Kutokana na maelezo yako, unavita kubwa katika ulimwengu wa roho, na vita vyako hutashinda kwa nguvu za kimwili. unahitaji maombi maalum ya ukombozi, ndio umeokoka lakini kuna vifungo utakuwa umefungwa kwavyo na inahitaji maombi maalum na ufunuo kwaajili ya kuvi deseable, inaonekana umekuwa ukiomba mara zote bila kujua specific nini cha kuombea, umekuwa ukiomba kwa ajili ya kupata kazi, lakini shida sio katika kupata kazi.
Ni kosa kubwa sana katika maombi kuomba bila target, au kulenga wrong target. kama inashindikana kabisa ni vizuri kuwa na mfungo wa utakaso na maombi katika Roho. ROMANS 8:26-28. MATTHEW 17:21. Ina bidi ufanye mfungo wa maombi kuomba Roho mtakatifu akufunulie ( akuonyeshe) wapi palipo na tatizo ili uweze ku deal direct na chanzo.
Kaa chini tafakari, angalia historia ya maisha yako, ya wazazi wako. kuna mahali palifanyika agano fulani la kiroho? Je kuna jambo wewe ulowahi lifanya ambalo linaweza kuwa sababu ya milango kufungwa? jaribu kuangalia hata yale madogo ambayo unaona ni irrelevant. Fanya sala ya toba ya ukombozi ( special deliverance) na kama kuna mahali kwa namna moja au nyingine unahisi ulifanya jambo ambalo lilimuumiza mtu sana, katengeneze nae, machozi ya mtu ni mabaya sana.
Ndugu, nashukuru sana kwa maelezo yako. Kiufupi, sio kweli kwamba muda wote naomba kwa ajili ya Kazi. Ukweli ni kwamba, toka nimeelewa siri za ufalme wa Mungu hata hamu ya kuajiriwa sina. ( Vyeti huwa naviweka tu mbele za Mungu ili mapenzi yake yatimizwe)
Mara nyingi huwa naomba kwa Rehema za Mungu, Anionyeshe ufalme wake, Anisamehe Makosa yangu, Anipe nguvu na Mamlaka za kufanya vitu hapa Duniani kama huko Mbinguni kwa ajili ya utukufu wake katika Kristo Yesu.
Ndugu, nielewavyo mimi, Mungu wetu ni mwema sana; Yeye yupo tayari kumsamehe Mwanadamu yeyote aliyetayari kuzifuata njia zake katika roho na kweli.
Ni kweli tunatakiwa kupatana na watu + kuishi nao vizuri. Kuna watu kama wakina Paul, walikua wakiwatoa machozi watu wengi sana. Mungu hafanyi Kazi zake kama wanadamu.
Yesu alidhaniwa kuwa kalaaniwa, kafungwa, katupiwa mikosi, n.k ; hivyo hivyo hata kwa kina ayubu na wengine.
Binafsi nafahamu kuwa , tunaishi katika Ulimwengu wa Uovu. Na ili tuweze kuushinda ni lazima kwanza tuutafute Ulimwengu wa Mema na Elimu yake yote. Kwahiyo basi ili tuweze kuyavuka mabaya ni lazima tujiandae ku - suffer, kuwa rejected, kuuliwa na kuwa resurrected kwa ajili ya utukufu wa Mungu.
Mtu yeyote ambae kaamua kweli kuwa karibu na Mungu lazima awe na mind set hiyo.
Kwahiyo basi ninayopitia ni sahihi kabisa mbele za Mungu , na ninafarijika sana kuona ananiongoza katika njia zake, sio kwenye njia za Uovu.
I mean, ningeweza kwenda kwa waganga au kuwa mharifu badala yake.
#GodKnowsTheBest