Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Ahaa basi sawa

Siwezi kuthibitisha kitu ambacho hakipo
Wewe ndiyo ulete ushahidi kwanini unasema uchawi upo.

Sawa mkuu, lakini hapo ndipo hoja ilipo: wewe ndiye uliyesema uchawi haupo, kwa hiyo si lazima mimi nibebe mzigo wote wa uthibitisho. Mimi nimeeleza kwamba ninaamini upo.

Kama msimamo wako ni kwamba “uchawi haupo kabisa”, basi lete sababu au ushahidi unaofanya hitimisho hilo liwe la lazima. Kutokuweza kuuthibitisha wewe mwenyewe hakumaanishi moja kwa moja kwamba haupo.

Sasa tuwekee ushahidi mezani, si dhana tu.
 
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Mimi naona hapa kuna vitu viwili vinavyopaswa kutenganishwa: imani na ushahidi. Mtu anaweza kuamini uchawi kwa sababu za kidini au kimila, lakini si kila tukio lisiloeleweka linakuwa ushahidi wa uchawi.

Mfano wako unaonyesha vizuri nguvu ya saikolojia. Ukiambiwa mara kwa mara kwamba umelogwa, akili inaweza kuanza kutafsiri kila dalili kwa mtazamo huo—hofu, ndoto, wasiwasi, hata mabadiliko ya mwili. Halafu mtu anaanza kuona kila kitu kama uthibitisho wa alichoambiwa.

Cha msingi ni kutafuta sababu kwanza. Mtu akiwa na maumivu ya kichwa, kizunguzungu au mabadiliko ya tabia, hospitali na uchunguzi vinapaswa kuwa sehemu ya kwanza kabla ya kuhitimisha kwamba ni uchawi.

Kuhusu hoja ya "kama uchawi unaweza kufanya mabaya, kwa nini usitumike kufanya mazuri?", hapo ndipo swali linakuwa zito. Kama tunadai kuna nguvu inayoweza kubadilisha akili, afya au uwezo wa mtu kwa kiwango hicho, tungehitaji ushahidi unaoweza kuchunguzwa na kuthibitishwa, si simulizi pekee.

Kwa hiyo mimi ningesema: tusikatae kila kitu tusichokielewa, lakini pia tusipe jina la uchawi kila tunapokosa maelezo. Kuna mambo mengi ambayo zamani yalionekana ya kimiujiza lakini baadaye yakapata maelezo ya kisayansi, kiafya au kisaikolojia.

Mwisho wa siku, imani ni suala la mtu binafsi; lakini tukianza kutoa ushauri unaohusu afya ya mtu, ni muhimu sana tusimnyime mtu nafasi ya kupata uchunguzi na matibabu sahihi.
 
Sawa mkuu, lakini hapo ndipo hoja ilipo: wewe ndiye uliyesema uchawi haupo, kwa hiyo si lazima mimi nibebe mzigo wote wa uthibitisho. Mimi nimeeleza kwamba ninaamini upo.

Kama msimamo wako ni kwamba “uchawi haupo kabisa”, basi lete sababu au ushahidi unaofanya hitimisho hilo liwe la lazima. Kutokuweza kuuthibitisha wewe mwenyewe hakumaanishi moja kwa moja kwamba haupo.

Sasa tuwekee ushahidi mezani, si dhana tu.
Hivi unawezaje kuthibitisha kitu ambacho hakipo😅😅

Wewe unaesema uchawi upo Thibitisha
 
Mimi naona hapa kuna vitu viwili vinavyopaswa kutenganishwa: imani na ushahidi. Mtu anaweza kuamini uchawi kwa sababu za kidini au kimila, lakini si kila tukio lisiloeleweka linakuwa ushahidi wa uchawi.

Mfano wako unaonyesha vizuri nguvu ya saikolojia. Ukiambiwa mara kwa mara kwamba umelogwa, akili inaweza kuanza kutafsiri kila dalili kwa mtazamo huo—hofu, ndoto, wasiwasi, hata mabadiliko ya mwili. Halafu mtu anaanza kuona kila kitu kama uthibitisho wa alichoambiwa.

Cha msingi ni kutafuta sababu kwanza. Mtu akiwa na maumivu ya kichwa, kizunguzungu au mabadiliko ya tabia, hospitali na uchunguzi vinapaswa kuwa sehemu ya kwanza kabla ya kuhitimisha kwamba ni uchawi.

