Je, ni uchawi au saikolojia?

Je, ni uchawi au saikolojia?

Uchawi upo, majini yapo na kila ulichoambiwa kipo wala sio saikolojia kama unavyoamini

Kwanini technolojia ya kupaa isihalalishwe ili kupunguza foleni hilo jambo haliwezekani kwa sababu lipo kiimani, litawezekana tu kama wote mnaimani ya uchawi maana litakuwa jambo la kawaida, ila as long as ipo nguvu kinzani na mambo ya giza hilo jambo halitakaa liwezekane
Mkuu madawa ya kulevya si na pingwa? Wizi si unapingwa? ………… kwahiyo uchawi kupingwa ndio ishindikane kuuthibitisha upo?
 
Uchawi upo, majini yapo na kila ulichoambiwa kipo wala sio saikolojia kama unavyoamini
Thibitisha uwepo wake
Kwanini technolojia ya kupaa isihalalishwe ili kupunguza foleni hilo jambo haliwezekani kwa sababu lipo kiimani, litawezekana tu kama wote mnaimani ya uchawi maana litakuwa jambo la kawaida, ila as long as ipo nguvu kinzani na mambo ya giza hilo jambo halitakaa liwezekane
Kwanini uchawi haifanyi kazi mpka uamini
Kuna kisa nimekisikia japo sijakishuhudia huku niliko, asubuhi hii nitakiweka 😃😃😃
Usisahau bro 😆
 
Mkuu hebu nyooka nikuelewe
Unaamini uchawi upo au haupo
Halafu tuendelee

Ndiyo, ninaamini uchawi upo. Lakini siamini kwamba kila tukio linaloitwa “uchawi” ni uchawi, baadhi unaweza kuwa udanganyifu, kisaikolojia au una maelezo ya kawaida.

Sasa nimejibu wazi. Tuende kwenye ushahidi: lete ushahidi unaothibitisha kwamba uchawi haupo.
 
Sawa ngosha
Ni hivi kuna taarifa jana niliisikia japo sikushuhudia kwa sababu hapa ni mgeni. Kuna jamaa alikamatwa ndani chumbani kwa Dada fulani. Usiku wa manane halafu milango ilikuwa imefungwa.

Baada ya kunasa mule ndani yule dada alipiga kelele watu wakajaa usiku wa manane, yule jamaa alikuwa ndani ya bukta tu hivi aliingiaje mule ndani ? Aliyekuwa anasimulia anasema mwamba alikuwa ana bonge la hirizi mkono wa kulia.

Huu ni uchawi kabisa aisee sio nadharia
 
Ndiyo, ninaamini uchawi upo. Lakini siamini kwamba kila tukio linaloitwa “uchawi” ni uchawi, baadhi unaweza kuwa udanganyifu, kisaikolojia au una maelezo ya kawaida.
Ahaa basi sawa
Sasa nimejibu wazi. Tuende kwenye ushahidi: lete ushahidi unaothibitisha kwamba uchawi haupo.
Siwezi kuthibitisha kitu ambacho hakipo
Wewe ndiyo ulete ushahidi kwanini unasema uchawi upo.
 
Ni hivi kuna taarifa jana niliisikia japo sikushuhudia kwa sababu hapa ni mgeni. Kuna jamaa alikamatwa ndani chumbani kwa Dada fulani. Usiku wa manane halafu milango ilikuwa imefungwa.

Baada ya kunasa mule ndani yule dada alipiga kelele watu wakajaa usiku wa manane, yule jamaa alikuwa ndani ya bukta tu hivi aliingiaje mule ndani ? Aliyekuwa anasimulia anasema mwamba alikuwa ana bonge la hirizi mkono wa kulia.

Huu ni uchawi kabisa aisee sio nadharia
Heeeeeeh watu walipeana miadi wakulane sijui wameshindwana nini
Mnasema mwanaume mchawi 🤣🤣
 
Heeeeeeh watu walipeana miadi wakulane sijui wameshindwana nini
Mnasema mwanaume mchawi 🤣🤣
Sina uhakika niliambiwa lakini Mwamba inaonekana domo zege 🤣 kwanini aingie usiku wa manane aafu amejifunga hirizi ?

Naendelea kudodosa hapa yule Dada alikuwa anaita mwiziii , mwiziii na jamaa sijui alikuta na firewall akashindwa kunasuka. Alipohojiwa akawa hana majibu
 
B
Hello jamii intelligence 👋

Wakuu hii habari ya uchawi nadhani sio jambo geni
Uchawi ulitajwa kwenye vitabu vya dini hasa hivi maarufu Bible&Qur'an

Kwa bible mfano Kutoka 22:18 inasema:

Usimwache mchawi kuishi
Huu ni ushahidi kua Bible inatambua uchawi

Uchawi umetajwa pia kwenye Qur’an, hasa Al-Baqarah 2:102 ambapo inazungumzia habari ya uchawi na watu kujifunza mambo hayo
Huu nao ni ushahidi Qur'an inatambua habari za uchawi

kwa mantiki hii dhana ya uchawi ni ya kale sana

Huku Africa watu bado wamekumbatia hii imani sana, sijui huko Ulaya ikoje

Utasikia mtu anasema
👇
Mtoto huyu karogwa, sio akili zake.

