?

Ndugu, nashukuru sana kwa maelezo yako. Kiufupi, sio kweli kwamba muda wote naomba kwa ajili ya Kazi. Ukweli ni kwamba, toka nimeelewa siri za ufalme wa Mungu hata hamu ya kuajiriwa sina. ( Vyeti huwa naviweka tu mbele za Mungu ili mapenzi yake yatimizwe)

Mara nyingi huwa naomba kwa Rehema za Mungu, Anionyeshe ufalme wake, Anisamehe Makosa yangu, Anipe nguvu na Mamlaka za kufanya vitu hapa Duniani kama huko Mbinguni kwa ajili ya utukufu wake katika Kristo Yesu.

Ndugu, nielewavyo mimi, Mungu wetu ni mwema sana; Yeye yupo tayari kumsamehe Mwanadamu yeyote aliyetayari kuzifuata njia zake katika roho na kweli.

Ni kweli tunatakiwa kupatana na watu + kuishi nao vizuri. Kuna watu kama wakina Paul, walikua wakiwatoa machozi watu wengi sana. Mungu hafanyi Kazi zake kama wanadamu.

Yesu alidhaniwa kuwa kalaaniwa, kafungwa, katupiwa mikosi, n.k ; hivyo hivyo hata kwa kina ayubu na wengine.

Binafsi nafahamu kuwa , tunaishi katika Ulimwengu wa Uovu. Na ili tuweze kuushinda ni lazima kwanza tuutafute Ulimwengu wa Mema na Elimu yake yote. Kwahiyo basi ili tuweze kuyavuka mabaya ni lazima tujiandae ku - suffer, kuwa rejected, kuuliwa na kuwa resurrected kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Mtu yeyote ambae kaamua kweli kuwa karibu na Mungu lazima awe na mind set hiyo.

Kwahiyo basi ninayopitia ni sahihi kabisa mbele za Mungu , na ninafarijika sana kuona ananiongoza katika njia zake, sio kwenye njia za Uovu.

I mean, ningeweza kwenda kwa waganga au kuwa mharifu badala yake.

#GodKnowsTheBest

Nina Vita kubwa sana katika Ulimwengu wa Roho, kwasababu shetani na majeshi yake yote wananifahamu vizuri sana , that I am a noble person ( A righteous branch and the repairer of the broken walls) ; Naelewa kuwa wanaumiza vichwa sana jinsi ya kunimaliza kwa muda mrefu wameshindwa.

Wakati nazaliwa, nilizaliwa nikatoka na chupa ya uzazi kama mnyama; na hata baada ya kuipasua chupa wakanikuta kondo la uzazi limeniviringa mara tatu shingoni.

Nikiwa na 3 years, niligundulika kuwa ni bubu, nikakatwa karimi.

Baadae nikapata mke mwenye HIV+ na nimeishi nae kwa zaidi ya 8 years bila kupata maambukizi wala watoto wangu kupata maambukizi. What a mighty God.

So nina elewa kuwa Mwili wangu sio wa kawaida, kwasababu ya kuepuka vifo vingi sana. Niliwahi kutekwa na Magaidi zaidi ya mara 2 na hawakuweza kunifanya kitu.

I know the truth, wa haya yote. Sio kwa nguvu zangu.
Asante mkuu kwa maelezo toshelevu, nimechangia mara mbili juu kutokana na mchango wako wa mwanzo, ungeandika haya mwanzo ningechangia tofauti. ILA habari yako it's too big kuwa katika topic hii, habari yako ni topic nyingine kabisa inayo jibeba, habari yako it's more than Majaribu, Siwezi changia kitu katika hili, ila kusoma tena na tena na kujifunza mengi katika testimony hii ya maisha yako, kama nilivyo changia above, Mungu anakusudio kuu katika masiha yako, wengi hawatakuelewa, wengi watakudhihaki lakini kusudio la Mungu lazima litimie, GOD BLESS YOU. AMEN
 
ukipitia magumu utaelewa ww ni wa ina gani na pia utawajua vizur watu wanaokuzunguka. Kila mtu hajiombei apitie wakat mgumu ila huja pasipo kutegemea. Hapa roho ngumu km ya paka maranying huzaliwa ikiwa kila mtu hayuko nawe. Haijalishi magumu yap ktk mahusiano, kifedha n.k
uvumilivu huitajika sana ktk kipind hiki.
 
Watoto wa Bakhresa, Mengi au Mo dewje ktk maisha yao yote kuanzia wakiwa tumboni mwa mama yao hawatokaa wajue maisha magumu ni kitu gani au waje wapitie maisha magumu! Na sis tutafute hela kwa bidii watoto wetu wasije kupitia njia tulizo pitia tujitume tuachane na siasa
Ina maana hao watoto haumwi kabisa?

Kitendo cha kuwa mgonjwa pia, ni kupitia hali ngumu
 
Kuna kitu ninajifunza kwenye uzi huu_maake aliyonifanyia boss wangu hapa ofcn....bila kosa ila just kunikomoa.....God knows.

Usife moyo mpendwa.... Nami pia bosi wangu kuna mambo alikuwa akinifanyia kuhakikisha naondolewa Kazini.... hakika sikukata Tamaa.... Nilimwamini Mungu na kuzidi kufanya Kazi kwa bidii.... Nilimshirikisha Mchungaji changamoto hiyo... Hakika Mungu si mwanadamu.... shimo alilotamani nidumbukie..... Tumbua Tumbua imempitia.... Amedumbukia katika lile lile shimo alilochimba mwenyewe..... Hakika mwanadamu hawezi kuziba riziki ya mtu....na kwa wenye vyeo.... wakumbuke ni dhamana tuu.... Mwisho wa ubaya Aibu....
 