Kuhusu hoja ya "kama uchawi unaweza kufanya mabaya, kwa nini usitumike kufanya mazuri?", hapo ndipo swali linakuwa zito. Kama tunadai kuna nguvu inayoweza kubadilisha akili, afya au uwezo wa mtu kwa kiwango hicho, tungehitaji ushahidi unaoweza kuchunguzwa na kuthibitishwa, si simulizi pekee.

Kwa hiyo mimi ningesema: tusikatae kila kitu tusichokielewa, lakini pia tusipe jina la uchawi kila tunapokosa maelezo. Kuna mambo mengi ambayo zamani yalionekana ya kimiujiza lakini baadaye yakapata maelezo ya kisayansi, kiafya au kisaikolojia.

Mwisho wa siku, imani ni suala la mtu binafsi; lakini tukianza kutoa ushauri unaohusu afya ya mtu, ni muhimu sana tusimnyime mtu nafasi ya kupata uchunguzi na matibabu sahihi.
Asante kwa maoni
 
Hivi unawezaje kuthibitisha kitu ambacho hakipo😅😅

Wewe unaesema uchawi upo Thibitisha

😅 Hoja yako inajigeuza yenyewe. Mimi nikisema uchawi upo, naweza kuonyesha ushahidi wa maandiko yanayouzungumzia: Kutoka 22:18, Kumbukumbu 18:10–12, Matendo 8:9–11, na Qur’an 2:102.

Sasa wewe ukisema “uchawi haupo kabisa,” lete ushahidi unaothibitisha kutokuwepo kwake.

Kusema “huwezi kuthibitisha kitu ambacho hakipo” si ushahidi kwamba hakipo. Lete ushahidi, si madai.
 
😅 Hoja yako inajigeuza yenyewe. Mimi nikisema uchawi upo, naweza kuonyesha ushahidi wa maandiko yanayouzungumzia: Kutoka 22:18, Kumbukumbu 18:10–12, Matendo 8:9–11, na Qur’an 2:102.
Sitaki hadithi za kwenye vitabu mimi
Nataka uweke ushahidi wa namna uchawi ulivyo na utendeji kazi wake
Sasa wewe ukisema “uchawi haupo kabisa,” lete ushahidi unaothibitisha kutokuwepo kwake.

Kusema “huwezi kuthibitisha kitu ambacho hakipo” si ushahidi kwamba hakipo. Lete ushahidi, si madai.

Nadhani hata hujui unachokisema
Kama nimesema uchawi haupo basi wewe unaesema upo Thibitisha

NB: siwezk kuthibitisha kitu hakipo!
 
Sitaki hadithi za kwenye vitabu mimi
Nataka uweke ushahidi wa namna uchawi ulivyo na utendeji kazi wake

Nadhani hata hujui unachokisema
Kama nimesema uchawi haupo basi wewe unaesema upo Thibitisha

NB: siwezk kuthibitisha kitu hakipo!

Sawa, hapo ndipo tunapotofautisha “sijui kama upo” na “haupo.” Wewe umechagua kusema “uchawi haupo”, si “sina ushahidi kwamba upo.”

Mimi nakuletea ushahidi wa maandiko yanayozungumzia uchawi: Kutoka 22:18, Kumbukumbu 18:10–12, Matendo 8:9–11 na Qur’an 2:102.

Kama unakataa kwamba uchawi upo, eleza kwa nini ushahidi huo hautoshi. Usibadilishe “sijui” kuwa “hakipo.”
 
Usiniletee hadithi za kale
Hizo ni abunuasi

Niambie matukio ya kichawi uliyokutana nayo na namna ulivyothibisha ni uchawi

Again uchawi haupo
Kama upo Thibitisha
Kwangu mimi uchawi ni theory 📌
 
Usiniletee hadithi za kale
Hizo ni abunuasi

Niambie matukio ya kichawi uliyokutana nayo na namna ulivyothibisha ni uchawi

Again uchawi haupo
Kama upo Thibitisha
Kwangu mimi uchawi ni theory 📌

Umesema uchawi ni theory, lakini bado unadai “uchawi haupo.” Kama ni theory, basi huwezi kuigeuza kuwa ukweli uliothibitishwa kwamba haupo.