Hapa tunaona uchawi unatajwa kama kitu ambacho kinaweza kubadilisha hali ya mtu
Alikuwa mzima, ghafla akawa kichaa au mtu asie sawa kama alivyokua kabla

Mtu anaumwa, unaambiwa karogwa

Sasa najiuliza...

Uchawi umetengenezwa au umeundwa kwa kufanya vitu negative tu?

Hakuna namna huo uchawi kama upo unaweza kutumika kwa njia positive?

Yaani tukaamua kutumia akili ya mtu kilaza akawa genius, kama vile inavyoaminika kwamba uchawi unaweza kumbadilisha genius kuwa kilaza?

Kuna hii pia👇

Ooh, wachawi wanapaa usiku...

Kwanini sasa kama hiyo technology ipo tusiitumie kupunguza foleni?

Huo usafiri wa kupaa uwe official sasa

Nyie wachawi wa JF(jokes)
haiwezekani kuwa hivi yaani huu uchawi ukawa na tija?

Hivi uchawi unafanya kazi kweli au ni mambo ya nadharia tu?

Niliwahi kua na matatizo ya kupata maumivu ya kicwa nakizunguzungu

Basi kuna mtu akamwambia mama:

Huyu ShesRise_1 amelogwa asifanye vizuri shuleni na si haba shuleni nilikua najitahidi kwahiyo huyo mama akamuambia mama angu huenda nimelogwa ili nirudi nyuma kimasomo🤔

Heh! 🤔

Nikastuka

Nikawaza, haya yatakuwa mambo gani?

Basi nikaanza kufanyiwa zile zinazoitwa tiba za Kisunna, visomo na mambo mengine

Ajabu ni kwamba kuanzia pale ndiyo kwanza nikaanza kupata maruerue.

Usiku naogopa kulala mwenyewe.

Naota ndoto za ajabu, heh... tafrani mtindo mmoja

Kumbe ile issue ya kuanza kuota mauza uza ni kwa sababu
ya saikolojia bana
Yaani saikolojia kwa maana baada ya kusikia nimelogwa na kupelekwa kwenye visomo

Ndiyo ubongo ukaanza kuniundia mapicha picha

So nilivyoambiwa tu vile, akili yangu na ubongo wangu vikaanza kujishughulisha na hayo mambo

Mara nione hiki...

Mara nisikie kile...

Mara nianze kujiuliza, Hivi huu ni uchawi gani?

Asieee!

Nikakaa nikasema:

Hapana, hizi mbona kama fix?

Na mimi by nature nina kaubishi fulani sipendi kumezeshwa mambo japo mwanzo wali ni win

Nikaacha kabisa huo upuuzi

Nikaamua ku-clean akili yangu

Kuanzia hapo nikiambiwa

Njoo kwenye visomo

Nawaambia

Mimi sina tatizo lolote

Na kweli, nilifanya vipimo hospitali nikambiwa kicwa kilikuwa kinauma kwa sababu sikuwa na damu ya kutosha, na ndiyo maana nilikuwa naumwa kicwa na kizunguzungu

Na hata sijui ilikuaje na mama akaingia kwenye mtego wa rafiki yake akaacha kunipeleka hospital kwanza akaanzia kwenye imani huku

Nikatumia zangu dawa nikawa fresh

Sijaumwa tena kicwa, labda cha mafua tu

Sioni mauza mauza wala nini

Naishi vizuri kabisa

Ndipo nikaja kugundua kumbe mambo mengine ni saikolojia tu

Wala hakuna cha uchawi wala nini

Na kuna hii pia ya majini kutaja uchawi bila majini sio sawa ni mtu na shoga yake

Sasa imagine eti mtu anapandisha mashetani anataka dhahabu...

Heh! Dhahabu sasa inatoka wapi yani?

Mashetani wana migodi yao huko?

Nimetoa mtazamo wangu kuhusu hii dhana ya uchawi

Je, uchawi ni nguvu halisi?

Au wakati mwingine tunaita kitu uchawi kumbe kuna sababu za kiafya, kisaikolojia au mazingira ambazo hatujazijua?

Na kama kweli uchawi una uwezo wa kumbadilisha mtu kutoka kuwa genius mpaka kilaza...

Kwanini usitumike kinyume chake?

Au kama wachawi wanaweza kupaa...

Kwanini bado tunakaa kwenye foleni?

Kama hii dhana ya uchawi haina tija kwanini tuna ing'ang'ania?

ShesRise_1 ✋️
Binafsi nimekua nikisimuliwa kuhusu uchawi...

Nimekuwa mtu mzima sasa SIJAWAHI KUSHUHUDIA UCHAWI KWA MACHO! Ama kuthibitisha!, wala kujiridhisha kwa tukio lolote lile nililoliona kwa macho na moyo wangu kujiridhisha na kuamini kuwa huu kweli ni UCHAWI!

Nachelea kusema ni dhahania tu!
 
Mimi pia mkuu hakuna tukio au mazingira niliyowahi kukumbana nayo nikasema hili tukio ni uchawi

Naunga mkono uchawi ni nadharia tena ya kale sana
 
Back
Top Bottom