Wazazi wengi wana msongo wa mawazo kutokana na stress za kutafuta ada za shule za kina junior wao wanaosoma english medium eg. Atlas, Tusiime, etc. Muda wa kulipa ada ukifika mzazi anakuwa na hasira hasira tu sababu ya msongo wa mawazo
Watoto na wao wana msongo wa mawazo kutokana na ratiba ya shule zao hizo za kisasa english medium. School bus inakuja saa 11 alfajiri na kumrudisha saa 12 jioni. Hapo mtoto kabebeshwa bonge la begi mgongoni lenye vitabu ma madaftari ya masomo yote.
Hapo hapo hapati muda wa kupumzika wala kucheza ku enjoy utoto wake, maana kila siku ana home work, na likizo hakuna kufunga shule kisingizio ni kujiandaa na mitihani. Hapo Mtoto anapata depression toka utotoni maskini.
Pili hizi shule zina fake lifestyle, zinamfundisha mtoto softlife ambayo mtaani hakuna hiyo soft life. Vitu kama kufanyiwa usafi, kufatwa na school bus, mtoto huyu huyu akija kukutana na maisha halisia ya kugombea mwendokasi ama daladala anaona anaonewa.
Hapo tena mtoto anakuwa na depression akikosa hiyo soft life after school. Tukumbuke schooling is a lifestyle not a place. Mtu aliyezoea soft lifestyle lazima apate depression akikutana na real life.
Pia hii tabia ya wazazi ku buy education at high price kunawafanya wazazi washindwe kuwekeza kwenye assets zingine ili watoto wao wapate hata pa kuanzia mbeleni.
Mzazi anaishi nyumba ya kupanga ila anatumia milioni 10 kila mwaka kulipia watoto wake ada Atlas ama Tusiime. Mzazi huyu anashindwa kujenga nyumba ya familia yake ama kuanzisha miradi. Siku huyu mzazi akiumwa ama kufukuzwa kazi anakunywa sumu.
Ushauri kwa wazazi ambao bado hatujawekeza vya kutosha tuwe makini na hizi shule za english medium za kisasa.
Serikali pia ibadilike. Demand ya hizi shule ni kubwa sana, waongeze shule za umma, english medium ziwe nyingi. Sio Olimpio na Bunge tu.
Pia Jeshi la kujenga taifa ( JKT) pia.. lisiishie kuwekeza kwenye kujenga kumbi za harusi, kujenga fremu, bar na mambo ya catering tu JKT lingewekeza kwenye low cost english medium primary schools kwenye miji mikubwa. Bei za ada zao ziwe kama olimpio na bunge.