Na mimi sijadai kila tukio lisiloeleweka ni uchawi. Hoja yangu ni kwamba uwezekano wa uchawi hauwezi kukataliwa kwa kusema tu “haupo.”

Swali langu kwako ni rahisi:

Ni kipimo gani cha kisayansi ulichotumia kuthibitisha kwamba uchawi haupo kabisa, badala ya kusema tu “mimi sijauona”?

Kama huna kipimo hicho, basi kauli yako sahihi ni “sijui kama uchawi upo,” si “uchawi haupo.”
 
Asante kwa maoni tukutane wakati mwingine kwenye mada nyingine

Hapa tutakesha sana
 
Asante kwa maoni tukutane wakati mwingine kwenye mada nyingine

Hapa tutakesha sana

Sawa, hakuna shida. 😊 Lakini kabla hatujaacha mada, kumbuka kwamba “sijui” si sawa na “hakipo.” Umesema uchawi haupo, lakini ulipoulizwa ushahidi wa kuthibitisha kutokuwepo kwake hukutoa.

Tukikutana tena kwenye mada hii, tuje na ushahidi na hoja, si madai. 👍
 
Hatutakutana kwa mada hii tena
Maana ni kama wewe unaongea kichina then mi naongea kiswahili

Vp unapenda siasa au ni uchawi tu mkuu 😅😅
 
Hatutakutana kwa mada hii tena
Maana ni kama wewe unaongea kichina then mi naongea kiswahili

Vp unapenda siasa au ni uchawi tu mkuu 😅😅

😅 Sawa mkuu, si lazima tukeshe. Ila kusema “uchawi haupo” bila kuthibitisha ni kama kusema “China haipo” kwa sababu hujawahi kufika China.

Kuhusu siasa, tunaweza kuzungumza pia 😂 lakini kwanza nilitaka tuone tofauti kati ya “sijui” na “hakipo.”

Kama uchawi ni theory tu kwako, kwa nini umefikia hitimisho la uhakika kwamba haupo?
 
Ina maana huyo mtoto alitembea papo hapo mara baada ya kuchanjwa?

Usikute muda wa kutembea mtoto ulikua ni huo

Hii baado haiwezi kua sababu tuseme uchawi upo

Hapo tukimuuliza aligunduaje huo ulikua uchawi hawezi kutoa majibu
Suala la watoto kufikia umri wa kutembea ila wanakuwa wazito au hawawezi kutembea hadi kuchanjiwa dawa ndipo wanaanza kutembea si jambo geni ila naona wewe ndio mara ya kwanza kusikia hili, kwahiyo huyo mtoto alishafika umri wa kuweza kutembea ila akawa mzito kutembea ndipo akapelekwa kwa mganga na mganga akasema mtoto karogwa na ndipo akamchanja dawa hivyo baada ya muda akaanza kutembea.

Nimeleta hili sio kukufanya useme uchawi upo ila uelezee hapo saikolojia imefanyaje kazi? Maana jambo hili la watoto kuchanjiwa kwa kuchelewa kutembea lipo sana tu.
 
Hili ndio TATIZO KUBWA SANA la watu wa IMANI………….. kazi yenu ni KUSIKIA kisa cha kichawi na kisha KUAMINI 100%

Ndio maana tunasema IMANI huwa haitaki matumizi sahihi ya AKILI………….. Nyie ndio mkiambiwa na wachungaji wenu chochote MNAKUBALI tu
Watu wa imani ndio watu gani?

Suala la watoto kuchelewa kutembea na hadi kuchanjiwa dawa ili waweze kutembea lipo sana katika jamii zetu, sasa mie napotoa mifano kama hiyo ili tuijadili unakuja kusema sie watu wa imani.

Watu wa imani ni watu gani? Hebu elezea ni kwa vp wewe unaishi kwa uthibitisho tu katika maisha yako ya kila siku.
 
Je una uwakika gani kwamba hiyo jamii haijishughulishi na uchawi? Au kwakuwa hawatuonyesho wazi wazi?

Hiyo jamii inatumia uchawi ingawa sio kwa kiwango ambacho tunakiona huku kwetu

Unaweza niuliza nimejuaje?

Kupitia sanaa zao kama sinema,tamthilia na mambo kama hayo, kazi yoyote ya sanaa huwa inatoa materials zake kwenye jamii husika

Huwa tunaona matumizi ya kupiga Ramli kwa kutumia karata au gololi au vitu vingine lakini vikiashiria dhana ya uchawi kwenye jamii yao

Siwezi kusema uchawi umeundwa na mwanadamu, bali umeumbwa na Mungu, kwa mujibu wa qur'an uchawi ulifundishwa na Malaika wawili ambo ni Haruti na Maruti kama kumbukumbu ipo sawa

Lengo ni mtihani kwa wanadamu,na kabla hawajamfundisha mtu yoyote yule,waliwaambia huu ni mtihani kwenu,yeyote atakaye taka kujifunza basi amekufuru na hata uona ufalme wa Mungu

Lakini pili Allah akasema hakika uchawi hauwezi kumdhuru mtu yoyote isipokuwa kwa idhini yake

Kwa maana Allah akiruhusu uchawi ukidhuru basi utakudhuru,na waeza jiuliza kwanini Mungu aruhusu hili? Jibu yote ni mitihani kwa waja wake
Kwaiyo kile kipapai alichopigwa Mudi Allah aliruhusu.!?

Kobazi jishikieni

Myahudi alimroga mtume kwa kuchukua nywele zake na kuzizika kisimani muhamadi Akawa ananyonyoka nywele tuseme ni mapenzi ya allah

Sio ajabu ndio maana Sule anajikuta professor wa majini.. Hamna akili nyinyi
 
Sio kuonekana………. Ni kwamba HAUPO kwasababu haujawahi KUTHIBITISHWA upo.
HIvi unafahamu hata meditation zamani watu walikataa kuwa ina faida kwa sababu ilikuwa haijathibitishwa kuwepo hizo faida kwenye meditation ila sasa hivi faida za meditation zimeweza kuthibitishwa kisayansi?
 
😅 Sawa mkuu, si lazima tukeshe. Ila kusema “uchawi haupo” bila kuthibitisha ni kama kusema “China haipo” kwa sababu hujawahi kufika China.

Kuhusu siasa, tunaweza kuzungumza pia 😂 lakini kwanza nilitaka tuone tofauti kati ya “sijui” na “hakipo.”

Kama uchawi ni theory tu kwako, kwa nini umefikia hitimisho la uhakika kwamba haupo?
😅 Sawa mkuu, si lazima tukeshe. Ila kusema “uchawi haupo” bila kuthibitisha ni kama kusema “China haipo” kwa sababu hujawahi kufika China.

Kuhusu siasa, tunaweza kuzungumza pia 😂 lakini kwanza nilitaka tuone tofauti kati ya “sijui” na “hakipo.”

Kama uchawi ni theory tu kwako, kwa nini umefikia hitimisho la uhakika kwamba haupo?
Yaani wewe bana 😅😅
Huo mfano wa china huoni haufanani?

Halafu kwanini unang'ang'a nithibitishe kitu ninachosema hakipo

Huku wewe unaesema uchawi upo umeshindwa kuthibisha

Ugumu upo wapi kunipa mifano hai ?
 
Suala la watoto kufikia umri wa kutembea ila wanakuwa wazito au hawawezi kutembea hadi kuchanjiwa dawa ndipo wanaanza kutembea si jambo geni ila naona wewe ndio mara ya kwanza kusikia hili, kwahiyo huyo mtoto alishafika umri wa kuweza kutembea ila akawa mzito kutembea ndipo akapelekwa kwa mganga na mganga akasema mtoto karogwa na ndipo akamchanja dawa hivyo baada ya muda akaanza kutembea.

Nimeleta hili sio kukufanya useme uchawi upo ila uelezee hapo saikolojia imefanyaje kazi? Maana jambo hili la watoto kuchanjiwa kwa kuchelewa kutembea lipo sana tu.
Huoni kama hiyo sababu ya mtoto kucwanjwa ni nyepesi sana kuthibitisha uchawi ?

Kama asingechanjwa unadhani asingetembea?

Kawaida watoto wanatofautiana sana
Kuna wale wanaowahi kutembea na kuna wale wanaochelewa kutembea

Wazazi wengi wanaenda kwa waganga mtoto ameshafikia kutembea

Akipewa dawa baada ya week
Mtoto akatembea anaona mganga kamsaidia 😅
 
Back
Top Bottom