Je, prem number ya wanafunzi darasa la pili kwenye shule ya English Medium ambayo bado haijakamilisha usajili zina kubalika kisheria?

Bongotunacheza

JF-Expert Member
Dec 7, 2018
718
1,643
Watoto walikuwa wanasoma kwenye shule ya English Medium nikawapeleka kwenye shule ya kiswahili. Shule ya English Medium hawakunipa uhamisho kwa sababu walikuwa bado wananidao so nikawa nalipa deni lao taratibu ili nikikamilisha wajue prem number za watoto. Now Mungu ameniinua tena kiuchumi hawa watoto nawapeleka kwenye shule nyingine ya English Medium ambayo ina la kwanza hadi la saba ( hii waliokuwa wanasoma awali ilikuwa na la kwanza hadi la tatu).

Kwenye shule hii mpya walitaka niwape majina ya watoto na shule wanayo soma. Mkuu wa shule alipopokea majina ya watoto akayawasilisha kwa afisa elimu. Afisa elimu anasema hiyo shule haijasajiliwa. But prem numbers za watoto zipo so watahamishwa hivyo hivyo. Swali langu ni je? Shule ya English Medium ambayo bado haija kamilisha usajili, prem numbers zake zinaweza kuwa valid? Au niachane nazo niwaambie uongozi wa shule hii mpya wanifanyie utaratibu upate prem numbers mpya?

Wajuzi wa mambo naomba mnisaidie kujua tafadhali
 
Maswala ya prem waachie walimu wanajua namna ya kuandikisha wewe lipa ada kwenye shule mpya. Pia shule ya Zaman hawana uwezo wa kuzuia uhamisho hata kama wanakudai,
 
Maswala ya prem waachie walimu wanajua namna ya kuandikisha wewe lipa ada kwenye shule mpya. Pia shule ya Zaman hawana uwezo wa kuzuia uhamisho hata kama wanakudai,
Unaipataje hiyo prem number kwa mfano? Na bila mwalimu mkuu kutuma jina la mtoto na prem number kwa anayempokea unafikiri utamuhamisha?
 
Shule haiingizwi kwenye mfumo wa prem number mpaka iwe imesajiliwa. Kama private ina wanafunzi wenye prem no na huku haijasajiliwa ni makosa
Shule ya private imenipa option hao watoto wapewe prem mpya. Je is it Okay?
 
Wakuu u taratibu wa kupata PREM number mpya kwa mtoto ambae hana kabisaaa yani alietoka nje ya nchi ukoje? Maana nimekwama apo
 
Back
Top Bottom