Your testimony is beyond imagination. Mungu anakusudi kubwa juu yako.
Ninaelewa hivyo 100% kwani toka nikiwa mdogo hadi leo hii nimekuwa nikitabiriwa na watu wengi sana kuhusu future yangu. Watu mbalimbali mashuhuri na wakawaida.

Nakumbuka zamani sana, nikiwa seminary nasoma. Mzee mmoja MWALIMU (Marehemu kwasasa) , aliniita mbele ya Wanafunzi wenzangu akaniambia, " HUYU NDUGU YENU ATAKUWA MTU MKUBWA SANA HAPO BAADAE, ; NA HUO MTIHANI WENU WA TAIFA MTAKAOUFANYA HIVI KARIBUNI ATAFAULU SANA" Mwisho wa kunukuu.

Baadae tulifanya ule MTIHANI na nikaongoza ki mkoa na kuwa miongoni mwa 10 best student waliofaulu KIkanda.

Katika maisha yangu hadi leo hii , nimekuwa nikikutana na watu mashuhuri sana katika Taifa letu na nje ya Taifa letu. Mara nyingi sana hushangazwa na maongezi / Uelewa wa mambo tunayokuwa tunazungumza kwa wakati huo.

Kuhusu Afya, nilikuwa nina miaka mingi sana mwili wangu kupokea aina yeyote ya vidonge. Sijawahi kuugua kwa miaka mingi sana zaidi ya 18. Ni majuzi tu nilichomwa sindano ya TT na vidonge vya kukausha kidonda baada ya kuanguka bafuni
 
Napitia huu uzi nikiwa sina hela ya kula mwanangu anaumwa sina hela ya kumpeleka hospital.Kazi nimeachishwa mafao yamezuiwa.Utakapowakumbuka wengine nami usinipite Mungu wangu.
So sad,...pole mkuu.
 
Usife moyo mpendwa.... Nami pia bosi wangu kuna mambo alikuwa akinifanyia kuhakikisha naondolewa Kazini.... hakika sikukata Tamaa.... Nilimwamini Mungu na kuzidi kufanya Kazi kwa bidii.... Nilimshirikisha Mchungaji changamoto hiyo... Hakika Mungu si mwanadamu.... shimo alilotamani nidumbukie..... Tumbua Tumbua imempitia....Amedumbukia katika lile lile shimo alilochimba. Hakika mwanadamu hawezi kuziba riziki ya mtu....na kwa wenye vyeo.... wakumbuke ni dhamana tuu.... Mwisho wa ubaya Aibu....
We Must always love+ pray for our enemies ,for God's Glory, in Jesus Christ Name.
 
Napitia huu uzi nikiwa sina hela ya kula mwanangu anaumwa sina hela ya kumpeleka hospital.Kazi nimeachishwa mafao yamezuiwa.Utakapowakumbuka wengine nami usinipite Mungu wangu.
Take heart my brother.!!! Jesus Christ is aware of your situation.

Binafsi, hali hiyo iliwahi kunipata na nilikuwa na rafiki mmoja kwenye mtandao wa kijamii.

Nakumbuka siku hiyo nilikuwa nasali nimepiga magoti kitandani. Baada ya kusali , nikafungua simu, nikaona meseji " xxxx do you have a bank account number? " ... nikamshukuru sana Mungu. Huyu mtu sikumuomba pesa . Akatuma 500USD. Baada ya mwezi tena akatuma 1000USD. Hatujawahi kuongea kwenye simu. Kila nikimpigia simu anakuwa anani avoid. Ni mtu wa Mungu sana. ( Binafsi namuona kama malaika )
 
Hata ndugu pia.
NDUGU, Jamaa, Marafiki, watu wa karibu sana , hata mke au Mme. Tizama hapa mke wa Ayubu , aliyekuwa amezoea maisha ya raha, na akaanza kuwa against Mme wake wakati wakiwa kwenye dhiki

#Job 2:9 ,"His wife said to him, "Are you still maintaining your integrity? Curse God and die!"

Kiufupi, mtu yeyote aliyekaribu sana na Mungu lazima areceive attacks ; na wakati mwingine kutoka kwa watu anaowapenda ili Mungu amtoe mahala alipo kwenda juu zaidi.
65553bf771746aaf954a85dbc217c466.jpg
c66408da119a29202f3cf52460118c56.jpg
 
Napitia huu uzi nikiwa sina hela ya kula mwanangu anaumwa sina hela ya kumpeleka hospital.Kazi nimeachishwa mafao yamezuiwa.Utakapowakumbuka wengine nami usinipite Mungu wangu.
......Elungata dislike this
 
Ina maana hao watoto haumwi kabisa?

Kitendo cha kuwa mgonjwa pia, ni kupitia hali ngumu
Mtu yeyote anayeishi chini ya Hisia zake, mara nyingi hufikiri kuwa matajiri wana maisha ya raha sana. Uhalisia ni kwamba, wanaishi maisha ya Tabu sana ( Hawana Amani, Misongo ya Mawazo, Maradhi sugu, Hawana Furaha , Muda wote wanaishi kwa wasiwasi, Kukosa hamu ya kula , Kukosa usingizi n.k )
 
Napitia katika hali ngumu sana ila namshukuru Mungu nasonga. Maisha yangu yanaenda km bahati tu vingnevyo ningekuwa nmeshakufa ila najua Mungu ana kusudi lake kwangu. Napitia ktk kipindi kigumu sana ila naimani nitakuja kuwa shuhuda kwa wengne. Mungu ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom